Ni nani anapaswa kujitathimini Kati ya Jeshi la Polisi na Chama cha Mapinduzi?

Ni nani anapaswa kujitathimini Kati ya Jeshi la Polisi na Chama cha Mapinduzi?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Binadamu tumeweka siasa Mbele maisha ya watu na utu wao nyuma. Katika kipindi chote ambacho matendo maovu ya Jeshi la Polisi yanafanyika hakuna aliyewahi kusikia Chama cha Mapinduzi wakikemea.

Tumesikia namna mwanachama wa CCM Bwana Sabaya alivyokuwa anakamata walinz wake nakuwapiga Kisha kuwaweka mahabusu, alivyotesa wananchi na wafanyabiashara Lakini hata siku Moja CCM haijawahi kumkemea.

Leo CCM inasema Polisi wajitathimini. Anayetoa tamko alikuwa DC Arusha akitokea U CCM Iringa, ambapo amewahi kutamka adharani Kwamba flan anapaswa kupotezwa; Leo anasema Polisi wajitathimini.

Uongozi wote uliopo Sasa Ndani ya chama ulikuwepo awamu ya Tano na Polisi walikuwa wanafanya KAZI Kwa kusifiwa sana , watu waleqale waliowasifia Polisi Leo Kwa sababu tu wanataka kumtoa IGP wamweke mtu mwingine wanakuja kumwambia IGP ajitathimini. Wakati anawasiadia kwanini hoja ya kujitathimini haikuwepo?

IGP ana mapungufu yake kama binadamu, ila makosa yaliyofanywa na Jeshi la Polisi IGP apaswi kubebeshwa lawama, lawama zinapaswa kwenda Kwa chama Cha Mapinduzi kinacholielekeza Jeshi la Polisi nini Cha kufanya Kila wakati.

Natambua hivi karibuni utafanyika UTEUZI wa viongozi wapya wa Jeshi la Polisi ikiwemo kuwapandisha vyeo baadhi ya maafisa kulingana na gap linalopigiwa makalele na wanaharakati mitandaoni ila niambiene Kati ya RPCs au wakuu wa vikosi waliopo Polisi Leo Nani msafi kuliko Siro? Je, hao viongozi wamejichafua au mfumo imewafanya wachafuke?

Siro anaweza akakaa benchi kama mlivyopanga ila ninyi pia mnaopanga Siro atoke tambueni anayeingia Hana usafi Kwa sababu mfumo wa chama Cha Mapinduzi ndio unaopanga wananchi wahudumiwe kikatili au wahudumiwe Kwa staha.

Siro kung'atuka siyo suluhu Kwa sababu Kila anayetaka kuishi Ndani ya Jeshi la Polisi atawajibika kumsikiliza Kila mjumbe wa chama cha Mapinduzi.

Jeshi la Polisi imara linategemea katiba inayoweka separation of power. Leo wanasiasa wamekwenda hata kupangua na kupanga Jeshi kubwa Jambo linalotishia ustawi na mipango ya vyombo hivi. CCM jitathiminini upya hasa mnapoingilia vyombo vya Ulinzi kuepusha kuwavunja Moyo askari wetu Kwa kile mnachoita hakuna aliyejuu ya chama Cha Mapinduzi.
 
Ingefaa iundwe sheria ambayo italifanya jeshi la polisi lijitegemee kwa kila kitu,
Ingefaa wakuu wa majeshi na vikosi mbalimbali wawe wanateuliwa na baraza maalum litakaloundwa kisheria na Bunge pamoja na judicial organ, baraza hili pia liwe linamulika matendo machafu ya jeshi la polisi kulifanyia uchunguzi na kulitolea hukumu.
 
Ingefaa iundwe sheria ambayo italifanya jeshi la polisi lijitegemee kwa kila kitu,
Ingefaa wakuu wa majeshi na vikosi mbalimbali wawe wanateuliwa na baraza maalum litakaloundwa kisheria na Bunge pamoja na judicial organ, baraza hili pia liwe linamulika matendo machafu ya jeshi la polisi kulifanyia uchunguzi na kulitolea hukumu.
Bunge hili au bunge lipi unazungumzia?
 
Ingefaa iundwe sheria ambayo italifanya jeshi la polisi lijitegemee kwa kila kitu,
Ingefaa wakuu wa majeshi na vikosi mbalimbali wawe wanateuliwa na baraza maalum litakaloundwa kisheria na Bunge pamoja na judicial organ, baraza hili pia liwe linamulika matendo machafu ya jeshi la polisi kulifanyia uchunguzi na kulitolea hukumu.
Bunge hili hili la Ndugai na Tulia?
 
Bunge hili au bunge lipi unazungumzia?

Sent from my moto g(7) power using JamiiForums mobile app
Ukisema Bunge inamaanisha chombo na sio watu... hao wabunge hawatokaa hapo Milele wataondoka na watakuja wengine walio Bora zaidi... point yangu kubwa hapo ni kuwe na chombo maalum chenye mamlaka inayojitegemea ya kulidhibiti jeshi la polisi.
 


Kwenye hili la jeshi la polisi wa kulaumiwa 90% ni serikali ya CCM na 10% ni lawama kwa jeshi lenyewe.

Ni ukweli usiopingika jeshi letu la polisi lina changamoto nyingi kuliko madhaifu yake, na hata hayo madhaifu yake huchangiwa kwa kiasi kikubwa na changamoto linazopitia.

Tiririka nami.

Serikali ya CCM ilaumiwe kwa kuliingiza jeshi la polisi kwenye siasa. Katika kipindi cha miaka kadhaa nyuma tumeshuhudia mambo ya ajabu na ya hovyo kabisa kuwahi kufanya ama kutekelezwa na jeshi letu hili. Tumeshuhudia viongozi wa chama tawala wakitoa maelekezo kwa jeshi kana kwamba polisi imekuwa ni tawi kama UVCCM!

Tumeshuhudia viongozi wakubwa kabisa wa chama wakijitapa kuwa wao wanatumia dola (jeshi) kubaki madarakani. Na hii ni kweli kabisa wametuonyesha vile walivyokuwa wakiwatumia polisi kuiba masanduku ya kura, kuzuia mikutano ya ndani ya chama, kubambikizia wapinzani kesi, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama pinzani na mambo mengine ya hovyo hovyo kabisa!

Kama hiyo haitoshi tulishuhudia vihoja na vitimbwi vingine, viongozi waandamizi wa jeshi walitembea na ilani ya chama, walihudhuria vikao vya chama, wengine walidiriki kusema kuwa CCM=Polisi na Polisi=CCM, na kutudhihirishia hilo hata wanachama wafuasi wa CCM walishona na kuvaa sare za Polisi (Jungle green)!

Viongozi wa Polisi ambao walionekana kukaidi maelekezo ya chama na kuamua kusimamia sheria na kanuni ama walitolewa kwenye nafasi zao (Aliyekuwa RPC Geita) na kurejeshwa kusoma magazeti makao makuu ya jeshi ama kuhamishwa pahala walipo na kupelekwa mahala ambapo hawatakuwa na madhara.

Katika hili la siasa tumeshuhudia mengi sana kwa kweli. Salamu ya chama ilikuwa salamu rasmi ya jeshi, (Kuna video huko youtube inamuonesha kiongozi wa CCM ngazi ya kata akimkoromea na kumfedhehesha koplo wa polisi huko mikoa ya pwani kwa vile tu aligoma kutamka 'Kidumu Chama Cha Mapinduzi').

Kwa makusudi kabisa Chama cha Mapinduzi kiliamua kulitumia jeshi la polisi kufanikisha maslahi yake ya kisiasa na hivi sasa leo hii kimeshafanikiwa basi polisi wamekuwa ni takataka hawana maana. Polisi mjifunze kitu hapa, muache kutumika!

Watanzania wenye mawazo mbadala wameishi kwa tabu sana. Ilifika mahali hata kuvaa sare za ACT, CHADEMA, CUF nk ikawa jinai! Mlifika mbali polisi jamani! Waliokuwa wanawatumikisha kufanya haya leo hii wamewageuka!

Ni dhahiri chaguzi za 2015, 2019, 2020 kama kama sio mambo ya hovyo hovyo mliyoagizwa kuyafanya basi leo hii hao waliowaagiza kufanya hayo mambo ya hovyo hovyo wasingekuwa madarakani. Ni nani asiyejua kilichofanyika 2015? Uchafuzi wa 2019? Uchafuzi mwingine wa 2020?
Haya leo hii wamewalipa nini hao CCM? Wamewanunulia magari? Wamewajengea nyumba? Wamewapandisha mishahara? Vielfu kadhaa mlivyolipwa kufanya mahovyo hovyo mnavyo leo hii? Au ndio wote tunaugulia ugumu wa maisha?

Chuki mlioijenga mioyoni mwetu Watanzania ni kubwa! Wengi wameumia kwa kutumika kwenu kisiasa.

Ili wananchi tuwe tena na imani na jeshi letu la polisi nashauri lifumuliwe upya!

Tunataka jeshi huru la polisi! Tunataka jeshi la polisi litakalokuwa halifungamani wala kupokea maelekezo kutoka kwa kiongozi yeyote wa kisiasa! Sheria ya jeshi la polisi na wasaidizi wake ibadilishwe, masuala ya waziri anayepatikana kisiasa kutoa maelekezo kwa jeshi hatuyataki, katiba ibadilishwe, masuala ya mkuu wa jeshi kuteuliwa na mwanasiasa hatuyataki!

Hii itatuepushia viongozi wa jeshi kujipendekeza kwa wanasiasa ili wapate promotion na vitengo vyenye maslahi.


Tuje kwenye changamoto nyingine inayolikabili jeshi la polisi ya uhaba wa vitendea kazi. Jeshi la polisi ni taasisi ya serikali, inaitegemea serikali kwa kila kitu ili iweze kutekeleza majukumu yake. Tutegemee nini ikiwa serikali haitimizi wajibu wake kwa taasisi hii nyeti?

Tunaambiwa ni mwaka wa6 huu siyo tu mavazi, au buti bali hata soksi hawajawahi kupewa hawa askari! Askari anajinunulia mwenyewe kitambaa anashona mavazi, anatoa hela mfukoni anajinunulia buti! Kwanini asiombe elfu5 pale barabarani? Kwanini asitusingizie kesi ili apate elfu 20 ya kununua kitambaa?

Tunaambiwa magari wanayotumia polisi walipewa mgao 2005 na 2015 ili wawawezeshe kubaki madarakani! Baada ya kufanikiwa hitaji lenu siyo tu magari mapya bali hata hayo mliowapa sio mafuta wala vipuri mnavyowapatia!

OCD ajiongeze gari lake linapoharibika, ajiongeze kuweka mafuta kwenye cruiser yake afanye doria mji mzima, afuate watuhumiwa Nanjilinji, akimbize majambazi Kasulu. Huyu OCD ana mgodi wa dhahabu kuhudumia vipuri magari yaliyooza?? Ana mgodi wa dhahabu kuweza lita 50 za mafuta kwenye gari kila siku?

Hapa mna tabu wananchi, maOCD wanatukamatakamata mtaani wapate hela ya kununua vipuri, RTO anatukamata apate hela ya kuweka mafuta, serikali ya CCM mmehalalisha haya!

Wapeni magari mapya hawa watu, wanunulieni vipuri, wapeni mafuta WATATUUA HAWA VIUMBE!

Tuje katika suala la maslahi. Hili ndio haswaa linapelekea tunaona watu wanadhulumiwa mali zao wanadhulumiwa hata na uhai wao! Hapa serikali inalaumiwa, polisi nao wanalaumiwa.

Hawa watu tumewapa mamlaka makubwa mno, sana lakini maslahi yao ni duni!

Nakumbuka kusoma mahala kuwa huko Kongo miaka fulani wakati wanajeshi wakimlalamikia kiongozi wa nchi kuhusu maslahi yao kuwa duni walijibiwa, 'Askari unalalamika maslahi duni na unamiliki bunduki'.

Hiki ndicho ninachokiona kinafanywa na serikali ya CCM kwa polisi leo hii! Mamlaka tuliyowapa hawa watu na ujira tunaowalipa haviendani! Hapa ni sawa na kuwapa go ahead wajiongeze kama ilivyokuwa huko Kongo kwa askari jeshi.

Huyu askari amepewa bunduki, amepewa mamlaka ya kukamata, kuweka kizuizini na kushtaki, lakini ana ujira haba kwanini asi'abuse mamlaka yake kwa maslahi yake binafsi?

Turejee kwenye madhaifu ya polisi. Ni kweli serikali ya CCM imewatelekeza sio tu ninyi bali wafanyakazi wake wa kada mbalimbali kwa takribani miaka sita sasa hakuna ongezeko lolote la mshahara. Hii isiwafanye kuwa makatili kiasi hicho. Tunafahamu wapo askari wachache wenye tamaa wanaochafua taswira ya jeshi la polisi kwa kudhulumu mali za watu kufikia hata kutwaa uhai ili tu kupora mali.


Nini kifanyike?

1. Kufumuliwa na kuundwa kwa jeshi huru, jeshi ambalo halitapokea maelekezo kutoka kwa mwanasiasa.

2. Serikali kutimiza wajibu wake kwa taasisi hii. Wapewe vitendea kazi; magari, pikipiki, vipuri na mafuta kila wakati kama ninyi mnavyojinunulia mavieite yenye viyoyozi na kujiwekea mafuta kwenye kadi zenu za toto na pumha. Wapatiwe uniforms

3. Wawezeshwe kimakazi. (Makao makuu ya chama na serikali yanaongoza kwa kutia aibu makazi ya hawa watu, unaweza kujionea mwenyewe kambi iliyo pembeni ya central police ni aibu).

4. Maslahi yaboreshwe, wapatiwe ujira wao kama inavyostahili, mishahara na posho mbalimbali.

5. Kuundwa kwa chombo huru kitakachokuwa kinasimamia utendaji kazi haswa pale yanapotokea mauaji ya kutatanisha.
 
Binadamu tumeweka siasa Mbele maisha ya watu na utu wao nyuma. Katika kipindi chote ambacho matendo maovu ya Jeshi la Polisi yanafanyika hakuna aliyewahi kusikia Chama cha Mapinduzi wakikemea. Tumesikia namna mwanachama wa CCM Bwana Sabaya alivyokuwa anakamata walinz
Mkuu umeongea ukweli japo ccm hatapenda huu ukweli mchungu
 
Ingefaa iundwe sheria ambayo italifanya jeshi la polisi lijitegemee kwa kila kitu,
Ingefaa wakuu wa majeshi na vikosi mbalimbali wawe wanateuliwa na baraza maalum litakaloundwa kisheria na Bunge pamoja na judicial organ, baraza hili pia liwe linamulika matendo machafu ya jeshi la polisi kulifanyia uchunguzi na kulitolea hukumu.
 
Ccm ndiyo imekuwa ikilitumia jeshi la polisi kufanikisha malengo yake ya kisiasa hasa nyakati za uchaguzi hivyo wao ndio walioshiriki kuharibu mwenendo wa polisi.
 
Back
Top Bottom