UDINI UKO WAPI!!?? KADINALI PENGO
by
Topscore Tanzania on Tuesday, December 7, 2010 at 12:08am
Askofu mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Polycap Kadinali Pengo alieleza kuwa hata kama walio kwenye mamlaka watawatishia, kanisa halitakuwa tayari kukaa kimya likiona kuna uovu. Kardinali Pengo alitoa msimamo huo wa kanisa hilo kubwa nchini wakati akitoa mahubiri yaliyorushwa na kituo cha redio ya kanisa hilo cha Tumaini katika ibada iliyofanyika kwenye Kanisa la Utoto Mtakatifu kituo cha Hija kilichopo Pugu jijini Dar es Salaam.
"Kamwe kanisa haliwezi kufumbia macho uovu ili kundi moja liweze kukaa kwenye mamlaka na uovu wao. Hata kama mamlaka hiyo itatoa vitisho kwa viongozi wakuu, Kanisa Katoliki halitakaa kimya. Katoliki linafahamu madhara yanayoweza kujitokeza katika jamii iwapo kanisa litampendekeza mtu kuwa kiongozi. Tuliombee taifa letu liepushwe na vitu vinavyotaka kuibuka katika taifa na kamwe kanisa haliwezi kumsimamisha mtu na kusema mumpigie kura."
Alisema kuwa kukemea uovu kusionekane kuwa ni udini na ifahamike kuwa Kanisa Katoliki halimsimiki mtu awe rais, diwani au mbunge wa mahali popote, hivyo uovu wowote unaofanywa na mamlaka utaendelea kukemewa bila uoga.
Alisema hawawezi kuwanyamazia wanasiasa wakati hata maaskofu pia wanakemeana wanapotenda uovu. "Uovu lazima ukemewe, si kitu ambacho mtu anafikiri kwamba mtu anaweza kutishia kwamba maaskofu wasikemee uovu," alisema Pengo.
Pengo alisema kuwa kutokana na kumbukumbu ya hapo zamani wakati wafalme walikuwa wakichaguliwa na mapadri na maaskofu, madhara yake yalijitokeza kwa kuwa jamii ilichaguliwa kiongozi asiyekubalika.
"Viongozi wa Katoliki wataendelea kukemea uovu huo kwa kuwa unaweza kusababisha mafarakano katika taifa linalotafuta ukweli na haki kwa ajili ya wote,"alisema Pengo.
Katika taifa lililo na watu takriba milioni 35 linaloundwa na idadi kubwa ya Wakristo na Waislamu wanaoshi pamoja, udini hauonekani kuwa silaha ya ushindi kwenye siasa.
Kadinal pENGO
Ukiona mwanasiasa au wanasiasa wanahangaika sana na agenda za udini ujue ni dalili za kuishiwa sera na kuanguka vibaya. Ni dalili mbaya saana na watu hao wanaozungumzia udini waogopwe manake wanataka huruma au wanataka kuleta mifarakano.