Kinkunti El Perdedo
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 5,200
- 12,762
Hii nchi ina wajinga wengi Sana mkuu walio kuwa wanatetea maslahi ya taifa waliitwa wasaliti na wanatumiwa na madume ya mbuzi uko ulaya wale wapiga meza ndo walijiona wazalendo nambari moja leo kiko wapi na ndo walikuwa wanaimba mapambio ya umeme wa gesi.Nakumbuka kipindi hicho wabunge wa upinzani wakiongozwa na Tundu Lissu na John Mnyika walipinga kweli kweli kupitishwa kwa ule muswada wa sheria kuhusu hiyo gesi ya Mtwara, kwa kutumia hati ya dharura! Tena usiku wa manane!
Ila cha kushangaza, wabunge wa ccm walikuwa wanagonga tu meza kwa furaha! Na JPM alikuwa ni mmoja ya hao wabunge, na pia Waziri. Wananchi wa Mtwara walipigwa mpaka mabomu!
Matokeo yake ndiyo haya sasa. Gesi ya Mtwara ni mali ya mabeberu.
Ndo Yale Yale ya bwana Ndugai kushangaa sheria ya tanapa kuhusu mifugo