KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,181
- 17,187
Hukusema kuwa wewe ni mwarabu?Kwanza kabisa sikusema popote pale kwamba mie ni mwarabu bali nimesema na narejea tena mie ni mzanzibari.
Pili wewe unajuwa wazi kwamba watu wote waliokuwa wakisafiri nchi za nje miaka 1000 iliyopita, walikuwa wakisafiri ili kutafuta kukuza uchumi wa nchi zao, waarabu, waejemi, wazngu na wachina walifanya hivyo. Watangayika wahakuwa na organised economy kwahivyo nini ikiwapeleke zanzibar au popote pale pemgine? Hawakuwa na organised government walikuwa wakiishi katika mfumo wa makabila na mfumo wa vijiji.
Kabla kuja wazungu, mulikuwa mukitawaliwa na Zanzibar, baade wakaja wajerumani na kufuatiwa na waingereza. Serikali ya mwanzo ya kiafrika ilikuwa ya Mwalimu Nyerere. Huo ndio ukweli labda uwe huutaki tu
Umesahau ulichoeleza humu maana ya "Mzanzibari" ni nini, au sasa unataka kuikana hiyo kauli?
Kama wewe unajiita "Mzanzibari", kwa maana yako uliyoileta hapa nani ni mzanzibari inakuweka kwenye uarabu.
Sasa ngoja nikueleze jinsi gani ulivyo kilaza: Una maana mataifa yote kasoro ya kiafrika walikuwa ni wasafiri kwenda kuvamia nchi za wengine ili kupata utajiri wa mataifa yao? Nchi zoote za wazungu walisafiri, wasingesafiri nchi zao zingebaki kuwa maskini?
Mbona waarabu kama si mafuta hadi leo wangekuwa na hali duni, hata pengine kuzidi ya waafrika? Saud pasingekuwepo na mafuta, utajiri wao ungetoka wapi, kwenye tende?
Yemen kuna utajiri gani, na hata hiyo Oman, hadi hivi karibuni tu, vinginevyo hali yao ilikuwa ni duni kabisa; halafu unakuja hapa kujigamba kana kwamba waarabu walivumbua chochote!
Ngoja nirudie, kama hunielewi ninachokueleza. Kutosafiri kwa waafrika toka walipokuwa haina maana hawakuwa na akili za kumudu maisha yao walipokuwa wanaishi. Kama binaadam mwingine yeyote, waliyamudu mazingira yao kwa nyenzo walizokuwa nazo. Hili hutaki kulielewa kwa sababu tu kichwani mwako unazo fikra za kujiona wewe kama mwarabu ni bora zaidi ya wengine - upuuzi mtupu.
Unaposema watanganyika hawakuwa na 'organized economy' ina maana huelewi kwamba ndani ya eneo hilo la Tanganyika na hata Zanzibar palikuwemo na makabila katika maeneo mbalimbali yaliyokuwa yameji'organise' kiutawala. Hilo hulijui?
Huko uarabuni kwenyewe, hamkuwa na makabila mbalimbali katika maeneo tofauti, kulikuwepo na seriakali moja kwenye kila nchi zinazotambulika sasa hivi kuwa ni nchi za kiarabu?
Zanzibar haikuwahi kuitawala Tanganyika.