Mkuu Kinja nadhani Watanzania wengi wangekuwa na mawazo mazuri kama yako tungeweza kuibadilisha nchi ikawa nzuri sana. Nakubaliana na wewe mia kwa mia kwamba haitajalisha hata angechagua dini moja wote. Muhimu ni wafanye kazi sawa sawa na watoe majibu na ufumbuzi wa kisayansi wa matatizo waliyo nayo wananchi na Taifa kwa ujumla. Mawazo ya wengi wetu tunaabudu sana wanasiasa "U-anasiasa". Hili linajitokeza wazi sana pale unapokuta hata wataalmu wanaacha kufanya kazi zao za kitaalam kwenda kuwa wanasiasa. Na wengi wao wanaharakisha sana kujiunga na CCM. Hii inaonyesha wazi kuwa kuna kitu rahisi kule! Kuna biashara huko! Na ndiyo maana kunaishia kuwa kuchafu maana hakuna anayekumbuka kufanya usafi.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Tanzania.