Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Mnajifanya hamjui Kakobe et al kumpigia kampeni Slaa makanisani eeh?
 
:whoo:Hivi Kikwete uwezo wake wa kufikiri umefika mwisho au hana anachokifikiria? kama ameshindwa kazi aondoke tu taratibu kwani sasa nchi inaendeshwa na ROSTAM AZIZI, LOWASSA NA FISADI CHENGE sasa yeye anakazi gani atoke ikulu ampishe FISADI ROSTAM AU LOWASSA WATUONGOZE PUMBAFU PUMBAFU WAKUBWA PUMBAFU ZAO
 
Udini umeletwa na huyo huyo anayeukemea so anajua anachokisema kwa mtu mkubwa kama rais kusema kitu siyo mchezo so he is the first mdini kabla ya wote.

Thinker Musa,
umeongea sahihi kabisa, Huyu jamaa bado ana wasiwasi na move za Dr Slaa na hajui DrSlaa ataongea nini, na hii yote inakuja baada ya kujua matokeo rasmi ya kura zilizopigwa
 
Kama CCM itashindwa kuona na kusikia ukweli huu ya kuwa main actors na successors wao hawataweza shindana na wale waliopo CHADEMA basi watakuwa wanamacho lakini hawaoni na masikio lakini yasiyosikia. Ukiangalia hata tafsiri ya results za uchaguzi inaonyesha kuwa behind CHADEMA kuna nguvu ya waelewa (Literate) ambao kutokana na history ya Siasa za zamani wameshindwa kujionyesha waziwazi so they play indirectly. Na in the front line CHADEMA ina vijana wasomi wenye confidance yakutosha na wenye uwezo wakujenga hoja ambayo itawafanya CCM wajikute mara zote wana resort kwenye kutumia stick measures (Kwasababu ya kuwa proveked) ambayo itasababisha public i sympathize na CHADEMA. Mwisho wa siku CCM itaji identify kama chama chenye kulazimisha mambo na hivyo kukosa public support ya kutosha hivyo kuwa weakened kiasi ambacho....well niishie hapo. Mwenye macho na atazame na mwenye sikio asikie....This is 2010. CCM angalien succession plan yenu!
 
Chadema safiiiiii

wabunge wa chadema muendelee kuwa na umoja hivyo hivo.

Yes, waonyeshe kwamba kura zetu zimeibwa.

Hatuwezi kuibiwa na kukaa kimya.

Ujumbe umefika
 
Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkuu wa nchi anaeneza propaganda zisizo na tija kwa taifa. Kutokana na wimbo huu wa udini ambao kikwete amekua akiuimba kila anapopata nafasi ya kuongea mbele ya hadhara watu wengi sasa wameanza kuamini kwamba tanzania kuna udini. Huu ni uchochezi wa hali ya juu tena unaoenezwa mkuu wa nchi. HII NI HATARI KUBWA HAKIKA RAIS ANALIPELEKA TAIFA PABAYA NAWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAMKEMEE MARA MOJA!
 
Mfa maji.........!Maji ukiyavulia.......!ZaMbi ya udini.....Rejea JK original wa Tz.
 

Swala si kwamba CHADEMA wamepiga kura ya ndiyo au hapana (kitu ambacho hatuwezi kujua kwa sababu kura ni siri)

Swala ni kwamba wamekubali kupiga kura at all. Kukubali kupiga kura tu kulikuwa ni kumtambua Kikwete. Ningepeleka mimi jina pale, kwa kuwa mimi hawanitambui kama rais, wala wasingejisumbua kupiga kura, wangenicheka tu.

Kwa kuwa wamekubali kupiga kura kuhakiki pendekezo la Kikwete, wamemkubali na kumtambua Kikwete kama rais tayari.

Kama wamebadilisha mawazo baada ya hapo watuambie.
 
Kama ilivyo kawaida yake, mambo mengi aliyoyazungumza JK katika hotuba yake ya ufunguzi wa mbunge ilikuwa ni porojo, isipokuwa hili suala la udini. Kwa kadri nilivyomuona kwenye luninga, inaelekea Jk anaamini kwa dhati ya kwamba matokeo mabaya dhidi yake katika uchaguzi mkuu uliopita yametokana na udini na wala siyo utendaji wake mbovu katika kipindi kilichopita. Hii ndiyo maana alisema ya kwamba serikali atakayohunda itaendelea kutekeleza sera zile zile ambazo ni dhahili wananchi walio wengi wanazikataa. Labda swali la kujihuliza, ni nani kampotosha JK katika suala hili? Ni wapambe wake, katika jitihada zao za kuficha ukweli ili wasije kulaumiwa ya kuwa nao wamechangia katika janga hilo? Au ni idara ya usalama wa taifa? Kwangu mimi, yeyote aliyempotosha JK kwa jambo hilo Haitakii mema nchi yetu; kwani kwa kadri anavyozidi kuzungumzia suala hilo, ndivyo anavyozidi kuchochea wananchi wengi,waanze kupima vitendo vyake kwa kutumia darubini ya udini, na hiyo ni hatari sana. Si busara kwa JK kumtafuta mchawi, amefika hapa alipo si kwa udini bali kutokana na kusaliti imani waliyokuwa nayo juu yake 2005. Wakati huo wanyonge walimwona JK kuwa ni mwenzao, baada ya kukwaa urais aliwaacha kwenye mataa na kukumbatia matajiri.
 
Sioni kama ilikuwa ni ushujaa wowote kwa sababu waliondoka ukumbi wa bunge na wakenda ukumbi mwingine kumwangalia kupitia luninga-Is a kindly shameful too!
Wewe kama wewe huwezi kuona maana umejifunika shuka yenye rangi za kijani na njano bila kuzingatia hupo kwenye jangwa ningumu kurudisha uoto wa asili ukiwa jangwani kwani ccm nikama jangwa siyo ccm tuliyozaliwa tukaikuta wakati huo ikiwa ni ya mfanyakazi na mkulima ila sasa ni ya mfanya biashara na mafisadi!!!:angry::A S 20:
 

Kaka hapa umepata hasiri ila Inaudhi president kuwa anaongozwa kwa remote:target::target:
 
kwa taalifa yako wewe hunijui na hata historia yangu huijui, tafuta kwanza nani alileta haya mambo source, iweje mtu aliyeanjisha udini nchini nimchekee hata siku moja! Ntamchukia mtu yeyote, naludia tena yeyote anayeleta udini! Unatetea mafisadi kujificha na huo mlango wa mafisadi unataka watu waanze kujadili udini we mheshimiwa wewe! Unasema mpaka bungeni eeti udini upooo wewe! Upo kwa vile dhambi ile inakufuata na itakumaliza tu! Mbona huko mitaani sisi tunaishi vizuri tuu huu udini upo wapi!?? Ndo maana nasema aliyeuanzisha ni yeye!
 

Mimi sikatai kwamba kuna haja ya protest, kuna haja ya mabadiliko. Nimesema hayo hapa mara nyingi.

Ila naona kama CHADEMA wana squander an opportunity. Dr. Slaa katuambia CHADEMA ni chama consistent, consistency yenyewe ndiyo hii ya kumtambua rais Kikwete kwa kushiriki katika kura ya kumhakiki Pinda, halafu baada ya hapo kutoka nje ya bunge kwa kusema hawamtambui Kikwete kama rais ?

CHADEMA wana a clear strategy au wana improvise as they go ? Kikwete akiteua mawaziri, mawaziri hawa wakija bungeni, wabunge wa CHADEMA watafanya kazi na hawa mawaziri? Watachangia mijadala?

Wakichangia, watachangia kwenye serikali inayoongozwa na nani? Watachangia miswada ya wizara zinazoongozwa na mawaziri walioteuliwa na nani?

Hii habari ya kutomtambua rais CHADEMA wana strategy gani long term? Wanataka ku sit out the rest of this 5 years au watarudi bungeni? Kama watarudi bungeni ni kwa misingi gani? Kama wata sit out watawaambia nini wananchi waliowatuma wawawakilishe bungeni?
 
Mimi ninacho kiona nikwamba watu wengi wanajua nini nisiasa nakila aliye na nafasi yakuongea kwenye jamii akiongelea siasa wakati yupo kanisani ccm wanasema niudini!mfano ni askofu kakobe aliongea kanisani na akatoa mistari inayoelekeza watu wakamchague kiongozi lakini ccm waliibebea bango!!wakasahau misikitini nini kilichokuwa kikisemwa kila siku kwenye miadhara hadi kwenye sala za ijumaa!!
 

Umenikumbusha issue moja ilitokea hapa Arusha jamaa aliiba akawa anakimbizwa na kundi kubwa la watu akaamua kwenda polisi mwenyewe jamaa wakamfuata, mwizi akaanza kusema mimi ni mwizi naombeni mniweke ndani, polisi wakagoma mara kundi likaingia tunamwomba huyo jamaa maana anaupungufu wa akili tunataka kumpeleka Hospitali polisi bila kufikiria akasema hata yeye anaona jamaa kama zimepungua vile, wakaondoka naye wakamkamwua. sasa hii ya mwizi mwizi......... imenikumbusha.
 
Mimi binafsi nampongeza Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hatua yake ya kukemea udini maana kweli upo.
Kama mnabisha angalieni: Kuna vyama vingine vimejaa watu wa dini moja tu na nafasi za juu zote zimeshikwa na watu wa dini hiyo hiyo tu!
Hata wakiambiwa wateue watu kwenye nafasi fulani basi watateua watu wa dini hiyo tu! Hata kama nafasi ni tatu, wote watakuwa ni wa dini hiyo tu! Kwa hili Watanzania wenzangu udini upo ila mimi ningekuwa na uwezo wa kumwuliza ningetaka kujua mtu hasa anayeendekeza huo udini ili nimjue. Ningemwomba rais wetu ambaye si mdini hata aniambie huo udini anao usema ni nani hasa ameupanda na kuupalilia!!
 

Hapo hamna dharau, kama tunataka utamaduni wa accountability, na tunataka accountability kutoka CCM, basi kanuni hiyo hiyo ya accountability inatakiwa kuwekwa kwa CHADEMA.

Hatutaki kuiondoa CCM, only kuiweka CHADEMA iendeleze ukiritimba kama wa CCM. Dr. katoa statement kuwa CHADEMA ni chama chenye consistency, ni lazima watu watake maelezo, consistency iko wapi katika kutomtambua rais?

Wabunge wa CHADEMA walipopiga kura kumhakiki Pinda walikuwa wanpigia kura pendekezo la nani? Hii habari ya kutomtambua rais imeanza lini? CHADEMA imejua lini kwamba matokeo yamevurugwa ? Kwa nini CHADEMA haikususia kupiga kura za kumhakiki Waziri Mkuu ? Je CHADEMA ni chama kinachoendeshwa kwa umoja wa kichama au kinaongozwa kwa mitazamo ya watu fulani tu? Kama kinaongozwa kwa miongozo ya kichama mbona wabunge hawakuelewa kwamba CHADEMA hakimtambui Kikwete kama rais wakaenda kupiga kura katika chaguo ambalo linatakiwa liwe la rais kutoka kwa mtu wasiyemtambua kama rais ?
 
Matokeo Halisi ya Uchaguzi ulioisha yalimstua sana JK na kampani yake, na kwa kweli aliiona nguvu ya Dr Slaa, na Bado anajua Slaa ni kipenzi cha watu wengi (kutokana na Kura zilizopigwa), Miongoni mwa hila nyingi alizotumia JK katika Kampeni zake ni Kauli ya Chadema kuwa Wa-dini (Wakristo),

Sasa uchaguzi umeisha na JK kaingia Madarakani (kwa Hila),
Kutokana na uongozi wake kutofanya kitu cha maana, na wala hawezi kufanya kitu cha maana ili wananchi wamkubali/warudishe imani kwake, JK na CCM hawana sera za kuwavutia wananchi, watu walikwisha vunjika moyo na uongozi wake, na mpaka sasa haonyeshi mwelekeo wa anapotaka kuanzia,

lakini pamoja na hayo yote, JK hana amani kabisa, bado analisikia Joto la Chadema na Dr Slaa, na kwa sababu amefirisika Sera na Hoja Kichwani, anataka Watanzania wasisahahu kuwa Chadema na Dr Slaa ni wa-Dini, anataka kuitumia hii sera ya udini kama patriotic weapon ya kujikinga na nguvu kubwa ya Chadema inayokuja, anawaunganisha CUF na CCM na pia anawatenga Waislamu wawe upande wake kwa kuwaahidi mahakama ya Kadhi na OIC (Balali wakati wa Sikukuu ya Iddi)

lakini anashindwa kujua kuwa hiyo sera Haikumsaidia kile kipindi cha kampeni, watu walipima hayo maneno na kuona pumba ni zipi na Mchele ni upi, Kuna Waislamu wengi mno waliompigia Kura Dr Slaa na wabunge wa Chadema

naomba akumbuke kuwa kuna kundi kubwa la watu lililowaweka Zitto, Sugu, Mnyika, Mdee, Wenje na wengineo wengi Madarakani, Hilo kundi halikudanganyika na hiyo sera yake ya Udini ambayo bado anaitumia na ni ukweli kuwa watu Hawatadanganyika

JK NGUVU YA UMMA INAKUJA
 
Sasa ndugu we sema chama gani hicho nyinyi ndo mnaleta udini sasa!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…