Ni nini huwa kinapelekea eneo fulani kujikuta limekuwa na Makazi ya Kishua (wealthy neighbourhoods)?

Ni nini huwa kinapelekea eneo fulani kujikuta limekuwa na Makazi ya Kishua (wealthy neighbourhoods)?

inatokea tu
Hapan mkuu hii ishu imekaa kimipango miji. Kuna mtindo flani wa kulipanga jiji ndo kunafanya maeneo yawe na thamani na kuuzwa ghali, hapo huwez kuta masikini anakaa. Hata akikaa Kuna siku atauza tu akanunue kimbiji bei chee apate na mtaji. Siku pakipanda thamani kimbiji pia atawauzia wanaopaweza akanunue mserereko - ngombelelo
 
Nimejaribu kufikiri lakini sijapata majibu.

Je, suala hili Ni coincidence au Kuna kuambizana?

Mfano kwa Dar es Salaam, maeneo Kama Masaki, Oysterbay, Mikocheni, Upanga, Mbweni, Msasani, Kijichi.

Je, haya maeneo huwa inakuwaje unashangaa watu wenye uwezo kiuchumi KUJENGA sana Mitaa hiyo kwa pamoja.

Kwa Mwanza Kuna Maeneo Kama Capripoint, Bwiru, Mwananchi, Isamilo n.k.

Na, Je ukiwa na Uchumi wako wa manati lakini ukawa na eneo huko unaporwa au Ni Nini hasa sababu kubwa ya hili?
Vipi Katoro haimo
 
Ukisema viwanja vinapimwa vikubwa unamaanisha kwa ukubwa gani?
Jibu la hapa ni kwamba labda kitongoji kimoja au kijiji alafu kuna maeneo yanakuwa yamepimwa na kwa ukubwa wowote wa kueleweka na bei yake inakuwa imechangamka kidogo mfano labda milioni kumi alafu maeneo jirani na hapo unakuta unapata eneo lisilo na vipimo maalumu labda kwa milioni na nusu au mbili
 
Mfano, vimekatwa viwanja vya low density halafu mtu ananunua anakata viwanja vyake vya 18*20 anauza?

Mtu kama huyo inakuwaje?
Hautaruhusiwa, kuuziana viwanja vilivyopimwa kuna process yake ambayo watu wa ardhi, nyumba na makazi lazima wahusike. Kuna sheria au sera za ujenzi chini ya mamlaka husika zinazoamua wapi pajengwe nini na pajengwe vipi. (sijui kama nimekujibu swali lako) Mimi sio mtaalamu wa mipango miji najaribu kutumia uzoefu nilioupata katika harakati za ununuzi/umiliki/ ujenzi.

Kwa mfano: kuna maeneo ukinunua tu kiwanja huruhusiwi kujenga nyumba ya chini, lazima ujenge ghorofa, huoni kuwa moja kwa moja hilo eneo litakuwa na hadhi ya wakuu pekee.
 
Eneo ambalo limepimwa viwanja linakuwa na thamani kubwa kuanzia kuuzwa kwa square meter hivyo wanaonunua wanakuwa ni watu wenye kipato cha kati kwenda juu. Mfano Mbezi beach, Mbweni, Boko beach na Bunju beach, Kibada kigamboni etc.

Vilevile katika eneo huwa kunakua na matabaka mfano mbweni ya matajiri na ya kishua ni Mbweni JKT, halafi inakuja ya kati Mbweni malindi halafu inakuja Mbweni Ubungo ya kajamba nani hata bei ya viwanja inatofautiana sana maeneo hayo. Mbweni JKT hata Bi mkubwa ana mjengo huko sasa hivi kunapigwa rami kote. Viberiti kama vyote yaani kama uko kwenye jumuia juko majirani unaosali nao ni ex mabalozi, wakurugenzi wa Tiss, Makamishna yaani hata hali ya hewa inakua inanukia tuu. Hata mbezi beach imegawanyika huko Tangibovu ni kwa hali ya chini, ukishuka Shoppers kule ni saizi ya kati na kule Jangwani sea breeze kwa kina Balozi kabisa na mpungwe ndio kwa mataikoni kote kwa kina diamond kwa matajiri. Huwezi kusema unakaa mbezi beach kwa komba huko kwa mbayuwayu hawana kitu.

Kwa sayansi ya mazingira North of Dsm ndio eneo linaloheshimiwa zaidi na linakuwa la kishua zaidi kuanzia mbezi beach mpaka Bagamoyo.
 
Nimejaribu kufikiri lakini sijapata majibu.

Je, suala hili Ni coincidence au Kuna kuambizana?

Mfano kwa Dar es Salaam, maeneo Kama Masaki, Oysterbay, Mikocheni, Upanga, Mbweni, Msasani, Kijichi.

Je, haya maeneo huwa inakuwaje unashangaa watu wenye uwezo kiuchumi KUJENGA sana Mitaa hiyo kwa pamoja.

Kwa Mwanza Kuna Maeneo Kama Capripoint, Bwiru, Mwananchi, Isamilo n.k.

Na, Je ukiwa na Uchumi wako wa manati lakini ukawa na eneo huko unaporwa au Ni Nini hasa sababu kubwa ya hili?
Nini kinapelekea maeneo hayo yaliyotajwa hapo juu kuwa na muonekano wa kishua kwa sababu maeneo hayo wanaishi wenye vipato vya juu au uwezo wao wa kimaisha upo katika hali nzuri kuwawezesha walakazi wa maeneo hayo kuishi bila tatizo lolote na pia hata ukiangalia hasa masaki bado kuna maeneo yanaonekana ni kama mapori kuwawezesha watu kujenga nyumba za maana . huwaga inakuwa vigumu kwa mtu masikini kuishi katika social organization ya watu wa kipato cha juu vice versa is true mkazi wa kipato cha chini huwa ni vigumuu kuishi katika organization ya watu wa kipato cha juu

Ukija maeneo ya buza , kawe na baadhi ya maeneo umaskini unatawala kwa kiasi kikubwa kama unavyojua watanzania wengi tuna maisha ya chini huko ndiko furaha yetu ipo kwa sababu ukali wa maisha unakuwa ni related to kipato chetu so ukija upande wa sensa ya watu na makazi utagundua maeneo ya uswazi yana watu wengi ambao wana asili ya kitanzania hii ina reflect maisha halis ya kitanzania ukilinganisha na maeneo ya watu wa masaki ambayo yana watu wachache lakini wenye kipato kikubwa hata mchango ukipita watu wa tano wanatosha kujenga kanisa mfano oysterby.
 
Swali langu Ni kwamba, wakati wa ununuzi wa viwanja inakuwaje matajiri wajikute wamenunua sehemu moja?
 
haitokei tu boss, bei ya kiwanja ina kuwa kubwa, ndio jibu. Kapuku tunajichuja wenyewe, unapiga hesabu bei ya kiwanja unaweza jenga vyumba vitatu, unakimbilia zako Chanika au Mbande.
Lakini Bei ya Kiwanja huwa haipandi ghafla.

Mara ya kwanza huwa Ni Bei za kawaida tu.

Mfano, Mbweni ila ikitokea watu wakaanza KUJENGA mijengo ya maana, pakajengwa barabara nzuri plus umeme na maji, unashangaa pamekuwa pa kishua ghafla.
 
Swali langu Ni kwamba, wakati wa ununuzi wa viwanja inakuwaje matajiri wajikute wamenunua sehemu moja?
Ni tofauti na unavyodhani au unavyofikiria embu chukua mfano mmoja wew unakipato cha hali ya juu hali yako ya kimaisha iko juu je utaweza kwenda kuishi maeneo ya uswazi? Jibu ni hapana
Kwa sababu zifuatazo kumbuka wewe una kipato cha juu hata expensive yako jinsi ya matumizi ya pesa yatakuwa makubwa kulinganisha na mtu ambaye anaishi uswazi so ku spend pesa ndogo kwa matumizi ya kiuswazi uswazi hautaweza , hautaweza kula mihogo kachumbali as breakfast so kuishi katika nyumba isiyo na AC za maana hautaweza ndio maana wenye vipato vya juu hawawezi kuishi uswazi
Wanaamua kuamia maeneo ambayo yana wakazi wenye hali sawa na wao kuhusu viwanja maeneo ya kishua bei huwa ni tofauti bei ni kubwa maskini hawez kununua kiwanja kikubwa .
Kuna facts ambazo zina influence watu wenye pesa kwenda kuishi maeneo hayo moja kati ya hayo ni usalama wa mali na raia wenye pesa wanaitaji usalama maeneo ya kishua wezi hawapo na kama wapo ni kwa kiasi kidogo ndio maana vituo vya polisi vipo vichache mfano oysterbay kina wahudumia wakazi wengi tofauti na mitaa ya temeke ambapo kila mtaa una kituo cha polisi.
 
Size na bei za viwanja ndiyo vigezo vinavyoweka watu katika madaraja.
1. High density- hivi ni kwa ajili ya watu wenye uwezo mdogo
2. Medium density- kwa watu wa uwezo wa kati
3. Low density-kwa wenye uwezo wa juu
Je, mtu akinunua Kiwanja Cha low density halafu akakikata mwenyewe na kuuza kwa watu wengine vipande anaruhusiwa?

Mfano, kwa Arusha Ni eneo la kishua lakini mbona huyu kiwanja chake inaonesha high density.

Screenshot_2022-04-30-17-08-29-484_com.opera.mini.native.png
 
Nimejaribu kufikiri lakini sijapata majibu.

Je, suala hili Ni coincidence au Kuna kuambizana?

Mfano kwa Dar es Salaam, maeneo Kama Masaki, Oysterbay, Mikocheni, Upanga, Mbweni, Msasani, Kijichi.

Je, haya maeneo huwa inakuwaje unashangaa watu wenye uwezo kiuchumi KUJENGA sana Mitaa hiyo kwa pamoja.

Kwa Mwanza Kuna Maeneo Kama Capripoint, Bwiru, Mwananchi, Isamilo n.k.

Na, Je ukiwa na Uchumi wako wa manati lakini ukawa na eneo huko unaporwa au Ni Nini hasa sababu kubwa ya hili?
Maendeleo utokana na upatikanaji wa huduma kama maji umeme na barabara pia viwanja kupimwa na ujenzi wa mpango mfano sasa hivi kama unapesa nunua kiwanja kama kigamboni baadae utashangaa bei yake.
Mfano mimi nilinunua kiwanja mwaka jana mwezi wa kumi kule Bamba beach kigamboni Gezaulole kwa milioni 35 juzi juzi Rafiki yangu alitaka kiwanja sehemu hiyohiyo saizi sawa akaambiwa bei ya sasa ni milioni 45 bei imeshapanda na viwanja hawauzi chini ya sqm 800
 
Hapana haya maeneo kwanza yasiwe na wenyeji wengi sabab wenyeji huaribu mazingira pia wale wataoanza kujenga waanze na bangaloo utakuta na jirani yake anajitutumua na mwingine anaandaa ramani kubwa ya kisasa itaenda hivyo hàdi mnajikuta panaitwa ushuwani.
Kuna eneo fulan watu waliporomosha mabangaloo we mtu mmoja tu ndo alikua na nyumba ya chini basi bwana alivyojiona kageuka maskin mtaan akajipiga akaunga nyumba yake upande ghorofa akajikuta wanaenda sawa.
Nimejaribu kufikiri lakini sijapata majibu.

Je, suala hili Ni coincidence au Kuna kuambizana?

Mfano kwa Dar es Salaam, maeneo Kama Masaki, Oysterbay, Mikocheni, Upanga, Mbweni, Msasani, Kijichi.

Je, haya maeneo huwa inakuwaje unashangaa watu wenye uwezo kiuchumi KUJENGA sana Mitaa hiyo kwa pamoja.

Kwa Mwanza Kuna Maeneo Kama Capripoint, Bwiru, Mwananchi, Isamilo n.k.

Na, Je ukiwa na Uchumi wako wa manati lakini ukawa na eneo huko unaporwa au Ni Nini hasa sababu kubwa ya hili?
 
Maendeleo utokana na upatikanaji wa huduma kama maji umeme na barabara pia viwanja kupimwa na ujenzi wa mpango mfano sasa hivi kama unapesa nunua kiwanja kama kigamboni baadae utashangaa bei yake.
Mfano mimi nilinunua kiwanja mwaka jana mwezi wa kumi kule Bamba beach kigamboni Gezaulole kwa milioni 35 juzi juzi Rafiki yangu alitaka kiwanja sehemu hiyohiyo saizi sawa akaambiwa bei ya sasa ni milioni 45 bei imeshapanda na viwanja hawauzi chini ya sqm 800
Na wale wanaoanza kujenga pale umeona matusi yao? Kila mmoja kainua msingi wa ghorofa, we unaanzia wapi kujenga ya chini 😂! Bado kila anaejenga ana bango la ujenzi kutoka manispaa, haya mwenzangu na mimi atatokea wapi aje kujenga kule? It's obviously kutakuwa kwa kishua tu, sio kwa mi-fensi ile........
 
Back
Top Bottom