Chief Rumanyika
Senior Member
- Dec 29, 2010
- 138
- 0
Nadhani taarifa za kiintelijensia zitakuwa zinapicha kamili, mkulu alitaja tu siku akihutubia Bunge kuhusiana na tatizo hilo na kwa kuwa yeye ndiye mwenye kulishwa taarifa na mikondo mbalimbali basi tuamini upo, ufafanuzi utafuata baadaye baada ya kupata njia mwafaka ya kutatua hili tatizo, njia ambayo itaponyesha majeraha yaliyoachwa na uchaguzi etcNdugu wana JF, dhana ya udini Tanzania ipo. Huu udini ukoje na uko wapi? Naomba tuchangie!
kwanini leo mwembechai na pemba? kila mbuyu na shetani wakeMagobe T,
Sijui umefikiria au umeona nini ndo ukaleta hii hoja. Ila kutoka na udini unavyoendelea na kupaliliwa taifa letu na watanzania wengi weshalemaa na kuzowea kulalama udini! udini! udini kila kona! Na kwa sababu hizo ndo maana hata mimi sikuhizi nimekuwa msomaji, na mara nyingi nipo kona za lugha yetu yaani kiswahili kwani udini kule haujaingizwa sana. Kwa wale wanaonifahamu watajuwa kuwa forum za zamani nilikuwa mstari wa mbele kuchangia na kuelimishana.
Kutokana na mawazo na michango ya wengi humu JF sioni hata sababu miye kutoa hoja zangu kwenye hoja nyingi za kisiasa kwani badala ya kuwa za maendeleo ya taifa au za kueleweshana nyingi zimejaa jazba za kidini na wengi wanachangia kishabiki utadhinia ni timu za mipira au ligi ya mpira wa miguu. Mtu badala ya kuangalia na kutumia lojiki anamshabikia kiongozi au mtu fulani tu kwa sababu jina lake ni John au Jamal!-bila kujua uungwana, uadilifu wake au utendaji wa huyo Jamal / John ki kazi.
Cha ajabu ni kuwa kuna watu hapa mauaji ya Arusha wao wanakaa kimya au wanashambulia serikali kwa mitizamo yao ya kidini bila kujua kuwa waliouwawa ni wanadamu na watanzania wenzetu. Pia wapo mpaka leo wanaoyakataa mauaji ya Pemba au Mwebechai (dar es salaam), kisa ati wale walikuwa wapemba au wavaa vibarghashia!!, bila kutafakari na kufahamu kuwa serikali inamwaga damu za watu bila ya sabau ya msingi ili wao waendelee kutawala nchi yetu (TZ)! Cha kustaajabisha ni kuwa waloshiriki kwenye hayo mauaji yote ni CCM ambayo imekuwa inaongozwa na watu wa dini tofauti katika muda tofauti wa mauaji yaliyotokea! Ndiyo maana nasema ushabiki umekuwa kama wa timu za mipira-akili na busara watu wanaziweka pembeni.
Sitaki kuandika gazeti humu, ila nipo tayari kurudi tena na kuelewesha sehemu yeyote yenye utata.
Ahsanteni.
Aliyekataza kumsema Mkapa ni fisadi mwenzie kikwete. Namnukuu akisema, "waacheni wazee wastaafu kwa amani". Kan kwamba hiyo haitoshi, Wikileaks imetuonyesha wazi kuwa Kikwete amempa amri Hosea wa PCCB kutokufatilia ufisadi wa akina Mkapa na Sumaye. Sasa udini hapa uko wapi ikiwa Kikwete ndio anakataa scrutiny siwepo kwa hawa mafisadi wenzie? Narudia tena na tena. Risasi iliyomuua muislamu marehemu Ismail kule Arusha, iliamriwa kupigwa na muislamu mwenzie Said Mwema (IGP) na akapata support ya kifedhuli toka kwa waislamu wengine kama Makamba na Tambwe Hiza. Udini upo wapi hapo? Mbona Meya anayetakiwa kujiuzulu Arusha ni mkristo tena mkatoliki kama mnavyosema CHADEMA ni ya wakatoliki? Mbona alisemwa Lowasa ambae ni mkristo mpaka alijiuzulu uwaziri mkuu? Udini upo wapi ikiwa watanzania wa dini zote wanakabiliana na mfumuko wa bei kwenye kila sekta ya uchumi wakati hata uyo fisadi Mkapa alirekebisha hili la mfumuko alipokuwa madarakani? Tatizo la wafuasi wa CCM kama Aikaotana mnaakili "brand new". Namaanisha hamzitumii kabisa katika kutoa misimamo yenu ndio maana bvado mpya. Hebu anzeni kuzitumia jamani maana mnatia aibu.
wanachosema kwamba, maaskofu wameuliwa wapemba na mwembechai walipongeza ccm. lkn arusha waliilani ccm. eti maaskofu huangalia nani kakaa Ikulu. yaani mkatoliki au muislam
katika misa moja chuo kikuu cha da, Pengo alisema cuf ndio wa kulaumiwa, alisema watu wa nje wanatumiwa na Cuf. lkn kwa chadema na arusha atoa kombora zitohakuna Askofu aliyeipongeza CCM kwa mauhaji ya Pemba na Mwembechai, wala Hakuna Askofu anayeilaani CCM kwa mauhaji ya Arusha
wanachosema kwamba, maaskofu mwembechai walipongeza ccm. lkn arusha waliilani ccm. eti maaskofu huangalia nani kakaa Ikulu. yaani mkatoliki au muislam
Sure na kama kuna ushahidi wa maaskofu kupongeza hayo mauaji ya pemba tuleteeni tuonehakuna Askofu aliyeipongeza CCM kwa mauhaji ya Pemba na Mwembechai, wala Hakuna Askofu anayeilaani CCM kwa mauhaji ya Arusha