Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
ninavyojua mimi ni kuwa Afrika hatuna dini ya kusema ni ya kwetu, Uislamu ni dini ya Waarabu na Ukristo ni dini ya Wazungu. Ninavyojua ni kuwa Uislamu na Waarabu ulituumiza sana enzi za utumwa na Ukristo na wazungu ulituumiza sana kwani ulitumika kutunyamazisha waafrika na kuwa nyenzo muhimu ya kueneza ukoloni. Binafsi nilisoma seminari miaka kadhaa ila sina sababu ya kuukashifu uisilamu japo sipendi na sitanyamaza pale dini yangu itakapokashifiwa. Nimeishi na Waisilamu zaidi ya miaka 10 na sijaona tatizo lolote.Kuepuka matatizo ya udini ni kutozungumzia dini kabisa,tuwaachie viongozi wetu!!

Are u still deserve as Great Thinker! or great tinker?
 
Hoja za udini zinatumiwa na waliokosa
hoja za msingi za kuwakomboa watz
mtaji wa wakubwa huo na tumeshastuka.
 
Udini umesaidia kuweka watu madarakani.
2005 jk alitumia wakristo wakasema jk ni chaguo la mungu na kusema lipumba na cuf ni waislamu
2010 wakristo wamemkimbia jk kwa sababu ya mahakama ya kadhi na kumutaka slaa na hili ndo tatizo
 
Kanisa Katoliki lagoma kuzika

Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga; Tarehe: 14th December 2010 @ 08:00

KANISA Katoliki Parokia ya Familia Takatifu Jimbo la Sumbawanga, limegoma kuendesha ibada ya maziko kwa marehemu wawili wakidai ibada haitaendelea mpaka pale waumini ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotengwa na kanisa hilo, watakapoondoka ndani ya kanisa hilo.

Marehemu hao ni aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Msua iliyopo Manispaa ya Sumbawanga, Mekitrida Maufi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa ambaye pia kwa sasa ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa, Patrick Maufi.

Maiti nyingine ambayo jina lake halikuweza kupatikana mara moja, ni ya mtoto wa darasa la nne ambaye pia shule aliyokuwa akisoma haijajulikana.

Tukio hilo lilitokea jana saa 8 mchana na lilidumu kwa saa tatu pale waombolezaji walipoleta miili ya marehemu hao kanisani hapo kwa ibada ya maziko.

Wengi wa waombolezaji hao walikuwa ni wanaCCM wakimsindikiza mfiwa na wengi wao walikuwa wameshatengwa kwa kinachodaiwa kuwa waliisaliti imani yao ya dini wakati wa Uchaguzi Mkuu kwa kumshabikia mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aesh Hilaly.

Baada ya waombolezaji kufika na majeneza ya miili hiyo mbele ya milango ya kanisa wakiwa tayari kuingia ndani, yalisomwa matangazo yaliyodai kuwa ibada ya kuombea marehemu haiwezi kufanyika hadi waumini waliotengwa (wanaCCM), watawanyike na wasionekane nje wala katika maeneo ya karibu na kanisa hilo.

Miongoni mwa waumini hao waliohudhuria, lakini wametengwa ni pamoja na mwenyekiti wa CCM Mkoa, Hypolitus Matete, Mwenyekiti CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Charles Kabanga, Katibu wa CCM Mkoa, Fraten Kiwango, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini aliyefahamika kwa jina moja la Tumombe na Diwani wa CCM Viti Maalumu Kata ya Sumbawanga, Aurelia Kanyengele.

Hali hiyo iliibua dhahama na kusababisha vurugu ya makundi mawili kati ya waliyotengwa na wanaounga mkono maamuzi hayo ambayo yalitiliwa nguvu na Paroko wa Parokia ya Kristu Mfalme, Pambo Mlongwa aliyefika maeneo hayo na kuwashinikiza mapadri waliokuwepo pale kuendelea na msimamo huo huo na kuwafanya waumini kuwataka waliokataliwa waondoke ili ibada ifanyike.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mjini, John Mzurikwao aliwataka waumini hao kwa kuwa wametengwa, watii maamuzi hayo na kuwasihi kuondoka hapo ili utaratibu wa ibada ya mazishi uendelee.

Viongozi hao baadhi walikubali na kurejea msibani, lakini baadhi ya waliotengwa walitoka nje ya uzio na kusubiri miili ya marehemu ili waungane na wenzao ili kwenda mazikoni. Ibada ya mazishi iliendelea.

Francis Chale ambaye ni Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM Wilaya ya Sumbawanga akizungumza na gazeti hili, alikiri si kutengwa tu, bali alivuliwa ukatoliki wake, akituhumiwa kumshabikia Hilaly ambaye ni Muislamu, aliyetuhumiwa na kanisa hilo kwa kuukufuru utatu mtakatifu katika moja ya mikutano yake ya kampeni alipojifananisha na Yesu Kristo kwa kuelezea dhana nzima ya mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani.

"Kitendo hiki kimetusikitisha sana, tulidhani kwamba tumezuiwa tu kuhudhuria ibada za misa takatifu kumbe hata ibada za mazishi. Sasa kama hali ndio hiyo na kanisa linajitambulisha kwamba ni wakala wa Chadema, basi na sisi tuliotengwa tunajipanga tupandishe bendera ya Chadema kwa kila Parokia iliyopo katika jimbo hili," alidai Chale.

Hivi karibuni, Parokia kadhaa za Jimbo Katoliki limewasimamisha waumini wake kwa madai ya kuisaliti imani yao kwa kutotii imani ya kanisa ambayo yaliwataka wasishabikie mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Katika msuguano huo wa kiimani, tayari kanisa hilo limewasimamisha na kuwatenga makatekista kwa madai wamelisaliti kanisa kwa kuwahamasisha waumini wao kumshabikia mgombea wa CCM.

Hata hivyo, kutokana na mchakato huo, kanisa hilo linajiandaa kutangaza orodha ya mapadri waliolisaliti hadharani ili nao waadhibiwe kama walivyoadhibiwa waumini hao.
 
ninavyojua mimi ni kuwa Afrika hatuna dini ya kusema ni ya kwetu, Uislamu ni dini ya Waarabu na Ukristo ni dini ya Wazungu. Ninavyojua ni kuwa Uislamu na Waarabu ulituumiza sana enzi za utumwa na Ukristo na wazungu ulituumiza sana kwani ulitumika kutunyamazisha waafrika na kuwa nyenzo muhimu ya kueneza ukoloni. Binafsi nilisoma seminari miaka kadhaa ila sina sababu ya kuukashifu uisilamu japo sipendi na sitanyamaza pale dini yangu itakapokashifiwa. Nimeishi na Waisilamu zaidi ya miaka 10 na sijaona tatizo lolote.Kuepuka matatizo ya udini ni kutozungumzia dini kabisa,tuwaachie viongozi wetu!!

Una maanisha wzungu waliumbwa wakiwa ni wakristu na waarabu waliumbwa wakiwa ni waislam?
 
.... Na hakuna yeyote mwenye ushahidi wa kutosha dhidi ya dini yake kua ndio ya kweli, ....

JOHN 14:6

"Jesus saith unto him, I am the way, the truth, and the life: no man cometh unto the father, but by me."
 
udini umetusaidia kujua wavivu wa kufikiria hufikiria imani tofauti kutafuta kura kupiga kampeni.
Kweli UDINI ni ugonjwa. UDINI ni Utaahira. UDINI ni uzandiki. UDINI ni upuuzi. UDINI ni upumbavu. UDINI ni ushenzi. UDINI ni UJinga.

KILAZA daima hushupalia visingizio. UDINI, UKABILA, RANGI, UZURI wa sura nk.
Kwa nini ushupalie jambo unaloliamini?
 
Ndg wana JF ni mtazamo wangu kwamba JK ndio aliyeimarisha udini na siasa za kidini hapa nchini.. Ni maono yangu kwamba kunaweza kutokea vurugu za kidini kabla hajaondoka madarakani.. Na hli linatokana na dalili tangulizi zinazoonekana mitaani juu ya mabishano ya dini na uhalali wa JK kuwa madarakani..

Nadhani njia sahihi ambayo Mh. angetumia si kukemea udini publicly (bungeni na kwenye hotuba mbalmbal) kwamba kuna udini, hvyo kusababisha hata wale waliokuwa hawaelewi udini kuanza kupata ufahamu..

Ambacho angefanya ni kuwaita viongozi wote wa dini na kuwatahadharisha.. Hao ndo wangeongea na waumini wao.. Nina waswas CCM kuishia kwnye uislamu na CHADEMA kuishia kwnye ukristu.. Soma gazeti la kiislamu la AN-NUUR utaujua udini wa nchi hii na vyama vya siasa.. NI mimi MBUMBUMBU..
 
Watanzania wenzangu na wana JF ninasikitishwa sana na dhambi hii mbaya iliyoanzishwa na CCM kwa mitazamo midogo ya kujipatia madaraka kwa gharama yeyote ile. Narudia tena wasipoitubu itaendelea kuwatafuna mpaka historia yao itakapofutika TZ. Ni jambo baya sana mlilolianzisha mpaka kufikia kuwavunjia heshima viongozi wa dini nawaasa tena tubuni ili mpate samehewa vinginevyo your days are numbered tupo hapa.
 
Watanzania wenzangu na wana JF ninasikitishwa sana na dhambi hii mbaya iliyoanzishwa na CCM kwa mitazamo midogo ya kujipatia madaraka kwa gharama yeyote ile. Narudia tena wasipoitubu itaendelea kuwatafuna mpaka historia yao itakapofutika TZ. Ni jambo baya sana mlilolianzisha mpaka kufikia kuwavunjia heshima viongozi wa dini nawaasa tena tubuni ili mpate samehewa vinginevyo your days are numbered tupo hapa.
Tunakuelewa sijuwi au ndio mauzauza yanaanza? Hivyo CCM ni dini gani? Na jee kuwavunjia heshima viongozi wa dini ndio udini?
 
Jamani mimi najiuliza swali nashindwa kupata majibu, hivi ni kwanini katika awamu ya 4 ambayo ipo Chini ya Kikwete neno Udini limetawala sana Tanzania, is it a researchable topic au kuna majibu ya haraka? nisaidieni plz
 
UDINI UMESHAMIRI MNO KIPINDI HIKI,
Tazama pale maandamano na vurugu za Arusha, badala ya vurugu kuelekezwa CCM/POLICE lakini zimeelekezwa kwa kupigwa mawe misikiti na wale BAKWATA wamelaani.
Waliopandikiza udini ni kwamba unatapakaa, sijui iundwe tena kamati kama ile ya kipindi cha Mwinyi ili viongozi wa dini wakae pamoja na kulinusuru taifa letu ama...?
Tunaelekea kubaya saana kiukweli, TUTAZAME NJIA ZA KUJINUSURU.
 
Kikwete anashindwa kusimamia mambo ya muhimu badala yake failures zake anaielekeza kwa wapinzani wake kwa kisinizio cha dini eti hawampende kwa sababu ni Muislam. Mbona wakati wa Mwinyi haya mambo hayakuwepo?
 
Wimbi la upinzani wenye akili limekuja kwa kasi mno na kila njia inatumika kulidhibiti.Watu wanaotumika kulidhibiti ni wa aina Tambwe Hiza na Makamba,watu ambao ni myopic.
Kiongozi mkuu amelisema lakini si katika kulikemea ila kutafuta sympathy.
Tunaofanya kazi vijijini hakuna udini kabisa lakini kwa kasi hii linavyozumgumzwa si ajabu yakatoakea makubwa,Mwenyezi Mungu aepushie mbali.
 
Mimi ni CCM damu.....ila nakiri kua Udini umeanzishwa na sisi CCM wenyewe maana katika kipindi cha uchaguzi sisi CCM tulifanya kampeni ktk nyumba za ibada..kwa hiyo wakulaumiwa ni CCM.
 
Chanzo Maaskofu!!!!! Kwani hamjui CHADEMA walikuwa wanapiga debe kanisani?

Hamuoni maaskofu wamekuwa wakali arusha? kama si dini ktk siasa kwanini wasilaani mauaji tu? Tena kwa taarifa yenu, naibu meya wa Arusha katangaza kujiuzulu Kanisani badala ya kwenda kuwaambia walio,chagua!

Eboooo, mnajifanya hamuoni wakati macho mnayo!?

Ningekuwa kikwete ningemrudisha Mahita kuwa IGP, wangekoma?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom