Ni nani aliyewaambia na kuwadanganya Wamisri kuwa wana umiliki wa 87% ya maji yote ya Mto Nile?

Ni nani aliyewaambia na kuwadanganya Wamisri kuwa wana umiliki wa 87% ya maji yote ya Mto Nile?

Cha kulaumu zaidi ni yule aliyetunyima akili, ni sawa na swala au pundamilia waanze kujilaumu huko porini kwa nini wanaliwa na Simba. That's nature my dear, lazima viumbe tutegemeane. Ulishawahi kujiuliza hivi hao wazungu kwa mfano waamue kuacha kuchukua dhahabu huku Afrika au madini mengine ambayo unasema yana thamani, utayafanyia nini? Hiyo thamani unayoiona wewe kwenye madini imesababishwa na hao wazungu la sivyo sisi tungekuwa tunayaona kama mawe tu.
Hakika mkuu wkt mwingine inabidi tukubali tu viumbe hai huishi kwa kutegemeana aisee in history si tunaambiwa wazee wetu huko Geita dhahabu walikuwa wakichezea Bao[emoji28]vitu vingine tunashupaza shingo tu ila ukweli tunaujua!!
 
Misry, kenya na tanzania ndio watakaoshinda. Na ethiopia hawezi bila msaada wa nduguye myahudi

Tanzania wanaweza vita na mbowe tu uko kwengine tusijalibu yani Tanzania hii hii ya kina sirro [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nilipoona tu tamko la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likisema kuwa haliwezi Kuingilia kati Mgogoro wa Matumizi ya Maji ya Mto Nile kati ya nchi za Misri na Ethiopia kwakuwa inajua kuwa Misri ina uhalali wa 87% ya Maji ya Mto huo nimeshtuka na kuwa na maswali mengi mno.

Hivi ni lini Waafrika na hasa huu Umoja wa Afrika (AU) utasimama imara kabisa Kutetea na Kusimamia Maslahi ya Bara la Afrika na Rasilimali zake kwa ujumla? Kwanini iliyokuwa (OAU) miaka ya nyuma ilishindwa kuwa Sauti ya Kujiamini kwa nchi zote za Afrika ili Afrika tusikike, tueleweke na tuheshimike mno.

Hainiingii Akilini kabisa leo hii kusikia nchi kama za Misri na Ethiopia kila Uchao tu zinagombania Umiliki wa Mto Nile wakati sehemu Kubwa na iliyoanzia hadi hata kupita nchi kama za Uganda na Sudan nazo zina haki ya Umiliki lakini zimenyamaza na zikiwaangalia kama hata si Kuwashangaa pia.

Wazungu wanapenda sana Kutuingilia na Kutupangia mambo yetu mengi Waafrika na kwa jinsi Viongozi wengi wa Bara la Afrika walivyo Goi Goi na wa hovyo hovyo kiasi cha Kuwaogopa Wazungu hawa Waafrika wote tunadharaulika na kuonekana hakuna tunalolijua na hata kuliweza zaidi ya kuwa Waongo, Wavivu na Wachawi wa Kutukuka.
Wapuuzi hao, wahuni kabisa, labda kuwa na ma pyramids wanajiona wako superior, silly and stupid Egypt..
 
Back
Top Bottom