Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Mimi ni CCM damu damu. Lakini yoote mmesema, mbona mnakwepa kusema udini uko CHADEMA ambako Dr Slaa ni Padre? Ebu niambieni wajameni, lakini naomba msinipige viboko maana huenda na mie ni kama yule mwandamanaji aliyetumbukia kwenye maafande wa IGP Mwema kule Arusha siku ileeeeeeeeeee!!
 
avatar3015_2.gif

Bokassa unakumbuka supu ya mapaja ya wanadamu uliyokuwa unakunywa Afrika ya Magharibi?

Arusha utaishia kutafuna meno
 
Hakuna pa kukimbilia kwa hiyo wanaona udini tu. Wanataka kutuchanganya watz...... Siasa nyingine za kiafrica is just bollocks....
 
Chanzo Maaskofu!!!!! Kwani hamjui CHADEMA walikuwa wanapiga debe kanisani?

Hamuoni maaskofu wamekuwa wakali arusha? kama si dini ktk siasa kwanini wasilaani mauaji tu? Tena kwa taarifa yenu, naibu meya wa Arusha katangaza kujiuzulu Kanisani badala ya kwenda kuwaambia walio,chagua!

Eboooo, mnajifanya hamuoni wakati macho mnayo!?

Ningekuwa kikwete ningemrudisha Mahita kuwa IGP, wangekoma?

sikuonei ila bila shaka nadhani we kibaraka wa CHAMA CHA MAUAJI(CCM)................kilaza wewe L...thinker
 
Ndugu wana JF, dhana ya udini Tanzania ipo. Huu udini ukoje na uko wapi? Naomba tuchangie!
 
Ndugu wana JF, dhana ya udini Tanzania ipo. Huu udini ukoje na uko wapi? Naomba tuchangie!
Dhana, in its name ipo, na ndiyo inayotumiwa na JK et al kubaki hapo walipo!
In real Tanzanian life hakuna kitu cha hivyo!...Kukemea uovu si UDINI, niwajibu sahihi wa watu wa dini!

Ahsante!
 
wanaosambaza maswal aya kuwapo udin ni ccm.hiyo ni moja ya mikakat yao ya kuwahadaa watu waone kwamba vyama vingine si vizur-kama udin ungekuwepo hali yanhapa nchini ingekuwa kama nigeria
 
wanaosambaza maswal aya kuwapo udin ni ccm.hiyo ni moja ya mikakat yao ya kuwahadaa watu waone kwamba vyama vingine si vizur-kama udin ungekuwepo hali yanhapa nchini ingekuwa kama nigeria

Ni kweli Kama kungekuwa na udini kama wanavyosambaza uvumi CCM basi ndoa katika ya vijana wa kiislamu na wa kikristo zisingekuwepo.
 
Magobe T,
Sijui umefikiria au umeona nini ndo ukaleta hii hoja. Ila kutoka na udini unavyoendelea na kupaliliwa taifa letu na watanzania wengi weshalemaa na kuzowea kulalama udini! udini! udini kila kona! Na kwa sababu hizo ndo maana hata mimi sikuhizi nimekuwa msomaji, na mara nyingi nipo kona za lugha yetu yaani kiswahili kwani udini kule haujaingizwa sana. Kwa wale wanaonifahamu watajuwa kuwa forum za zamani nilikuwa mstari wa mbele kuchangia na kuelimishana.

Kutokana na mawazo na michango ya wengi humu JF sioni hata sababu miye kutoa hoja zangu kwenye hoja nyingi za kisiasa kwani badala ya kuwa za maendeleo ya taifa au za kueleweshana nyingi zimejaa jazba za kidini na wengi wanachangia kishabiki utadhinia ni timu za mipira au ligi ya mpira wa miguu. Mtu badala ya kuangalia na kutumia lojiki anamshabikia kiongozi au mtu fulani tu kwa sababu jina lake ni John au Jamal!-bila kujua uungwana, uadilifu wake au utendaji wa huyo Jamal / John ki kazi.

Cha ajabu ni kuwa kuna watu hapa mauaji ya Arusha wao wanakaa kimya au wanashambulia serikali kwa mitizamo yao ya kidini bila kujua kuwa waliouwawa ni wanadamu na watanzania wenzetu. Pia wapo mpaka leo wanaoyakataa mauaji ya Pemba au Mwebechai (dar es salaam), kisa ati wale walikuwa wapemba au wavaa vibarghashia!!, bila kutafakari na kufahamu kuwa serikali inamwaga damu za watu bila ya sabau ya msingi ili wao waendelee kutawala nchi yetu (TZ)! Cha kustaajabisha ni kuwa waloshiriki kwenye hayo mauaji yote ni CCM ambayo imekuwa inaongozwa na watu wa dini tofauti katika muda tofauti wa mauaji yaliyotokea! Ndiyo maana nasema ushabiki umekuwa kama wa timu za mipira-akili na busara watu wanaziweka pembeni.

Sitaki kuandika gazeti humu, ila nipo tayari kurudi tena na kuelewesha sehemu yeyote yenye utata.

Ahsanteni.
 
Magobe

Sitaki kuandika gazeti humu, ila nipo tayari kurudi tena na kuelewesha sehemu yetote yenye utata.
<bm
Ahsanteni.

Bro, you got it spot on! Huwezi kuwa sahihi zaidi ya hapa. Na wewe unayetafuta TZ udini uko wapi njoo JF! Imefika mahali huwezi kutofautisha issue ya ukristo na CHADEMA. Imefikia mahali kila anayetete CCM au kupinga CDM Inabidi apewe uislam ili atukanwe vizuri! Umeiona ile thread Mary Chitanda anaitwa jina la kiislam? What kind of evidence do u need?
 
Aisee wote wa2 mko sawa kabisa.Hapa JF udini wakutisha.Rejea post zangu uone matusi yalivyorushwa we acha!Post kama inaelezea Uislam itakaa front page na
kuchangiwa kwa hoja mbovu hadi kinyaa. Ukiweka post kueleza ukweli juu ya ukandamizaji wa kidini nchini lo? muda kidogo hiyo post inapotelea mbali.Gusa cdm na kanisa uone matusi ndani ya JF! LO! JF.
 
udini haupo kwani jamii zinazotuzunguka zimechanganyika katika masuala ya jamii eg ndoa,mazishi,burudani,makazini,usafiri,afya!udini upo kwenye elimu eg seminary za dini fulani tuu,na katika ajira za serikalini na mahali panapokua na mtawala eg manager,director muislam ndipo panapopigwa vita na kuonekana pana udini!
 
Kuna ndugu yangu yupo Nzega kanitumia ujumbe kwenye sms unasema hivi;
Laa mzee M.MUNGU HAMFICHI Mnafiki. Maaskofu hatimaye wajihirisha kuwa chadema ni chama chao walipopinga matokeo ya umeya Arusha. Katibu wa CCM mkoa wa Arusha aliwapaka kishenzi , kuwa wakasajili chama chao ili waje kugombeya wasijifanye wanasiasa uchwara, wala hatashiki na matamshi yao. Chadema wamekuwa wajinga, unashindaje ukiwa unazidiwa wajumbe? Mbona hawadai uspika kuwa haukuwa wa haki!. Vipi kuna mapya kwenye internet?.

Hii ndiyo DHANA ya UDINI ilivyo na pia inaonyeha Udini uko wapi. Mwanzoni sikuielewa thread hii lakini ndugu yangu huyu kanisaidia kuielewa.
Naomba mwanzilishi anikosoe! Nimefikisha.
 
Udini ulioko Tanzania ni wa mtu mmoja mmoja, wapo watu wanafanya upendeleo katika kutoa fursa kwa kuangalia udini na ukabila....mfano waajiri wa NSSF....uchunguzi wa juu unaonyesha upendeleo wa kidini katika kuajiri na kutoa vyeo.
 
Ndugu wanajamvi mmeamka salama bila shaka katika siku yetu hii ya kuweka historia kwa kuwapumzisha kwa amani wale wazalendo wa Arusha waliokimbizwa mbele ya HAKI Kwa maslahi ya wana CCM.

Nimejaribu kuangilia hatari ya udini unaoenezwa na wenzetu wa ccm kwa makusudi kwa maslahi yao lakini huku wakisahau kuwa na wao wenyewe itawatafuna. Hii haina tofauti na mtu anayekula nyama ya mtu. Laana ile itammaliza tu.
Mwenye akili akifuatilia atagundua suala la waisalamu kwenda kuwaambia watu maaskofu wamekosea kusema hawamtambui meya aliyechaguliwa katika mazingira ya kihuni ni cha utovu wa heshima mbele ya jamii. Katika hali ya kawaida usingetegemea kuona waislam na viongozi ndio wananchi watakaoongozwa na huyu meya aliyechakachua kura. Bila kujali wewe unatimiza wajibu wako katika jamii au lah lakin lazima suala la kuongozwa na kiongozi mwenye ridhaa ya wananchi ndio la kwanza.

Cha ajabu wakati wananchi wanakasirika na sisim ambayo kwa hila na ujinga wao wameiingiza hili suala la udini viongozi wetu wastafu ukiachilia Malecela wamekaa kimya na hata kusema kuwa hili suala sasa ni hatari kwa ustawi wa nchi hii. Hii ni ajabu sana.

Lazima akina Warioba, Mkapa waseme, huu ukristu au uislam wa kudandia tu mambo siyo tabia yetu watanzania
 
Pole pole, tutatafika tu. Kwanza hata huyo meya sijui anajisikiaje. Yeye akiwa ni miongoni mwa chanzo cha vifo vya marehemu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom