Ni nini huwa kinapelekea eneo fulani kujikuta limekuwa na Makazi ya Kishua (wealthy neighbourhoods)?

Ni nini huwa kinapelekea eneo fulani kujikuta limekuwa na Makazi ya Kishua (wealthy neighbourhoods)?

Hapana haya maeneo kwanza yasiwe na wenyeji wengi sabab wenyeji huaribu mazingira pia wale wataoanza kujenga waanze na bangaloo utakuta na jirani yake anajitutumua na mwingine anaandaa ramani kubwa ya kisasa itaenda hivyo hàdi mnajikuta panaitwa ushuwani.
Kuna eneo fulan watu waliporomosha mabangaloo we mtu mmoja tu ndo alikua na nyumba ya chini basi bwana alivyojiona kageuka maskin mtaan akajipiga akaunga nyumba yake upande ghorofa akajikuta wanaenda sawa.
Hii ni story ya mtaani kwangu kabisaaa!! Mwaka 2014 wakati napanunua palikuwa ni mashamba tu ya Korosho. Mangi mmoja alikuwa anauza miguu 22x22 milioni 1½. Nilijipinda nikachukua viwanja viwili. Then majirani zangu nao wakaanza kuongeza wakati awali walichukua kiwanja kimoja kimoja. Automatically pakaanza kuwa medium density na wale wenye kiwanja kimoja kimoja wakaanza kuviuza vyao kwa bei juu, watu wakija wanakuta mtaa umepangika so wananunua wanaunganisha. Mwaka 2020 kuna mtu kanunua 40x20 (double hizo) kwa milioni tisa.
So factor kubwa ni watu wanaoanzisha makazi (kwa maeneo ambayo hayajapimwa) ndio huchangia uelekeo wa eneo husika kuwa either uswazi au ushuani. Hivi pia huchagizwa na waasisi kuzingatia kanuni za mipango miji.
Mfano pale kwetu wakati tunanunua tulikuta muuzaji kaacha barabara za mtaa na sharti la kwanza kabla ya mtu kununua kiwanja ni kukubali kuachia hatua mbili za barabara. So kuna miguu minne zaidi kutoka kwenye barabara ya awali hivyo tunazo barabara kubwa tu.

Mie nimezungumzia maeneo yasiyopimwa kwa sababu ndio nna uzoefu nayo.
Nawasilisha
 
Hatokei wala nini...
Msijipe moyo.....
Ni inaitwa "Gentrification"....
Unauzwa mzima mzima na shamba lako....au kijumba chako cha matope.....
kwa hela ndogo tu....halafu baadae unawahadithia watoto wako wakati mnaishi Manerumango kuwa walizaliwa Avic Town.....
Ahahhahh
 
Hatokei wala nini...
Msijipe moyo.....
Ni inaitwa "Gentrification"....
Unauzwa mzima mzima na shamba lako....au kijumba chako cha matope.....
kwa hela ndogo tu....halafu baadae unawahadithia watoto wako wakati mnaishi Manerumango kuwa walizaliwa Avic Town.....
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkoa fulani miaka 3 iliyopita nilinunua kiwanja SQM 600 kwa million 7.7 watu walikua wamejenga wachache tu, sasa hivi ukienda hapafai watu wameporomosha majumba ya maana. Thamani ya kiwanja ni kuanzia 15 Million. Sababu ya watu kujenga nyumba za kifahari kwanza hilo eneo hakuna wazawa na lipo karibu na ofisi kubwa ya serikal na rami imepita...
Watu wenye pesa huangalia na eneo limekaaje wakiona lina wazawa hawajengi nyumba, wanapenda maeneo yaliyo pimwa na makubwa na yana huduma zote za kijamii na wanaangalia na watangulizi wamejenga nyumba za thamani ipi kama zina hadhi basi ilo eneo wenye hela watalikimbilia sana
 
uswahilini mnanunuliwa Wooote!! yanapandishwa majighorofa!! buguruni,Ilala Boma, Magomeni, SInza nk Kariakoo ya miaka ya 70!! utakaa chini unye!! vilikuwa ni vijumba vya matope tupu na hizo zipo mpaka leo!

kuleee kijito nyama, Mbezi beach yooote ile , sinza yoote yalikuwa mashamba ya mipunga tupu!!...kajimlima kalikuwa paleee mwenge tuuu!,,,,Mabibo yoote! Manzese! maweeee!! pana nunuliwa mpaka sasa!

hutaki kuuza jenga ghorofa lako, sharti ni kuanzia tano kwenda juu!....nyumba yako ikibomoka hakuna kukarabati!.....uza kama huna uwezo!....

Kiwalani, Majumba sita ,Banana, kipunguni na Kipawa yake yoote wewe ni kujenga lijikiwandatu hutaki uza tembea wenye hela tujenge!...kerege, Bunju kwenda mbele huko mwendo ni huo huo!
 
Halafu kule usijifanye unaenda kuroga roga kule!! ile mijitu ni michawi hatare ile ni michawi mistaraabu!! hairogi mtu ila usiichokoze! ukijaribu tu kuchawia!! hee! utakufa humo ndani mwako na utajizika mwenyewe!

yale majitu yako ivo!! ndani ni ndani tuuu kimyaaa!! hakuna cha kuomba chumvi wala mchiriku kule. sijui ngoma! ukifanya ngoma ya kumtoa mwali utacheza mwenyewe! wao wanapita tuuu!! vyuum! vyuum!

Yakipata Msiba sasa Mitajri mirefuuu! mineneee! itatoka mbali huko! sijui yanachaguana yale majitu!! sijui, kuja kutoa kampani kwa mfiwa...hakuna kutembea eti unaenda Msibani,

nakwambia ukifanya ivo utapita chocho!! na kutokomea hukoo, kusiko julikana! na hutarudipo tena japo ni kaka yako amekufa ni migari tuuu!,...na pole za maana! mweee!

Usijifanye eti mie Mganga Mkuu wa Temeke na kigari cha serikali cha Mawazo!! kuleee!! Daaa lkn ni sawa hudhuria ujambiwe kimaumivu upate uzoefu!...lkn inahitaji Moyo harooooo!

Kipa imara sijui Harusi ndo kabisaaaa!...utayamba kifukuto....wakati weye unakiduka kariakoo, sijui mtumishi wa Umma! kunamijitu kule inamiliki....VIwanda, Miji Meli, visima vya wese, visiwa ughaibuni, lkn hayasemi........ sasa hao utalingana nao kweli!
 
Kuna maeneo ni ya kishua kwasababu
A.WAKOLONI
-Kuna mitaa ilipangwa kwa ajili wazungu kuishi kabla ya uhuru,Masaki,Oysterbay na Ada Estate and Regent.
-Mingine waarabu na wahindi e.g Kariakoo

B.MAKAO YA UTAWALA
-Maeneo ambayo yapo karibu na utawala ,huvutia watu wenye pesa kukaa coz ya urahisi wa huduma.
-e.g Mitaa ya Uzunguni kule Arusha na Mbeya

C.KUPANGWA
-Kuna maeneo coz yamepangwa
-Urahisi wa kufikika
-Viwanja bei juu
-e.g Ununio,Mbweni Teta,Bunju B
 
Back
Top Bottom