Mi nadhani ni vyema Rais wetu (tutake tusitake) akaacha kampeni baada ya uchaguzi, sula la udini aliliibua yeye (na wenzake katika chama chake) kama silaa ya kupambana dhidi ya wagombea wa chadema! jambo ambalo hata hivyo aliingii akilini ikichukuliw kwamba, wagombea, wanachama na wapenzi wa vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi walikuwa dini mchanganyiko na hivyo kushindwa kuelewa jinsi walivyokuwa wakiendesha kampeni za udini kama ilivyodaiwa.
wengi tulijua hayo ni mambo ya kampeni, uchaguzi ukipita yataisha maana hakukuwepo udini katika kampeni kwa sababu nyingi tu zilizowahi.
KWANZA, ungekuwepo waliokuwa wanaundekeza wangechukuliwa hatua si kukemewa tu, kwani ni kosa kisheria kubagua watu kwa misingi ya dini.
PILI iweje wanachama na wagombea wa dini tofauti watumie udini kutafuta ushindi dhidi ya wagombea wa chama ambacho nacho kimesheheni wanachama na wapenzi wa ni dini tofauti! Kwani wana CHADEMA si mchanganyiko wa waisilamu, wakristo, na hata wahindu? hali kadharika na CCM si wamejaa wakristo, waisilamu, na dini nyingine? sasa chama au mgombea atakayetumia uislamu wake au ukiristo wake atategemea kupata wapi kura maana atakuwa anawabagua hata wanachama wake.
suala kwamba mgombea urais wa CHADEMA alikuwa mkristo na kwa bahati mbay au nzuri aliwahi kuwa kiongozi wa kanisa, wakati wa CCM na CUF walikuwa waislamu haiweza kujenga hoja kwamba Chadema au waliokiunga mkono waliendesha kampeni za kidini, maana kwa kufanya hivyo wangejipotezea kura za wale ambao hawakuwa wakristo, wengine ambao wako ndani ya chama hicho au ni wapenzi na mashabiki wake. , na kusema kweli kila mgombea, awe wa CCM, CHADEMA na hata CUF waliungwa mkono na wapiga kura wa dini zote.
suala kwamba kuna baadhi ya viongozi wa kanisa walikuwa wakionya wananchi kutounga mkono na kupigia kura wasiokuwa waadilifu, wala rushwa na mafisadi, si udini hata kidogo!, kwani wagombea wa CCM ndiyo mafisadi, wasiokuwa waadilifu na wala rushwa?! hata kama wamo si wote na hiyo haiwezi kujenga picha kuwa anayepinga wagombea wa aina hiyo anapinga wagombea wa CCM peke yao kwa sababu za kidini!
Kwa CCm kuendelea kukumbatia kwamba waliokuwa wakilengwa na viongozi wa dini walipoonya wasichaguliwe mafisadi ni wagombe wao (CCM) ni kudhiirisha kwamba hata wao wanajijua hivyo kwamba wengi wa wagombea wao ni mafisadi na wasiokuwa waadilifu, na wala kamwe huo si udini.
nilidokeza kwamba wengi tulichukulia ni mbinu (japo chafu) wakati wa kampeni na kwamba uchaguzi ukiisha hatutasikia tena madai hayo kwa kuwa si mara ya kwanza CCM na wagombea wake kuibua madai kama hayo, huko nyuma walioelekezewa mashambulizi walikuwa CUF ambao kwa wakati huo walikuwa tishio, licha ya kuwa wagombea wote - rais na makamu wake (mwaka 2005) wa CUF na CCM walikuwa waislamu, lakini bado CCM ilidai CUF ilikuwa ikitumia misikiti kuwataka waislamu wawachague wagombea wasiokuwa waislamu, (sasa hapo sijui wao - CCM wagombea wao wakati huo walikuwa wakristo na sasa wamegeuka na kuwa waislamu!) ndiyo maana tukasema zilikuwa mbinu (chafu) za kampeni za kutaka kuonewa huruma na kupakaziana.
hata hivyo kwa kuwa sasa Rais wetu ameendelea kushikilia msimamo wake huo hata baada ya uchaguzi, wengine tunaanza kupata wasiwasi, kwamba pengine udini ulikuwepo kabla, wakati na hata sasa baada ya uchaguzi.
kama si chadema kushiriki dhambi hiyo na hivyo kuhatarisha mstakabari wa taifa letu, na kama ni hivyo ni jambo la kushangaza kwa mkuu wa nchi kuendelea kulalamikia jambo kubwa kama hilo. alipaswa kuwa ameagiza vyombo vyake kukusanya ushahidi na wahusika kupelekwa katika vyombo vya sheria.
Vinginevyo asitufanye tukaamini kwamba pengine CCM (uongozi wa sasa au yeye na wenzake) ndo wadini, wameshaanza kuendesha nchi kwa misingi ya dini, wameshiriki uchaguzi kwa misingi ya dini, au wana mpango wa kuendesha nchi kidini katika ngwe hii yao ya mwisho.
na hivi visingizio, kelele na tuhuma ni kuficha nia zao ili wananchi wakengezwe na madai hayo waione ya kwao.
sitaki kuhesabu viongozi wasilamu na wasiokuwa wakristo walio katika nafasi mabalimbali ambao wamewekwa au wameingia katika nafasi hizo kipindi cha serikali ya awamu ya nne, maana hicho si kipimo cha udini, bali kama huo ni mkakati hilo ni jambo lingine.
na vilevile najizuia kuhoji kuridhika(kunyamaza) kwa waslamu kipindi hiki, ambao katika chaguzi zilizopita walikuwa mstali wa mbele kutetea maslahi yao hususani mahakama ya kadhi hadi kutishia kutopigia mgombea wa CCM, japokuwa kwa wakati huo sula hilo lilikuwa moja ya ahadi za CCM na mgombea wao na ilikuwa nadani ya ilani.
sasa pamoja na kutotekelezwa waislamu katika uchaguzi huu wametulia tuli!.. kwa vyovyote wana hakika kwamba mambo yao yatanyooka. ni vema rais wetu akawaeleza umma wa watanzania ni yapi wamekubaliana na waislamu kiasi cha kuwafanya watulie wala wasilete chokochoko kipindi hiki, vinginevyo hatuwezi jua ni nini wamekubaliana! usiri huu na kuendelea kupakaziana udini kwa wapinzani wao inaweza ikawa kichaka cha kuleta mambo yasiyokubalika kwa mpenda amani hapa nchini, awe muislamu au mkristo. ni vyema ikajulikana nani anadai nini na ameahidiwa nini ili akitekelezewa asije mtu kuuliza kwamba hapo vipi!