Ni Nani hasa Mwenyeji wa Zanzibar? Je, ni Muafrika, Muarabu, Mshirazi au wote?

Waarabu gani mkuu? Kuna muarabu mwenye shida na Zanzibar? huko uarabuni unakufahamu kulivo?
Hapana, sifahamu uarabuni kulivyo, lakini nafahamu tabia za binaadam kutaka kutawala binaadam wenzao. Hilo halijalishi hali ya huko waliko ipoje.
Bila shaka utakuwa umenielewa nisemalo hapa.

Hata kama hali ya huko arabuni ingekuwa ni ya neema kiasi gani, tamaa ya kutawala kwingine haiweza kumtoka binaadam.
 
Ni kweli mkuu hayo megine ni makosa, lakini yanachangiwa na situation ya mazingira ilivo.
Hebu tizama chuki dhidi ya wasukuma ilivyokua katika miaka mitano hii hapa bara, kwani hivi ni wasukuma wote waliokuemo kwenye system ya Serkali? Lakini chuki zinazotokana na uonevu huvuka mipaka, nakama Marehemu angeendelea kutawala Miaka 10 tu mengine hivi unahisi watu wangekua wanachuki kiasi gani na wasukuma? Hii inatokana na uonevu ambao mwisho wa siku binaadamu anakosa cha kufanya Zaidi kuzalisha chuki kwa anaefanyia
Haya yote hayahalalishi sisi kuwaonea wasukuma wote tuwaone kama ni wabaya wakati ubaya unafanywa na wasukuma wachache tu.

Huu sio uungwana hata kidogo lakini kwa kuwa ndo tumekua hivyo acha maisha yaendelee ila kukemea tabia kama hizi ni wajibu ili zisikite mizizi katilka jamii
 
Labda kweli ikiwa utaanza kutizama kijuu juu utaona maneno hayo ni ya upendeleo kwa upande fulani. Lakini Zanzibar ni visiwa, wewe unajuwa wazi kwamba hata leo hii ukitaka kuja znz ni lazima upande boti au ndege. sasa miaka ya maelfu iliyopita unadhani mwafrika gani wa afrika mashariki alokuwa hakuhitajia usafiri wa baharini kufika znz. Jiulize Mtanganyika alikuwa ana shida gani znz? Znz haikuwa pori la wanyama ukasema wamekuja kuwinda, wala watanganyika hawakuwa na uhaba wa matunda yao na vyakula vayo nini kilikuwa kiwapeleke znz?
Mkuu kitu ambacho unakosea ni kwamba Mwafrika gani alikuwa anahitaji kwenda umbali wa zanzibar ilhali kila kitu kinajitosheleza bara? tambua kuwa uvuvi ulikuwa sehemu ya Maisha kwa muda mrefu na watu waliingia baharini kwa ajili ya kujitafutia kitoweo na kupitia uvuvi ndio waliweza kufika maeneo mbalimbali na ndio chanzo cha kufika kwenye visiwa vya pembezoni, na wengi waliweka kambi za uvuvi katika visiwa walivyofika...
 
Ndugu Wana Jukwaa

Kuna maneno mengi yasioningia katika mizani ya akili yanayozungumzwa na watu hasa wenye asili ya Tanganyika kuhusu Zanzibar na Uzanzibari. Watu wamekuwa wakiunda historia ya zanzibar kutoka katika hisia na wivu wao binafsi. Historia ya kuunga unga vipande, historia isio na kichwa wala miguu.

Ikiwa unahaitaji kuijuwa Zanzibr na Wazanzibari, soma hadi mwisho

Mtu wa mwanzo kabisa kuweka mguu wake katika ardhi ya Visiwa vya Zanzibar ni wa Iran and waarabu. Ukitaka kujuwa hilo tizama katika picha na vifaa vya kale. Kwahivo Zanzibar imejengwa na kuimarishwa na waarabu na wairani. Ni haki kabisa kusema kwamba Zanzibar ni sehemu ya Urabuni. Hilo si ajabu kwasababu ndani ya Afrika zipo nchi za Kiarabu. Kwahivyo wachilia mbali kwamba Zanzibar iko pembeni kwa Afrika. Muafrika wa kwanza kufika Zanzibar katika wanaume aliletwa kwa ajili ya kuimarisha kilimo kwasababu waafrika walionekana ni wakulima mahiri sana na katika wanawake waliletwa kwa ajili ya kuolewa. Hakuna Mtanganyika au Muafrika yoyote Zanzibar alokuja kwa hiyari yake katika miaka ya mwanzoni ya karne za 13, 14, 15, 16 na 17 hata mwanzoni mwa karne ya 18

Kwanini Waarabu na Wa Irani ndio walikuja mwanzo Zanzibar?

Kwasababu watu wa Tanganyika walikuwa hawana sababu yoyote ya kuvuuka bahari na kuja Zanzibar. Watanganyika walikuwa na maisha yao yanayowatosha wenyewe, matunda, kilimo na wanyama. Na hakuna ushahidi wowote kwamba watanganyika walikuwa wakiunda majahazi au kama walikuwa ni mabaharia kama vile walivyokuwa Waarbu na Wa Irani.

Nani Kaitwala Zanzibar katika historia

Waarabu walifanya utawala wa kwanza na bora sana Zanzibar. Na nakuombeni musibabaishwe na majina ya watawala wa zamani wenye majina kama vile Mkama ndume an Mwinyi Mkuu, wote hao walikuwa waarabu. Katika utawala bora wa Zanzibar maendeleo yakawa makubwa watawala wakaona haja ya kuitanua dola ya zanzibar, ndio Tanganyika na nchi zote za afrika mashariki ikiwemo na DRC na Mozambique zikawa katika Zenj empire. Neema kubwa zilipatika kwa kufikiwa na utawala bora, watu wengi kwa mara ya kwanza wakafundishwa kuvaa nguo na usafi na mengineo.

Kwanini kuna Wazanzibari weusi?

Baada ya maisha kuanza, watu wa Zanzibar (waarabu na wairani) wakawa wanahitajia kuowa ndio hapo walipoanza kulekea mrima kutafuta wachumba. Bagamoyo, Kilwa kivinje na kwengineko. Hilo lililetea kupatika wazanzibari wenye rangi nyeusi. Marco Polo alipofika zanzibar alikuta wenyeji wa hapo ni weusi wenye nywele za singa.

Maisha bora yalikuwa zanzibar

zanzibar chini ya uongozi shupavu wa waarabu ilifika mbali kimaisha. Zanzibar ilikuwa na simu majumbani manano mwaka 1886, undersea cable zilitoka znz kupita Aden hadi London. Zanzibar ilikuwa nchi ya Mwanzo Afrika kutumia elevator, pale Beit el Jaibu. Zanzibar ilikuwa nchi ya tatu kutumi aumeme duniani.

Elimu ilikuwa kubwa sana zanzibar hata NASA waliweka tracking station Zanzibar. Zanzibar ilikuwa nchi tajiri sana katika Africa, wafanyakazi wa zanzibari walikuwa wakisafiri kama watalii wakati wakipata likizo zao makazini. Gari la kwanza kutembea Kuwait lilinunuliwa Zanzibar, nchi za Uarabubi zilikuwa zinakuja znz kununua vyakula na nguo kama leo tunavyokwenda Dubai sasa.

Zanzibar ilikuwa nchi huru ndio maana waafrika waliokuja kufanyakazi na kutafuta maisha yao tu waliachiliwa kuingia katika siasa, kosa kubwa sana hilo. Wakafanya mapunduzi na kuuwa wazanzibari 17,000 usiku mmoja. Baada ya hapo Zanzibar inaakza kufa kidogo kidogo. Leo hii watuna ten

Zanzibar iligunduliwa rasmi na Waajemi wakati Bantu expansion ililuwa inasogea polepole
Waarabu wa Oman.Yaani huku Bara tunawaita Wamanga.
 
Waajemi ni watu wa Taifa Liitwalo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.Wana lugha yao ambayo sio kiarabu,wana maandiko yao siyo kiarabu,na hata kwenye lugha ya kiswahili hakuna neno la kiajemi.Washirazi ni ukoo mkubwa uliokuwa Nchini Oman ,ambao hadi leo wanapingana na ukoo ule ule uliokuwa unatawala Zanzibar Na Pemba yaani unaitwa Bin said.hawa washirazi utawakuta katika maeneo ya mpakani na nchi ya Yemen ya Kusini ambapo pana kisiwa kinaitwa zanjibar.Pia kama Msumbiji pana mji unaoitwa Pemba.
 
Ndugu Wana Jukwaa

Kuna maneno mengi yasioningia katika mizani ya akili yanayozungumzwa na watu hasa wenye asili ya Tanganyika kuhusu Zanzibar na Uzanzibari. Watu wamekuwa wakiunda historia ya zanzibar kutoka katika hisia na wivu wao binafsi. Historia ya kuunga unga vipande, historia isio na kichwa wala miguu.

Ikiwa unahaitaji kuijuwa Zanzibr na Wazanzibari, soma hadi mwisho

Mtu wa mwanzo kabisa kuweka mguu wake katika ardhi ya Visiwa vya Zanzibar ni wa Iran and waarabu. Ukitaka kujuwa hilo tizama katika picha na vifaa vya kale. Kwahivo Zanzibar imejengwa na kuimarishwa na waarabu na wairani. Ni haki kabisa kusema kwamba Zanzibar ni sehemu ya Urabuni. Hilo si ajabu kwasababu ndani ya Afrika zipo nchi za Kiarabu. Kwahivyo wachilia mbali kwamba Zanzibar iko pembeni kwa Afrika. Muafrika wa kwanza kufika Zanzibar katika wanaume aliletwa kwa ajili ya kuimarisha kilimo kwasababu waafrika walionekana ni wakulima mahiri sana na katika wanawake waliletwa kwa ajili ya kuolewa. Hakuna Mtanganyika au Muafrika yoyote Zanzibar alokuja kwa hiyari yake katika miaka ya mwanzoni ya karne za 13, 14, 15, 16 na 17 hata mwanzoni mwa karne ya 18

Kwanini Waarabu na Wa Irani ndio walikuja mwanzo Zanzibar?

Kwasababu watu wa Tanganyika walikuwa hawana sababu yoyote ya kuvuuka bahari na kuja Zanzibar. Watanganyika walikuwa na maisha yao yanayowatosha wenyewe, matunda, kilimo na wanyama. Na hakuna ushahidi wowote kwamba watanganyika walikuwa wakiunda majahazi au kama walikuwa ni mabaharia kama vile walivyokuwa Waarbu na Wa Irani.

Nani Kaitwala Zanzibar katika historia

Waarabu walifanya utawala wa kwanza na bora sana Zanzibar. Na nakuombeni musibabaishwe na majina ya watawala wa zamani wenye majina kama vile Mkama ndume an Mwinyi Mkuu, wote hao walikuwa waarabu. Katika utawala bora wa Zanzibar maendeleo yakawa makubwa watawala wakaona haja ya kuitanua dola ya zanzibar, ndio Tanganyika na nchi zote za afrika mashariki ikiwemo na DRC na Mozambique zikawa katika Zenj empire. Neema kubwa zilipatika kwa kufikiwa na utawala bora, watu wengi kwa mara ya kwanza wakafundishwa kuvaa nguo na usafi na mengineo.

Kwanini kuna Wazanzibari weusi?

Baada ya maisha kuanza, watu wa Zanzibar (waarabu na wairani) wakawa wanahitajia kuowa ndio hapo walipoanza kulekea mrima kutafuta wachumba. Bagamoyo, Kilwa kivinje na kwengineko. Hilo lililetea kupatika wazanzibari wenye rangi nyeusi. Marco Polo alipofika zanzibar alikuta wenyeji wa hapo ni weusi wenye nywele za singa.

Maisha bora yalikuwa zanzibar

zanzibar chini ya uongozi shupavu wa waarabu ilifika mbali kimaisha. Zanzibar ilikuwa na simu majumbani manano mwaka 1886, undersea cable zilitoka znz kupita Aden hadi London. Zanzibar ilikuwa nchi ya Mwanzo Afrika kutumia elevator, pale Beit el Jaibu. Zanzibar ilikuwa nchi ya tatu kutumi aumeme duniani.

Elimu ilikuwa kubwa sana zanzibar hata NASA waliweka tracking station Zanzibar. Zanzibar ilikuwa nchi tajiri sana katika Africa, wafanyakazi wa zanzibari walikuwa wakisafiri kama watalii wakati wakipata likizo zao makazini. Gari la kwanza kutembea Kuwait lilinunuliwa Zanzibar, nchi za Uarabubi zilikuwa zinakuja znz kununua vyakula na nguo kama leo tunavyokwenda Dubai sasa.

Zanzibar ilikuwa nchi huru ndio maana waafrika waliokuja kufanyakazi na kutafuta maisha yao tu waliachiliwa kuingia katika siasa, kosa kubwa sana hilo. Wakafanya mapunduzi na kuuwa wazanzibari 17,000 usiku mmoja. Baada ya hapo Zanzibar inaakza kufa kidogo kidogo. Leo hii watuna tena chetu,
Hiyo historia unaijua mwenyewe. Historia rasmi inatambua uwepo wa waafrika waliyotokea tanganyika au kenya kabla kuja waarabu. Kama unawapenda sana waarabu hamia kwao
 
Hakuna mwenyeji kule wote ni wahamiaji. Hata ukoo wa akina Karume ni wamalawi. Aliyeongoza mapinduzi ya Zbar ni Okelo mganda. Wakati Karume alikula kona akakimbilia Dar kwa Julius
 
Hiyo historia unaijua mwenyewe. Historia rasmi inatambua uwepo wa waafrika waliyotokea tanganyika au kenya kabla kuja waarabu. Kama unawapenda sana waarabu hamia kwao
Mkubwa hata jina Zanzibar maana yake ni eneo la watu weusi, mwanzoni kwenye uzi huu niliweka historia ya nano Zanzibar, na ukiangalia wageni wa kwanza kuja Zanzibar si waarabu kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha, inawezekana kabisa kuwa ni waajemi.
Lakini historia ina upungufu wake. Kwa mfano ukisoma vitabu leo utasikia kuwa Columbus dio aligundua Amerika, lakini ukweli ni kuwa America kulikuwa na wenyeji. Bahati mbaya ni kuwa wenyeji hawakuandika hiyo historia, lakini hiii haina maana kuwa wenyeji hawana historia.
Ila usimwambie huyu ndugu ahamie uarabuni, yeye sasa ni sehemu ya Zanzibar kama alivyokuwa Karume kutoka Malawi, au kama aliyokuwa Natepe, Thabit Kombo au hata John Okello. Hajawazidi hao na wala hayuko chini ya hao.
 
Unashikilia hili la kuunda vyombo vya majini.

Hujui kwamba watu walikuwa wakivua samaki na kutumia mitumbwi, na hata magogo yaliyoelea na kusafiri?
Hivyo visiwa kijiolojia vilikuwa sehemu ya nchi kavu iliyoungana na Tanganyika.
Itakuwaje visiwe na watu na wanyama waliokuwa bara baada ya kumeguka kwa miaka mingi toka bara?

Ikiwa watu walikuwa na mitumbwi ya kuvulia samaki haiwezekani mkuu wavuvi wa siku hizo wafike zaidi ya mile 2, samaki walikuwa wengi mno.

Haiwezakani mtu yoyote awepo zanzibar kabla ya wageni wengine kama hao kutoka Iran na Arabuni. Wewe unajuwa Mzanzibari asilia ni yule mwenye kabila ya Shirazi. Sasa ikiwa mzanzibari hasa original ni mshirazi vipi awe ametokea Afrika. Shiraz iko Iran.

Miaka hiyo unayozungumzi weye mkuu hata east afrika yote labda haikuwa na watu wanzaidi 1000 tu, wewe unazungumzia maika bilioni iliyopita. Na kama kulikuwa na watu zanzibar miaka hiyo basi walikufa wote na mgawanyiko huo wa ardhi, maana Hassan bin Ali hakukuta mtu znz.
 
Hili ni jibu la kipuuzi unalolirudia rudia hapa.

Jibu la kipuuzi kwasababu hona jona ya kulipinga. Hoja ya kitaalamu. Ikwa Zanzibar walikuwepo watu walikuwa sehemu ipi mbona hawakuonekana na watu walipofika kama huyo Hassan Bin Ali?
 
Mkuu kitu ambacho unakosea ni kwamba Mwafrika gani alikuwa anahitaji kwenda umbali wa zanzibar ilhali kila kitu kinajitosheleza bara? tambua kuwa uvuvi ulikuwa sehemu ya Maisha kwa muda mrefu na watu waliingia baharini kwa ajili ya kujitafutia kitoweo na kupitia uvuvi ndio waliweza kufika maeneo mbalimbali na ndio chanzo cha kufika kwenye visiwa vya pembezoni, na wengi waliweka kambi za uvuvi katika visiwa walivyofika...

Mkuu Omera

Labda suala la uvuvi lilikuwepo katika pwani pwani ya Afrika mashariki katika miaka elfu na nusu iliyopita. Siwezi kukataa juu ya hilo. Lakini ikiwa unataka kutizama mantiki hiyo ni bora kujiuliza kwa neema ilikuwepo baharini miaka hiyo wavuvi walihitajika kufika maili ngapi ili kujipatia samaki wengi tu. Jee kulikuwa na ulazimu wowote jwa wavuvi kufika maili 50? Jawabu No. Kama kulikuwa na wavuvi mika hiyo basi wasingehitajia kuvuuka hata maili 2. WHY? Miaka elfu na nusu iliyopita kama walikuwepo wavuvi basi walikuwa hawana jarife, lazima wakitumbia miundo mbinu ya siku hizo. Madema na mitego mengine kama hiyo. Kwahivyo hakukua na haja ya kuvua samaki zaidi ya mila 10 katika depth. Zanzibar ni mbali sana kwao.
 
Ikiwa watu walikuwa na mitumbwi ya kuvulia samaki haiwezekani mkuu wavuvi wa siku hizo wafike zaidi ya mile 2, samaki walikuwa wengi mno.

Haiwezakani mtu yoyote awepo zanzibar kabla ya wageni wengine kama hao kutoka Iran na Arabuni. Wewe unajuwa Mzanzibari asilia ni yule mwenye kabila ya Shirazi. Sasa ikiwa mzanzibari hasa original ni mshirazi vipi awe ametokea Afrika. Shiraz iko Iran.

Miaka hiyo unayozungumzi weye mkuu hata east afrika yote labda haikuwa na watu wanzaidi 1000 tu, wewe unazungumzia maika bilioni iliyopita. Na kama kulikuwa na watu zanzibar miaka hiyo basi walikufa wote na mgawanyiko huo wa ardhi, maana Hassan bin Ali hakukuta mtu znz.
Ardhi ya Zanzibar haikung'olewa toka arabuni na kuja kusimikwa ukingoni mwa bara la Afrika.

Zanzibar imekuwa sehemu ya Afrika karne na karne, na vilivyokuwemo barani Afrika ndivyo vilivyokuwemo Zanzibar, ikiwa ni pamoja na viumbe vyote, pamoja na watu.

Kwa hiyo hiyo dhana ya Zanzibar kuwa pori tupu lililookotwa na waarabu ni ya kipuuzi kabisa. Hata haihitaji mtu kwenda shule kuwa na akili ya kutambua jambo kama hilo.
Sasa sijui wewe hapo nikuweke kundi la namna gani, kama huna elimu ya kutosha, hata akili ya kawaida tu ya kutambua mambo huna?

Wachina, Wahidi, Wareno wote walikwishatembelea hapa hata kabla ya ujio wa waarabu, kwa nini ujione waarabu ndio walikuwa wa mwanzo kutembelea pwani hii, na kutaka kuhalalisha historia ya kipumbavu na kibaguzi?
 
Jibu la kipuuzi kwasababu hona jona ya kulipinga. Hoja ya kitaalamu. Ikwa Zanzibar walikuwepo watu walikuwa sehemu ipi mbona hawakuonekana na watu walipofika kama huyo Hassan Bin Ali?
"Hoja ya kitaaluma" ya kusema Zanzibar hawakuwepo watu?

Hiyo historia ya kuwepo Zanzibar imeanza na waarabu kufika Zanzibar? Hiyo ndiyo unayoiita "taaluma"?

Huyo aliyeandika hiyo taaluma ndiye aliyeiumba Zanzibar?

Kama "taaluma" hiyo si upuuzi, tuiite kitu gani!

Sasa elewa, pamoja na "taaluma" feki yako hiyo, Zanzibar haiwezi tena kurudishwa kwenye ujinga wa namna hiyo. Zanzibar sasa ni sehemu ya Tanzania, na daima itakuwa hivyo.
 
Mkuu Omera

Labda suala la uvuvi lilikuwepo katika pwani pwani ya Afrika mashariki katika miaka elfu na nusu iliyopita. Siwezi kukataa juu ya hilo. Lakini ikiwa unataka kutizama mantiki hiyo ni bora kujiuliza kwa neema ilikuwepo baharini miaka hiyo wavuvi walihitajika kufika maili ngapi ili kujipatia samaki wengi tu. Jee kulikuwa na ulazimu wowote jwa wavuvi kufika maili 50? Jawabu No. Kama kulikuwa na wavuvi mika hiyo basi wasingehitajia kuvuuka hata maili 2. WHY? Miaka elfu na nusu iliyopita kama walikuwepo wavuvi basi walikuwa hawana jarife, lazima wakitumbia miundo mbinu ya siku hizo. Madema na mitego mengine kama hiyo. Kwahivyo hakukua na haja ya kuvua samaki zaidi ya mila 10 katika depth. Zanzibar ni mbali sana kwao.
Hii ndiyo aina ya akili inayokuongoza, hivi hata huoni aibu?

Mwarabu alipotoka huko alikotoka na kufika Zanzibar, alikuwa akitafuta nini?

Sasa ngoja nikueleze kama hujielewi?

Haya unayoyaweka hapa ni kujiona wewe mwarabu kuwa bora zaidi kuliko mwafrika. Hii dhana unaitoa wapi?

Wewe ulikuwepo kati ya waafrika na kujua kwamba kazi waliyoweza ni kupata kitoweo tu basi?
Maana yako ni kwamba akilini mwako huwezi kamwe kumwona mwafrika akiwa na udadisi juu ya mazingira yake?

Ni akili hiyo hiyo inayokuongoza hapa na kubeza uwezo wa waTanganyika kulinda mali zao, kama unavyoonyesha humu.
Wamekwishakuonyesha kwamba wanaweza kukudunda na kukuondoa kwenye kukandamiza unaowatawala, bado akili haikuingii tu kichwani?

Kwa hiyo, baki tu hivyo hivyo, lakini huwezi tena kutuchezea ukidhani wewe ni bora zaidi.
 
Mwarabu alipotoka huko alikotoka na kufika Zanzibar, alikuwa akitafuta nini?

Sasa ngoja nikueleze kama hujielewi?

Haya unayoyaweka hapa ni kujiona wewe mwarabu kuwa bora zaidi kuliko mwafrika. Hii dhana unaitoa wapi?

Kwanza kabisa sikusema popote pale kwamba mie ni mwarabu bali nimesema na narejea tena mie ni mzanzibari.

Pili wewe unajuwa wazi kwamba watu wote waliokuwa wakisafiri nchi za nje miaka 1000 iliyopita, walikuwa wakisafiri ili kutafuta kukuza uchumi wa nchi zao, waarabu, waejemi, wazngu na wachina walifanya hivyo. Watangayika wahakuwa na organised economy kwahivyo nini ikiwapeleke zanzibar au popote pale pemgine? Hawakuwa na organised government walikuwa wakiishi katika mfumo wa makabila na mfumo wa vijiji.

Kabla kuja wazungu, mulikuwa mukitawaliwa na Zanzibar, baade wakaja wajerumani na kufuatiwa na waingereza. Serikali ya mwanzo ya kiafrika ilikuwa ya Mwalimu Nyerere. Huo ndio ukweli labda uwe huutaki tu
 
Hoja ya kitaaluma" ya kusema Zanzibar hawakuwepo watu?

Hiyo historia ya kuwepo Zanzibar imeanza na waarabu kufika Zanzibar? Hiyo ndiyo unayoiita "taaluma"?

Huyo aliyeandika hiyo taaluma ndiye aliyeiumba Zanzibar?

Kama "taaluma" hiyo si upuuzi, tuiite kitu gani!

Sasa elewa, pamoja na "taaluma" feki yako hiyo, Zanzibar haiwezi tena kurudishwa kwenye ujinga wa namna hiyo. Zanzibar sasa ni sehemu ya Tanzania, na daima itakuwa hivyo.

Kalamu,

Regardless, wewe pia uanweza kuamini utakavyo, lakini hakuna kitabu chochote kilondikwa na watu waliokuwepo zanzibar hadi miaka 500 iliyopita kinachoonyesha zanzibar ilikuwa na uhuisnao wowote na Afrika, ukiondosha geographical location tu.

siamini kwamba watu wa mrima walikuwa na sababu yoyote ya kuja znz hadi miaka 500 iliyopita. Na bado ninaamini kwamba waliokuja znz waliletwa kwa kaazi maalumu tu.
 
Ardhi ya Zanzibar haikung'olewa toka arabuni na kuja kusimikwa ukingoni mwa bara la Afrika.

Zanzibar imekuwa sehemu ya Afrika karne na karne, na vilivyokuwemo barani Afrika ndivyo vilivyokuwemo Zanzibar, ikiwa ni pamoja na viumbe vyote, pamoja na watu.

Kwa hiyo hiyo dhana ya Zanzibar kuwa pori tupu lililookotwa na waarabu ni ya kipuuzi kabisa. Hata haihitaji mtu kwenda shule kuwa na akili ya kutambua jambo kama hilo.
Sasa sijui wewe hapo nikuweke kundi la namna gani, kama huna elimu ya kutosha, hata akili ya kawaida tu ya kutambua mambo huna?

Kalamu

Inanibidi kurejea maneno yale yale lakini ukweli nikwamba sema utakavyo lakini Zanzibar ilikaliwa mwanzo na waaejemi na waarabu. Katika miaka hiyo tunayozungumia watanganyika bado wanavaa ngozi au kujifunika majani tu, maana kama umewahi kusikia nguo ziitwazo kaniki zilikuwa zikitoka znz kupelekewa watu wa mrima. Miaka 500 kwendea chini zaidi tembo angeweza kupita katika tundu ya shindano kabla mtangayika kufika znz.

labda unaweza kusema mie najihisi mwarabu kwahivyo ninawazadharu waafrika, no, brother mie ni mzanzibari na ninasema historia kama ilivyo tu.
 
Geographical visiwa vya Unguja na Pemba vipo karibu sana na Tanganyika, na kwa vile nature ya wakazi wa pwani ni wavuvi, kufika kufanya makazi ya kudumu kwenye visiwa hivi ni jambo linalowezakana kabisa, sema visiwa hivi hakuishia kuvutia wavuvi wa bara tu, hata wageni toka mbali pia.
 
Back
Top Bottom