Ni nani huyu Oumilkheir wa DW!!?

umriheri ni mweusi toka Mombasa Kenya na sekioni kitojo ni mbongo alitokea radio Tanzania katikati ya miaka ya tisini enzi za kusikiliza redio kwa mwenyekiti Wa kijiji,kamanda Wa sungusungu au kwa mwalim mkuu

Umuru Kheir ni kutoka Comoro, kama hujui kitu piga kimya.
 
Ana mahirizi huyu jamaa yanapumua kama kinyonga

Naweza kukuamini, maana kutoka mpiga picha wa mitaani mpaka kuwa kwenye Top delegation ya Rais!! Kweli kuna watu wanajuwa kuroga mwe!
 
Huyu mtangazaji ni shida, me mwenyewe natamanigi kumfahamu anastahili fulani hiv ya kutangaza inayovutia sana kumsikiliza

Ni shida ina maana anamatatizo?? me unamaanisha ni mwanaume?? namtamanigi ndio unamtamani au unapenda anavyotangaza?? anastahili una maanisha anapaswa kuwa hapo au unamaanisha nini??.... michango mingine inazua maswali kuliko majibu!! Jirekebishe kwa faida yako mwenyewe!!!
 
Mimi simkubali hata kidogo huyu mtangazaji

yaani kwa kuwa ana rafudhi ya kizungu basi waswahili huwaambii kitu!! kila mtu anasema anamkubali!! angekua na rafudhi ya kisukuma hapa angedhalilishwa yeye na wazazi wake!! ama kweli ujinga mzigo! miafrika ndivyo tulivyo
 
Mambo mengine, una google tu!,
All and all, best wangu Abou Liongo, alikuwa DW, nitawaulizia na kuwajuza!.

Thanks.

Pasco

Mkuu Pasco, hivi Abdulrahim Katani ni mtanzania? Alikuwa mtangazaji mahiri Deutsche Welle Radio- Idhaa ya Kiswahili. Na je una taarifa zake yuko wapi siku hizi?Inatajwa kuwa hapo zamani kabisa BBC na DW zilikuwa moja, je mkuu Pasco ushasikia jambo hilo?

Je mkuu Pasco, Shida Waziri na Shida Masamba ni mtu mmoja pale TBC(RTD enzi hizo)?

Kama kuna mwenye audio clip za milio hii ya iliyokuwa RTD atuwekee tujikumbushe:-
1. Mazungumzo baada ya Habari
2. Kipindi cha Jambo
3. Kipndi cha pole kwa kazi
4. Kipindi cha Majira
5.Kipindi cha Michezo
6. Ugua pole
7.Pwagu na Pwagusi
8. Mahoka
9.Mkulima wa Kisasa
10. Kipindi cha Idara ya Uhamiaji
11. Ijue Mahakama yako kilichokuwa kinaratibiwa na marehemu SS Nkamba( sound track ya kipindi hiki ni wimbo wa Baba Jane Bye Bye Namba 2 ambao ni wa Hamza Kalala akiwa na Bantu Group Band)
12.Club Raha leo Show

Milio yote au baadhi kama mtu anayo atakuwa ametukumbusha mbali sana na nitashukuru mimi binafsi na naamini hata wadau wengine watafurahi!
 
Mkuu Pasco umekosa yote hayo niliyoyaomba?
 
Huyu ni Mzanzibari mwenye asili ya Comoro! though ana close tie na jamaa zake wa comoro kama ilivyo destruri ya watu wenye asili ya comoro.wananyumba zao maeneo ya kikwajuni zanzibar.
 
Duruu za umoja wa mataifa au maafisaa waandamizi nchini lebanon........kwa kwel na mm nlkua cfaham jinsia yake ila saut yake hakuna dunia nzima mwana mama mkareee balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…