Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zumbe,
Unaitwa Mtanzania, una haki kukaa popote utakako maana ni nyumbani kwako, kwa asili.
- Hapana katiba haiwezi kubadilishwa kienyeji namna hii, yaani wananchi 46 tu wawe na nguvu ya kutubadilishia katiba wananchi 45 Millioni kwa sababu eti wanatoka Rais akihutubia, sasa hili litakua taifa gani mkuu?
- Hili ni la ridhaa ya wananchi wangewapa wabunge majority bungeni kweli, lakini wabunge 46 tu, hapana, NEC ina matatizo sawa, serikali iyasikilize na kuyatafutia ufumbuzi on its time lakini in the meantime wawache wabunge wa Chadema waendelee kugomea, maana hapa ndio tutajua ukweli ulipo, kama CCM na Rais hawahusiki na kinacholiliwa haina sababu yoyote ya kuhangaika, unless wamehusika kweli ndio tutaona wakihangiak kuwabembeleza!
William.
nimesoma maswali magumu ya Ngurumo kwenye tz la leo.
eti ngurumo hajui maana ya udini anauzungumzia jk
ni baada ya maaskofu kuwa wakali katika kipindi hichi cha jk, wakati wakiwa kimya wakati wa utawala wa aawamu ya 3.
ni maaskofu walikuwa wakali sana ktk wakati wa mzee mwinyi na kuwa kimya wakati wa awamu ya 1.
sasa hapa anaona jk pana udini, siasa zimejaa udini.
lkn mfanoi mwengine wa gazeti la tz daima ambapo baada ya kuchaguliwa wabunge watatu viti maalum ambapo ni mama zakia, nahodha na mwengine kutoka Pemba. gazeti hilo liliandika udini eti kwa kuwa wamechaguliwa waislam watupu. huu ndio udini anaouzungumzia jk
Pengine hamkumbuki history ya tanganyika, mahakama ya kadhi ilikuwepo kabla ya uhuru na miaka ya mwanzoni mwa uhuru. sio kitu kigeni, kama wakoloni waliruhusu na hawakuwa waislam, je sisi watz wenyewe. Fuatilieni Mahakama ya kadhi ni nini na inafanya kazi zipi. Baada ya hapo toa hoja. Tusiingize Ushabiki wa Simba na Yanga. Tujadili Mafisadi awe Muislam, Mkristo au Kama kingunge.
Tanzania Fact sheet: Christians 30% Muslims 35% Others 35% Source: CIA Website. Choko choko za udini mara nyingi huanzishwa na kundi la pili hapo juu. Nawashauri wasifanye hivyo kwa sababu mwishowe hawatakuja kutawala Tanzania TENA kwa sababu kundi la tatu ni rahisi zaidi kujiunga na la kwanza katika uongozi kuliko kwenda la tatu ambalo mara nyingi huogopwa na wengi. NI USHAURI TU, NAWAKILISHA.
Tatizo nu kuwa wengi wetu tuna macho lakini hayaoni au yanaona vile yanayotaka kuona tu na vingine huwa blind. Masikio, hali kadhalika, yanasikia tunavyotaka kusikia tu na mengine, yanakuwa yana nta.
Mfano 1: Dokta Slaa, elimu yake 90 kwa mia ni ya kidini na mpaka ana udaktari wa sheria za kanoni, what do we expect from him? Jibu: udini tu.
Mfano 2: Dokta Slaa, ana kesi ya kupora mke wa mtu, ingawa amri kumi kazisoma, what do we expect? Jibu: ukosefu wa maadili.
Panga panguwa, kama hayo hamuyaoni au hamuyasikii itakuwa ndio katika kundi lileee, la wenye macho lakini hawaoni na wenye masikio lakini hayasikii.
Mungu Ibariki Tanzania.
Pengine hamkumbuki history ya tanganyika, mahakama ya kadhi ilikuwepo kabla ya uhuru na miaka ya mwanzoni mwa uhuru. sio kitu kigeni, kama wakoloni waliruhusu na hawakuwa waislam, je sisi watz wenyewe. Fuatilieni Mahakama ya kadhi ni nini na inafanya kazi zipi. Baada ya hapo toa hoja. Tusiingize Ushabiki wa Simba na Yanga. Tujadili Mafisadi awe Muislam, Mkristo au Kama kingunge.
udini anaozungumza mheshimiwa rais ni ule alousema mstaaf mkapa pale jangwani siku yakufunga kampeni ..kwamba walimwendea makuhani wa kanisa na majoho yao ati wamchague mtu kwa sababu ni wa dini yao...udini ule wa kutoa ilani au mwongozo kwamba wana dini wachague yule ambae anatoka kundini ambae atawasikila wao wavaa majoho...udini ambapo viongozi hao wako tayri kumbeba mtu wao wa dini yao hata kama kama hana sifa za kuleta utengemano katika jamii.udini ambapo emails kutoka ndani ya nyumba za idada kwa kutumia emails address zao zinatumwa kwa waumini kumchagua mtu wa dini yao...udini ambapo sms zilitumwa kuwaomba watu wamchague mtu wa dini yao.....udini ambao ndani nyumba za ibada waumini wanalazimishwa na viongozi wao kumchagua mtu wa dini yao..udini ambapo magazeti kariu yote yanambeba mtu wa dini moja....udini ambao akichaguliwa mtu kushika nafasi ya uongozi basi wana dini wengine wanampiga vita
kwa sababu ya dini yake...si kwa sababu ya utendaji wake bali dini yake ndio tatizo...udini ambapo matamko na mandiko matakatifu hayatolewi rais wa nchi akiwa wa dini yao..hata kama migodi yote amewapa wazungu..na makaburu...na benki zote za umma zime binafsishwa kwa bei ya kutupa...hata kama wamenunua rada bovu..kwa fedha nyingi .....hata kama wamenunua ndege ya rais kwa bei kutupwa na kufilisi nchi...haka kama mawaziri wake kwa jeuri watasema tutanunua mkitaka msitake na hata kama kula majani mule .....lakini wavaa majjoho hapa watakaa kimya kwa sababu ni wa dini yao...huu ndio udini..anaozungumza kikwete......
Thanks watanzania wengi hawakuwasikiliza wakuu wao wa dini kwani wao sio mitume ni binadamu...uwezo wao wa kufikiri ni wa kibinaadamu kama wao ..hivo wametumia akili yao na kuchagua kwa maslahi ya nchi yao...lakini hiii ni hatari kama haitakemewa siku zijazo ...na kama alivosema kikwete ..'tutakuwa kama wengine tu' yukatae udini...huu....tafakari kama kila mtu kwenye uchaguzi ampgie kura mtu wa dini yake ...nchi itafika wapi....nchi kama tanzania ambayo ina dini 2 kubwa ni hatari kugawana kwa misingi ya dini...watu ni bora waweke utanzania mbele na dini iwe ni jamabo la binafsi..tuendelee kuishi pamoja kusheherea krismas pamoja ..kusheherekea eid pamoja ....familia ngapi zina watu wa dini tofauti hapa tanzania ? Nyingi tu..na wanaishi pamoja..tukubaliane ya kwamba kazi ya maskofu na masheikh ni kutukumbusha kumjua muungu na kufanya yalio mema kutuongoza katika sala ..lakini kiongozi wa dini anapokwambia mchague ama mtii mtu wa dini yako huyo hajui alifanyalo......muogopeni kama ukimwi.....just fikiria uongozi wote wa kisiasa uwe wa dini moja na nafasi zote za kiutawala ziwe za dini hiyo... na kila sehemu iwe hivo hivo..fikiria kwa nchi kama tanzania itakuwaje....
utanzania kwanza na dini baadae kinyume cha hapo hatuna nchi tutakua kama wengine tu
Watu wenye fikra ndogo huzungumza watu. Kaa na wenye fikra pevu uzungumze mawazo yakinifu. ataja fananishwa na wanaofiri kwa kutmia matumbo badala ya ubongo kichwani
tatizo la chadema wana wivu wa kike!