Ni nani nje ya CHADEMA alimfahamu Mzee Ally Kibao kabla ya mkasa uliotokea?

Ni nani nje ya CHADEMA alimfahamu Mzee Ally Kibao kabla ya mkasa uliotokea?

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
22,898
Reaction score
33,309
Matukio mengi ya utekaji, na kuuawa kwa vijana wengi; hasa wafuasi wa CHADEMA yamehusishwa na maneno waliyo husishwa nayo yakielekezwa kwa viongozi au chama cha Mapinduzi. Maneno yaliyosemwa au kuandikwa kwenye mitandao.

Tofauti na hao wengine wote, yaliyomtokea Mzee Kibao kidogo yanaonekana kuwa tofauti na haya ya wengine. Huyu mzee, nje ya CHADEMA hakufahamika, na wala hakuwahi kuhutubia mkutano wa hadhara na kutamka maneno ambayo watu wangeyafikiria kuwa sababu ya yaliyo mtokea.

Na wala yeye asingeweza kuhusishwa na mkasa uliomfuata Padre Kitima; kwa sababu, hata kuhojiwa na vyombo vya habari hakuwahi kufanya hivyo.


Sababu inayoelezea kilicho mtokea, ni maswala yaliyokuwa yanasemwa ndani ya chama chake; bila ya kuyatoa nje ya chama.

Lakini kwa sababu hiyo, matokeo ya kilicho mata ni kile kile kilichowapata na wenzie wote; wale vijana waliopotea na wengine kuuawa; na wengine kunusurika, kama ilivyotokea kwa Padre Kitima.

Kwa sababu hiyo, ni sahihi kuhitimisha kwamba, mhusika wa matukio yote hayo anatokea sehemu moja.
Mzee Kibao aligusa maslahi ya mtu/kundi lile lile linaloguswa na hawa wengine wote waliopatwa na mikasa ya kupotea au kuuawa.
 
Sababu inayoelezea kilicho mtokea, ni maswala yaliyokuwa yanasemwa ndani ya chama chake; bila ya kuyatoa nje ya chama.
Utekwaji na kuuliwa Kibao una utata mwingi.

Kuna sehemu Chalamila kanukuliwa akisema si wote wanaotekwa na kuuliwa serikali inahusika nao. Hii maana yake ni kwamba wapo baadhi ya wanaotekwa na kuuawa na serikali, na wengine kuhusishwa na makundi mengine.

Nakubaliana naye 100%.

Kinachotatiza pengine ni vipi serikali ishindwe kuyafahamu na kuyadhibiti makundi hayo mengine?
 
Pale chadema inaonekana kuna /?mtu/watu ambao kazi yao ni kupeleleza, kukusanya taarifa, kuzichambua na kuzifikisha kunaohusika..
Huyo mtu/watu bado wanachadema wenyewe hawajamjua.

Yupo cool sana, ni mchapakazi mzuri wa kazzi za chama, hapati bughhdha kutoka kwnye vikundi vya watekaji

Na hata akibughdhiwa huwa ni kwa ajili ya kuwazuga raia.

Ni kama MOSSAD ndani ya IRAN

huyo ndie huwachoma wenzake na kwemye misiba ni mhudhuriji mzuri
 
Mzee Kibao alisema juu ya hela aliyokuwa anagawa Abdul kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa Chadema na aliahidi kuweka wazi kila kitu na kabla ya kufanya hivyo yakamkuta yaliyomkuta. Hapa lazima kuna mkono wa mtu mzito ndani ya Chadema alihusika kwa kushirikiana na Dola. Jee ndani ya Chadema nani alikuwa na mahusiano yanayotia shaka na mhimili uliojichimbia,na kilichotokea kwenye maziko ya Mzee Kibao kule Tanga na kwa kumalizia na huu ukimya wake na kujitenga kabisa na Chadema. Asomae na aelewe.
 
Na mimi nilikuwa sijui, baadae nikasikia alikuwa mwanajeshi, akawa karibu na mkiti wa sasa kuandaa namna ya kuunda Jeshi la uasi kwa siri, na yeye ndiye aliandaa mpango kazi, baadae kila gololi ikatumbukia katika shimo lake
 
Hii ilinipita, kulitokea nini kwenye mazishi?
Waombolezaji walichukizwa na uwepo wa Waziri wa Mambo ya ndani kwenye maziko hayo na walitaka aondoke na asipewe nafasi ya kuongea lakini Mbowe alimkingia kifua jambo ambalo liliwaudhi sana waombolezaji kwani waliamini Waziri huyo ndiye boss wa waliotuhumiwa kumuua Mzee Kibao. Kwa nini Mbowe alikuwa upande wa mtuhumiwa wa mauaji?
 
Utekwaji na kuuliwa Kibao una utata mwingi.

Kuna sehemu Chalamila kanukuliwa akisema si wote wanaotekwa na kuuliwa serikali inahusika nao. Hii maana yake ni kwamba wapo baadhi ya wanaotekwa na kuuawa na serikali, na wengine kuhusishwa na makundi mengine.

Nakubaliana naye 100%.

Kinachotatiza pengine ni vipi serikali ishindwe kuyafahamu na kuyadhibiti makundi hayo mengine?
Unataka kusema wale waliobeba silaha na kusimamisha Basi njiani kwamba sio watu wa system?

Iko wazi serikali inahusika na mauwaji ya mzee Kibao kwa asilimia mia.

Kama haihusiki Kwanini mpaka leo majibu ya uchunguzi wa Kifo chake hayajatolewa?
 
Pale chadema inaonekana kuna /?mtu/watu ambao kazi yao ni kupeleleza, kukusanya taarifa, kuzichambua na kuzifikisha kunaohusika..
Huyo mtu/watu bado wanachadema wenyewe hawajamjua.

Yupo cool sana, ni mchapakazi mzuri wa kazzi za chama, hapati bughhdha kutoka kwnye vikundi vya watekaji

Na hata akibughdhiwa huwa ni kwa ajili ya kuwazuga raia.

Ni kama MOSSAD ndani ya IRAN

huyo ndie huwachoma wenzake na kwemye misiba ni mhudhuriji mzuri
Je bado yupo??????
 
Back
Top Bottom