Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
1. Kura ilikuwa ya siri, habari ya nani alipiga vipi kura ni propaganda, Hata wabunge wenyewe hawajui wenzao walivyopiga kura. Kila mtu anajijua yeye tu alivyopiga kura.


2. Hata ukipiga kura ya Hapana, maana yake unakubali Pinda alistahili kupigiwa kura, maana yake unakubali aliyependekeza jina la Pinda ana mamlaka ya kupendekeza hilo jina, maana yake Kikwete unamtambua kama rais.

Sasa CHADEMA washamtambua Kikwete kama rais, halafu wanataka kusema hawamtambui, wanatuchanganya.

Kina Tundu Lissu na Mnyika si walitoa madukuduku yao kuhusu uchaguzi wa PM? Si walisema habari za serial numbers and all? Mbona hawakusema aliyeleta jina si rais tunayemtambua kwa sababu hii na ile ?

Kiranga mbona unajitafuna-tafuna sana?, hivi usichotaka kuelewa hapo ni kipi au unachotaka kulazimisha watu wakielewe ni kipi?.

Viongozi wa CHADEMA wanajitahidi kwa kila hali kuepusha vurugu na kwa taarifa yako kuna watu wengi tu ambao wangependa kuingia mtaani kulianzisha hata leo hii lakini viongozi wanajaribu kuonyesha mfano kwa ku-protest kistaarabu, kwanza kuna nchi nyingine wabunge huwa wanatandikana makonde mle mle mjengoni sembuse kutoka tu nje ya ukumbi?

Kung'ang'ania kuwa wabunge wa-CHADEMA walimpigia kura Pinda ni kuonyesha jinsi gani unavyodharau kazi inayofanywa na wapiganaji wetu walioko mstari wa mbele.

We endelea na kujiliwaza na dharau zako lakini ujumbe umeshafika kunako loud and clear na kama Mkwere hataki kusikia basi aelewe yeye ndio mwanzilishi wa ile safari kuelekea huko wote tusikokutaka...
 
Sioni kama ilikuwa ni ushujaa wowote kwa sababu waliondoka ukumbi wa bunge na wakenda ukumbi mwingine kumwangalia kupitia luninga-Is a kindly shameful too!

do you know the meaning of protesting?
 
asalaam aleykum,

jana nilikuwa miongoni mwa mamilioni ya watanzania tuliokuwa tukiangalia tv mida ya saa 10:30 jioni kuona mambo yanayojiri bungeni.

Lengo la kuangalia ilikuwa si kusikiliza hotuba ya rais jakaya kikwete bungeni, bali ni kushuhudia ni uamuzi gani ambao wabunge wa chadema watachukua.

Kulikuwa na tetesi kuwa wabunge wa chadema hawatahudhuria bungeni kama ambavyo hawakuhudhuria kwenye utangazaji wa matokeo ya uchaguzi wa rais, uapishwaji wa rais na kuapishwa kwa waziri mkuu.

Nilipata taarifa kuwa kulikuwa na jitihada kubwa zilizofanywa na kikwete kuhakikisha kuwa wabunge wa chadema watahudhuria hotuba yake bungeni.

Jitihada hizi ni pamoja na kikwete kutuma wajumbe kuongea na chadema na kuwasihi wahudhurie hotuba ya bungeni.

Wajumbe waliotumwa na kikwete kuongea na chadema ni pamoja na waziri mkuu wa zamani aliyejiuzuru kutokana na kashfa ya ufisadi ya richmond, edward lowassa (ni ajabu lakini kweli) na spika wa bunge, anne makinda, ambaye ccm wamepanga kumtumia ipasavyo kama rubber stamp baada ya kumfukuza kazi samuel sitta.

Pia zilifanyika jitihada za kuwaweka sawa baadhi ya wabunge wa chadema ambao wako karibu na vigogo wa ccm ili kukwamisha mpango huu.

Naelewa kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa ndani ya chadema, huku baadhi ya wabunge pengine kwa mtazamo wao huru au kuwekwa sawa na vigogo wa ccm walipinga wazo la ku walk out.

Hivyo basi, ilipofika saa 10:30 jioni ambapo kikwete aliingia bungeni, nilipata hofu kubwa sana kuona kambi ya upinzani ya chadema ikiwa ndani ya ukumbi wa bunge nikajua kuwa mafisadi wamefanikiwa kuwarubuni wamsikilize kikwete.

Kikwete alisimama, akanywa fundo la maji na kutaka kuanza kuhutubia bunge.

Ghafla, freeman mbowe, kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, akasimama na kuongoza kundi kubwa la wabunge wanaokaribia kufika 50 wa chadema kuondoka bungeni.

Hii ilimfanya kikwete abaki kapigwa na butwaa na kushindwa kuhutubia kwa dakika kadhaa. Wabunge wa ccm wakazomea na wale wa cuf na wengineo wakabaki bungeni kama tulivyotarajia.

Kwa kweli mwili ulinisisimka kutokana na kitendo cha kishujaa kilichofanywa na wabunge wa chadema kuonyesha kuwa hawakubaliani na matokeo yaliyompa urais kikwete kwa kutumia wizi mkubwa wa kura ulio bayana.

Kitendo kile kilikuwa na impact kubwa sana na kilimuaibisha kikwete mbele ya watanzania na mabalozi wa nchi za nje waliokuwepo bungeni. Na ni sahihi kabisa kwani amepata urais kwa njia za kidhalimu.

Kwa faida ya wasiojua the political significance ya wabunge wa chadema kutoka nje wakati rais anaanza kuhutubia, naomba wasome yafuatayo kutoka kwenye mtandano:

A bunge walkout is the act of mps collectively leaving parliament as an act of protest.

A walkout can also mean the act of leaving a place of work, school, a meeting, a company, or an organization, especially if meant as an expression of protest or disapproval.

A walkout can be seen as different from a strike in that a walkout can occur spontaneously, and need not necessarily involve all the workers present, whereas a strike is often voted on beforehand by the workers, giving notification both to all of the workers and to the company affected.

Walkouts have often been staged against the presence of a speaker (muongeaji in this case kikwete) or the content of an in-progress speech at a meeting.

the protest, which is often a silent, non-violent means of expressing disapproval, is often interpreted as an exercise of the freedom of association while allowing the speaker (mtoa hotuba) to exercise the freedom of speech, albeit with a reduced audience in attendance.


mkuu gwaride ndio linaandaliwa hivyo alijaanza muulize makinda na makinda zake wanavyohaha wanajuta kufanza uchaguzi
 
It is error alone which needs the support of government. Truth can stand by itself.
 
Mkandara,
Thanks. Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kui spin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomb kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.
i) Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita. Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Ni kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena. Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa.Hata hivyo,baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" . Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP. Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena. Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye) Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo:
i) Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao. Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo. Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari. ii) Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa). Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724 = Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000). Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450(iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252 hapa nako uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi) Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 ( Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445 = Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taariffa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba). Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 (iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137. Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu. Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. (Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.
Hivyo basi kutokana na Dosari hiyo kubwa mgombea yeyote anayekubali kupokea matokeo atakuwa mwendawazimu. Ndiyo maana nikakataa kutambua matokeo na kumtambua Rais aliyepatikana kwa matokeo hayo.

2:Tarehe 15 November, katika Press Conference iliyofanyika Dodoma, Dr. Slaa, alikabidhi rasmi majukumu kwa Chama kwa kuwa kazi ya Mgombea Urais imefikia mwisho wake Baada ya Rais kutangazwa kwa mujibu wa Katiba (Mbovu) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa chombo ambacho kilikasimiwa madaraka na Kamati Kuu ya Chama ( Sekretariat) mbele ya Wabunge wa Chama. Chama kilipokea majukumu na kuelekeza utekelezaji na ufuatiliaji maazimio hayo ya kukataa matokeo na kumkataa Rais kufanyika kuanzia siku hiyo na Vyombo mbalimbali na ngazi mbalimbali za Chama, na Wabunge wa Chama. Hivyo kilichotokea Bungeni ni utekelezaji wa maamuzi ya Chama hadi pale ngazi za juu za Chama zitakapobariki au kubadilisha msimamo huo. Ni dhahiri basi, i) Wabunge wetu wala Dr. Slaa, hawakuhitaji kurudia madia ya msingi ikiwa ni pamoja na kurudia uchaguzi. Madai ya Mabadiliko ya Katiba au Katiba ya Wananchi na kudai Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kujiuzulu na Kuundwa kwa Tume ya uchunguzi ni madai yaliyotolewa katika Press Conference ya Tarehe 15/11. Hata hivyo, msisitizo wa awali ni kwa kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi ambayo inaweza kutupelekea kwenye yote hayo. Mtu yeyote asiyemakini kufuatilia mtiririko huo anaweza kupotosha na kusababisha vurugu na uchochezi ambao Chadema, pamoja na jitihada zake za kudai haki zake na za wananchi waliochakachuliwa kura zao inapenda kufuata njia za kistaarabu na za amani. Ni vema yeyote anayetaka kufanya analysis ya hatua za Chadema kwanza akajielimisha vizuri badala ya kuweka hisia zake ( hakuna sababu ya kuandika na mate wakati wino upo, na wakati wowote Chadema tuko tayari kutoa ufafanuzi utakao hitajika, isipokuwa ule unaopaswa kupitia kwenye vyombo vyetu vya maamuzi kama chama cha kidemokrasia.

Looks like hili ndilo tamko rasmi la chama ambalo ndio ushahidi ama maelezo kamili ya sababu ya Dr Slaa ama Viongozi na Wabunge wa Chadema kutomtambua Rais Kikwete.........

Poleni sana kama huu ndio ushahidi mnaotegemea kuwafanya watanzania kwa wingi wao ambao unaweza kuleta mabadiliko, watanzania wasomi wa tabaka la kati ambalo ndio ngome yenu lakini pia jumuiya ya kimataifa ambayo katika masuala kama haya ndio huwa nguzo pekee ya utetezi wa UPINZANI katika hali kama hii. Lakini pia nawashauri mliondoe, mlipitie na mlipatie baraka za chama kwa maana ya vikao rasmi kabla ya kuendelea makosa haya ambayo yanahoji UMAKINI wenu....

Mkandara, ukisoma kwa umakini hili jibu/tamko ni wazi hii ni cut and pest ya mtu wa Chadema na pengine mwana Sekretariat na sio matamshi ya Dr Slaa hivyo unapojibu tambua kuwa hubishani na Dr Slaa......
 
Kikwete na kikundi chake ndani ya CCM wameamua kutumia udini kama tatizo ili kufunika mambo muhimu yenye utata katika nchi kwa sasa. Nchi ina matatizo ya kifisadi, utendaji mbovu wa serikali, maisha magumu kwa wananchi na mengine muhumu. Udini sio tatizo Tanzania, unatumika kugeuza upepo.
 
UDINI tz upo, lakini haukuwa applied kipindi cha uchaguzi, labda alikuwa anawasema cuf. lakini haikuwa issue kabisa hii, wasn't serious na haikutakiwa alitamke lile. Mr.president mimi huwa namshangaa sana.
 
ASANTE SANA mwanakijiji ila inasemekana siku zako zinahesabika , jiangalia brother

Mbona ni kama unamtishia mtu. Unaposema Siku za mweanakijiji zinahesabika una maana gani (nani kasema na ana maana gani?). Jamani tufike mahali tutumie jamvi hili kwa hekima. Tupime kile tunachoandika kabla ya kukipost.
 
Kwani Isaac Sepetu hajawahi kushika madaraka Zenj?
ndio nani huyo jamani? na angalia kwa cabinet hii ya sana na ya awamu ya karume, tutajieni tuwaone walikuwepo kina nani?hakuna sehamu yenye udini wa kuwabagua wakristo kama ilivyo zanzibar.
 
Mimi nimejitahidi sana kudadisi, kuchunguza na kusikiliza wapi udini/ukabila ulijitokeza Tz nimeshindwa....! Ingewezekana, JK angebanwa aseme ni chama gani hiyo, na wapi hapo ndani ya Tz ambapo udini, au ukabila, au vyote vimejitokeza hata kwa ishara....!
Hii inanishangaza mno kwa maana kila mgombea alikuwa na dini yake na kabila moja wakati Tz kuna makabila zaidi ya 125....! Kila chama ilikuwa na mchangantiko wa dini na makabila tofauti....! Hakuna mtu aliyetamka kumchagua mgombea yeyote kwa itikadi za dini, kabila, au eneo alilotoka....! Bali kila mmoja alikuwa akivutiwa na sera za chama na mgombea wake....! Kwa kweli mi niko :confused2::confused2::confused2:
 
JMT Raisi,Makamu WOTE ni waislam labda alimaanisha ilo
 
anatakiwa aongee, udini aliousema ulionekana wapi, nani aliendekeza udini? awe wazi tu kama kitu ni cha kweli...au la anawaamsha watz waanze kuweka kwenye fikra zao udini...na wakianza hivyo, watahoji vyeo vinavyotolewa na yeye kwa kupendelea dini moja, na ccm ilivyokuwa ya kibaguzi...point a finger Mr.president.
 
hata wbunge alioteua ni wawapi kama si.........
 
Mkandara hii issue ya CHADEMA ni tata saana. Si hivyo tu bado wanaonekana wanaimani na serikali ya Kikwete maana wanasema watapeleka matatizo yao. Hivi kama humtambui baba yako, unawezaje kudai matunzo?
Halafu hawa CHADEMA wanapatikana bungeni na huko watakuwa wanahoji utendaji wa serikali. Serikali ipi wakati hawaitambui? Strategy yao bado inapwaya saana.



Moyo wangu huwa unasikitika sana napoona watu wenye uelewa wanakuwa wajinga simply wanapo jiunganisha na ccm.

Kama ulikuwa ni mtu wa kufatilia matukio ungejua Waziri Mkuu amepigiwa kura ngapi na tofauti ya kura ungegundua ni za upande upi.

Ilijidhihirisha wazi kabisa kuwa Wabunge wa Chadema hawakumpigia kura waziri mkuu.

naomba mjue Mbunge linaendeshwa na kanunu,Raisi haendeshi Bunge.

Tujifunze bunge ni Raisi na Wabunge,kumkataa Raisi na uteuzi wake siyo kulikataa mbunge na kanuni zake mambo haya ni mawili na tofauti kabisa.

Raisi ataendesha serikali lakini bunge linawakilisha wananchi,si kila mtu ndani ya serikali anakubaliana na Raisi.

Tukumbuke.

wakati Dk slaa ameshutumu vyombo vya usalama alisisitika mkuu wa vyombo vya usalama atoe majibu ya msingi kwa taifa,juu ya shutuma alizotoa.sisi sote ni mashahidi Mkuu wa vyombo vya usalama hakutoa taarifa yoyote badala yake majibu ya shutuma hizo yalitolewa na mtu mwingine katika nafasi hiyo ambayo sote hapa tulijadili bila kufikia muafaka.
kwa mtu mwenye kufikiri lazima aligundua kuna tatizo la mawasiliano katika ngazi za juu.

Hata shutuma ya Pili ya usalama wa taifa ,pia tuliona mtu aliyejitokeza kujibu shutuma hizo wengi tulijiuliza ni nani na kwa misingi gani.

mwisho wa siku tuligundua wote walitumiwa kujibu shutuma ni watu ambao kwa namna moja au nyingine niwale wanaotumika na wenye masilahi fulanni.

sote Tulishuhudia siku Rais anaapishwa hata viongozi wote wa juu wa dini waliohudhuria sio wale tuliowazoea.

watanzania nchi yeti iko icu tusiendekeze ushabiki utakaotugharimu siku za usoni,tatizo la Kikwete ni kubwa na hakuanza kukataliwa tu baada ya matokeo hata katika mchakato mzima wa kampeni na hatimae uchaguzi,dosari zipo nyingi na wengi tulishuhudia.

Leo wapo watu wanaweza kuthubutu kusema damu haikumwagika,watu wangapi waliumizwa na kufanyiwa matendo ya kuchomewa nyumba nk.je hii ni Demokrasia au demokrasia ni maneno tu.

leo Kikwete anatoa hotuba ambayo kwa namna moja inaonyesha hakubali kabisa kama kulikuwa na dosari katika uchaguzi.anathubutu kusema amechaguliwa kwa kishindo.Kura 5,000,0000 katika taifa la watu 45,000,000.

hiki siyo kitu cha kujivunia kabisa.mambo haya yatawatesa watoto wetu na ndugu zetu nyakati zijazo.


tuache ushabiki kwani ushabiki siyokitu cha msingi jana tumewashuhudia wabunge walivyokuwa wakipiga makofi katika kila jambo,sijui kama kuna mtu anaweza kutueleza katika hotuba yote Tanzania yetu ya leo itakuwa wapi kesho.
 
KIKWETE alitafuta mlango wa kutokea baada ya kuelemewa na hoja za wapinzani waliokuwa wakimbana aeleze yako wapi maisha bora kwa kila Mtanzania. Akaamua kupoteza lengo. Hata hivyo awashukuru viongozi wa KIKRISTO waliompigia ndogo ndogo kwa kusema yeye ni CHAGUO la MUNGU. Hawezi kuwasahau kina ASKOFU KULOLA, ASKOFU GAMANYWA aliyemwalikwa Kanisani kwake na kumwahidi kushughulikia mgogoro wa ardhi kanisani, ASKOFU KILAINI n.k. Huo udini anaousema unasomeka kwenye gazeti la AL_NUR lililokuwa likihubiri NDOA YA SLAA NA KANISA. Huko ndiko kwenye propaganda za udini na KIKWETE hajawahi kukemea gazeti hilo. Inawezekana Mhariri wa gazeti hilo ndiye anayemshauri MZEE juu ya udini.
 
Huo udini anaotuletea utamtafuna yeye,familia yake na maswahiba.Siye hatutakubali kamwe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom