Ni Nani hasa Mwenyeji wa Zanzibar? Je, ni Muafrika, Muarabu, Mshirazi au wote?

Ni Nani hasa Mwenyeji wa Zanzibar? Je, ni Muafrika, Muarabu, Mshirazi au wote?

Mkuu mzanzibari huru.

Wewe unajiita Mzanzibari tena uliyekuwa huru, je na wewe ni mzanzibara??.

Juu ya yote usiogope kusema ukweli kwani ukweli huumiza pia huleta faraja na kuwaweka watu huru.

Ili tupate faraja na uhuru wa mawazo basi hunabudi kuweka jambo hilo wazi, hiyo ni historia na wala sio ngano za Alfu lela ulela.

Mkuu Mokaze

Mimi kwa bahati mzuri ni 50/50 Mzanzibari + Mzanzibara, siwezi kuliepuka hilo.

Nikijiita mzanzibari huru maana yake najisikia niko huru kifikra, ikiwa fikra zangu mzuri au mbaya it doesnt matter to me. Pamoja na kwamba najihisi niko huru kifikra, lakini bado mada ya mapinduzi sihisi kwamba ni sahihi kuizungumza tena katika karne hii, sijawahi kuwazungumzia watoto na wajuu zangu. Na kwa bahati mzuri nahisi watoto wa kizanzibari asilia ijapokuwa wamemix kidogo lakni ndio wanaotawala sasa kote kote.
 
Zanzibar iligunduliwa rasmi na Waajemi wakati Bantu expansion ililuwa inasogea polepole
 
Kwa hiyo Zanzibar ilikuwa na kiwanda Cha kutengeneza magari?

Mkuu Saigoni

Hili ndio tatizo la kuubana ukweli kwa jamii. Zanzibar haiukuwa na kiwanda chochote wachilia mbali cha gari. Zanzibar ilikuwa kituo kikubwa chao cha biashara kwa afrika mashariki na kati. Kama vile unavoona Singapore na Dubai leo.

Hilo soko lilijengea zanzibar sifa kubwa sana. Katika mwaka 1837 USA ilifungua ubalozi wake Zanzibar, balozi wa kwanza alikuwa Mr. Richard Waters kutoka Salem, Massachusetts. British alifungua ubalozi 1841. French 1844, German 1857.

Si hapo tu, wale explorers wote waliotaka kuingilia maeneo ya Africa mashairki walikuwa wakija znz kwanza ili kupanga safari zao hizo. Wavumbuzi kama vile Richard Button 1856, John Speke, Dr Livingston 1866 na kaburi lake lipo znz, Henry Stanley 1871. Huy Stanley ndie anliejidai kulivumbuwa lake Victoria, lakini ukweli ni kwamba alipekwa safari hiyo na Mzanzibari maarufu sana Tip Tip.
 
Mkuu Mokaze

Mimi kwa bahati mzuri ni 50/50 Mzanzibari + Mzanzibara, siwezi kuliepuka hilo.

Nikijiita mzanzibari huru maana yake najisikia niko huru kifikra, ikiwa fikra zangu mzuri au mbaya it doesnt matter to me. Pamoja na kwamba najihisi niko huru kifikra, lakini bado mada ya mapinduzi sihisi kwamba ni sahihi kuizungumza tena katika karne hii, sijawahi kuwazungumzia watoto na wajuu zangu. Na kwa bahati mzuri nahisi watoto wa kizanzibari asilia ijapokuwa wamemix kidogo lakni ndio wanaotawala sasa kote kote.


Kumbe wewe ni: Mzanzibari+ Mzanzibara, sasa kwanini ujiite Mzanzibari (waarabu na Wairani) pekee???, uzanzibara wako unauweka wapi??
 
Pia kuna zambi ya kudhulumu Waajemi walidhulumiwa na Waomani na Waomani wamedhulumiwa na Mataga

Ogopa dhambi ya kudhulumu
 
Kuna mtu wa ajabu anadai, mtu mweusi wa kwanza alipelekwa Zanzibar kufanya kazi? Aliokotwa mahali fulani, sijui wapi, Tanganyika(?) akapelekwa Zanzibar!
Maana yake ni kwamba, hao watu weusi waliopo Zanzibar, wote sio watu wa hapo!

Sasa maajabu ni kwamba, kuna baadhi yao wanajivunia kuwa Wazanzibari, bila kujua kwamba wenye nchi yao wanawaona wao kuwa wageni/ watumwa tu!

Mkuu Kalamu

Najuwa hili ni shida kukubaliana lakini wewe umesoma sana. Hebu tafuta sababu moja tu ya msingi kwanini mtanganyika au muafrika mwengine yoyote alikuwa na shida ya kusafiri hadi visiwani zanzibar katika miaka ya 500s AD.

Tukizingatia kwamba Waafrika walikuwa wamejiweka kikabila, shida zao zilikuwa kuwinda, kulima na jioni kudance. Mtazamo wa Maisha yao hayakuwa wa malengo ya maendeleo yoyote, yaani walikuwa wakiishi kwa mila na desturi zao tu. Kitu gani unadhani kingewafanya kusafiri hadi znz?
 
Kumbe wewe ni: Mzanzibari+ Mzanzibara, sasa kwanini ujiite Mzanzibari (waarabu na Wairani) pekee???, uzanzibara wako unauweka wapi??

Mkuu

Ukweli hauna mwenyewe. Kwani kuna kosa gani kusema ukweli?
 
Kabla Wabantu na wengine wa kuja hawajafika Tanganyika toka Kaskazini, waliwakuta wenyeji ambao bahati nzuri mpaka leo Kabila moja jasiri bado lipo, hawa ni Wasandawi wa Kondoa. Wairan na Waarabu ambao walikuja Karne nyingi baadaye, walikuta Zanzibar haina watu? Stupid Msukuma!
 
Mkuu Kalamu

Najuwa hili ni shida kukubaliana lakini wewe umesoma sana. Hebu tafuta sababu moja tu ya msingi kwanini mtanganyika au muafrika mwengine yoyote alikuwa na shida ya kusafiri hadi visiwani zanzibar katika miaka ya 500s AD.

Tukizingatia kwamba Waafrika walikuwa wamejiweka kikabila, shida zao zilikuwa kuwinda, kulima na jioni kudance. Mtazamo wa Maisha yao hayakuwa wa malengo ya maendeleo yoyote, yaani walikuwa wakiishi kwa mila na desturi zao tu. Kitu gani unadhani kingewafanya kusafiri hadi znz?
Zambi mbaya


Ila ukweli ni kwamba zanzibar ni hao watu wanaoishi hapo
Asili hutengenezwa,mila pia huundwa, lugha nayo ni sanaa kama sanaa nyingine kikubwa ishi acha kufuatilia vitu ambavyo havina msingi
 
Mara nyingi huwa ninajiuliza, hivi huu muungano wetu mbona una kelele nyingi hivi. Sasa sina shaka yoyote na mahala kelele zinapotoka.

Bila shaka, wengi watakaoisoma hii makala wataielewa barabara kama nilivyoielewa mimi.

Sijui kama kutakuwepo na mzalendo yeyote wa nchi hii atakayekuwa na mashaka zaidi tena juu ya hatma ya nchi yetu Tanzania.

Ni hivi: Iwe Wazanzibar au Wazanzibara - Hawa wazanzibara hata kama hawakuwepo huko wakati babu zako wakivamia ardhi ya waafrika toka mbali huko kwao, sasa hivi hawa wazanzibara Zanzibar ni yao, Tanzania ni yao.
Huna njia tena ya kuwaondoa hapo walipo hata kama hawakuwepo hapo mwanzo kama unavyodai wewe.

Huwezi kuwafukuza, huwezi kuwafanya watwana/watumwa tena na wala huwezi kuwaua wote ili ubaki na Zanzibar.

Sasa ni juu yako ukubali wewe kuwa mtumwa wa hawa uliowafanya watumwa wako enzi za babu yako.

TANZANIA ITADUMU MILELE.

Mkuu Kalamu

Kuhusu muungano, labda litakushangazi hili, mimi binafsi naupenda na ninauhitajia. Muungano unalinda usalama wa zanzibari wa aina fulani fulani, ni bora kwetu kuwepo milele. Mie halinikeri kwamba rasi wetu wanachaguliwa dodoma, wacha achaguliwe popote pale lakini muungano uwepo na udumu.

Ikiwa kutakuwa na issue yoyote kuhusu kuwepo kwa Tanznaia, lizingatie hili, shida hiyo itafanywa na Watanganyika, na katika uchaguzi uliopita tumeanza kuona cheche zikianza. soon watanganyika watalazimisha kuwepo kwa nchi na serikali yao ya tanganyika.

Mwarabu hakuchukuwa ardhi ya mtu kwa sababu hapakuwa na mwenyewe zanzibar. Hilo halitaki darubini.

Kuhusu utumwa, ndio ulokuwa mtindo wa siku zile kabla ya industrila revolution, kwahivyo waarabu wazaungu, hata waafrika wenyewe kwa wenyewe walifanyana watumwa.
 
Mkuu Bongolander

Nikisema Iran, kila anayejua historia anafahamu kwamba ninazungumiza Persia au Uajemi. Kwahivyo mkuu sipotoshi mtu bali najaribu kuweka wazi zaidi kwa wasomaji wote.

Jengine labda wewe huoni umuhimu wa kuwa na umeme na malift na simu, siwezi kukulaumu kwa hilo sio kosa lako baba, hayo ndio matunda ya ukomunist. Yaani nakumbuka mukiambia TV ni anana, simu ni anasa, mulilelewa hivyo, yaani ndivo mulivoelekezwa kufahamu. Mandeleo kwenu labda sio muhimu sana,

Ninaposema Waafrika walikuja zanzibar nimekusidia waafrika walikuja zanzibar, yaani waliletwa kwa ajili ya kusaidia kazi, wazanzibari walikuwa hawatoshi kuendesha uchimi wa siku hizo. Na si waafrika bali watu wengine pia kwahivyo watanganyika, wakenya, wamalawi, waturuki, wanganzija wote waliletwa znz kusaidi kupandisha uchi zaidi. Zanzibar ilikuwa ni kituo cha biashara kama vile Dubai leo.

Zanzibar ilikuwa tajiri sana sana sana sana katika mwaka huo wa 1886. Miaka michache nyuma pale 1862 Kiongozi imara, shupavu, mwenye kuona mbele, mjasirimali mkubwa Sultan Majid Bin Saeed aliamua kujenga mji mpya huko tanganyika katika eneo lilokuwa likiitwa mzizima, mji huo akauita kwa jina zuri sana "Dar es Salaam". Bila pesa hujengi nyumba wachilia mbali mji mpya.
We naona unawapigia debe waarabu
Unachotaka kutuaminisha zanzibar ni
Nchi ya waarabu
Ila elewa hii zanzibar ni sehemu ya tanzania
Siyo waarabu,tunajua hapo marabou aliacha mbegu

Ova
 
Ndugu Wana Jukwaa

Kuna maneno mengi yasioningia katika mizani ya akili yanayozungumzwa na watu hasa wenye asili ya Tanganyika kuhusu Zanzibar na Uzanzibari. Watu wamekuwa wakiunda historia ya zanzibar kutoka katika hisia na wivu wao binafsi. Historia ya kuunga unga vipande, historia isio na kichwa wala miguu.

Ikiwa unahaitaji kuijuwa Zanzibr na Wazanzibari, soma hadi mwisho

Mtu wa mwanzo kabisa kuweka mguu wake katika ardhi ya Visiwa vya Zanzibar ni wa Iran and waarabu. Ukitaka kujuwa hilo tizama katika picha na vifaa vya kale. Kwahivo Zanzibar imejengwa na kuimarishwa na waarabu na wairani. Ni haki kabisa kusema kwamba Zanzibar ni sehemu ya Urabuni. Hilo si ajabu kwasababu ndani ya Afrika zipo nchi za Kiarabu. Kwahivyo wachilia mbali kwamba Zanzibar iko pembeni kwa Afrika. Muafrika wa kwanza kufika Zanzibar katika wanaume aliletwa kwa ajili ya kuimarisha kilimo kwasababu waafrika walionekana ni wakulima mahiri sana na katika wanawake waliletwa kwa ajili ya kuolewa. Hakuna Mtanganyika au Muafrika yoyote Zanzibar alokuja kwa hiyari yake katika miaka ya mwanzoni ya karne za 13, 14, 15, 16 na 17 hata mwanzoni mwa karne ya 18

Kwanini Waarabu na Wa Irani ndio walikuja mwanzo Zanzibar?

Kwasababu watu wa Tanganyika walikuwa hawana sababu yoyote ya kuvuuka bahari na kuja Zanzibar. Watanganyika walikuwa na maisha yao yanayowatosha wenyewe, matunda, kilimo na wanyama. Na hakuna ushahidi wowote kwamba watanganyika walikuwa wakiunda majahazi au kama walikuwa ni mabaharia kama vile walivyokuwa Waarbu na Wa Irani.

Nani Kaitwala Zanzibar katika historia

Waarabu walifanya utawala wa kwanza na bora sana Zanzibar. Na nakuombeni musibabaishwe na majina ya watawala wa zamani wenye majina kama vile Mkama ndume an Mwinyi Mkuu, wote hao walikuwa waarabu. Katika utawala bora wa Zanzibar maendeleo yakawa makubwa watawala wakaona haja ya kuitanua dola ya zanzibar, ndio Tanganyika na nchi zote za afrika mashariki ikiwemo na DRC na Mozambique zikawa katika Zenj empire. Neema kubwa zilipatika kwa kufikiwa na utawala bora, watu wengi kwa mara ya kwanza wakafundishwa kuvaa nguo na usafi na mengineo.

Kwanini kuna Wazanzibari weusi?

Baada ya maisha kuanza, watu wa Zanzibar (waarabu na wairani) wakawa wanahitajia kuowa ndio hapo walipoanza kulekea mrima kutafuta wachumba. Bagamoyo, Kilwa kivinje na kwengineko. Hilo lililetea kupatika wazanzibari wenye rangi nyeusi. Marco Polo alipofika zanzibar alikuta wenyeji wa hapo ni weusi wenye nywele za singa.

Maisha bora yalikuwa zanzibar

zanzibar chini ya uongozi shupavu wa waarabu ilifika mbali kimaisha. Zanzibar ilikuwa na simu majumbani manano mwaka 1886, undersea cable zilitoka znz kupita Aden hadi London. Zanzibar ilikuwa nchi ya Mwanzo Afrika kutumia elevator, pale Beit el Jaibu. Zanzibar ilikuwa nchi ya tatu kutumi aumeme duniani.

Elimu ilikuwa kubwa sana zanzibar hata NASA waliweka tracking station Zanzibar. Zanzibar ilikuwa nchi tajiri sana katika Africa, wafanyakazi wa zanzibari walikuwa wakisafiri kama watalii wakati wakipata likizo zao makazini. Gari la kwanza kutembea Kuwait lilinunuliwa Zanzibar, nchi za Uarabubi zilikuwa zinakuja znz kununua vyakula na nguo kama leo tunavyokwenda Dubai sasa.

Zanzibar ilikuwa nchi huru ndio maana waafrika waliokuja kufanyakazi na kutafuta maisha yao tu waliachiliwa kuingia katika siasa, kosa kubwa sana hilo. Wakafanya mapunduzi na kuuwa wazanzibari 17,000 usiku mmoja. Baada ya hapo Zanzibar inaakza kufa kidogo kidogo. Leo hii watuna tena chetu,
Hii story yako naifananisha na ile ya Waisrael na Wapalestina ya nani mwenye haki na nchi ya Palestina. Kwa hii story yako ni wazi Waisrael wanahaki na nchi ya Israel na hao waarab au wapalestina ni wavamizi
 
Mkuu

Ukweli hauna mwenyewe. Kwani kuna kosa gani kusema ukweli?


Sijakuelewa au hujanielewa. (Hatujafahamiana).

Kama nilikuelewa vyema, ulisema MzanzibarI ni Muarabu au Muirani na MzanzibarA ni Muafrika kutoka nje ya Zanzibar, Wewe ni mchanyiko wa MzanzibarI na MzanzibarA, swali ni hili; Kwanini wewe wajiita MZANZIBARI na umesahau kwamba wewe ni mchanganyiko kati ya MzanzibarI na MzanzibarA huo uzanzibarA unautupa wapi???
 
Kabla ya kufikiwa na Hassan Bin Alli na watoto wake saba, Zanzibar ilikuwa tupu hakuna mtu hata mmoja. Kumbuka kwamba Zanzibar ni visiwa na nilazima uvuke bahari kuvifika. Waafrika wa Afrika Mashariki kazi zao ilikuwa kuwinda na kulima sio kuunda majahazi. Siamini pia kwamba waliweza kuogelea baharini wakafika Zanzibar. Pia kusafiri kwa miaka ile ilitokana na utashi wa kutaka kukusanya mali zaidi, watanganyika leo hii hawaijali mali yao unadhani walikuwa na utashi wa kutafuta mali zaidi katika maelefu ya miaka iliyopita? Besides, Zanzibar haikuwa na mali yoyote isipokuwa majahazi yalikuwa yakuchukuwa maji tu hapo miaka hiyo. Mtanganyika alikuwa hana shida na maji ya Zanzibar kipindi hicho.

Muafrika wa kwanza kufika znz aliletwa kwa ajili ya kazi tu.
Na hapa mimi ndio nilihitimisha kwa kusema kuwa hawa wazenji weusi wote ni watanganyika tu ambao pengine asili yao ilikuwa ni wale watumwa waliopelekwa kule zenji
 
Sijakuelewa au hujanielewa. (Hatujafahamiana).

Kama nilikuelewa vyema, ulisema MzanzibarI ni Muarabu au Muirani na MzanzibarA ni Muafrika kutoka nje ya Zanzibar, Wewe ni mchanyiko wa MzanzibarI na MzanzibarA, swali ni hili; Kwanini wewe wajiita MZANZIBARI na umesahau kwamba wewe ni mchanganyiko kati ya MzanzibarI na MzanzibarA huo uzanzibarA unautupa wapi???
Hahah yeye atakuwa mzanzibaria huyo
 
Labda kweli ikiwa utaanza kutizama kijuu juu utaona maneno hayo ni ya upendeleo kwa upande fulani. Lakini Zanzibar ni visiwa, wewe unajuwa wazi kwamba hata leo hii ukitaka kuja znz ni lazima upande boti au ndege. sasa miaka ya maelfu iliyopita unadhani mwafrika gani wa afrika mashariki alokuwa hakuhitajia usafiri wa baharini kufika znz. Jiulize Mtanganyika alikuwa ana shida gani znz? Znz haikuwa pori la wanyama ukasema wamekuja kuwinda, wala watanganyika hawakuwa na uhaba wa matunda yao na vyakula vayo nini ikilikuwa kiwapeleke znz?
Kwa hiyo unasema kuwa wabara hawakuwepo zanzibar ila wazenji walikuwepo huko wakiendelea na maisha miaka hiyo ?
 
Mkuu mzanzibari huru.

Wewe unajiita Mzanzibari tena uliyekuwa huru, je na wewe ni mzanzibara??.

Juu ya yote usiogope kusema ukweli kwani ukweli huumiza pia huleta faraja na kuwaweka watu huru.

Ili tupate faraja na uhuru wa mawazo basi hunabudi kuweka jambo hilo wazi, hiyo ni historia na wala sio ngano za Alfu lela ulela.

Mkuu tungenanzia hapa unafahamu maana ya hilo neon Mzanzibara?
 
Back
Top Bottom