Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.

Kiranga mbona unajitafuna-tafuna sana?, hivi usichotaka kuelewa hapo ni kipi au unachotaka kulazimisha watu wakielewe ni kipi?.

Viongozi wa CHADEMA wanajitahidi kwa kila hali kuepusha vurugu na kwa taarifa yako kuna watu wengi tu ambao wangependa kuingia mtaani kulianzisha hata leo hii lakini viongozi wanajaribu kuonyesha mfano kwa ku-protest kistaarabu, kwanza kuna nchi nyingine wabunge huwa wanatandikana makonde mle mle mjengoni sembuse kutoka tu nje ya ukumbi?

Kung'ang'ania kuwa wabunge wa-CHADEMA walimpigia kura Pinda ni kuonyesha jinsi gani unavyodharau kazi inayofanywa na wapiganaji wetu walioko mstari wa mbele.

We endelea na kujiliwaza na dharau zako lakini ujumbe umeshafika kunako loud and clear na kama Mkwere hataki kusikia basi aelewe yeye ndio mwanzilishi wa ile safari kuelekea huko wote tusikokutaka...
 
Sioni kama ilikuwa ni ushujaa wowote kwa sababu waliondoka ukumbi wa bunge na wakenda ukumbi mwingine kumwangalia kupitia luninga-Is a kindly shameful too!

do you know the meaning of protesting?
 


mkuu gwaride ndio linaandaliwa hivyo alijaanza muulize makinda na makinda zake wanavyohaha wanajuta kufanza uchaguzi
 
It is error alone which needs the support of government. Truth can stand by itself.
 

Looks like hili ndilo tamko rasmi la chama ambalo ndio ushahidi ama maelezo kamili ya sababu ya Dr Slaa ama Viongozi na Wabunge wa Chadema kutomtambua Rais Kikwete.........

Poleni sana kama huu ndio ushahidi mnaotegemea kuwafanya watanzania kwa wingi wao ambao unaweza kuleta mabadiliko, watanzania wasomi wa tabaka la kati ambalo ndio ngome yenu lakini pia jumuiya ya kimataifa ambayo katika masuala kama haya ndio huwa nguzo pekee ya utetezi wa UPINZANI katika hali kama hii. Lakini pia nawashauri mliondoe, mlipitie na mlipatie baraka za chama kwa maana ya vikao rasmi kabla ya kuendelea makosa haya ambayo yanahoji UMAKINI wenu....

Mkandara, ukisoma kwa umakini hili jibu/tamko ni wazi hii ni cut and pest ya mtu wa Chadema na pengine mwana Sekretariat na sio matamshi ya Dr Slaa hivyo unapojibu tambua kuwa hubishani na Dr Slaa......
 
Kikwete na kikundi chake ndani ya CCM wameamua kutumia udini kama tatizo ili kufunika mambo muhimu yenye utata katika nchi kwa sasa. Nchi ina matatizo ya kifisadi, utendaji mbovu wa serikali, maisha magumu kwa wananchi na mengine muhumu. Udini sio tatizo Tanzania, unatumika kugeuza upepo.
 
UDINI tz upo, lakini haukuwa applied kipindi cha uchaguzi, labda alikuwa anawasema cuf. lakini haikuwa issue kabisa hii, wasn't serious na haikutakiwa alitamke lile. Mr.president mimi huwa namshangaa sana.
 
ASANTE SANA mwanakijiji ila inasemekana siku zako zinahesabika , jiangalia brother

Mbona ni kama unamtishia mtu. Unaposema Siku za mweanakijiji zinahesabika una maana gani (nani kasema na ana maana gani?). Jamani tufike mahali tutumie jamvi hili kwa hekima. Tupime kile tunachoandika kabla ya kukipost.
 
Kwani Isaac Sepetu hajawahi kushika madaraka Zenj?
ndio nani huyo jamani? na angalia kwa cabinet hii ya sana na ya awamu ya karume, tutajieni tuwaone walikuwepo kina nani?hakuna sehamu yenye udini wa kuwabagua wakristo kama ilivyo zanzibar.
 
Mimi nimejitahidi sana kudadisi, kuchunguza na kusikiliza wapi udini/ukabila ulijitokeza Tz nimeshindwa....! Ingewezekana, JK angebanwa aseme ni chama gani hiyo, na wapi hapo ndani ya Tz ambapo udini, au ukabila, au vyote vimejitokeza hata kwa ishara....!
Hii inanishangaza mno kwa maana kila mgombea alikuwa na dini yake na kabila moja wakati Tz kuna makabila zaidi ya 125....! Kila chama ilikuwa na mchangantiko wa dini na makabila tofauti....! Hakuna mtu aliyetamka kumchagua mgombea yeyote kwa itikadi za dini, kabila, au eneo alilotoka....! Bali kila mmoja alikuwa akivutiwa na sera za chama na mgombea wake....! Kwa kweli mi niko :confused2::confused2::confused2:
 
JMT Raisi,Makamu WOTE ni waislam labda alimaanisha ilo
 
anatakiwa aongee, udini aliousema ulionekana wapi, nani aliendekeza udini? awe wazi tu kama kitu ni cha kweli...au la anawaamsha watz waanze kuweka kwenye fikra zao udini...na wakianza hivyo, watahoji vyeo vinavyotolewa na yeye kwa kupendelea dini moja, na ccm ilivyokuwa ya kibaguzi...point a finger Mr.president.
 
hata wbunge alioteua ni wawapi kama si.........
 



Moyo wangu huwa unasikitika sana napoona watu wenye uelewa wanakuwa wajinga simply wanapo jiunganisha na ccm.

Kama ulikuwa ni mtu wa kufatilia matukio ungejua Waziri Mkuu amepigiwa kura ngapi na tofauti ya kura ungegundua ni za upande upi.

Ilijidhihirisha wazi kabisa kuwa Wabunge wa Chadema hawakumpigia kura waziri mkuu.

naomba mjue Mbunge linaendeshwa na kanunu,Raisi haendeshi Bunge.

Tujifunze bunge ni Raisi na Wabunge,kumkataa Raisi na uteuzi wake siyo kulikataa mbunge na kanuni zake mambo haya ni mawili na tofauti kabisa.

Raisi ataendesha serikali lakini bunge linawakilisha wananchi,si kila mtu ndani ya serikali anakubaliana na Raisi.

Tukumbuke.

wakati Dk slaa ameshutumu vyombo vya usalama alisisitika mkuu wa vyombo vya usalama atoe majibu ya msingi kwa taifa,juu ya shutuma alizotoa.sisi sote ni mashahidi Mkuu wa vyombo vya usalama hakutoa taarifa yoyote badala yake majibu ya shutuma hizo yalitolewa na mtu mwingine katika nafasi hiyo ambayo sote hapa tulijadili bila kufikia muafaka.
kwa mtu mwenye kufikiri lazima aligundua kuna tatizo la mawasiliano katika ngazi za juu.

Hata shutuma ya Pili ya usalama wa taifa ,pia tuliona mtu aliyejitokeza kujibu shutuma hizo wengi tulijiuliza ni nani na kwa misingi gani.

mwisho wa siku tuligundua wote walitumiwa kujibu shutuma ni watu ambao kwa namna moja au nyingine niwale wanaotumika na wenye masilahi fulanni.

sote Tulishuhudia siku Rais anaapishwa hata viongozi wote wa juu wa dini waliohudhuria sio wale tuliowazoea.

watanzania nchi yeti iko icu tusiendekeze ushabiki utakaotugharimu siku za usoni,tatizo la Kikwete ni kubwa na hakuanza kukataliwa tu baada ya matokeo hata katika mchakato mzima wa kampeni na hatimae uchaguzi,dosari zipo nyingi na wengi tulishuhudia.

Leo wapo watu wanaweza kuthubutu kusema damu haikumwagika,watu wangapi waliumizwa na kufanyiwa matendo ya kuchomewa nyumba nk.je hii ni Demokrasia au demokrasia ni maneno tu.

leo Kikwete anatoa hotuba ambayo kwa namna moja inaonyesha hakubali kabisa kama kulikuwa na dosari katika uchaguzi.anathubutu kusema amechaguliwa kwa kishindo.Kura 5,000,0000 katika taifa la watu 45,000,000.

hiki siyo kitu cha kujivunia kabisa.mambo haya yatawatesa watoto wetu na ndugu zetu nyakati zijazo.


tuache ushabiki kwani ushabiki siyokitu cha msingi jana tumewashuhudia wabunge walivyokuwa wakipiga makofi katika kila jambo,sijui kama kuna mtu anaweza kutueleza katika hotuba yote Tanzania yetu ya leo itakuwa wapi kesho.
 
KIKWETE alitafuta mlango wa kutokea baada ya kuelemewa na hoja za wapinzani waliokuwa wakimbana aeleze yako wapi maisha bora kwa kila Mtanzania. Akaamua kupoteza lengo. Hata hivyo awashukuru viongozi wa KIKRISTO waliompigia ndogo ndogo kwa kusema yeye ni CHAGUO la MUNGU. Hawezi kuwasahau kina ASKOFU KULOLA, ASKOFU GAMANYWA aliyemwalikwa Kanisani kwake na kumwahidi kushughulikia mgogoro wa ardhi kanisani, ASKOFU KILAINI n.k. Huo udini anaousema unasomeka kwenye gazeti la AL_NUR lililokuwa likihubiri NDOA YA SLAA NA KANISA. Huko ndiko kwenye propaganda za udini na KIKWETE hajawahi kukemea gazeti hilo. Inawezekana Mhariri wa gazeti hilo ndiye anayemshauri MZEE juu ya udini.
 
Huo udini anaotuletea utamtafuna yeye,familia yake na maswahiba.Siye hatutakubali kamwe.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…