Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Mkuu Kinja nadhani Watanzania wengi wangekuwa na mawazo mazuri kama yako tungeweza kuibadilisha nchi ikawa nzuri sana. Nakubaliana na wewe mia kwa mia kwamba haitajalisha hata angechagua dini moja wote. Muhimu ni wafanye kazi sawa sawa na watoe majibu na ufumbuzi wa kisayansi wa matatizo waliyo nayo wananchi na Taifa kwa ujumla. Mawazo ya wengi wetu tunaabudu sana wanasiasa "U-anasiasa". Hili linajitokeza wazi sana pale unapokuta hata wataalmu wanaacha kufanya kazi zao za kitaalam kwenda kuwa wanasiasa. Na wengi wao wanaharakisha sana kujiunga na CCM. Hii inaonyesha wazi kuwa kuna kitu rahisi kule! Kuna biashara huko! Na ndiyo maana kunaishia kuwa kuchafu maana hakuna anayekumbuka kufanya usafi.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Kwa wakokoni kazi yake ilikuwa wagawe uwatawale. kwa sasa kazi yake itakuwa karibuni waarabu (uislamu) na marufuku wazungu (makafiri)

mimi nafikiri lipo tatizo. Kuendelea kwenu kuzungumzia habari ya udini ni Picha tosha kwamba hata nyinyi mnaojadili mmekumba au kuathirika na tatizo la udini na mwisho mtatukanana. Ushauri wangu acheni ushabiki kwani Mungu hasaidiwi na mwanadamu. Alafu kiongozi Mwenye kufokea udini hasiruhusu kujadiliwa hoja zakuruhusu mahaka ya kadhi wala ya wakristo. Serikali ipo na utawala wake na wananchi watii na kushika sheria. Pia mambo Yao ya kiimani yabaki ndani ya taasisi za dini. Acheni kuruhusu cheche za vita ya udini wakati fire yakuzima moto Wa udini hatuna. Watu watateketea hasa wasio na maisha mazuri. Wenye vyeo katika serikali na dini watasepa ulaya. Chamsingi kiongozi hakitaka kuleta ubaguzi tumtimue yeye kwanamna yoyote kabla ya balaa. Mambo hayo ndio yalitokea Burundi. Tusiburuzwe na wabinafsi
 
Kweli katika suala la udini aliloleta JK siku ya hotuba yake bungeni hata mimi nimebaki kwenye mataa!!!!!!!!!! Kwenye face value ya mada hii, JK, serikali yake na sisiemu yake ndiyo wadini kutokana na ushahidi huu hapa:-
1) JK binfsi ni dini A
2) Serikali yake: rais dini A; makamu wa rais dini A-assignment ya kwanza ya makamu ni mahakama ya kadhi!!!!!!!!
3) sisiemu ya JK: mwenyekiti-JK- dini A; Katibu mkuu maropes dini A
4) ZBR: sisiemu/rais Dr, dini A; 1st makamu (sawa sawa!!) dini A; 2nd makamu (seif....) dini A

Kwa watanzania wa kawaida huu ngiyo udini!!!!!!!!!!!!! Labda suala la msingi ni kwa jinsi gani set up hii inatishia rule ya JK????????????? mbona hatujasikia mtanzania anayequestion set up hii??????? By logical reasoning, katika suala hili JK ana agenda ya siri ambayo anajenga namna ya kuwaingiza innocent citizens kwenye ugomvi kinyume cha dhamiri yao pamoja na mimi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
even though wengi mnamchukia... lakini kuna kweli ndani ya maneno yake try to read btw his lines ...

Watu wamechukia hadi wamekuwa viziwi na vipofu. JK is right.
 
Tatizo JK (sisim) ndio waasisi (imepanda mzizi) wa udini Tz toka 2005 CUF walipoambiwa ni chama cha waisilam, 2010 kipao kikaamishiwa
Chadema..
JK tutamkumbuka kwa kupandikiza UDINI Tanzania....

KAMWE DAMU YA WAtZ HAITAMSAMEHE....
 
l
uchaguzi wa mwaka 2010 umepita salama na tushukuru hakuna machafuko ya umwagaji
damu kama ilivyokuwa inahisiwa na wengi hili ni jambo la kushukuriwa sana kwa kila mwenye mapenzi na nchi hii.Lakini wana JF tuwe wakweli na wawazi juu ya namna ya kampeni za mwaka huu 2010 zilivyoendeshwa.Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia viongozi wa dini walivyokuwa mstari wa mbele kuelekeza viongozi wa kuchaguliwa.Sio kwa sifa za uongozi bali tuchague mtu wa dini yetu.Ndugu zangu tumewashuhudia baadhi kwenye runinga,Radio,Magazeti na katika majumba ya ibada wakihimiza kura kwa misingi ya udini.Ni kweli viongozi wa dini wana haki tena ya kimsingi kuwafundisha waumini wao elimu ya uraia.Lakini safari hii wameenda mbali zaidi,kiasi cha kuwaelekeza nani apigiwe kura ya ndio.
Wapo waliotetea sera na ilani za vyama tena hadharani kabisa,wengine walifikia kutaka kufanya maandamo ya kutoa tamko la nani au chama gani kipigiwe kura na waumini wao.Ndugu zangu wote sisi ni mashahidi wa matukio haya.Kama hukuyaona basi utakuwa umeyasikia.Tusiwe vipofu juu ya ukweli.Tukemee hali hii isije ikashika kasi.Tukemee pepo hili la udini kwa kila mtu kwa nafasi yake.Hata baba wa taifa mwl nyerere ktk kipindi chake cha uhai alilikemea sana pepo hili la udini.
Tuamke watz tupingane kwa hoja za sera,ilani za vyama na si dini.
Nawasilisha
 
Mkuu naomba usizungushe maneno, kuwa specific , unajua masuala ya udini siyo ishu ya uzushi, Hapa kwa kuwa ni sehemu ya kukemea unatakiwa useme kuwa Kiongozi fulani wa dini fulani , Taja na tarehe na mahali alisema mambo fulani yanayoashiria udini, hapo tunaweza kuwa kitu kimoja vinginevyo usilete Habari za kizushi.
 
please check what is theology..... "draw on the resources of a tradition to address some present situation or need"
source wikpedia
 
jamani please for the sake of my heart's condition, naomba msizungumzie haya mambo ya udini jamani.
 
udini, udini, udini...
Wewe huoni jinsi Njaadema waliojaa humu wanavyotaka kumuondoa Zitoo Kabwe. Kwa sababu wanaona kuwepo kwa Zito Kabwe as a senior figure in the party, they won't be able to openly perpetuate their "galatia" agenda.
You may fantasize that you can oust him just like that, as if you made him the politician he is today, while it is well known that the boy has screwed his way to the top of the game and has earned his place.
Zitto Kabwe... love him or loathe him, that boy is a maverick and he is njaadema to stay.

May Allah subhaana wa ta'ala protect you brother Zitto
 
Wewe ndio unaleta Udini!! kwani Zitto Mwenyewe ndio Muislamu ndani ya Chadema?????
 
Wewe ndio unaleta Udini!! kwani Zitto Mwenyewe ndio Muislamu ndani ya Chadema?????

Lugha gani umeandika hapo? mbona swali lako halieleweki? "kwani Zitto Mwenyewe ndio Muislamu ndani ya Chadema" maana yake nini?
 
l
uchaguzi wa mwaka 2010 umepita salama na tushukuru hakuna machafuko ya umwagaji
damu kama ilivyokuwa inahisiwa na wengi hili ni jambo la kushukuriwa sana kwa kila mwenye mapenzi na nchi hii.Lakini wana JF tuwe wakweli na wawazi juu ya namna ya kampeni za mwaka huu 2010 zilivyoendeshwa.Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia viongozi wa dini walivyokuwa mstari wa mbele kuelekeza viongozi wa kuchaguliwa.Sio kwa sifa za uongozi bali tuchague mtu wa dini yetu.Ndugu zangu tumewashuhudia baadhi kwenye runinga,Radio,Magazeti na katika majumba ya ibada wakihimiza kura kwa misingi ya udini.Ni kweli viongozi wa dini wana haki tena ya kimsingi kuwafundisha waumini wao elimu ya uraia.Lakini safari hii wameenda mbali zaidi,kiasi cha kuwaelekeza nani apigiwe kura ya ndio.
Wapo waliotetea sera na ilani za vyama tena hadharani kabisa,wengine walifikia kutaka kufanya maandamo ya kutoa tamko la nani au chama gani kipigiwe kura na waumini wao.Ndugu zangu wote sisi ni mashahidi wa matukio haya.Kama hukuyaona basi utakuwa umeyasikia.Tusiwe vipofu juu ya ukweli.Tukemee hali hii isije ikashika kasi.Tukemee pepo hili la udini kwa kila mtu kwa nafasi yake.Hata baba wa taifa mwl nyerere ktk kipindi chake cha uhai alilikemea sana pepo hili la udini.
Tuamke watz tupingane kwa hoja za sera,ilani za vyama na si dini.
Nawasilisha
Mwambie JK asitupelkee kubaya kwani udini ameufanya muda mrefu angalia alio wateua asilimia 90 ni wa dini gani?
 
Au ndiyo wale wale wagala wasiojua kiswahili wala kiingereza? isipokuwa kupenda kujifanya kujua mambo tuu?
 
Wakuu,
Wengi wetu tunajiuliza kwa nini suala la UDINI lishike kasi wakati huu wa uongozi wa jk? Binafsi ninaungana na mwandishi wa habari wa Tanzania Daima Bw. Ansbert Ngurumo kwamba hayo ni madhara ya kuendekeza udini kama kete ya kisiasa wakati wa kampeni. Mwl. Nyerere aliwahi kusema kuwa mwanasiasa akiishiwa sera ataanza kujihalalisha kwa ukabila, udini, n.k. ccm walipoona chadema inachanja mbuga walikimbilia hoja ya udini kwa lengo la kuwatisha wapiga kura. J

Ikumbukwe kuwa Mch. Mtikila pamoja na kuwa na kauli zinazorejea mara kwa mara vifungu vya Biblia, hajawahi kutuhumiwa kuwa ni mdini hata mara moja. Hiyo inatokea kwa sababu chama chake hakina tishio lolote kwa ccm.

Nionavyo mimi, hisia za udini zimeletwa na timu iliyoratibu kampeni za jk kama kete yao ya ushindi baada ya kuelemewa na nguvu ya chadema.
 
Wakuu,
Wengi wetu tunajiuliza kwa nini suala la UDINI lishike kasi wakati huu wa uongozi wa jk? Binafsi ninaungana na mwandishi wa habari wa Tanzania Daima Bw. Ansbert Ngurumo kwamba hayo ni madhara ya kuendekeza udini kama kete ya kisiasa wakati wa kampeni. Mwl. Nyerere aliwahi kusema kuwa mwanasiasa akiishiwa sera ataanza kujihalalisha kwa ukabila, udini, n.k. ccm walipoona chadema inachanja mbuga walikimbilia hoja ya udini kwa lengo la kuwatisha wapiga kura. Jambo la kushangaza ni kwamba Mch. Mtikila pamoja na kuwa na kauli zinazorejea mara kwa mara vifungu vya Biblia, sijawahi sikia akituhumiwa kuwa ni mdini hata mara moja.

Nionavyo mimi, hisia za udini zimeletwa na timu iliyoratibu kampeni za jk kama kete yao ya ushindi baada ya kuelemewa na nguvu ya chadema.

Sure!...Hii inafanyiwa amplification ili kuhalalisha agenda zao (ccm)walizokuwa wamezisimamia wakati wa kampeni!...Sisi raia wa kawaida ndio tungekuwa tunalalamikia udini huku mitaani in case ungekuwepo, lakini ajabu viongozi peke yao ndio wamekazana sana kuongelea huo udini, najiuliza wanauona au kukumbana nao wapi!...Pia bahati mbaya hawajaweza kucite mfano wowote wa udini wanaoutolea mishipa ya shingo!...i smell a rotten fishy-fish here!
 
Hakuna udini Tanzania ila mawazo ya udini yanaingizwa vichwani mwa wananchi.
Mawazo hayo yakifanyiwa kazi yakawa vitendo, hali itakuwa mbaya sana.
Ni muhimu sana mjadala huo ufungwe!
 
Jana nilikuwa naangalia Mlamani TV. Kuna kipindi kimoja cha mjadala (sifahamu jina), kulikuwa na mjadala wa hotuba ya rais. Nilipendezwa na maelezo ya kijana mmoja mwandishi wa habari; alisema wakati wa kampeni wanasiasa wanavitumia vyombo vya habari kuchonganisha wagombea kwa udini na mengine. Wanasiasa hao hao wakishachaguliwa wanaviomba vyombo vya habari 'vitibu majeraha' ya uchaguzi na mianya ya udini. sasa yule mwandishi akauliza, kwa nini hao wanasiasa wasingejiepusha na udini wakati wa kampeni kuliko kuutumia na baadae kuomba msaada wa kuumaliza? Kwa kiasi fulani alikuwa anaongelea hoja ya JK kwamba uchaguzi huu umeacha mpasuko wa kidini, lakini watu wengi wanashangaa kwa nini rais alisema vile, maybe alitumia udini kwenye kampeni. Tuwe makini na wanasiasa wanaotumia udini jamani!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom