Mleta uzi haujatenda haki kwa wanajamiiforums kwa ujumla wapo member waliotoa mchango wao wa hali na mali kwa maslahi ya taifa ila hawapo in the list. Kifupi naomba kuwatambua wafuatao:
CHIEF MKWAWA kwa watuamiaji wa jukwaa la Teknolojia watakubaliana nami kuwa huyu ni mtu wa kipekee na mwenye moyo wa kusaidia wengine. Naomba mchango wake utambuliwe kama mtoa ushauri wa masuala ya kiteknolojia bora zaidi jukwaani.
Amesaidia wengi katika kufanya maamuzi sahihi juu ya simu zinazofaa na utambuzi wa simu halisi na kuwakinga members na utapeli. Pia mkuu huyu hujibu maswali yote kwenye uzi na PM. Kwangu mimi anastahili tuzo ya MwanaJF analiyeitumikia Jamii.
Pili naomba utambuliwe mchango wa
joka kuu,
nguruvi,
Rutashubanyuma Mkandara na
BAK kama members bora wanaotekeleza dhana ya great thinking kwa vitendo. Mfuatiliaji wa mijadala iliyoshiba na yenye hoja atakubaliana nami kuwa hawa jamaa hujadili facts backed by data na huweka hoja zilizoshiba Mezani zikiambatana na uchambuzi mujarabu. Hawa wanastahili tuzo ya Great Thinkers of the Year.
Tatu wapo wanaowakilisha jamiiforums kweye anga la kimataifa wakitanguliza maslahi ya taifa mbele. Hawa ni wazalendo wa kweli na hututetea bila kuchoka na kuteteleka, hawa ni wanajeshi wetu katika at ardhi ya ugenini wakipigana vita dhidi ya propaganda chafu na kutangaza mazuri ya taifa letu kwenye majukwaa ya ughaibuni. Kwangu mimi JF Foreign Dignitary Award of the Year goes to
Geza Ulole.
Kundi la mwisho ni kundi la maripota bora wa mwaka. Watu hawa wametuhakikisha kauli ya be the first to know kama ilivyoada yetu. Tuzo hii pia naomba iende kwa live coverage reporter wa mwaka. Am honoured to nominate
Mwanahabari Huru kama best reporter of the Year na mwanaJF
Francis12 kwenye category ya live coverage reporter of the Year.
Wa mwisho kabisa ni mwanaJF aliyeimpact maisha ya wanaJF na Watanzania kuondokana na umasikini na kuingia kwenye ujasiriamali. Yupo mwanaJF ambaye alitumia platform hii kuhubiri ujasiriamali na kufundisha ujasiriamali kwa vitendo. Mjasiriamali huyu leo hii ameunganisha mamia ya WanaJF na jamaa zao kufungua makampuni na kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji na mazao ya misitu. I am humbled to represent JF Entrepreneur of the Year Mr.
Malila
Ombi langu kwa uongozi wa JF kama mna funds ningependelea muwaaward members hawa kwa mchango wao uliotukuka.