Mara zote mimi nimekuwa napiga vita hisia za udini zinazoendelea kujengeka Tanzania. Kwa nyakati tofouti kama leo nalazimika kuandika kile nisichokipenda kukijadili, lakini kwa faida yetu sote ni lazima tuwe wakweli na weledi.
Ndugu Rutashubanyuma, kauli mbiu yako ni kuwa wewe ni public policy analyst, na ninaanza kuingiwa na shaka juu ya hili hata kama ni kweli.
Kama wewe ni Mtanzania, basi utakuwa hujaipitia vema historia ya nchi yako. Nukta yako ya tatu inanitia wasi wasi kama kweli una nia njema na nchi hii ya Tanzania unayoishi.
Kwanza naomba urejee miaka 23 ya Mwalimu Nyerere uwiano ulikuwaje ili ujenge hoja ya uwiano wa sasa.
Pili, viongozi hawachaguliwi ili kuongoza dini, wao ni public servants, sijui unataka kutuaminisha nini juu ya uteuzi wa viongozi.
Tatu, mbona hujaangalia huko nyuma Nyerere,Mwinyi,Mkapa uteuzi ulikuwaje ili utupe ulinganifu na huu wa sasa.
Nne, Suala la kadhi limeanza kitambo lakini ni wakati wa mkapa ndipo liliposhika kasi, sijui kama unajua aliyeibua hoja ya kadhi na kuifanya agenda ya uchaguzi Ni A.L.Mrema akimtumia sheikh mtopea.!!!
Tano, Mkapa alifanya nini kama kiongozi wa Chama kuzuia hoja ya Kadhi isiingizwe ndani ya ilani 2005. Iweje suala lililopata baraka za chama leo liwe la JK peke yake. Je nani aliandaa ilani ya ccm 2005, na kwanini halmashauri kuu na CC ziliafiki suala la kadhi.
Sita, Suala la OIC lilianza miaka ya akina Mwinyi na Malecela, na kama unakumbuka hili ni miongoni mwa mambo yaliyozaa G55 na hatimaye Mzee Malecela kuwekwa pembeni katiak u-PM. Suala hili liliendelea wakati wa Mkapa, je yeye alilishughulikiaje? na kwanini leo ionekane ni agenda ya JK ili hali viongozi wawili [miaka kumi kumi] hawakulishughulikia!
Napenda kuweka wazi kuwa sijengi hoja kujibu au kufanunua hoja za Gazeti la Tanzania au JK, ninachokifanya hapa ni kutaka kuwafahamisha wana forum wenzangu kuwa ni vema mtu akatuliza akili kabla hajaandika na kuhukumu, na kuwa hizi thread za kidini zisizo na mantiki zinataka kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini, jambo la kipumbavu sana kama alivyowahi kusema mwalimu Nyerere, na sijui kama wanaoandika ni watanzania kweli au ni watu wanaotaka tuingie katika machafuko kama ya Rwanda, Burundi au Nigeria.
Kuna msemo unasema [tafsiri isiyo rasmi] '' Kama hujui jambo ni bora ukae kimya, maana unaweza kusema na kuwatoa watu mashaka waliyokuwa nayo dhidi yako''
Mwisho, mkuu Rutashubanyuma, wewe kama analyst hebu wape ma analyst wenzako hoja hii wakusaidie. Mimi simwangali kiongozi kwa misingi ya dini yake bali uwezo wake. Simwangalii mtu kwa dini yake bali utu wake. Dini zinazoongelewa sijui ni zipi maana mzee Kingunge hana dini, je huyu hapaswi kuwa kiongozi eti kwasabau si mwislam au Mkristo.
Rutashubanyuma, nikuulize kama unajua historia ya nchi yetu, je Mkwawa alikuwa dini gani, je Kinjekitile alikuwa dini gani, Rumanyika na Mirambo walikuwa dini gani. Kama unaamini ukristo na uislam ndiyo dini pekee, nitakuomba urejee tena darasani. Tukiendekeza mambo ya kijinga ipo siku tutawakana ndugu zetu eti ni wapagani. Lakini Pia Rutashabanyuma unapaswa kutueleza, iwapo wizara au idara X ina watu wa dini fulani, je kuna faida gani inapatikana hapo.
Ahsante. Nguruvi3, mchukia thread za udini.