Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Hata mimi nashangaa, JK na Makamba Ndo waliohubiri dini wakati wa kampeni sasa wanataka kutuambia nini, maanake mimi nikimwangalia kisaikolojia nagundua ni kama anahisi sisi wananchi tumeshayajua mambo maovu ya udini waliyokuwa wanafanya wakati wa kampeni sasa dhamira yao inawasuta.

Ukimwambia JK atoe ushahidi wa nani alihubiri udini utakuta moja kwa moja ni yeye na CCM, sahivi anaogopa mambo yanaweza kuwa mabaya.

Mimi namshangaa, embu angalia jamaa katika uteuzi wake, ni watu wa dini yake alafu anakuja kutuambia nini, na washikaji wake bila kuangali hata kama ni wachafu kiasi gani.

Watanzania tusikubali huyu Mkwere atugawe kama ambavyo amekuwa akihubiri siku zote.
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.
Hii dhana ya Serikali tuelezane kwa mapana yake, kwani serikali ni nini? Palestina hawaitambui Israel lakini kwenye mazungumzo ya kuleta amani Mashariki ya Kati wanakaa meza moja na Israel, hii Maana yake nini!!?
 
- Wakuu kuuliza si ujinga ninauliza hivi: Chadema wana tatizo na NEC kwa sababu kikatiba ndio wenye mamlaka ya kuamua nani awe Rais kutokana na kura za wananchi walizonazo mikononi,

- Au wana tatizo na Rais kwa sababu amewaibia kura ambazo zinaonyesha kwamba Dr. Slaa ndiye aliyeshinda U-Rais?

William.

William,

Mie mwenyewe nilikuwa sitaki kulifuatilia hili suala hili sasa nataka kujua

1.Hivi Dr. Slaa ameshinda kwa kura ngapi?(kwa mujibu wa CHADEMA)

2.WAnchotaka kwa Kikwete ni nini?

labda wakiaddress vizuri JK atawapa ila kuendelea kumpinga tu itachukua miaka mitano
 
NILISHTUSHWA NA KAULI ZAKE KUHUSU UDINI, KIKWETE NI MCHOCHEZI! MBONA SISI WANANCHI WENYEWE HATUJUI KAMA KUNA TATIZO HILO, MIMI NAONA KWA SABABU YEYE ANA HIYO ROHO YA UDINI NDANI YAKE NA ILIVYOMKOLEA NDIO MAANA ANADHANI KILA MTU YUKO HIVYO, KWELI NAWAPA POLE WALIOMCHAGUA ETI RAIS, RAIS UNAKUWA MCHOCHEZI!!:nono::nono::nono::nono::nono:
 
lets wait and see!!jinsi atavoshughulikia "ilo swala"alilolisema
 
Mpaka hatua hii siwezi kumlaumu tusubiri tuone wakikamilika kumi watakua vipi Japo hata kama labda wakisto watakua wachache sizani sana kama ni issue ya kukomalia cha msingi watakao chaguliwa wasilete udini wala wasiunge mkono sera zozote ambazo zitakuwa zinalipeleka taifa kwenye udini.
 
Usiyeelewa zaidi ni wewe ambaye umeshindwa hata kusema nisipoelewa ni wapi.

Hatuimbi chorus hapa.

kuna post no 128 jamaa kasema wewe ni empty can. we huon hoja unazoleta hapa hazina mashiko!!

yes wewe ni emmpty can
 
Tena hata hiyo jana alipokuwa anaitaja serikali yake, aliwataja viongozi wa kislaam pekee, kwani huyo waziri mkuu PINDA sio sehemu ya serikali yake?? kwanini hakumtaja?hii inamanisha yeye ndo analeta udini kwenye nchi yetu.
 
MSG sent to donors bse wengi watajiuliza hasa mabalozi ambao walikuwa arround.
Na donors wakikomaaaaaaaa CCM watanyoka bse ata Nyasi tutakula ili mradi haki inatendeka
 
Mbaya zaidi kama anaweza kufikia hatua kuweka demokrasia mezani na kuichezea atakavyo ni sawa na kutawala kinyume na matakwa ya watu utawala huo hauwezi kuwajibika kwa watu bali kwa waliouweka ambao ni mwanzo wa matabaka ni migawanyiko hatima yake ni uharibifu.
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.

Wewe umeathirika na Ufisadi au si mtanzania halali unatuibia hapa waTZ tumeshsamka.
 
Sikiliza audio vizuri, soma katiba, tafakari. ndio utagundua CHADEMA wako sahihi. Hata Madikteta nao ni marais.
 
kuna post no 128 jamaa kasema wewe ni empty can. we huon hoja unazoleta hapa hazina mashiko!!

yes wewe ni emmpty can

Afadhali mie empty can, wewe ni "empty can't"
 
CCM ndio waanzilishi wa hoja za udini (eg hoja za OIC & Mahakama za Kadhi), watu wengine waki-react wanajivua magamba kama nyoka na kujifanya ni watu safi wanaostahili kukemea udini!

Huyu Msanii Aache Usanii, CCM ndio wadini wakubwa na hii ndio agenda yao ingawa wanataka kujificha uli wasijulikane.
Kilichofanyika katika speech yake ya udini ni Pre-emptive stike ili atakapoendeleza sera zake za udini (eg hoja za OIC & Mahakama za Kadhi) asitokee mtu kumpinga ili asijekuwa branded Mdini.

Aache kulialia, Akitenda haki hakuna atakaemwandama, lakini akiendeleza dhuluma lazima waonaji watasema na kukemea.

Historia itamhukumu huyu mtu kwa kutaka kuiharibu Tanzania kwa sababu ya udini wake uliokithiri.
 
Nchi haitawaliwi kiivyo! The man will be in trouble all the times because he is taking wrong steps each time! Namsikitikia mwalimu wake aliyemfundisha pale pugu! Jamani mwenye kujua education background ya huyu mweshimiwa tujuzeni hasa perfomance yake ya degree ya kwanza maana siamini mambo anayoyafanya! Subirini mtaona madudu yatakayofanyika awamu hii! Jamani watanzania hivi hatuna macho! Jamaa mweupe kabisa! Anasema MDG ndo vision ya Taifa! Jamani kama taifa halina vision yake linasubiri wazungu walipangie dira na raisi anarihutubia bunge kwa dira hizo bila kuweka bayana nini dira ya taifa kama taifa ambayo kimsingi itakuwa tofauti na MDG ukizingatia MDG ni ya watu waliotutawala na fikra zao bado zimekaa kikoloni! Kama mnakumbuka kwenye mkutano wa kupima achievement za MDG 2010 ilionekana nchi fadhiri haziko serious kuona MDG inafanikiwa bado rais na wabunge wa ssm wanashangilia! Hivi tatizo ni nini sisi watanzania!
 
1. Kura ilikuwa ya siri, habari ya nani alipiga vipi kura ni propaganda, Hata wabunge wenyewe hawajui wenzao walivyopiga kura. Kila mtu anajijua yeye tu alivyopiga kura.

2. Hata ukipiga kura ya Hapana, maana yake unakubali Pinda alistahili kupigiwa kura, maana yake unakubali aliyependekeza jina la Pinda ana mamlaka ya kupendekeza hilo jina, maana yake Kikwete unamtambua kama rais.

Sasa CHADEMA washamtambua Kikwete kama rais, halafu wanataka kusema hawamtambui, wanatuchanganya.

Kina Tundu Lissu na Mnyika si walitoa madukuduku yao kuhusu uchaguzi wa PM? Si walisema habari za serial numbers and all? Mbona hawakusema aliyeleta jina si rais tunayemtambua kwa sababu hii na ile ?
Hoja yako ni nzito na ina Mantiki, lakini katika siasa si kila kitu kinapelekwa kama kwa kufuata kanuni za hisabati. CHADEMA wanawakilisha wananchi wa majimbo na Pinda kachaguliwa na wananchi wa Jimbo lake. Wanachopinga CHADEMA ni mfumo uliotumika kumpata Rais lakini hawampingi Rais mwenyewe. kitendo chao ni kumuonesha Kikwete kwamba wewe ni Rais lakini hukupatikana kihalali.
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.

Abraham Lincolin The father of Democracy alipata misukosuko ya hapa na pale ili kupata Democracy ya kweli, sio kazi rahisi kupata uhuru wa kweli, siku moja utafahamu ni nini kinaongelewa hapa, ni mapambano kuelekea Democracy ya kweli sio chenga chenga tunazoziona sasahivi,
nafikiri tunapaswa kuishi karne ya 21 na siyo kurudi nyuma tena. i thought you'll be the one to support! mapambazuko ndiyo hayo, endelea kufuatilia yanayotokea.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom