Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
alichosema ni sahihi kabisa.
wanasiasa nyoka wanatumia udini kama mtaji wa kujificha.
kwanini viongozi wa dini wasikemee uovu unaofanywa na viongozi na wakati viongozi hao hao ndio wanaojikomba kwa viongozi wa dini kuwaomba wakemee uozo?
 
sasa wewe hutaki maovu yakemewe au nini shida yako, au wewe unanufaika na maovu hayo?

Wanayosema wakina Pengo sio wanayotenda, ni watu hatari sana na wakuogopa kama ukoma aiseee. Walinitia sana kichefu chefu siku ambayo wasaidizi wake wakaanza kumpigia debe Slaa, huyu ni mwenzetu. Hapo hapo nilitoka kanisani , hii haikuwa kazi ya kanisa .
 
Siasa na Dini ni kama Mafuta na Moto,

Penda Usipende, LAZIMA vitenganishwe,

Mafisadi wanaojificha kwenye dini SAA yao imewadia!
Wanasiasa wajifichao kwenye Udini SAA yao imewadia!

TUNAWAJUA, kwa masikio yetu tumesikia wakiongea kwa Vinywa vyao,
MIOYO yetu ikawajua kuwa hawa sio wenzetu.

TOA KWANZA BORITI NDANI YA JICHO LAKO NDIO UTOE KIBANZI KWA JICHO LA JIRANI YAKO.
 
Hiyo midini yenu mngekuwa mnaifuata walau kwa asilimia 20, we wouldn't need to have this conversation.

BTW, viongozi wa dini nao ni sehemu ya tabaka tawala hivyo wote ni walewale tuu..same shyt different toilets.

Umewastukia !!!. Wengi hapa dini zimeanza kuwa ethnic identity lakini sio moral values.
 
Umewastukia !!!. Wengi hapa dini zimeanza kuwa ethnic identity lakini sio moral values.
Si ndio mi nawashangaa.

Midini imekuwa ndio topic kuu humu JF siku hizi, spirit mpya, ndio maana wengine taratiib tunaanza kuingia kwa 'kugusa'. Mijadala ya kujadili ishuz za maana kama kipindi kile cha Jamboforums haipo tena. Midini yenyewe asavali ingekuwa inawasaidia basi, yaani unakuta dini inalifanya jitu ndio linazidi kuwa lijinga kabsaa hakuna mfanoe.
 
Pengo,

Kemea udini unao fanywa na kondoo wako pale Tanzania Investment Bank. Kondoo wameitawala Bank na kueneza sera zao za kidini na kuwakandamiza baadhi ya waajiriwa wa dini nyingine

Anghalia Walokole walivyojipanga hapa Tanzania Investment Bank:


MANAGEMENT TEAM


Mr. Peter Noni Managing Director

Mr. Thomas M. F. Samkyi

Head of Business Development & Appraisal
+255 22 2411111

Mr. Bernard P. Mono

Head of Treasury & Funding
+255 22 2411112


Mr. Bahati J. Sanga

Head of Information & Communication Technology
+255 22 2411099


Mr. Leonard O. Mlewa

Head of Portfolio Management
+255 22 2411110


Mrs. Stella M. Nghambi

Head of Human Resources & Administration
+255 22 2411096


Ms. Martha J.J. Maeda

Legal Counsel & Secretary to the Bank
+255 22 2411117


Mr. Isaack E. Kiputa

Chief Internal Auditor
+255 22 2411116


Najua MOD utaifuta hii topic kwa sababu na wewe ni jamii ya kondoo waliopote.

Kama huna sera za msingi za kujadili kaa pembeni. Toa ushahidi kwamba hao wote uliowataja hawana sifa na dini ndo imewapa hizo nafasi. Na je hao wamewekwa kwenye nafasi hzo na walokole...? Tatizo elimu ndogo na kutokuwa na sifa mnatafuta sababu ya dini mara ukabila...!
 
Si ndio mi nawashangaa.

Midini imekuwa ndio topic kuu humu JF siku hizi, spirit mpya, ndio maana wengine taratiib tunaanza kuingia kwa 'kugusa'. Mijadala ya kujadili ishuz za maana kama kipindi kile cha Jamboforums haipo tena. Midini yenyewe asavali ingekuwa inawasaidia basi, yaani unakuta dini inalifanya jitu ndio linazidi kuwa lijinga kabsaa hakuna mfanoe.

Ningekuwa mods, topics zote zenye udini hata kama ni positive ningezifutilia mbali. Sijaona watu wanaleta moral values za kabila zao hapa. Wanaogopa kuonekana primitives. Kumbe hata dini ni Moral values za makabila fulani.
 
Ningekuwa mods, topics zote zenye udini hata kama ni positive ningezifutilia mbali. Sijaona watu wanaleta moral values za kabila zao hapa. Wanaogopa kuonekana primitives. Kumbe hata dini ni Moral values za makabila fulani.
Mi nawashangaa kama wanazipenda sana dini zao kwa nini bado wapo Tz? Katiba ya Tz inasema wazi Tz haifagilii dini yeyote..Kuna nchi za kidini huko kama wanataka kuwa karibu na mbingu..kama bado wanataka kuepo Tz yenye akina sisi chapombe ina maana hawaamini existence ya hiyo mbingu in the first place, unless otherwise mi nawaona wasanii tu , kama ulivyosema, wanastahili server ban maana wanatupotezea wakati.
 
Nadhani viongozi wa dini yeyote kukemea uovu si udini. Tatizo linakuja pale hawa viongozi wanapokuwa na double-standards. Kwa mfano kiongozi wa kiislamu hayupo tayari kukemea uovu wa mwislamu mwenzeke aliyepo serikalini na vilevile viongozi wa makanisa hawako tayari kukemea uovu iwapo aliyepo serikalini ni mkristo mwenzao. Ushahidi ni pale Mheshimiwa Mkapa alipokuwa madarakani ndipo ufisadi mkubwa ulipoanzia, rejea kesi za akina Mramba, Mgonja, Liyumba hata hizo kampuni za kifisadi zilianzishwa wakati wake, ulimsikia PENGO akikemea? Jibu ni hapana. Sasa anapata ujasiri kwa sababu aliyepo madarakani si wa dini yake. Ndipo mawazo ya kuwa kuna UDINI yanapoanzia. Tuwe wakweli.



Kuongoza jamii ya watu wenye ushabiki wa kidini ni kazi ngumu mnio. Hasa pale baadhi ya hao viongozi wenyewe wa kisiasa wanapolazimika kuwa sehemu ya huo udini. Uovu hauna dini na cha kushangaza zaidi ni pale malimbukeni wa kidini zaidi sana ni wale wanaojiita waislamu na wakristo. Kwa ushabiki wao hujisahaulisha kwa makusudi kwamba maovu kama sii yote basi asilimia zaidi ya 99 serikalini hutendwa nao. Tatizo lao kuu ni moja nalo ni mbaya zaidi ya ukimwi kwao, wanafikiri Mungu muumba ni wa dini yao. Hapo ndipo walipoanzishia ukengeufu wao wa mnyukano katika maongozi yao ya kisiasa. TIA AKILI, ZINDUKA!!
.
 
Naamini watu wote wenye utashi wanatambua ya kuwa suala la udini unakuzwa na kupigiwa debe na kundi ndani ya CCM kwa maslahi yao. Lakni wakumbuke ni double edged sword.
 
Wataingia kwa njia moja watatoka kwa njia saba, wanatumia dhana ya udini kama kigezo wakati ni wao wenyewe ndio wanaeneza sumu ya udini
 
Sas bwana Pengo yale majeshi yako ya wapiga kura yalikwenda wapi?
Jipange upya na 2015 ugombee wewe uankubalika aiseeeee
 
WAZIRI Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba amesema udini unaotajwa kuwapo nchini, hasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, umo miongoni mwa viongozi si wananchi wa kawaida.

Kauli hiyo ya Jaji Warioba ni sehemu ya maoni yake ya maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, Desemba 9, mwaka 1961 yanayofanyika kesho Alhamisi.

Amesema licha ya viongozi waasisi kufanikiwa kujenga Taifa moja, dalili za sasa si njema na kwamba kasi ya viongozi kugawanyika hata katika vyama vyao vya siasa inaelekea kutishia umoja wa nchi.

Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema yaliyochapishwa katika kurasa za tisa na 10 za toleo hili, Jaji Warioba anasema wananchi kawaida wamekuwa wakiendelea na shughuli zao bila kuulizana dini wala kabila zao.

“Wanafanya shughuli zao za kawaida iwe za biashara au uzalishaji. Ukikuta kundi la Wamachinga utawakuta vijana wa kutoka sehemu mbali mbali, dini mbali mbali na kabila mbali mbali wanafanya shughuli moja, hawajibagui hata kidogo.

“Inapofika wakati wa uchaguzi ndipo unasikia haya mambo ya ukabila, ukanda na udini. Haya yanaletwa na hawa ambao wanatafuta madaraka. Hawa wanaotafuta madaraka ndio wameleta matumizi ya fedha katika kutafuta uongozi,” alisema Jaji Warioba.

Katika hatua nyingine, Jaji Warioba ambaye amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere, ameonyesha kukerwa na tabia mpya ya kutojiamini kama nchi kiasi cha kutegemea zaidi wafadhili.

“Kwa nini waasisi wetu walijiamini zaidi kuliko sasa hivi? Mimi nadhani wakati ule TANU inadai Uhuru tukiwa vijana ndiyo tumeingia kwenye siasa, hali ilikuwa ngumu sana.

“Watu wengi walikuwa wanasema huyu Nyerere anahangaika…hana uwezo wa kupambana na Mwingereza amuondoe. Kwamba bila msaada hauwezi kumuondoa Mwingireza lakini walijiamini na Uhuru ukapatikana.

“…sasa hivi hatujiamini tunazungumzia sana ufadhili, Serikali inazungumzia ufadhili, wananchi wanazungumzia wafadhili. Tumekuwa na imani kuwa hatuwezi kufanya chochote bila kuwa na wafadhili.

“ Nadhani tunachohitaji sasa ni kubadili akili na mtazamo wetu. Lazima tujiamini hata raia nao wanasema Serikali itufanyie hivi na hivi. Ni lazima tuanze kujiamini mtu mmoja mmoja mpaka jumuiya nzima.

“ Kama tunaendelea hivi na katika nchi tunasema kuna partners in development (wadau wa maendeleo) maana yake sisi hatuwezi kushughulikia maendeleo yetu bila hao wabia na ubia huo uko wapi zaidi?

“ Sina matatizo na mfadhili ambaye anataka kujua fedha alizotoa zimetumika vizuri, lakini nadhani wafadhili wengi wanatia masharti ambayo ndiyo yanaamua ni sera ya aina gani tuwe nayo na kuitekeleza.

“ Ni kama tumepoteza uwezo wetu wa kuamua sera zetu. Nadhani tuanze kuwa wakorofi katika eneo hili. Inawezekana, kwamba siku hizi mwananchi hahusishwi sana katika kuunda sera zetu, inakuwa ni viongozi na hawa wanaoitwa partners wanakubaliana kisha ndiyo inapelekwa kwa wananchi wakubali au wakatae na mara nyingi wanakubali. Inabidi sasa tuanze kuwa na kiburi kile tulichokuwa nacho.”

Katika kusisitiza anaongeza: “Naamini kama tukiamua kwamba hapana, mambo ya sera tutaamua wenyewe, siamini kama hawa wafadhili watatulazimisha tuwasilikize, lakini nadhani tumezoea hii ya wafadhili. Uhuru wetu sasa unaanza kupungua, kwa mawili yale tuliyoanzisha…umoja wa nchi na uhuru wa kuamua mambo ya nchi yetu tukaweka misingi, haya yameanza kuingiliwa.”

Alionyesha pia kutofurahia kuingia mwaka wa 49 wa Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika wakati vyombo vya dola Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zikiwa zinaingiliwa kisiasa.
 
Kasema kweli......... Hawa watu sijui kwanini mpaka watuambie kwamba udini upo au haupo kwani sisi hatuma macho ya kuona.... This people they always use anything just to get a vote.... Its sad because we have not seen their true colours
 
Kiongozi akifilisika huleta hoja na ishu za ajabu ili kujihalalishia kutawala.
Mungu ibariki na kuilinda Tanzania
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom