Magobe
Sijui umefikiria au umeona nini ndo ukaleta hii hoja. Ila kutoka na udini unavyoendelea na kupaliliwa taifa letu na watanzania wengi weshalemaa na kuzowea kulalama udini! udini! udini kila kona! Na kwa sababu hizo ndo maana hata mimi sikuhizi nimekuwa msomaji, na mara nyingi nipo kona za lugha yetu yaani kiswahili kwani udini kule haujaingizwa sana. Kwa wale wanaonifahamu watajuwa kuwa forum za zamani nilikuwa mstari wa mbele kuchangia na kuelimishana.
Kutokana na mawazo na michango ya wengi humu JF sioni hata sababu miye kutoa hoja zangu kwenye hoja nyingi za kisiasa kwani badala ya kuwa za maendeleo ya taifa au za kueleweshana nyingi zimejaa jazba za kidini na wengi wanachangia kishabiki utadhinia ni timu za mipira au ligi ya mpira wa miguu. Mtu badala ya kuangalia na kutumia lojiki anamshabikia kiongozi au mtu fulani tu kwa sababu jina lake ni John au Jamal!-bila kujua uungwana, uadilifu wake au utendaji wa huyo Jamal / John ki kazi.
Cha ajabu ni kuwa kuna watu hapa mauaji ya Arusha wao wanakaa kimya au wanashambulia serikali kwa mitizamo yao ya kidini bila kujua kuwa waliouwawa ni wanadamu na watanzania wenzetu. Pia wapo mpaka leo wanaoyakataa mauaji ya Pemba au Mwebechai (dar es salaam), kisa ati wale walikuwa wapemba au wavaa vibarghashia!!, bila kutafakari na kufahamu kuwa serikali inamwaga damu za watu bila ya sabau ya msingi ili wao waendelee kutawala nchi yetu (TZ)! Cha kustaajabisha ni kuwa waloshiriki kwenye hayo mauaji yote ni CCM ambayo imekuwa inaongozwa na watu wa dini tofauti katika muda tofauti wa mauaji yaliyotokea! Ndiyo maana nasema ushabiki umekuwa kama wa timu za mipira-akili na busara watu wanaziweka pembeni.
Sitaki kuandika gazeti humu, ila nipo tayari kurudi tena na kuelewesha sehemu yetote yenye utata.
<bm
Ahsanteni.