Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Nchi haitawaliwi kiivyo! The man will be in trouble all the times because he is taking wrong steps each time! Namsikitikia mwalimu wake aliyemfundisha pale pugu! Jamani mwenye kujua education background ya huyu mweshimiwa tujuzeni hasa perfomance yake ya degree ya kwanza maana siamini mambo anayoyafanya! Subirini mtaona madudu yatakayofanyika awamu hii! Jamani watanzania hivi hatuna macho! Jamaa mweupe kabisa! Anasema MDG ndo vision ya Taifa! Jamani kama taifa halina vision yake linasubiri wazungu walipangie dira na raisi anarihutubia bunge kwa dira hizo bila kuweka bayana nini dira ya taifa kama taifa ambayo kimsingi itakuwa tofauti na MDG ukizingatia MDG ni ya watu waliotutawala na fikra zao bado zimekaa kikoloni! Kama mnakumbuka kwenye mkutano wa kupima achievement za MDG 2010 ilionekana nchi fadhiri haziko serious kuona MDG inafanikiwa bado rais na wabunge wa ssm wanashangilia! Hivi tatizo ni nini sisi watanzania!

Ana degree moja tu ambayo ni ya uchumi.alipata pass point 2.1
 
Hivi msimamo wa Serikali juu ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Khadhi ikoje? Mchakato wa kuanzisha hiyo mahakama umefikia wapi? Tafadhali mwenye data...!
 
Kikwete ni mnafiki,wakati wa kampeni bado alikuwa rais,ni kwanini asingekemea magazeti na redioi ile ya morogoro iliyokuwa inahubiri kutokuwachagua watu wa dini nyingine.Kama anajua fulani anahubiri udini katika siasa ni kwanini asimuenye moja kwa moja badala ya kuzunguka?
 
udini tanzania upo sana, yote hayo yanatokana na ignorance tuu... watu hawajui ata hizo dini zilitokea wapi! There is no way you can make me see my fellow countryman as less than someone from elsewhere with the same religion as me. That is brainwashing and we should say no to it. We are one, our problems are the same, our environment is the same, division has no meaning except one, foreign forces aim to : divide and rule. That is why China strongly rejects foreign religions encroaching on their population, simply because it negates rationality.
 
Kikwete ni mnafiki,wakati wa kampeni bado alikuwa rais,ni kwanini asingekemea magazeti na redioi ile ya morogoro iliyokuwa inahubiri kutokuwachagua watu wa dini nyingine.Kama anajua fulani anahubiri udini katika siasa ni kwanini asimuenye moja kwa moja badala ya kuzunguka?
Radio gani hiyo ya morogoro ilikuwa inahubiri watu wasichague mtu wa dini nyingine? pia, ni lini Kikwete alishawahi kuwakemea wale watu wa RAdio Kheri na magazeti ya al nuur ambayo yanaongea udini wa waziwazi? sasa tuseme mdini ni nani, yeye au? manake kwa wakristo amewakamata masikio wachungaji, wawe wanamwita yeye ni chaguo la Mungu, hakuna shehe hata mmoja alishawai kusema kikwete ni chaguo la mungu au slaa ni chaguo la Mungu...kikwete angekuwa mkristo,tungesema wachungaji na maaskofu wanahubiri udini...lakini yeye ni mwislam....tuseme nini hapo sasa?

atayakumbatia magazeti ya kiislam yanayohubiri udini na radio za kiislam, na wale watu wa Muslim brotherhood wanaoendeza udini tz (baada ya kufukuzwa Misri nchi ambayo ni ya kiislam lakini imewakimbiza?)
 
Ukitaka kumjua mtu aliefilisika sera kiurahisi atapenda kuzungumzia udini-udini au ukabila. huyu ndio baba riziwan.
 
Sioni kama ilikuwa ni ushujaa wowote kwa sababu waliondoka ukumbi wa bunge na wakenda ukumbi mwingine kumwangalia kupitia luninga-Is a kindly shameful too!

Nakusikitikia ... ubongo unao, kuutumia inakuwa tabu. Pole !!
 
Naona jambo la kusikitisha kuliko vyote ni kwamba kiongozi Mkubwa kama yule si vizuri kuwaaminisha watu kuwa kuna Udini, Namimi naamini mtu anapoliona baya kwa mwenzake ni kweli kabisa huyo mtu ana tatizo la namna hiyo.... Na huu tunauita unafiki..... Kwa taarifa yake Mr. Prez ....... kati ya misingi Bora ambayo Mwalimu aliweka tangu kupatikana kwa TANZANIA nasisitiza TANZANIA ni kwamba hatuna Udini ana jambo la kwanza ni kuwa aliweka mbali kabisa na siasa kwa kuwa alijuwa kuwa Siasa ni Divisive in Nature sasa hakutaka kulichanganya na hili. I wonder If the guy is really ever a Mwalimu student as He has claimed

He was wrong during the campaign and He is wrong now....... Akubali ili tumuone kwamba ni Mwanaume aliyekua Kiakili na Kifikra
 
Mungu anisamehe, mi kikwete namuona ni mtu hatari sana. Yeye kaanzisha issue ya udini. Ukiacha CUF ni ccm peke yake imetumia dini kama silaha ya kupambana na chadema. Huyu bwana anaendelea kutaja dini kama njia ya kupambana na chadema.

Mi naona kapotea. Wafuasi na wanachama wa chadema ni watu tofauti sana, wana uwezo wa kuchambua mambo kabla ya kupokea maoni tofauti na wafuasi na wanachama wa ccm. ccm hawawezi kuchambua pumba na facts, akishaongea kikwete wao wanaamini. ni watu wa kupokea maagizo na hoja bila wao kuzichambua kuwa ni kweli au la.

Kwa hali hiyo Chadema ni chama makini na kitafika mbali katika harakati zake za kupigania haki na maslahi ya watu wote kwa ujumla.

Kwa wafugaji mnaweza kunielewa ukiwa na mfugo wako una matatizo. jinsi ya kuutibu mfugo wako lazima kutumia nguvu kuufunga na kama utautibu kwa kutumia sindano, utafanya hivo. mwisho wa siku ndo utajikuta mfugo wako umepona. Ndivyo ilivyo kwa wana ccm wanaopinga vyama vya upinzani esp. chadema, kwani vina fanya mambo kwa maslahi ya wa Tz lakini wao ccm hilo hawalioni kwa sasa.

Blavo Chadema, endelea kushika kasi kwa maslahi ya watanzania wote, wale wanao wapinga ni kama mifugo ikiwa inaumwa, tunatumia nguvu kuifunga kamba ili tuitibu na baadaye ikipona faida inaonekana baadaye.
 
<p>
Sioni kama ilikuwa ni ushujaa wowote kwa sababu waliondoka ukumbi wa bunge na wakenda ukumbi mwingine kumwangalia kupitia luninga-Is a kindly shameful too!
</p>
<p>&nbsp;</p>
Hakuna mbunge aliyekwenda ukumbi mwingine kuangalia luninga wote walitoka nje wakongea na waandishi wa habari kidogo baadae kila mtu akaondoka zake,
 
kwa hapo chini

NO COMMENTS



Mpeni sifa Yesu
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
user-online.png
JF Senior Expert Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join DateSun May 2010LocationDar es SalaamPosts382Thanks1Thanked 148 Times in 83 Posts Rep Power21kwa hapo NAFUNGA MDOMO WANGU
 
Unachozungumza hukielewi, kwanza kama unamjua Adam Mwakanjuki, huyu ni mkristo na ameshakuwa waziri katika SMZ kwa miaka isiyopongua 10, na wengine wapo..., (naomba laki yangu kwa hili). Pili mazingira ya Bara ndugu yangu tofauti na znz? zanzibar wakristo walio wengi hawana sifa za uzanzibari, sio kuchaguliwa kuwa mawaziri bali hata kupiga kura hawakubaliki, unategemea nini hapo? kwa ufupi wakristo wa znz walio wengi ni wageni ambao kisheria wanaruhusiwa kuishi na kufanya kazi zao tu, lakini ili waweze kushiriki chaguzi za znz ni lazima watimize masharti ya kuwa wazanzibar ambayo wengi hawayawezi kwani ni magumu kwa mtu anayependa kwao (Tanganyika). Soma katiba ya Zanzibar ujue hayo masharti.
 
Sioni kama ilikuwa ni ushujaa wowote kwa sababu waliondoka ukumbi wa bunge na wakenda ukumbi mwingine kumwangalia kupitia luninga-Is a kindly shameful too!

Unatakiwa kufikiri kwanza kabla ya kuropoka, Mungu akusamehe maana hujui uyanenayo
 
It was an ACT of confidence that is very true but for how long is this going to last? Mwisho wa siku sie wananchi tutaumia sana kusipokuwa na umoja huko bungeni, we are damned!!
 
Tunachotaka ni huduma bora za afya, maji, elimu, umeme wa uhakika,matumizi mazuri ya rasilimali alizotupa Mwenyezi Mungu,uwajibikaji wa viongozi kwa umma. Nilitegemea Rais kama mtu mwenye mamlaka na dhamana kubwa angetaja moja kwa moja kwamba ni nani ni mdini na ushahidi upi na amtangazie adhabu hapo hapo at least up to his mandate!No research no right to speak, he is not exceptional to this rule. Otherwise mi naona ni kama habari 'light' isiyo na back-up.
Kila mtu mwenye akili nzuri anajua ufisadi hauna dini! Na asiyepambana na hili means that he is not pulling with patriots.
 
Kitendo cha kishujaa? hapana! JK hajatisha kiasi cha kuwa kiwe kitendo cha kishujaa, wala chadema sio WEAK kiasi cha kuwa JK awe goliath

Katiba itabadilishwa na NEC itabadilishwa na CHADEMA wametumwa na watanzania wote hata na wana ccm wenyewe bila wao kujijua!!!

No coming back aluta continue!!
 
ndio nani huyo jamani? na angalia kwa cabinet hii ya sana na ya awamu ya karume, tutajieni tuwaone walikuwepo kina nani?hakuna sehamu yenye udini wa kuwabagua wakristo kama ilivyo zanzibar.

Babake Wema sepetu...
 
Unachozungumza hukielewi, kwanza kama unamjua Adam Mwakanjuki, huyu ni mkristo na ameshakuwa waziri katika SMZ kwa miaka isiyopongua 10, na wengine wapo..., (naomba laki yangu kwa hili). Pili mazingira ya Bara ndugu yangu tofauti na znz? zanzibar wakristo walio wengi hawana sifa za uzanzibari, sio kuchaguliwa kuwa mawaziri bali hata kupiga kura hawakubaliki, unategemea nini hapo? kwa ufupi wakristo wa znz walio wengi ni wageni ambao kisheria wanaruhusiwa kuishi na kufanya kazi zao tu, lakini ili waweze kushiriki chaguzi za znz ni lazima watimize masharti ya kuwa wazanzibar ambayo wengi hawayawezi kwani ni magumu kwa mtu anayependa kwao (Tanganyika). Soma katiba ya Zanzibar ujue hayo masharti.
sasa kuna umuhimu gani kuwa na muungano huu, kwanini tusiwe tu na tanganyika na zanzibar? kwasababu wazanzibari wakija hapa bongo wanapata haki zote, wabara wakienda zenji hawapati haki zote, hawa watu wanatusaidia nini sasa sisi wabara?
 
Jamani,hivi udini ambao mr. prezzo ametangaza mbele ya bunge kwamba tz imeanza kugawanyika kwa udini, upo wapi uo udini? ktk uchaguzi udini ulikuwa wapi?, si angemention tu kama kidonda kipo kipone?...kwasababu hatujaona watu wakimchagua mtu kwa udini wake, bali kwa sera, hasa ukichukulia vijana wengi wakristo kwa waislam walimpigia Dr.slaa au Lipumba. udini uko wapi? ange mention chama basi tujue.

kwasababu kama ni udini, ccm haina balance kabisa ya dini, basi ccm ndo alikuwa anaiongelea kuwa ni ya kidini. pili, uteuzi wa wabunge wale wa mwanzo wote walilalia upande wa dini moja, kuanzia zakia mehgi ambaye wananchi hawampendi lakini kikwete anampenda. wale wawili za zenji pia mtu mwingine angefikiri kuwa ni udini, lakini hakuna mkristo hata mmoja aliyelalamika kuhusu udini, kwasababu tz hatujali sana udini kwenye selikali.

angalia, mbona rais, makamu wa rais mara zote mbili ni wa dini moja, lakini hilo haliko mioyoni mwa watu, udini ni tatizo kweli hapa tz kiasi cha president kulitangaza mbele ya bunge?

Nijuavyo mimi, yaliyomjaa mtu moyoni ndiyo atakayoyaongea. kama mtu ni mdini, ataongea sana udini tu. pia, wakati mwingine, hata kama wananchi hawakuwa wadini, sasa kwasababu mr.president amelitangaza, atawa alart wananchi waanze kuwa wadini. hivi mr. president anajipanga kwanza kabla ya kuongea hotuba kweli au anazima moto?

Zanzibar ni lini hata siku moja Mkristo alishawahi kushika madaraka, kwani zenji hakuna wakristo? lakini sisi wakristo hatulalamiki...NITAJIENI KIONGOZI YOYOTE HATA WAZIRI TU WA KIKRISTO AMBAYE ALISHAWAI KUPEWA MADARAKA ZANZIBAR. ukinitajia nakupa laki hapahapa...hayupo

MKUU naomba kuwakilisha !

Brigedia Adam .C. Mwakanjuki huyu alikuwa ni waziri serikali ya Zanzibar katika wizara ya mawasiliano na uchukuzi kwa muda Mrefu tuu from 2006 not sure kama mpaka sasa !
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom