Ni Nani hasa Mwenyeji wa Zanzibar? Je, ni Muafrika, Muarabu, Mshirazi au wote?

Ni Nani hasa Mwenyeji wa Zanzibar? Je, ni Muafrika, Muarabu, Mshirazi au wote?

Maneno haya hapa pekee yanakufanya uonekane kama kituko.

Labda kweli ikiwa utaanza kutizama kijuu juu utaona maneno hayo ni ya upendeleo kwa upande fulani. Lakini Zanzibar ni visiwa, wewe unajuwa wazi kwamba hata leo hii ukitaka kuja znz ni lazima upande boti au ndege. sasa miaka ya maelfu iliyopita unadhani mwafrika gani wa afrika mashariki alokuwa hakuhitajia usafiri wa baharini kufika znz. Jiulize Mtanganyika alikuwa ana shida gani znz? Znz haikuwa pori la wanyama ukasema wamekuja kuwinda, wala watanganyika hawakuwa na uhaba wa matunda yao na vyakula vayo nini kilikuwa kiwapeleke znz?
 
Zanzibar ilikuwa nchi huru ndio maana waafrika waliokuja kufanyakazi na kutafuta maisha yao tu waliachiliwa kuingia katika siasa, kosa kubwa sana hilo. Wakafanya mapunduzi na kuuwa wazanzibari 17,000 usiku mmoja. Baada ya hapo Zanzibar inaakza kufa kidogo kidogo. Leo hii watuna tena chetu,

Mkuu hebu tafadhali fafanua jambo hili zaidi.--- lijazie nyama.
 
Weka picha
download.jpg

NASA project Mercury Tracking Centre. Tunguu hapo.
 
Mnazunguuka nadhani mantiki ya thread yenu mnataka kujua nanii katokea wp hasa?
 
Mkuu hebu tafadhali fafanua jambo hili zaidi.--- lijazie nyama.
Mkuu Mokaze

Hili tukio linawaumiza wazanzibari kwa miaka mingi sana sasa. Ni heri yetu tusilizungumze. Lakini chukuwa dondoo hili, ukisikia mtu anayejiita Mzazibari na akawa analifuhaikia hili tukio basi huyo ni wale waitwao wazanzibara. bora niishie hapo tu.
 
Baada ya yote hayo ya ajabu niliyoyasoma leo kutoka kwa mleta mada hii, maajabu hayakuishia hapo.

Nilitaka kujua angalao kidogo mwandishi huyu yupo vipi?

Kabla sijaenda mbali nikakutana na haya maneno:

"MJINGA ANAWEZA KUWA HATA NA Phd (PhD) IKIWA ANATUMIA AKILI BANDIA"

Nikiri, imenichukua muda kidogo kuyatafakari kwa kina maana ya maneno hayo kumi; na kama yana maana, hata kama imefichika.

Baada ya tafakuri hiyo, nimetambua kwamba mwandishi hana lolote kichwani.

Hii si kumshambulia yeye binafsi kwa mawazo yake, bali ni katika kutafuta ukweli wa mambo anayoyawasilisha hapa.

Kuna haya mengine niliyoyaokota humo yanayomfunua mwandishi:

"Mwafrika wa kwanza kufika Zanzibar aliletwa kwa ajili ya kazi tu" - Yaani utumwa. Yaani hivyo visiwa hata wanyama pori hawakuwemo humo, na wao waliletwa baada ya waarabu kuishi humo?

"Pia kusafiri kwa miaka ile ilitokana na utashi wa kutaka kukusanya mali zaidi. Watanganyika leo hii hawajali mali yao unadhani walikuwa na utashi wa kutafuta mali zaidi katika maelfu ya miaka iliyopita?" -Kama huelewi maana ya maneno haya ni kwamba huu ndio uamini alio nao juu ya watanganyika mwandishi huyu.

"Zanzibar ilikuwa nchi huru (yaani raia wake wakiwa waarabu, na siyo waafrka weusi)
"Ndio maana waafrika walikuja kufanya kazi na kutafuta maisha yao tu (yaani hawa waafrika hawakuwa raia wa Zanzibar).
"Hawa wafanya kazi wasiokuwa raia wa Zanzibar (wafanyakazi wa kuja) wakaingia kwenye siasa na kufanya mapinduzi.

"Wakawaua wazanzibari (waarabu) 17,000 usiku mmoja"
Hivi hakuna mwafrika hata mmoja aliyeuawa katika mapinduzi yale? Maana hawa hawakuwa raia wa Zanzibar!

"Baada ya hapo Zanzibar inaanza kufa kidogokidogo.
"Leo hii hatuna tena chetu -
Yaani Waarabu wa Zanzibar, ambao walikuwa ndio raia halali wa Zanzibar (Wazanzibari)

Swali ninalojiuliza hapa, hivi hawa ndugu zetu waliopo Zanzibar ambao sio waarabu, wanayaelewa haya?

Binafsi nilikuwa silielewi hili. Leo nimefunguka macho kwa mara ya kwanza kabisa.
 
Mkuu Mokaze

Hili tukio linawaumiza wazanzibari kwa miaka mingi sana sasa. Ni heri yetu tusilizungumze. Lakini chukuwa dondoo hili, ukisikia mtu anayejiita Mzazibari na akawa analifuhaikia hili tukio basi huyo ni wale waitwao wazanzibara. bora niishie hapo tu.

Mkuu mzanzibari huru.

Wewe unajiita Mzanzibari tena uliyekuwa huru, je na wewe ni mzanzibara??.

Juu ya yote usiogope kusema ukweli kwani ukweli huumiza pia huleta faraja na kuwaweka watu huru.

Ili tupate faraja na uhuru wa mawazo basi hunabudi kuweka jambo hilo wazi, hiyo ni historia na wala sio ngano za Alfu lela ulela.
 
Hii si kumshambulia yeye binafsi kwa mawazo yake, bali ni katika kutafuta ukweli wa mambo anayoyawasilisha hapa.

Raha ya kutoa maoni na kupokea maoni ni uhuru wa kuamini au kutoamini. By the way, yote niliyasema hayatoki kichwani kwangu. Yameandikwa.
 
Kabla ya kuja waarabu hapo kisiwani! Kulikuwa na watu gani?ukipata jibu hapo
Basi

Ova
Kuna kisiwa hapo mbele jina lake kama Chato, walihamishwa wote raia wengine wakapelekwa Uk leo wanadai nchi yao wengine walihamishiwa Mauritios .
Yaani pale ni UK,US military base in Africa.
Jamaa wapo pale mda tu na ni command point.
Wakati wanawahamisha walikua si zaidi ya 60000.
Tukija Zenjbar pale wamatumbi tumo, waarabu wamo, wahindi wapo, wote tunajuana.
Ila mziki wa kimakonde ukianza hao wengine wanataftaga mlango wa kutokea.
Muulize yule Sultan Seyid Uk.
 
Mtahangakai sana, Zanzibar ni ya waafrika 'watu weusi'

Na hata kiasili, kimazingira inafanana na pwani ya Afrika, na ilimeguka kutoka bara Afrika miaki milioni kadhaa iliyopita
Asante mkuu kwa mchango huu.

Kuna mtu wa ajabu anadai, mtu mweusi wa kwanza alipelekwa Zanzibar kufanya kazi? Aliokotwa mahali fulani, sijui wapi, Tanganyika(?) akapelekwa Zanzibar!
Maana yake ni kwamba, hao watu weusi waliopo Zanzibar, wote sio watu wa hapo!

Sasa maajabu ni kwamba, kuna baadhi yao wanajivunia kuwa Wazanzibari, bila kujua kwamba wenye nchi yao wanawaona wao kuwa wageni/ watumwa tu!
 
Kuna kisiwa hapo mbele jina lake kama Chato, walihamishwa wote raia wengine wakapelekwa Uk leo wanadai nchi yao wengine walihamishiwa Mauritios .
Yaani pale ni UK,US military base in Africa.
Jamaa wapo pale mda tu na ni command point.
Wakati wanawahamisha walikua si zaidi ya 60000.
Tukija Zenjbar pale wamatumbi tumo, waarabu wamo, wahindi wapo, wote tunajuana.
Ila mziki wa kimakonde ukianza hao wengine wanataftaga mlango wa kutokea.
Muulize yule Sultan Seyid Uk.
DIEGO GARCIA
 
Raha ya kutoa maoni na kupokea maoni ni uhuru wa kuamini au kutoamini. By the way, yote niliyasema hayatoki kichwani kwangu. Yameandikwa.
Sawa kabisa.

Hoja ni nani kayaandika na katika muonekano gani.

Na yule ambaye hakuandika je, tuchukulie kwamba yeye hakuwepo, hakuwa na lolote?

Na kama kaandikwa sivyo, tukubali tu kwamba ndio ukweli kwa kuwa kaandikwa hivyo?
 
Wewe unajiita Mzanzibari tena uliyekuwa huru, je na wewe ni mzanzibara??.
Naona hukumsoma na kumwelewa vizuri.
Swali lako limeelezewa vizuri kwenye andiko lake.

Wazanzibari - ni raia wa Zanzibar, yaani waarabu, waliokuja na kukuta visiwa vikiwa tupu bila ya kuwepo na binaadam mwingine mwenye rangi nyeusi.
Baada ya kutaka wawepo wafanyakazi, ndipo ikalazimu wakatafutwe watu weusi (watumwa), wakaletwa visiwani. Hawa hawakuwa raia; na kwa msamiati wa leo, hawa ndio "Wazanzibara"

Yeye hawezi kuwa "Mzanzibara"
 
Swadaqta.
Sasa yeye hivi leo ni Muarabu au Muirani (muajemi)???, ---kwasababu yeye anajiita Mzanzibari aliyehuru kana kwamba wapo wazanzibar waliopo utumwani.
 
Sawa kabisa.

Hoja ni nani kayaandika na katika muonekano gani.

Na yule ambaye hakuandika je, tuchukulie kwamba yeye hakuwepo, hakuwa na lolote?

Na kama kaandikwa sivyo, tukubali tu kwamba ndio ukweli kwa kuwa kaandikwa hivyo?

Mkuu Kalamu

Yapo mengi yaliondakiwa na watu tuliowaona siku wanafika znz na baba zao kwa ajili ya kuchuma karafuu. Ukitaka kusoma historia ya znz waloziandika hao, uwe unasoma kabla ya kupata chakula kwasababu uanweza kutapika. Wamedanganya sanaaa.
 
Mtoa mada anapotosha, sijui kama anajua kuwa hakuna watu wanaoitwa Wairan. Iran kuna waajemi, waarabu, wayahudi na waazeri. Hoja ya kuwa wa kwanza kuwa na umeme, lift au simu ni hoja mufilisi.

Unaposema waafrika walikuja Zanzibar unataka kumaamisha kuwa waafrika walivamia waarabu? Zanzibar ilikuwa tajiri mwaka 1886? Utajiri ulitokana na nini?

Mkuu Bongolander

Nikisema Iran, kila anayejua historia anafahamu kwamba ninazungumiza Persia au Uajemi. Kwahivyo mkuu sipotoshi mtu bali najaribu kuweka wazi zaidi kwa wasomaji wote.

Jengine labda wewe huoni umuhimu wa kuwa na umeme na malift na simu, siwezi kukulaumu kwa hilo sio kosa lako baba, hayo ndio matunda ya ukomunist. Yaani nakumbuka mukiambiwa TV ni anasa, simu ni anasa, mulilelewa hivyo, yaani ndivo mulivoelekezwa kufahamu. Mandeleo kwenu labda sio muhimu sana,

Ninaposema Waafrika walikuja zanzibar nimekusidia waafrika walikuja zanzibar, yaani waliletwa kwa ajili ya kusaidia kazi, wazanzibari walikuwa hawatoshi kuendesha uchimi wa siku hizo. Na si waafrika bali watu wengine pia kwahivyo watanganyika, wakenya, wamalawi, waturuki, wanganzija wote waliletwa znz kusaidi kupandisha uchumi zaidi. Zanzibar ilikuwa ni kituo cha biashara kama vile Dubai leo.

Zanzibar ilikuwa tajiri sana sana sana sana katika mwaka huo wa 1886. Miaka michache nyuma pale 1862 Kiongozi imara, shupavu, mwenye kuona mbele, mjasirimali mkubwa Sultan Majid Bin Saeed aliamua kujenga mji mpya huko tanganyika katika eneo lilokuwa likiitwa mzizima, mji huo akauita kwa jina zuri sana "Dar es Salaam". Bila pesa hujengi nyumba wachilia mbali mji mpya.
 
Back
Top Bottom