Ni nani yuko nyuma ya uozo Shule za Wazazi (CCM)?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Nimepita kwenye shule mbili za jumuiya ya wazazi CCM hapa mkoani mbeya yaani Meta sc na Sangu SC, ambazo kwa miaka ya nyuma zilisifika na kutukuka kwa kufanya vizuri sana na kuvutia watu wengi ndani na nje ya nchi.

Kilichonisikitisha ni namna shule hizi zilivyotafunwa na uongozi mbovu na kila aina ya uozo ambao umezifanya hizo shule kuporomoka vibaya sana.

Niliongea na baadhi ya waalimu wanalalamika kwamba kila kiongozi anayejaribu kuja kutatua changamoto za shule hizo, anatishwa na kunyamazishwa.

Waalimu na watumishi wengine wa hizo shule Wana madai mengi sana na kusema kweli wamekata tamaa ila cha ajabu ni kwamba hakuna anayethubutu kutatua kero zao!
 
Shule ya Wazazi Meta, Mbalizi sec na Sangu pia Ivumwe zinafanya vizuri academically kwa huku Mbeya. Sijajua hizo Dumila za Morogoro.
 
Umezipitia lini mkuu au na wewe ni mnufaika w kuporomoka kwa shule hizo, maana si kwa utetezi huu!!
 
Nimepita kwenye shule mbili za jumuiya ya wazazi CCM hapa mkoani mbeya yaani Meta sc na Sangu SC, ambazo kwa miaka ya nyuma zilisifika na kutukuka kwa kufanya vizuri sana na kuvutia watu wengi ndani na nje ya nchi.

Kilichonisikitisha ni namna shule hizi zilivyotafunwa na uongozi mbovu na kila aina ya uozo ambao umezifanya hizo shule kuporomoka vibaya sana.

Niliongea na baadhi ya waalimu wanalalamika kwamba kila kiongozi anayejaribu kuja kutatua changamoto za shule hizo, anatishwa na kunyamazishwa.

Waalimu na watumishi wengine wa hizo shule Wana madai mengi sana na kusema kweli wamekata tamaa ila cha ajabu ni kwamba hakuna anayethubutu kutatua kero zao!
Hata shujaa kwa miaka yake 5 hakusovu hizo chalenji?
 
Warudishe soko la uhindini ukipiga nyama choma(mishkaki)na ugali kisha ukazamia maktaba ya mkoa ndio utajua unajua nyakati za digit za maana. Likizo ni nondo tu.
 
Umezipitia lini mkuu au na wewe ni mnufaika w kuporomoka kwa shule hizo, maana si kwa utetezi huu!!
Juzi kati tu hapa. Sema Nini ukisema shule zote zimeporomoka naweza kutataa ila ukisema baadhi ya shule naweza kukubali.
 
Juzi nilipita Kanawa Secondary School (Kishapu) na Lalago Secondary School (Maswa) zote ziko Chini ya jumuiya ya Wazazi na hali zake ni mbaya
 
Bulembo huyo
Ongeza na UDALALI ULIOTUKUKA miradi ya REA phase 3. Ni kichefuchefu. Ila huwa najiuliza JEURI ya watu aina hii "kubaka" haki, .. rushwa ni adui mkuu wa haki... wanaupata wapi. Au tuamini ya kwamba "GODFATHER" wa kudumu yupo na akipata mrabaha wake wabakaji wanapeta tu?
 
Juzi kati tu hapa. Sema Nini ukisema shule zote zimeporomoka naweza kutataa ila ukisema baadhi ya shule naweza kukubali.
Ndugu sio kificho pale mbeya mjini hakuna mwenye ubavu wa kufanya lolote kwenye shule hizi labda aje mwenyekiti taifa zimeandikwa barua nyingi za malalamiko lakini hakuna mwenye ubavu wa kuzitatua
 
Rafiki angu, Kuna kitu kidogo Sana tumetofautiana. Kwanza Mimi binafsi Sina historia kamili za ubora wa hizi shule hapo awali japo shule kama Sangu ilikuwa maarufu Sana zamani,Hata meta pia.Kwa Sasa zinatembelea umaarufu wa zamani.

Sasa ukija kwenye taaluma bado performance zipo kawaida sana.lakini kwa Miundombinu Sangu na Mbalizi ziko powa sijajua kwa Meta.Dumila secondary nilifika mara moja,mazingira yalikuwa ya kawaida kwa shule za private.
Lakini pia ukiondoa Meta shule zote Zina wanafunzi wengi tu.Inamaana bado zinapata pesa za kutosha hata kujiendesha.

Kwa hiyo kama Kuna changamoto zote basi ni suala la uongozi mbaya kwa kuwa bado shule zinawanafunzi wengi na wanalipa ada kubwa tu.

Ni Suala la CCM wenyewe kukaa na kurekebisha.wakishindwa shule zitakuwa zinaliwa na wachache.Wakuu wengi wa hizi shule wa Zamani ,Sasa hivi wana shule zao,ambazo pesa bila shaka walipiga kutoka shule za wazazi.

Ukiondoa shule za wazazi,bado Kuna usiri kwenye miradi mingineyo ya chama kama vile viwanja wa michezo na maduka/masoko.
 
Bulembo alifaa awe Jela, kwa kuhujumu hizi shule na nyingine kuuzwa kinyemela.
 
Nimepita kwenye shule mbili za jumuiya ya wazazi CCM hapa mkoani mbeya yaani Meta sc na Sangu SC, ambazo kwa miaka ya nyuma zilisifika na kutukuka kwa kufanya vizuri sana na kuvutia watu wengi ndani na nje ya nchi.

Kilichonisikitisha ni namna shule hizi zilivyotafunwa na uongozi mbovu na kila aina ya uozo ambao umezifanya hizo shule kuporomoka vibaya sana.

Niliongea na baadhi ya waalimu wanalalamika kwamba kila kiongozi anayejaribu kuja kutatua changamoto za shule hizo, anatishwa na kunyamazishwa.

Waalimu na watumishi wengine wa hizo shule Wana madai mengi sana na kusema kweli wamekata tamaa ila cha ajabu ni kwamba hakuna anayethubutu kutatua kero zao!
Mkuu kwa Bahati nzuri nilisoma shule inayomilikiwa na CCM inaitwa Nyangao Secondary School inapatikana jimbo la Mtama Mkoani Lindi.

Nafaham kuwa ile shule iliuzwa na Jumuiya ya Wazazi chini ya Mzee Bulembo.

Kwasasa muonekano wake ni huu hapa chini.
PMO_6154.jpg
 
Kumbe ccm inafanya biashara ya elimu kwa kumiliki shule pia? Ahaaa! Ndiyo maana hawataki kuweka sawa mazingira ya shule za wananchi???????
 
Back
Top Bottom