Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
mhhh sina cha kusema, ila jk anasikitisha sana.
-Amefanikiwa kuwarubuni mapadri, wachungaji, maaskofu, masheikh wakaamini kuwa chadema ni cha udini na yeye ni chaguo la Mungu.
-Kwa ujinga wao (yes nasema ujinga) wakamkumbatia, wamembariki kwa kuiba kura-wamembariki mwizi wa haki na hatima ya watu.
-ukiangalia kimuundo kati ya chadema, cuf na ccm huhitaji kufika ahata darasa la nne utajua chadema ina mchanganyiko mzuri wa udini na ukanda ila ccm ni chama cha kidini 80%. cuf-is obvious.
 
Kuna haja ya kupima IQ za hawa jamaa. Maana wanaongea vile midomo inavowatuma na ndo maana hata miili yao huwa haioneshi ushirikiano wakati wa kuongea, wanabakia wakiongea taarabu tu.!!!!!!!!!!
 
Hivi ni lazima kwa uongozi wa Chadema kusema wanamtambua Kikwete kama Rais ili apate uhalali wa kura Rais? Sote tunajua tume imemtangaza kuwa ni Rais na kisheria ni Rais; lakini hakuna mahali ambapo Mtanzania analazimishwa kumtambua kwani kumtambua au kutomtambua hakumfanyi asiwe Rais. Lakini dhamira safi ikisema haimtambui ni kwa ajili ya dhamira hiyo.

Mkuu Mwanakijiji,
watu wana ugumu tu wakutotaka kufikiri. Nimemsikiliza Mbowe akiongea BBC asubuhi; nimemsikia Slaa akiongea hapa.
Kuna mambo ambayo hayana ubishi:
1. CHADEMA wanatambua kuwa NEC wamemtangaza Kiwete..sorry, I mean Kikwete kuwa kuwa Rais wa Tanzania.
2. CHADEMA wanatambua haki zao za Kikatiba; wanajua sheria na Kanuni za Bunge; na walichokifanya kiko well within the two; ndo maana hakuna hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa na Spika dhidi yao hadi sasa.
3. CHADEMA sio wa kwanza kufanya hivyo; CUF walifanya; wengine wamefanya
4. CHADEMA hawana historia ya kukurupuka; Kikwete ni bingwa wa kukurupuka; mfano mdogo sana wa matamshi yake kwa wafanyakazi na alivyokuja kuyarudia matapishi yake. Tukianza kulist matamshi au vitendo alivyowahi kuvifanya kwa kukurupuka ni issue ya wiki nzima. CHADEMA wamempita rank sana kwa hilo. Naamini hata kwa hili hawajakurupuka; the guys knows what they are doing. Plus; kama wameboronga, why all the fuss? si tuwache walinywe wenyewe?
5. Hivi anaeondoka kimyakimya na anayemzomea nani mjinga? au, kichaa na anayemkimbiza kichaa nani kichaa?
6. Lastly, waingereza wanamsemo wa " THERE ARE SO MANY WAYS OF SKINNING A CAT.." kwa maoni yangu, CHADEMA has employed just one means out of many; and it is perfectly okay with me.

Kujibu swali lako; sio lazima mtu amtambue Rais aliyepitishwa na NEC. Kumbuka kuna watu huku Tanzania katika uongozi wa Kikwete wao bado walikuwa wanatambua Nyerere (RIP) ndo rais wao; and rightly so I think... [kutokubalika kuna njia nyingi ya kuelezewa; like watu kutumia fedha za nje kununulia shati kwenye nchi yako nk. all this is protest..]
 
Ni aibu na hatari sana kuwa na rais wa namna hii,kalianzisha la udini halafu anageuka upande wa pili na kusema kuna tatizo la udini ana akili timamu kweli huyu?kama angekuwa nazo basi asingethubutu tangu mwanzio kutamka swala la udini.Yuko madarakani kimabavu na hatujui kwa mtazamo wa akili zake atatuletea nini tena manake la udini limeshindwa,tuiombee nchi ibaki salama.
 
Hofu yangu mimi CHADEMA wanafanya kama CUF ilivyofanya Zanzibar. Hawatalimaza suala hili kama CUF walivyolimaliza kule? Sasa hivi Maalim Seif yuko kivulini, Juma Duni Haji yuko peponi. Lipumba wetu huku Bara amekuwa Gorbachev. Siasa ni hasa!
 
Hata kama watu hawakubaliani na kilichotokea, ni muhimu kutambua umuhimu wake katika siasa za Tanzania. Kuna mambo ambayo Tanzania bara hayakuwahi kudhaniwa yanaweza kutokea lakini safari hii karibu yote yametokea. Kuna watu ambao wanapenda kuona Tanzania ya zamani ambapo mtu akisema "umoja na mshikamano" basi wote wanapanga foleni na kadi zao zimeandikwa "umoja na mshikamano".. wakiulizwa wana umoja na mshikamano kwenye kitu gani? ndipo songombingo inapoanza. Tanzania ya sasa ni Tanzania yenye kuhitaji majibu.


  1. Hivi, kwanini Tume ya Uchaguzi haikuamua kusitisha hata kwa muda kutangaza matokeo ya Urais ili kusikiliza malalamiko ya CHADEMA? Kwa sababu tume hailazimishwi na sheria kutangaza matokeo katika kipindi fulani ingeweza kuchelewesha hata kwa siku mbili ili kusikiliza na kupitia ushahidi ambao Chadema walisema wanao. Ingeupitia na kuamua na kuendelea na matangazo au kufanyia kazi. Kwanini hawakusitisha kutangaza kura za Rais?
  2. Kwanini, tume ilikataza vyombo vya habari visitangaze matokeo ya Urais kutoka Tanzania bara wakati matokeo yake yalikuwa tayari majimboni na badala yake ikaanza kutangaza matokeo ya Zanzibar, Mtwara na Lindi wakati yale ya sehemu za Dar, Mwanza, Tanga Mjini, Mbeya, Arusha Mjini yalikuwa tayari kabla ya kura za Zanzibar kuanza kutangazwa?
 
Sawa.

Lakini hii gharama ya udini itawatokea puani.

Unalo Mkwere
 
Hata kama watu hawakubaliani na kilichotokea, ni muhimu kutambua umuhimu wake katika siasa za Tanzania. Kuna mambo ambayo Tanzania bara hayakuwahi kudhaniwa yanaweza kutokea lakini safari hii karibu yote yametokea. Kuna watu ambao wanapenda kuona Tanzania ya zamani ambapo mtu akisema "umoja na mshikamano" basi wote wanapanga foleni na kadi zao zimeandikwa "umoja na mshikamano".. wakiulizwa wana umoja na mshikamano kwenye kitu gani? ndipo songombingo inapoanza. Tanzania ya sasa ni Tanzania yenye kuhitaji majibu.


  1. Hivi, kwanini Tume ya Uchaguzi haikuamua kusitisha hata kwa muda kutangaza matokeo ya Urais ili kusikiliza malalamiko ya CHADEMA? Kwa sababu tume hailazimishwi na sheria kutangaza matokeo katika kipindi fulani ingeweza kuchelewesha hata kwa siku mbili ili kusikiliza na kupitia ushahidi ambao Chadema walisema wanao. Ingeupitia na kuamua na kuendelea na matangazo au kufanyia kazi. Kwanini hawakusitisha kutangaza kura za Rais?
  2. Kwanini, tume ilikataza vyombo vya habari visitangaze matokeo ya Urais kutoka Tanzania bara wakati matokeo yake yalikuwa tayari majimboni na badala yake ikaanza kutangaza matokeo ya Zanzibar, Mtwara na Lindi wakati yale ya sehemu za Dar, Mwanza, Tanga Mjini, Mbeya, Arusha Mjini yalikuwa tayari kabla ya kura za Zanzibar kuanza kutangazwa?
Mkuu Mwanakijiji

Maswali hayo majibu yake hatuwezi kuyapata wakati rais alilshatangazwa.CHADEMA wana matokeo yao ya kila sehemu wayalete basi na kuonesha ni nani alishinda..

mie huw sipendi story na speculation bila kuwapo na facts...tutaanzia hapo ila hili suala la kulia lia tu
 
Dr., Since umeanza kwa kuongelea consinstency, swali langu mimi ni, kama hamumtambui Kikwete mlipopiga kura pendekezo lake bungeni kwa kiti cha Waziri Mkuu, mlikuwa mnapigia kura pendekezo la nani? Je pale mlimtambua halafu mkashauriana na sasa hamumtambui? Kuna consistency gani hapo ?



Utasemaje unaonyesha kutomtambua rais kwa kutohudhuria hafla ya kuapishwa Waziri Mkuu wakati umehudhuria, kushuhudia na kushiriki upigaji kura zilizompitisha huyo waziri mkuu aliyependekezwa na rais ? Kipi muhimu, kura za kumpitisha au tafrija ya kumpongeza baada ya kupitishwa ? Hivi kweli mnataka tuwachukulie seriously kwa mwendo huu ?



Muda wa ishara umekwisha, tunataka matendo yenye lengo la kuleta mabadiliko ya kisheria.



OK, kwanza unasema serikali haiwasikilizi, halafu unaendelea kusema unategemea serikali itawasikiliza, au hata inaweza kuwaahidi marekebisho. Wanasema kufanya kitu vile vile na kutegemea matokeo tofauti ni kichaa, sasa CHADEMA mnafanya nini tofauti na nyuma ? Au "mnapiga makelele" tu kama unavyosema mwenyewe mkitumaini CCM wataona haya na kuwapa mabadiliko katika kisahani cha dhahabu? Kama hawana haya na hawawapi mabadiliko je, mtafanya nini ?



Again, huwezi kushiriki kumpitisha Waziri Mkuu, halafu ukasusia hafla, halafu uniambie uko serious. This is a big joke.



Mimi ningekusifu na kukupongeza zaidi kama ungesusia kila kitu cha rais huyu, pamoja na kupigia kura uhakiki wa chaguo lake la waziri mkuu.



Njia unayotumia wewe haizai matunda, actually ni the worst of both worlds. Wataka mabadiliko wa kweli kama mimi tunakuona haufanyi vya kutosha, wapenda ushirikiano wa vyama vya kisiasa watakuona unawagawa Watanzania kwa misingi ya vyama. Utawapata wafuasi wako hao hao wanaoamini CHADEMA kama dini.

Kama kweli unataka kutomtambua rais huyu itisha migomo na maandamano nchi nzima.

La, mkubali uende kutaka mabadiliko bungeni. Zaidi ya hapo unazua maswali mengi kuliko majibu.

Nakupongeza KIRANGA kwa kusimamia unachoamini, ni wazi umeonyesha utata uliojionyesha wazi ktk hotuba ya DKT SLAA na mwisho kutoa msimamo wako na wapenda mabadiliko wengine. Ni wazi utata uliohuainisha unataka majibu kwa watanzania na wapenda mabadiliko.

Lakini mimi narudi ktk msimamo wangu, AMANI kwa waTZ masikini wasio kuwa na uhakika wa kesho yao. Kuwatafutia ukombozi hawa si kwa kuwainginza ktk maandamano maana serikali Dhalimu nyingi za Afrika zimetuonyesha nini zinachowafanya Raia wao Masikini wanapodai haki zao, na serikali yetu ya Tanzania ni imeshawahi kuonyesha DEMO huko Pemba mwaka 2000, na mwaka huu kwa watanzania wote waliokuwa wana linda kura zisichakachuliwe vituoni KARAGWE,SHINYANGA MJINI, KIBAHA,MBEYA MJINI, MWANZA nk. Na mbaya Zaidi machafuko yakitokea suluhisho la AFRIKA na JUMUIA ya kimataifa kututaka kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa chini ya mwizi wa kura mf. ZIMBABWE,KENYA na ZANZIBAR na hali hii ambayo wenyewe wanahita ndio suluhisho la kuleta AMANI imeshakuwa DEMOKRASIA INAYORASIMISHWA kwa nchi za AFRIKA.
NINAWEZA KUWA NA MAWAZO TOFAUTI NA WENGI lakini kwangu ktk mgogoro uliopo mbele yetu falsafa za MAHTIMA GHANDI zinaweza kutumika ktk kupigania HAKI/USHINDI ulioporwa.
 
Wabunge wa chadema hawakumpigia kura za ndio pinda, hiyo ni njia ya kutomtambua kikwete
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.

Hata Idd Amini alikuwa Rais je alikubalika kwa wananchi wake? Ni sawa na Kikwete, ni raisi hata Chadema wanajua hivyo kwani sheria inasema tume ikishatangaza basi. Hata hivyo tunachosema ameingia kama alivyoingia Iddi Amini, amefanya mapinduzi kwenye sanduku la kura, na hakubali na sehemu kubwa tu ya watanzania ambao tumeshabaini kuwa ameingia kwa wizi. Sasa tunataka tupeleke ujumbe huu kwa watanaznia na wasio watanzania kuwa kuna kitu hakiko sawa hapa. Period.
 
kuna haja ya kupima iq za hawa jamaa. Maana wanaongea vile midomo inavowatuma na ndo maana hata miili yao huwa haioneshi ushirikiano wakati wa kuongea, wanabakia wakiongea taarabu tu.!!!!!!!!!!
hiyo point mkuu kuna watu inafaa wapimwe iq yao kabla hawajaingia kwenye uongozi!
Eeeti kuna ufa ni nani kauleta huo ufa!?????
Ubaguzi uliuanzisha jk na lazima uitafune ccm!
 
Tume ipi jamani; its as good as dead. Walishakabidhi integrity yao siku nyingi. Imagine sheria inasema akishaapishwa Rais huwezi pinga; mtu anapinga beforehand kwa kufuata sheria; bado wanaendelea; this people wanastahili kuchapwa viboko; I wish yule aliyepigwa makofi na Mbowe angekuwa mwenyekiti wa hito Tume. mtu mwenye akili zake hawezi kumtambua mtu mwenye kupata madaraka kwa wizi; kama hawakuiba kwanini walifanya walichokifanya? siwangeacha vyombo vua habari viendelee kutangaza tuhesabu kura hata majumbani kwetu; leo mimi nikimtambua huyu rais nitakuwa nashusha heshima yangu sana. Lakini asitegemee nitaacha kwenda kazini kwasababu simtambui; nitafanya kazi; akinipa cheo ntakula; lakini simtambui; he is just there; a figure; makes no difference to me whether he is making a joke of it or not; but it will make a lot more difference if he is not there at all; thats my prayer
 
Ubaguzi uliuanzisha jk na lazima uitafune ccm! mimi nashangaa sana mkuu wa kaya maana yeye ni mmoja wapo wa watu wanaochangia udini
 
Mh.JEIKEI uzee waanza kumchanganya. Naamini ana afya bora,akili nzuri ila sasa uzee umeanza kumuingia. Siku zinavozidi ndio matamshi yake yanavoanza kujichanganya. Nasema kujichanganya mana yeye tu ndo anajichanganya,sisi hatuoni anachokimaanisha anajichanganya. Ukweli ni kwamba Tz hamna udini na kama upo basi upo kwenye muundo wa serikali ya awamu ya nne tu! Hapa inawezekana udini upo ktk kuunda baraza la mawaziri,kuteua wakurugenzi,kuteua wakuu wa wilaya,kuteua wakuu wa mikoa. Hapa kweli kunaweza kukawa na udini na si ktk mikusanyiko ya wananchi. Ivi niwaulize swali kama kuna mkiristo ambaye ktk ndugu zake hamna mwislamu,au vice versa!ukichunguza upande wa mjomba,shangaz au kwingneko zimejaa dini kibao. Kauli ya dr.jk ni kauli ya kupingwa na kulaaniwa kwa njia za amani. Huyu mkulu ameanza ile "divide n rule policy" baada ya ile ya uchaguzi ya kamanda shimbo kuisha ya "gun but diplomacy" Hatutakubali kuhubiriwa udini,kwa ili mkulu ashindwe na alegee. Tuiache nchi ya mwl.Nyerere ikae ilivokuwa.
 
Naipongeza sana CHADEMA kwa msimamo waliyouonyesha!hiki ndiyo chama makini cha upinzani kilichobaki!!
 
Mkuu Mwanakijiji

Maswali hayo majibu yake hatuwezi kuyapata wakati rais alilshatangazwa.CHADEMA wana matokeo yao ya kila sehemu wayalete basi na kuonesha ni nani alishinda..

mie huw sipendi story na speculation bila kuwapo na facts...tutaanzia hapo ila hili suala la kulia lia tu

hakuna mwenye kesi anayetanguliza kuweka hadharani ushahidi wake kabla hata hajafungua mashtaka; tena kwa nchi ya mabingwa wa kuchakachua huo ushahidi ukitolewa tu leo kesho washamaliza kuchakachua.

Likewise kuwataka CHADEMA kuandaman ni kupigana mieleka na nguruwe, kucheza matopeni ndo mahali pake pa kujidai; leo CCM wanasubiri CHADEMA wafanye the slightest mistake ya kuanza maandamano wapate mahali pa kujisafishia machoni pa jamii ya kitaifa na kimataifa; hapo naona ndo karata yao turufu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom