Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Mashujaa wa mabadiliko ya kweli Arusha Marehemu Denis Shirima na Ismail Omary wametuunganisha katika azima yao ya kufia mabadiliko nchini pasipo kuonyesha hizo tofauti za kidini ambazo CCM huendekeza kutugawa nayo ili waendelee kutafuna nchi hadi mifupa.

Isitoshe, CCM ilipokua inawaua Watanzania pale Pemba, Unguja, Arusha, Shinyanga na sasa Mbarali, kwa kudai kwao HAKI KUTENDEKA, chama hiki hakikuwauliza dini zao kabla ya kuachia mmiminiko wa risasi kama mvua miilini mwao.

Hakuna wa kutugawa tena wala wa kuturudisha nyuma kudai mabadiliko.
Watanzania Vita mbeeellllee!!
 
Ukifilisika kimawazo ni rahisi sana kukimbilia vitu kama udini,ukabila ni mambo ya kipumbavu sana yanayopenyezwa na wale walishindwa kufikiri zaidi ya urefu wa pua zao. Utashangaa eti ni watu waliokuwepo wakati wa Mwalimu na eti wanamuenzu. Hii ndio gharama ya cheep popolarity.
 
Kwa hali ya sasa watawala wanataka kubaki madarakani kwa kudhoofisha jamii. Namna pekee ya kupunguza kuporomoka kwa umaarufu wa watawala kutokana na mapungufu mbali mbali wameamua kutumia mbinu ya wakoloni ya divide and rule. Ndivyo wazungu walifanya walivyo taka kuchukua raslimali zetu. Machifu wakagonganishwa na kupiganishwa kwa faida za wakoloni. Leo WATAWALA wetu wameona last resort waliyonayo ni kuwagawa wananchi kwa udini. Katika issue yoyote sasa kama wanajaribu kuiendea kwa kuwagonganisha wakristo na waislamu. Si uchaguzi, matatizo ya kijamii kama kupanda bei ya umeme, Dowans, matatizo ya wanafunzi kunyimwa mikopo na kutoenda field, Umeya Arusha n,k Nyingi ni shida za jumla za kijamii, kwa vile nchi ina watu wa dini mbali mbali bila shaka kuna mtu wa dini fulani ataibua tatizo hapa na pale. Sasa kwa vile watawala hawana jawabu kwa shida za watu wana jibu moja. Aliyeibua ni mwislamu anataka kuvuruga nchi au ni mkristo waislamu angalieni. Hivyo badala ya kushughulika na tatizo unamrukia aliyeibua tatizo. Watawala waovu hutumia njia hizi na wananchi wajinga hukubaliana nazo.
 
Kaka hilo hawaliwezi kabisaaa, maana wanaotoa matamko kwa mfano ya kiislamu ni wahuni wachache ambao wanajiita bakwata. Hawa wanajulikana kwa kuwa karibu sana na serikali, sidhani kama mimi naweza kuchukiana na waislamu ambao nakaa nao karibu na majirani zangu au marafiki. Na waislamu wanajua maovu yanayotendeka hivyo hawawezi kuwa stepping stone ya mafisadi, la hasha
 
Na bado watasema yote mwisho wataishiwa na watahamia kwenye jinsia kwamba hao ni wanawake tu au hao ni wanaume(siyo gender sensitive) achaneni nao wabaya wakubwa hao.

Hao ndo si si em bwana.
 
Ndugu wana JF, dhana ya udini Tanzania ipo. Huu udini ukoje na uko wapi? Naomba tuchangie!
Nadhani taarifa za kiintelijensia zitakuwa zinapicha kamili, mkulu alitaja tu siku akihutubia Bunge kuhusiana na tatizo hilo na kwa kuwa yeye ndiye mwenye kulishwa taarifa na mikondo mbalimbali basi tuamini upo, ufafanuzi utafuata baadaye baada ya kupata njia mwafaka ya kutatua hili tatizo, njia ambayo itaponyesha majeraha yaliyoachwa na uchaguzi etc
 
Magobe T,
Sijui umefikiria au umeona nini ndo ukaleta hii hoja. Ila kutoka na udini unavyoendelea na kupaliliwa taifa letu na watanzania wengi weshalemaa na kuzowea kulalama udini! udini! udini kila kona! Na kwa sababu hizo ndo maana hata mimi sikuhizi nimekuwa msomaji, na mara nyingi nipo kona za lugha yetu yaani kiswahili kwani udini kule haujaingizwa sana. Kwa wale wanaonifahamu watajuwa kuwa forum za zamani nilikuwa mstari wa mbele kuchangia na kuelimishana.

Kutokana na mawazo na michango ya wengi humu JF sioni hata sababu miye kutoa hoja zangu kwenye hoja nyingi za kisiasa kwani badala ya kuwa za maendeleo ya taifa au za kueleweshana nyingi zimejaa jazba za kidini na wengi wanachangia kishabiki utadhinia ni timu za mipira au ligi ya mpira wa miguu. Mtu badala ya kuangalia na kutumia lojiki anamshabikia kiongozi au mtu fulani tu kwa sababu jina lake ni John au Jamal!-bila kujua uungwana, uadilifu wake au utendaji wa huyo Jamal / John ki kazi.

Cha ajabu ni kuwa kuna watu hapa mauaji ya Arusha wao wanakaa kimya au wanashambulia serikali kwa mitizamo yao ya kidini bila kujua kuwa waliouwawa ni wanadamu na watanzania wenzetu. Pia wapo mpaka leo wanaoyakataa mauaji ya Pemba au Mwebechai (dar es salaam), kisa ati wale walikuwa wapemba au wavaa vibarghashia!!, bila kutafakari na kufahamu kuwa serikali inamwaga damu za watu bila ya sabau ya msingi ili wao waendelee kutawala nchi yetu (TZ)! Cha kustaajabisha ni kuwa waloshiriki kwenye hayo mauaji yote ni CCM ambayo imekuwa inaongozwa na watu wa dini tofauti katika muda tofauti wa mauaji yaliyotokea! Ndiyo maana nasema ushabiki umekuwa kama wa timu za mipira-akili na busara watu wanaziweka pembeni.

Sitaki kuandika gazeti humu, ila nipo tayari kurudi tena na kuelewesha sehemu yeyote yenye utata.

Ahsanteni.
kwanini leo mwembechai na pemba? kila mbuyu na shetani wake
 
Niliwahi kumpigia simu live Jenerali Ulimwengu wakati anarusha kipindi chake maarufu kama Jenerali on Maonday,Topiki ilikuwa ni mchango wa Nyerere ktk amani ya Tz.Nilimwambia kuwa amani ya Tz imejengwa juu ya tope kwa sababu kuna watu haki zao zinanyongwa kwa sababu ya dini zao halafu linafanywa ni jambo nyeti watu hawataki lizungumzwe.Nilimpa mfano hai kuwa mimi binafsi niliwahi kunyimwa kazi kwa sababu ya dini yangu.Hii ilikuwa ni utawala wa Mkapa.Kesho yake nikapigiwa simu na mtu amabe nilihisi alikuwa ni usalama wa Taifa.Akaomba nijibu maswali yake atakayoniuliza.Swali la kwanza.Je wewe ni mtanzania wa kuzaliwa au wa kuomba uraia? nikmjibu kuwa ni mtz wa kuzaliwa.swali la pili.Je unavyoiona tz ni nchi nzuru sana ya kuishi? nzuri kiasi au wastani? nikamjibu ni wastani.Akanishukuru akakata simu.
Kwa hiyo Tz udini upo tena haukuanza leo ila ulifanywa jambao nyeti sana lakini watu tumeumizwa sana na udini.Wengine wanatafsiri kuwa hakuna udini kwa vile tunaishi pamoja mitaani na hatugombani tunashirikiana.Hili limewezekana kwa sababu wale wanao nyimwa haki kwa sababu za dini wamekuwa kimya.Ninaamini hali iliyopo tz kwa watu wa dini moja kuwa juu ya wengine ingekuwa ni other way round amani isingekuwepo.Nitoe mfano:Wakati mkiristo anaweza kwenda sehemu za waislamu wengi akagombea uongozi akashinda,hilo haliwezi kutokea Muislam kwenda sehemu za wakristo wengi akagombea akashinda.Kama ninadanganya nipewe mfano japo mmoja tu hasa kwa ngazi ya ubunge
 
Soma magazeti ya Uhuru na Habari leo ya leo tarehe 14 jan 2011 utafakari kwa makini
 
Aliyekataza kumsema Mkapa ni fisadi mwenzie kikwete. Namnukuu akisema, "waacheni wazee wastaafu kwa amani". Kan kwamba hiyo haitoshi, Wikileaks imetuonyesha wazi kuwa Kikwete amempa amri Hosea wa PCCB kutokufatilia ufisadi wa akina Mkapa na Sumaye. Sasa udini hapa uko wapi ikiwa Kikwete ndio anakataa scrutiny siwepo kwa hawa mafisadi wenzie? Narudia tena na tena. Risasi iliyomuua muislamu marehemu Ismail kule Arusha, iliamriwa kupigwa na muislamu mwenzie Said Mwema (IGP) na akapata support ya kifedhuli toka kwa waislamu wengine kama Makamba na Tambwe Hiza. Udini upo wapi hapo? Mbona Meya anayetakiwa kujiuzulu Arusha ni mkristo tena mkatoliki kama mnavyosema CHADEMA ni ya wakatoliki? Mbona alisemwa Lowasa ambae ni mkristo mpaka alijiuzulu uwaziri mkuu? Udini upo wapi ikiwa watanzania wa dini zote wanakabiliana na mfumuko wa bei kwenye kila sekta ya uchumi wakati hata uyo fisadi Mkapa alirekebisha hili la mfumuko alipokuwa madarakani? Tatizo la wafuasi wa CCM kama Aikaotana mnaakili "brand new". Namaanisha hamzitumii kabisa katika kutoa misimamo yenu ndio maana bvado mpya. Hebu anzeni kuzitumia jamani maana mnatia aibu.
 
Aliyekataza kumsema Mkapa ni fisadi mwenzie kikwete. Namnukuu akisema, "waacheni wazee wastaafu kwa amani". Kan kwamba hiyo haitoshi, Wikileaks imetuonyesha wazi kuwa Kikwete amempa amri Hosea wa PCCB kutokufatilia ufisadi wa akina Mkapa na Sumaye. Sasa udini hapa uko wapi ikiwa Kikwete ndio anakataa scrutiny siwepo kwa hawa mafisadi wenzie? Narudia tena na tena. Risasi iliyomuua muislamu marehemu Ismail kule Arusha, iliamriwa kupigwa na muislamu mwenzie Said Mwema (IGP) na akapata support ya kifedhuli toka kwa waislamu wengine kama Makamba na Tambwe Hiza. Udini upo wapi hapo? Mbona Meya anayetakiwa kujiuzulu Arusha ni mkristo tena mkatoliki kama mnavyosema CHADEMA ni ya wakatoliki? Mbona alisemwa Lowasa ambae ni mkristo mpaka alijiuzulu uwaziri mkuu? Udini upo wapi ikiwa watanzania wa dini zote wanakabiliana na mfumuko wa bei kwenye kila sekta ya uchumi wakati hata uyo fisadi Mkapa alirekebisha hili la mfumuko alipokuwa madarakani? Tatizo la wafuasi wa CCM kama Aikaotana mnaakili "brand new". Namaanisha hamzitumii kabisa katika kutoa misimamo yenu ndio maana bvado mpya. Hebu anzeni kuzitumia jamani maana mnatia aibu.

wanachosema kwamba, maaskofu wameuliwa wapemba na mwembechai walipongeza ccm. lkn arusha waliilani ccm. eti maaskofu huangalia nani kakaa Ikulu. yaani mkatoliki au muislam
 
wanachosema kwamba, maaskofu wameuliwa wapemba na mwembechai walipongeza ccm. lkn arusha waliilani ccm. eti maaskofu huangalia nani kakaa Ikulu. yaani mkatoliki au muislam

hakuna Askofu aliyeipongeza CCM kwa mauhaji ya Pemba na Mwembechai, wala Hakuna Askofu anayeilaani CCM kwa mauhaji ya Arusha
 
hakuna Askofu aliyeipongeza CCM kwa mauhaji ya Pemba na Mwembechai, wala Hakuna Askofu anayeilaani CCM kwa mauhaji ya Arusha
katika misa moja chuo kikuu cha da, Pengo alisema cuf ndio wa kulaumiwa, alisema watu wa nje wanatumiwa na Cuf. lkn kwa chadema na arusha atoa kombora zito
 
wanachosema kwamba, maaskofu mwembechai walipongeza ccm. lkn arusha waliilani ccm. eti maaskofu huangalia nani kakaa Ikulu. yaani mkatoliki au muislam

Mkuu hizi kesi ni tofauti sana nianze na ya mwemb chai nadhani unakumbuka kuwa ile ilikuwa live ugomvi kuanzia mabucha ya nguruwe hadi "Yesu si Mungu" umeelewa? Hii kesi ya Arusha sijui kama umeifuatilia kwa makini!
 
hakuna Askofu aliyeipongeza CCM kwa mauhaji ya Pemba na Mwembechai, wala Hakuna Askofu anayeilaani CCM kwa mauhaji ya Arusha
Sure na kama kuna ushahidi wa maaskofu kupongeza hayo mauaji ya pemba tuleteeni tuone
 
Udini ni dhana iliyoletwa kupoteza harakati za kudai uhuru kamili wa watanzania kwa manufaa ya ccm iendelee kutufisadi!hakuna udini tupambane na huu utawala!tunisia wameweza sisi jee?tena vijana ndiyo wameikomboa nchi yao kwa kukosa ajira vitu kupanda bei sisi tuna sababu zaidi ya hizo,ufisadi umaskini uliokithiri huduma za afya, maji, elimu duni
 
Mfa maji haishi kutapatapa ccm wameishiwa sera na kung'ang'ania Udini Jamani Watanzania tusidanganyike na upuuzi wa watu wachache kutugawa pande mbili.
 
tazameni majadiliano ya watu hawa kwenye facebook na muone jinsi wananchi wanapoelekea



pale mapadri na mashehe wanapotofautiana kwa waumini itakuwaje?

4 hours ago · LikeUnlike · Comment · View Feedback (13)Hide Feedback (13)
    • Salum Masudi ‎@gocha, kwani mapadri na masheikh hawatofautiani?4 hours ago · UnlikeLike ·
      tddUIK01p63.png
      1 personLoading...

    • Godwin Chacha kawaida watu wanatakiwa kutofautiana lakini kikubwa zaidi ni namna ya siasa ya nchi yetu inavyoanza kutenga watu kwa makundi ya dini mimi nashindwa kujua hivi tunaenda wapi?kwani inavyoonekana watu wanaanza kutofautiana si kimitazamo bali kwa dini zao. inabidi ifike wakati mapadri na mashehe wakae pamoja na kuagalia nini athari za migongano yao katika ustawi wa taifa letu3 hours ago · LikeUnlike

    • Salum Masudi ‎@gocha! si masheikh kukaa na mapadri kinachotakiwa ni mapadri kutambua kuwa waislamu wana haki sawa kama wakristo katika nchi hii hivyo wabadilike ingawa wao (Mapadri) ndio wanaotawala hii nchi kupitia mawakala wao walio wengi serikalini, ...mifano ni mingi ya waislamu kunyanyaswa na serikali lakini hakuna hata mfano mmoja wa wakristo kunyanyaswa na serikali kwani wao ndio serikali yenyewe! waislamu kupata haki ya kujisitiri kwa hijjab tu iliwagharimu kuachishwa kazi na hadi leo kuna wanaonyanyaswa kwa kuvaa hijjab na me ngine mengi, wanaojua historia ya nchi hii hawawezi kubisha na hata wakibisha miyoni mwao wanajua ukweli, wakati nasoma ilboru kuna mzungu jirani alikuwa akilalamika eti tunampigia kelele kwa adhana lakini hakuzungumzia kengele za shule kuanzia asubuhi hadi jioni na kengele za kanisa za siku ya JUMAPILI, I think u get a picture of the problem now!See More
      3 hours ago · LikeUnlike ·
      tddUIK01p63.png
      1 personLoading...

    • Godwin Chacha kwanini mapadri watawale nchi wakati rais, makamu wa rais, jaji mkuu, mkuu wa polisi na ata director wa usalama wa taifa ni waisilamu? huoni kuwa kama watu hawa wakitawaliwa basi wamejitakia? kwa upande wa wakristo pia wanaona mgawanyo huu wa vyeo vya juu si sawa na ni kama msikiti kutawala nchi na ata kutaka kuingiza mahakama ya kadhi kwenye katiba3 hours ago · LikeUnlike

    • Salum Masudi ha ha ha ha! I knew utasema hivyo! ni kama watu fulani waliosema udom kuna udini eti kwa kuwa vc ni prof kikula ambaye ni muislamu na kusahau walio chini wote ni wakristo na ndio watendaji yeye anapelekewa taarifa tu, ok unaona sasa! mahak...ama ya kadhi ni ya waislamu na itawahukumu waislamu na kizuri zaidi serikali ilitumia fedha nyingi kuunda tume kujiridhisha kuhusu mahakama ya kadh ambayo kenya ipo na hata zanzibar ipo na imegundua hakuna madhara lakini haitekelezwi kwa sababu tu mapadri kwa maslahi ya ukristo hawaitaki, hata OIC Membe alitangaza bungeni kuwa ina faida nyingi tu lakini mapadri wakamwita na kusitisha ili waislamu wasipate misaada LAKINI SIKU MOJA HAKI ITAPATIKANA INSHALLAHSee More
      3 hours ago · UnlikeLike ·
      tddUIK01p63.png
      2 peopleLoading...

    • Salum Masudi wakristo lazima waone mgawanyo huo c sawa kwa kuwa walishazoea kututenga eti waislamu hawakusoma na hawa tunaowaona sasa kwenye hivi vyeo hawakusoma, walikuwa wapi, MKAPA aliwahi kuvunja bodi ya PAROLE kwa kuwa haikuwa hata na muislamu mmoja ilijaa mapadri na maaskofu, mnajisahau mnadhani mko peke yenu hii ni nchi yetu wote3 hours ago · LikeUnlike ·
      tddUIK01p63.png
      1 personLoading...

    • Godwin Chacha sasa umeona jinsi jamii inavyoweza kutafsiri mambo tofauti vivyo hivyo pande zote hizi kila moja inaweza kuwa inalalamika kutawaliwa na mwenzake huoni jawabu ni kukaa na kujadili matatizo yao na kufikia jawabu.kwa upande wangu sioni tofauti... kati ya mtawala mkristo na muislamu kwani imekuwa kawaida kwa watawala wetu kujinufaisha wenyewe na kutojali wananchi. wameuza rasilimali zetu na kutuacha masikini . cha msingi ni umoja wa wananchi kuzuia ufisadi na mmomonyoko wa maadili ya viongozi....kwa upande wako je ungependa utawaliwe na mtu kwakuwa ni dini yako tuu au anayeleta manufaa kwa jamii? je mashehe na mapadri wanavyolumbana kuna nini jipya tunalolingoja?See More
      3 hours ago · LikeUnlike

    • Salum Masudi Inaonekana Gocha hujagundua tatizo, kama wewe hauko biased ni rahisi kugundua sisi waislamu hatuna tatizo lakini wakristo mnatuchukia na mnapenda sisi tufuate mila zenu ambacho haiwezekani kwa mfano ninyi mnajua fika sisi hatuli nguruwe iwe...je pale minaki mwalimu atumie vyombo vya shule kupikia nguruwe? na kama TZ kuna ubalozi wa Vatican vipi ishindikane TZ kujiunga na OIC? na mifano iko mingi inayoonesha chuki ya makanisa na hasa mapadri dhidi ya uislamu, sasa hao watu inabidi wabadilike kimtazamo kabla ya kukaa pamoja na wasidhani kwamba mtu anaweza akajiunga kwenye imani yao kwa kumnyanyasa, hoja ndio itakayombadilisha mtuSee More
      3 hours ago · LikeUnlike ·
      tddUIK01p63.png
      1 personLoading...

    • Salum Masudi kwa kuwa jumapili nyinyi mnaenda kanisani mmelazimisha iwe mapumziko ila mnajua umuhimu wa ijumaa kwetu lakini mpaka tulipofikia kupata ruhusa ya kwenda kuswali ijumaa iliwagharimu waislamu kupigwa, kunyanyaswa na hata kufukuzwa kazi, au haya huyajui?3 hours ago · LikeUnlike ·
      tddUIK01p63.png
      1 personLoading...

    • Salum Masudi tatizo tumerithi mfumo kristo ambao unataka kutofanya kazi jumapili kwa kuwa mnaenda kanisani, wanawake wawe uchi kwa sare mlizoziweka kwa kuwa dini yenu inaruhusu, kutumiwa pombe kwenye sherehe kwa kuwa dini yenu inaruhusu, sasa sisi tukisema hapana kwa kuwa dini yetu hairuhusu inakuwa sisi tunaleta udini! matatizo ni makubwa na majibu hayawezi kuwa rahisi, inabidi upande mmoja ukubali kwamba wakati umefika sasa wa EQUAL RIGHTS 4 ALL3 hours ago · LikeUnlike ·
      tddUIK01p63.png
      1 personLoading...

    • Godwin Chacha vaticani ni nchi kama ilivyo iran na saudia na kwanini turuhusu iran kuwa na ubalozi tuzuie vatikani...iran ni nchi ya kiislamu na vatikani ni nchi ya kikristo sasa huoni kuwa kujiunga na oic ni kusema nchi yetu ni ya kiislamu? je wakristo ...tukiomba katiba itambue tz ni nchi ya kikristo itakuwaje? ha ha ha minaki ni shule ya kikristo sasa ni sawa na mkristo akisoma islamiki school agome kuvaa hijabu....kuna wakati jamii inaweza kulalamika ata vitu vidogo kwa mfano wakristo wakilalamika kwanini waislamu wao tuu ndio wanachinja kwenye machinjio yote nasi tunakula na sisi tumezuia kuchinja katika machinjio yote unadhani malalamiko haya yana mantiki yoyote?See More
      2 hours ago · LikeUnlike

    • Salum Masudi vatican ni wakala wa kanisa katoliki hapa hivyo haina manufaa kwa taifa na ndio maadui wakubwa wa waislamu, minaki ni shule ya serikali siyo ya kanisa na hata kama ingekuwa ya kanisa ina maana hawaruhusiwi kusoma waislamu na kama wanaruhusi...wa vipi haki zao zisizingatiwe na hapo ndo kwenye kiini cha tatizo, kuhusu OIC nchi iliunda tume kufanya research na imegundulika hakuna madhara na hata Membe alitangaza bungeni hilo kwa hiyo hatuheshimu tume tulizoziunda sisi wenyewe? kuhusu kuchinja nyinyi wakristo hamna utaratibu wa kuchinja nyinyi mna nyonga tu na kama mnao semeni kila watu wawe na wachinjaji wao kwani tatizo liko wapi hapo? halafu unasema vitu vidogo kula nguruwe kwa muislamu siyo kitu kidogo! uislamu ni mfumo kamili na ndio maana una utaratibu katika kila aspect ya maisha kama ndoa, mirathi, mavazi, mazishi n.k. Tatizo tukifuata sisi dini yetu tunakuwa wadini ila mkifiata ninyi inakuwa ndio sawa!See More
      2 hours ago · LikeUnlike ·
      tddUIK01p63.png
      1 personLoading...

    • Godwin Chacha ni wakala lakini ni nchi inayotambulika na umoja wa mataifa, na pia minaki ni shule ya kikristo bali natambua haki ya muislamu kutokutumia nguruwe lakini mbona mnawalazimisha dada zetu kuvaa hijabu(vazi la kiislamu) pia kama wamefanya utafi...ti wakagundua kuwa oic haina madhara je wewe umeona madhara ya vatikani kuwa na ubalozi wake? ha ha ha kijana kama unaweza kuona pande nyingine wananyonga hawachinji basi na wao wanaweza kuwa na mtazamo kama wako. kwani kuchinja ni lazima kuwe na dua la kiislamu? kuwa na aspect ya maisha ya dini ni vema kwanini mfumo wa maisha yenu lazima yaingizwe kwenye katiba? kwani kama mkianzisha mahakama za kadhi kwenye misikiti pasipo kuingiza kwenye katiba nani atalalamika?
      mbona ata sasa mna kadhi mkuu kuna mtu amelalamika? vile vile irani ni wakala wa uislamu nasi tusinge penda iwe na balozi wake...mbona amlalamiki uingereza ambayo ni wakala wa anglikani?See More
      2 hours ago · Like

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom