Ni nini kinachopelekea ukoo kuwa na nguvu na ukoo mwingine kukosa nguvu kwenye jamii zinazotuzunguka?

Nitapitia pia hili bandiko asante
 
Nyumba imara hujengwa juu ya msingi imara...

Mara nyingi nguvu za koo fulani huwa ni za kurithi toka kizazi kimoja hadi kingine...

Ukiona familia au ukoo fulani una nguvu, basi ujue wakati fulani huko nyuma kuna mtu aliyehusika kujenga msingi...
 
Kwaio pesa ndio kiini cha umoja, upendo na mshikamano
Umesoma kwa makini kichwa cha habari na mada inasemaje mkuu?. Mada inasema Koo na familia zenye nguvu. Kama tena ni kuhusiana na umoja,upendo na mshikamano,kafungue mada ingine.
 
Ningependa tupate kiini kabisa maana sio kila ukoo unaasili ya pesa
Kama hawana asili ya pesa basi wana mali zingine. Kama zamani ilikuwa unahesabiwa una mali kama ng'ombe,unalima sana,una wake wengi,watoto wengi. Vyote hivyo huwezi kuwa navyo kama huna uwezo. Kama wasukuma na wamasai wengi wana mali,japo wao hawajijui kwamba ni matajiri. Mfano mtu mmoja anamiliki ng'ombe 2000,3000,huyo ni tajiri na familia yake lazima iwe na nguvu
 
Tuangalie sana wanaume au wanawake tunaooa au mnaokwenda kuolewa nao.

Kuna mwanamke unaoa na umetoka familia ya kifukara inakufanya urudi kule kule sababu umechagua ambaye ni wa level zile zile za kukubali maisha ya chini.

Ila kuna ambaye unakutana nae anajua unapotoka so anakuwa sehemu ya energy unayohitaji kutoka katika hali ya ufukara.

Anyways, swala la familia kuwa na uwezo mdogo huanza na malezi kwanza watoto kutokuwa na ile spirit ya team work, kujitoa ili mwenzako apate, wengi hutaka ile jitoe wewe kwanza mimi nitakusaidia baadae.

Yaani ile tabia ya kuweka utegemezi mbele kwanza badala ya jitihada binafsi ili kutoka kimaisha maana kila m'moja kwa nafasi yake akitia jitihada hatokuwa mzigo kwa wenzake.
 
Exquisite.....

Umemaliza.πŸ‘πŸ‘ŠπŸ‘Š
 
Sure mkuu
 
Tuangalie sana wanaume au wanawake tunaooa au mnaokwenda kuolewa nao.

Kuna mwanamke unaoa na umetoka familia ya kifukara inakufanya urudi kule kule sababu umechagua ambaye ni wa level zile zile za kukubali maisha ya chini.
 
Zamani koo tajiri (hasa katika ulimwengu wa roho) ndizo zilizotoa Mangi(kiongozi)wa sehemu husika . Ukoo masikini hata kama ni wengi kutoa kiongozi ni shida.
 
Zamani koo tajiri (hasa katika ulimwengu wa roho) ndizo zilizotoa Mangi(kiongozi)wa sehemu husika . Ukoo masikini hata kama ni wengi kutoa kiongozi ni shida.
Yani kwanini hizi koo masikini pia hazina hata mshikamano kama hata uongozi hawawezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…