Kuna demu mmoja mzuri hivi anapenda kuvaa mavazi ya kujisitiri, shape anayo ila si wa kuvaa zile nguo za kubana yeye,vitenge u sketi zile za kuachia kuna mwanagu mmoja Engineer yupo vizuri ila ni mtu ambaye yupo simple sana kimwonekano hata kimavazi ila financial yupo vizuri.
Basi si kamtokea yule binti, binti akampa namba ya simu ,kumpigia simu hata dk tano za kutambuana hazijaisha anasema ana shida ya 40000,nywele chafu, bundle limeisha na simu kioo kimepasuka.
Jamaa akapiga chini, basi yule demu akawa anamponda mwana ,ila siku anakuja kupata file la mwana alijiona bonge fala sana bada ya kujua status ya mwana.
Ficheni tamaa zenu hizo mwanzoni, mnawapoteza watu wa maana sababu ya tamaa zenu, mwana si kwamba alikuwa anashindwa kumpa hiyo hela ila kwake yy alimuona kama malaya na jamaa mwenyewe mstaarabu yule demu sasa hivi angekuwa anakula mema ya nchi.
Halafu unaweza ukakuta anapewa mimba na fala mmoja tu kisa ana gari,tena gari lenyewe la kuazima au mwana mjanja mjanja ,msanii.