Ni nani anatakiwa kuwa na VFD/EFD?

Ni nani anatakiwa kuwa na VFD/EFD?

Esokoni

Senior Member
Joined
Aug 1, 2018
Posts
100
Reaction score
122
Karibu sana, kwanza kabisa Utaratibu wa kutumia Mashine za VFD/EFD ulianzishwa kwa lengo la kumrahisishia mfanyabiashara katika utunzaji wa kumbukumbu za mauzo/biashara za kila siku ili kuondoa usumbufu wakati wa ukadiriaji wa kodi (usikadiliwe kodi kubwa kuliko biashara yako au usikadiliwe kodi ndogo kilingana na mauzo yako).

Wanaotakiwa kutoa risiti za EFD ni wale Mauzo ghafi kwa mwaka ni shilingi milioni 14 na zaidi ambayo ni sawa na Tsh. 38,888 kwa siku.

Kwa maana hiyo wale Wenye maduka ya vipuri, Mawakili, Maduka ya jumla (Sub wholesale shops), Wafanyabiashara wakubwa wa Mbao, Migahawa mikubwa, Maduka ya simu na vipuri vyake, Baa na vinywaji baridi, Studio za picha, “ Catering Services”, Wauzaji wa Pikipiki, Maduka makubwa ya nguo Na biashara zinginezo wanatakiwa kuwa na mashine hizo.

Kwahiyo Wafanyabiashara zisizo rasmi aina ya Mama Ntilie na wale wanaotembeza bidhaa barabarani hawahusiki kwa sababu hawana sehemu maalum ya kufanyia biashara.

Baadae tutaangalia Faida za kutumia VFD na EFD kwenye biashara zako...

NB: Unaweza kuokoa garama kwa zaidi ya 50% kwa kujiunga na mfumo wa kisasa wa VFD. Huu ni mfumo mpya uliothibitishwa na TRA kutoa risiti za EFD zenye QR CODE kwa kutumia simu ya mkononi au kompyuta, Ni Bora na rafiki kwa wafanyabiashara na watoa huduma utakuwezesha kutoa risiti popote ulipo bila kikomo.
 
Back
Top Bottom