Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Zumbe,

Unaitwa Mtanzania, una haki kukaa popote utakako maana ni nyumbani kwako, kwa asili.

asante mchungaji, nilipatwa na hofu tu pale mkuu wa jamvi aliposema kwa msisitizo kuwa kuna ufa mkubwa wa kidini, halafu usemi wake ukawekewa msisitizo na msaidizi wake mtoto wa mkulima, kuanzia pale mtoto wa mkulima nimemtoa kwenye fungu la wanyonywaji.
 
Mwenye Macho Haambiwi Tazama,
ni habari gani na nini magazeti ya kidin yalikuwa yanaandika kuhusu kampeni na wagombea?
wkt wa kampeni ulisilikiza redio amani ya morogoro kila siku sa 2 ivi?
je wkt wa kampeni ulisikiliza redio safina ya arusha?
je ulimsikia yule askofu wa maisha wa tag pale mwenge anasemaje na alikuwa anawaelekeze nini waumini wake?
kabla ya hapo ulishasoma waraka wa kanisa flani ivi la kadinali mmoja wa katoliki?
na baada ya hapo ulisoma waraka (counter) wa waislamu?
Je izo message za walokole za kumchangua na kumwombea mgombea flani hamkusikia, wala kuona?

kwa ilo hakuna wa kupona, Wanasiasa na viongozi wa dini woote hakuna atakaye kwepa!!!!
udin upo tena sana hasa wkt wa kampeni, baada ya kampeni udin unapotea taratibu.
 
- Hapana katiba haiwezi kubadilishwa kienyeji namna hii, yaani wananchi 46 tu wawe na nguvu ya kutubadilishia katiba wananchi 45 Millioni kwa sababu eti wanatoka Rais akihutubia, sasa hili litakua taifa gani mkuu?

- Hili ni la ridhaa ya wananchi wangewapa wabunge majority bungeni kweli, lakini wabunge 46 tu, hapana, NEC ina matatizo sawa, serikali iyasikilize na kuyatafutia ufumbuzi on its time lakini in the meantime wawache wabunge wa Chadema waendelee kugomea, maana hapa ndio tutajua ukweli ulipo, kama CCM na Rais hawahusiki na kinacholiliwa haina sababu yoyote ya kuhangaika, unless wamehusika kweli ndio tutaona wakihangiak kuwabembeleza!

William.

Naomba kufahamu elimu yako tafadhali, rudia kuisoma tena na tena na tena comment yako, halafu ujione ulivyo mbumbumbu kupita maelezo.
1. kikwete ametangazwa amepata kura millioni 5. je ana haki ya kuongoza watu million 40?
2. waliompigia kura alizotangazwa na nec ni 27% ya waliojiandikisha kupiga kura, je huyu anamuwakilisha nani?
nipe jibu la maswali hayo mawili kwanza ili nijuwe wewe ni kiwango gani.
 
Jakaya Kikwete alipoona hakubaliki na wananchi walio wengi alizua hoja ambayo haikuwepo, na kuwataka watanzania tuamini kuwa kutokukubalika kwake hakukutokana na kuzorota kwa uongozi wake katika kipindi cha miaka mitano iliyopewa bali alikuwa akikosa kuungwa mkono kutokana na dini yake. Kwa kufanya hivyo alikuwa anatafuta sympathy ya waislam ili anufaike na kura za udini huku pia akipata kura zisizo za udini kutoka kwa watanzania wengine ambao walikuwa wakimwunga mkono pamoja na utendaji wake usioridhisha bila ya kuegemea kwenye imani za kidini.

Hivi ndivyo alivyofanya Mugabe kule Zimbabwe. Mugabe alipolaaniwa sana kwa kugandamiza demokrasia na kulaaniwa na mataifa mbalimbali aliamua kutaifisha mashamaba ya wakulima wa kizungu. Alipolaaniwa kwa kugandamiza demokrasia na haki za Wazimbabwe, yeye alikazania kusema kuwa kupingwa kwake na mataifa mengi kulitokana na utaifishaji wa ardhi ambayo aliwagawia Wazimbabwe maskini waliokuwa wakitaka ardhi kwa miaka mingi bila ya mafanikio. Akafanikiwa kuonewa huruma na baadhi ya Wazimbabwe ambao waliamini kuwa Rais wao alikuwa akishutumiwa kwaajili ya kuwatetea wananchi wake katika kupata haki ya kumiliki ardhi yao.

Hii ni hulka ya viongozi ambao huwa wanapenda sana madaraka, wao hawahitaji kupata madaraka kwa sababu watu wanapenda wawe viongozi wao bali hufanya kila linalowezekana alimradi wawepo kwenye madaraka. Viongozi wa namna hii ndiyo husababisha maafa katika nchi nyingi duniani. Viongozi wa namna hii huendesha uchaguzi kama njia ya kuidhinisha madaraka yao lakini siyo kwa nia ya kuamua nani awe kiongozi kadiri ya matakwa ya wapiga kura.
 
udini anaozungumza mheshimiwa rais ni ule alousema mstaaf mkapa pale jangwani siku yakufunga kampeni ..kwamba walimwendea makuhani wa kanisa na majoho yao ati wamchague mtu kwa sababu ni wa dini yao...udini ule wa kutoa ilani au mwongozo kwamba wana dini wachague yule ambae anatoka kundini ambae atawasikila wao wavaa majoho...udini ambapo viongozi hao wako tayri kumbeba mtu wao wa dini yao hata kama kama hana sifa za kuleta utengemano katika jamii.udini ambapo emails kutoka ndani ya nyumba za idada kwa kutumia emails address zao zinatumwa kwa waumini kumchagua mtu wa dini yao...udini ambapo sms zilitumwa kuwaomba watu wamchague mtu wa dini yao.....udini ambao ndani nyumba za ibada waumini wanalazimishwa na viongozi wao kumchagua mtu wa dini yao..udini ambapo magazeti kariu yote yanambeba mtu wa dini moja....udini ambao akichaguliwa mtu kushika nafasi ya uongozi basi wana dini wengine wanampiga vita
kwa sababu ya dini yake...si kwa sababu ya utendaji wake bali dini yake ndio tatizo...udini ambapo matamko na mandiko matakatifu hayatolewi rais wa nchi akiwa wa dini yao..hata kama migodi yote amewapa wazungu..na makaburu...na benki zote za umma zime binafsishwa kwa bei ya kutupa...hata kama wamenunua rada bovu..kwa fedha nyingi .....hata kama wamenunua ndege ya rais kwa bei kutupwa na kufilisi nchi...haka kama mawaziri wake kwa jeuri watasema tutanunua mkitaka msitake na hata kama kula majani mule .....lakini wavaa majjoho hapa watakaa kimya kwa sababu ni wa dini yao...huu ndio udini..anaozungumza kikwete......
Thanks watanzania wengi hawakuwasikiliza wakuu wao wa dini kwani wao sio mitume ni binadamu...uwezo wao wa kufikiri ni wa kibinaadamu kama wao ..hivo wametumia akili yao na kuchagua kwa maslahi ya nchi yao...lakini hiii ni hatari kama haitakemewa siku zijazo ...na kama alivosema kikwete ..'tutakuwa kama wengine tu' yukatae udini...huu....tafakari kama kila mtu kwenye uchaguzi ampgie kura mtu wa dini yake ...nchi itafika wapi....nchi kama tanzania ambayo ina dini 2 kubwa ni hatari kugawana kwa misingi ya dini...watu ni bora waweke utanzania mbele na dini iwe ni jamabo la binafsi..tuendelee kuishi pamoja kusheherea krismas pamoja ..kusheherekea eid pamoja ....familia ngapi zina watu wa dini tofauti hapa tanzania ? Nyingi tu..na wanaishi pamoja..tukubaliane ya kwamba kazi ya maskofu na masheikh ni kutukumbusha kumjua muungu na kufanya yalio mema kutuongoza katika sala ..lakini kiongozi wa dini anapokwambia mchague ama mtii mtu wa dini yako huyo hajui alifanyalo......muogopeni kama ukimwi.....just fikiria uongozi wote wa kisiasa uwe wa dini moja na nafasi zote za kiutawala ziwe za dini hiyo...
na kila sehemu iwe hivo hivo..fikiria kwa nchi kama tanzania itakuwaje....
utanzania kwanza na dini baadae kinyume cha hapo hatuna nchi tutakua kama wengine tu
 
Tatizo nu kuwa wengi wetu tuna macho lakini hayaoni au yanaona vile yanayotaka kuona tu na vingine huwa blind. Masikio, hali kadhalika, yanasikia tunavyotaka kusikia tu na mengine, yanakuwa yana nta.
Mfano 1: Dokta Slaa, elimu yake 90 kwa mia ni ya kidini na mpaka ana udaktari wa sheria za kanoni, what do we expect from him? Jibu: udini tu.

Mfano 2: Dokta Slaa, ana kesi ya kupora mke wa mtu, ingawa amri kumi kazisoma, what do we expect? Jibu: ukosefu wa maadili.

Panga panguwa, kama hayo hamuyaoni au hamuyasikii itakuwa ndio katika kundi lileee, la wenye macho lakini hawaoni na wenye masikio lakini hayasikii.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
:angry: Ni jambo la kushangasa sana wa swahili wana sema tembea uone duniani kweli kuna maajabu huyu Mheshimiwa kang,ang,a nia Udini wakati Tunaishi maisha ya umasikini wa kupindukia Udini utakupeleka wapi? Udini kwa lipi hasa kwani ndiyo maendeleo ? sisi huku Uraiani tunaishi na Wakristo, Waislam na wapagani vizuri sana,Tukiendekeza mambo ya Udini utatugawa wananchi na Kura ulizo pata mwaka huu ni za Waislam,wakristo na wapagani bora hata wenzetu ulishawahidi mahakama ya Kadhi na nafasi nyingi za uongozi serkalini wao wanapewa kipaumbele.chonde chode Mhe umepita tukwamue nchi yetu imegubikwa na wimbi la umasikini wa kutisha, na kushuka kwa dhamani ya Fedha ,Vita vya kidini ni Vibaya sana.
 
Puuh-lease we kaka/dada malariasugu hivi hujish2kii tu kuwa the tanzanians of ''dr.Slaa era'' dont buy cheap propagandas anymore, the most recent example being ''nyufa za udini'', mastered and engineered by the unjust shameless president and he addresses that whenever he get a chance! But what's even more suprising is NOT EVEN A SEVENer buys that!?
 
nimesoma maswali magumu ya Ngurumo kwenye tz la leo.
eti ngurumo hajui maana ya udini anauzungumzia jk

ni baada ya maaskofu kuwa wakali katika kipindi hichi cha jk, wakati wakiwa kimya wakati wa utawala wa aawamu ya 3.
ni maaskofu walikuwa wakali sana ktk wakati wa mzee mwinyi na kuwa kimya wakati wa awamu ya 1.
sasa hapa anaona jk pana udini, siasa zimejaa udini.
lkn mfanoi mwengine wa gazeti la tz daima ambapo baada ya kuchaguliwa wabunge watatu viti maalum ambapo ni mama zakia, nahodha na mwengine kutoka Pemba. gazeti hilo liliandika udini eti kwa kuwa wamechaguliwa waislam watupu. huu ndio udini anaouzungumzia jk

Kwahiyo Sultan anaona wakristo wanamuonea yeye na waislamu
 
Pengine hamkumbuki history ya tanganyika, mahakama ya kadhi ilikuwepo kabla ya uhuru na miaka ya mwanzoni mwa uhuru. sio kitu kigeni, kama wakoloni waliruhusu na hawakuwa waislam, je sisi watz wenyewe. Fuatilieni Mahakama ya kadhi ni nini na inafanya kazi zipi. Baada ya hapo toa hoja. Tusiingize Ushabiki wa Simba na Yanga. Tujadili Mafisadi awe Muislam, Mkristo au Kama kingunge.

Kimtokacho mtu ndicho kinacho ujaza moyo wake. Hivyo mdini ni yeye wengine wana muiga. mkoloni alikuwa anatumia divide and rule mahakama ya kazi ikiwa moja ya vitu vilivyo tumika. Sasa mnataka muianzishe mlimuwekutugawa na mtutawale kwa urahi,si au?
 
Tanzania Fact sheet: Christians 30% Muslims 35% Others 35% Source: CIA Website. Choko choko za udini mara nyingi huanzishwa na kundi la pili hapo juu. Nawashauri wasifanye hivyo kwa sababu mwishowe hawatakuja kutawala Tanzania TENA kwa sababu kundi la tatu ni rahisi zaidi kujiunga na la kwanza katika uongozi kuliko kwenda la tatu ambalo mara nyingi huogopwa na wengi. NI USHAURI TU, NAWAKILISHA.

Masahihisho Wakristo 35% Waislamu 30% Na Wengine 35%
 
Tatizo nu kuwa wengi wetu tuna macho lakini hayaoni au yanaona vile yanayotaka kuona tu na vingine huwa blind. Masikio, hali kadhalika, yanasikia tunavyotaka kusikia tu na mengine, yanakuwa yana nta.
Mfano 1: Dokta Slaa, elimu yake 90 kwa mia ni ya kidini na mpaka ana udaktari wa sheria za kanoni, what do we expect from him? Jibu: udini tu.

Mfano 2: Dokta Slaa, ana kesi ya kupora mke wa mtu, ingawa amri kumi kazisoma, what do we expect? Jibu: ukosefu wa maadili.

Panga panguwa, kama hayo hamuyaoni au hamuyasikii itakuwa ndio katika kundi lileee, la wenye macho lakini hawaoni na wenye masikio lakini hayasikii.

Mungu Ibariki Tanzania.

Watu wenye fikra ndogo huzungumza watu. Kaa na wenye fikra pevu uzungumze mawazo yakinifu. ataja fananishwa na wanaofiri kwa kutmia matumbo badala ya ubongo kichwani
 
Pengine hamkumbuki history ya tanganyika, mahakama ya kadhi ilikuwepo kabla ya uhuru na miaka ya mwanzoni mwa uhuru. sio kitu kigeni, kama wakoloni waliruhusu na hawakuwa waislam, je sisi watz wenyewe. Fuatilieni Mahakama ya kadhi ni nini na inafanya kazi zipi. Baada ya hapo toa hoja. Tusiingize Ushabiki wa Simba na Yanga. Tujadili Mafisadi awe Muislam, Mkristo au Kama kingunge.

Kwa wakokoni kazi yake ilikuwa wagawe uwatawale. kwa sasa kazi yake itakuwa karibuni waarabu (uislamu) na marufuku wazungu (makafiri)
 
udini anaozungumza mheshimiwa rais ni ule alousema mstaaf mkapa pale jangwani siku yakufunga kampeni ..kwamba walimwendea makuhani wa kanisa na majoho yao ati wamchague mtu kwa sababu ni wa dini yao...udini ule wa kutoa ilani au mwongozo kwamba wana dini wachague yule ambae anatoka kundini ambae atawasikila wao wavaa majoho...udini ambapo viongozi hao wako tayri kumbeba mtu wao wa dini yao hata kama kama hana sifa za kuleta utengemano katika jamii.udini ambapo emails kutoka ndani ya nyumba za idada kwa kutumia emails address zao zinatumwa kwa waumini kumchagua mtu wa dini yao...udini ambapo sms zilitumwa kuwaomba watu wamchague mtu wa dini yao.....udini ambao ndani nyumba za ibada waumini wanalazimishwa na viongozi wao kumchagua mtu wa dini yao..udini ambapo magazeti kariu yote yanambeba mtu wa dini moja....udini ambao akichaguliwa mtu kushika nafasi ya uongozi basi wana dini wengine wanampiga vita
kwa sababu ya dini yake...si kwa sababu ya utendaji wake bali dini yake ndio tatizo...udini ambapo matamko na mandiko matakatifu hayatolewi rais wa nchi akiwa wa dini yao..hata kama migodi yote amewapa wazungu..na makaburu...na benki zote za umma zime binafsishwa kwa bei ya kutupa...hata kama wamenunua rada bovu..kwa fedha nyingi .....hata kama wamenunua ndege ya rais kwa bei kutupwa na kufilisi nchi...haka kama mawaziri wake kwa jeuri watasema tutanunua mkitaka msitake na hata kama kula majani mule .....lakini wavaa majjoho hapa watakaa kimya kwa sababu ni wa dini yao...huu ndio udini..anaozungumza kikwete......
Thanks watanzania wengi hawakuwasikiliza wakuu wao wa dini kwani wao sio mitume ni binadamu...uwezo wao wa kufikiri ni wa kibinaadamu kama wao ..hivo wametumia akili yao na kuchagua kwa maslahi ya nchi yao...lakini hiii ni hatari kama haitakemewa siku zijazo ...na kama alivosema kikwete ..'tutakuwa kama wengine tu' yukatae udini...huu....tafakari kama kila mtu kwenye uchaguzi ampgie kura mtu wa dini yake ...nchi itafika wapi....nchi kama tanzania ambayo ina dini 2 kubwa ni hatari kugawana kwa misingi ya dini...watu ni bora waweke utanzania mbele na dini iwe ni jamabo la binafsi..tuendelee kuishi pamoja kusheherea krismas pamoja ..kusheherekea eid pamoja ....familia ngapi zina watu wa dini tofauti hapa tanzania ? Nyingi tu..na wanaishi pamoja..tukubaliane ya kwamba kazi ya maskofu na masheikh ni kutukumbusha kumjua muungu na kufanya yalio mema kutuongoza katika sala ..lakini kiongozi wa dini anapokwambia mchague ama mtii mtu wa dini yako huyo hajui alifanyalo......muogopeni kama ukimwi.....just fikiria uongozi wote wa kisiasa uwe wa dini moja na nafasi zote za kiutawala ziwe za dini hiyo... na kila sehemu iwe hivo hivo..fikiria kwa nchi kama tanzania itakuwaje....
utanzania kwanza na dini baadae kinyume cha hapo hatuna nchi tutakua kama wengine tu

Umesema mengi lakini umeshindwa kueleza kiini. ona zaidi ya urefu wa pua yako na fikiri zaidi ya ulicholishwa. Ilani ya ccm na mahakama ya kadhi umesahau? Hicho ndicho chanzo kikubwa na 2010-2015 tutaona maajabu makubwa mno. muda ni hakimu wa haki. tusuburi
 
Watu wenye fikra ndogo huzungumza watu. Kaa na wenye fikra pevu uzungumze mawazo yakinifu. ataja fananishwa na wanaofiri kwa kutmia matumbo badala ya ubongo kichwani

Ama kweli, mwenye macho haambiwi tazama, jee umeiona mada inazungumzia nini? Mtu, tena kwa jina, sasa wewe ndio unaleta utumbo kweli kweli, au JMK sio mtu? Anatisha eeh?
 
Again , JK kaipanda mwenyewe mbegu ya UDini, chochote atakachofanya hata kikiwa cha busara watu watasema udini, hakupaswa kuongelea udini siku ile.
 
Tanzania haina UDINI ila inawezekana baadhi wa viongozi ndio wanaoleta UDINI, na inawezekana wanaoimba kuwa wa Tanzania tusiingie kwenye udini ndio hao wanataka udini uanze kwa manufaa yao binafsi,

Watanzania tufunguke macho na tuamue nini tunataka, kwa miaka kadhaa tumekuwa na amani na uhuru wa kweli, je inakuwaje leo 2010 udini uanze.
 
Huo udini unatoka sehemu gani.? Tunamuomba aliyeutaja atufafanulie jamani maana tunapatwa na hofu kubwa mno. Mtu mkubwa kama Rais anaweza kuongea kitu ambacho kina kusudi fulani jamani? Je na hilo kusudi ni lipi basi, na linalenga nini hasa. Naomba wadau mjaribu kunitafakuria maana mimi nashikwa na hofu kubwa nikiambiwa kuna mgawanyiko wa kidini na hali sijaona wala kusikia tangu kampeni mpaka matokeo yanatangazwa.
 
tatizo la chadema wana wivu wa kike!

ndugu yangu unajua ukisema wivu wakike unakosea. Kwani wanachofanya Chadema nimadai ya msingi Kwa manufaa ya Taifa. Uwezi kutangazwa umeshinda Kwa kulazimisha ukategemea kukubalika ktk kila eneo. CCM walichofanya sio demokrasia Bali ni mabavu na tamaa ya madaraka. Ambayo mwisho wake uzaa udikteta. Hakuna sababu ya kusimamisha vyama vya upinzani ukiwa upendi mabadiliko. Ni heli tujue tunaongozwa na utawala wakidikteta kuliko kudanganywa. Alafu kula ni sehemu yakipimo kinachokuonyesha unafaha au la. Unakubalika au la. Pia watu wanabadilika. Mfano Jiji la mwanza mjini kuanzia madiwani hadi uraisi ni chadema. Ni Picha kamili yakuonyesha wananchi wamebadilika na hawataki kuburuzwa na uongozi wakibinafsi na ufisadi. Hilo ni Oigo Kwa CCM. Meya Wa Jiji lazima atoke chadema yani pigo hili nisawa na jaribio la osama kupiga Pentagoni. Unazani Kwa mtu anayetazama mbali anaona jinsi gani Mabadiliko yatatokea nchi hii. Huwezi zuia mabadiliko. Ila unaweza kuyachelewesha. Hata ivyo kubaki Kwa CCM madarakani haimanishi kuwa watakao teseka ni wanachama Wa vyama vya upinzani! Bali hata wote. Na mafanikio ya utawala mwengine haina maana kuwa watafaidika wao tu. Bali wote.
Tumechoshwa na ahadi za uongo!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom