Ngoja nikuambie kuu kwanza sio kila mwanaume ni kicheche!
Kuna watu wanakijua kitabu cha MUNGU vizuri mno kwa hio mambo ya uzinzi yako mbali na wao. Hakuna mtu wa MUNGU atakae tembea na mke wa mtu kwani anajua anajitaftia kifo! Hao manabii wa uongo wasiwadanganye kwa mtu anaejua maandiko hawezi tembea na mke wa mtu soma Methali 6:26-29 utanielewa huyo mtu wa Mungu mwenye akili timamu achepuke na mke wa mtu.
Kwa mwanaume mjanja atajiongeza ili ampe mkewe kile anachokihitaji kama hakipatikani basi huyo mke mwema atakubaliana na hali. Tatizo binadamu wamejaa tamaa sana na hawaridhiki na walivyonavyo... Pesa ni tatizo sana kwa kweli na ni chanzo cha maovu yote hapa duniani kwa inafikia mahali binadamu hawatahamini watu wao kwa sababu ya pesa na ndio umalaya uko huko... nimegundua wanawake wengi ni Malaya sio kwa sababu ya mahitaji ya ngono bali fedha na maisha ya starehe.
Mnasema wanaume tunatamani wanawake hilo ni kweli kwa sababu sisi ni dhaifu kwa wanawake, Wewe wajua namna wanawake wanavyopendezesha ulimwengu na pengine ukamtamani mwanamke mwenzako sasa vipi sisi wanaume?
Nategemea kwa mwanamke mwenye akili utajiongeza na ku copy na situation.
Kulingana na uwezo wa mtu wapo wanaotosheka na mke mmoja na wengine mke mmoja hawatoshi kabisa ndio maana wanaweka wazi kabisa kwa wake zao.
Nawashauri sana wanawake muacha tamaa za pesa ridhikeni na uwezo wa waume zenu.