Uchaguzi 2020 Ni nini mwelekeo na nafasi ya Tundu Lissu kisheria kugombea nafasi yoyote ya uongozi hususani Ubunge na Urais katika uchaguzi mkuu mwaka - 2020?

Daaah . . . . naona watanzania tumemiss amsha amsha. Anyway, uchaguzi utakuwa wa kipekee kutokana na utani na vijembe na hoja zitakazokuwepo
 

Wewe kuna kila dalili kuwa hujui siasa...

Lengo kuu la chama cha siasa chochote ni kushika dola...

Ndilo lengo la CHADEMA, ndilo lengo la CCM na vivyo hivyo CUF ama ACT Wazalendo...

Kuchukua dola huhitaji mtu mwenye sifa fulani maalumu fixed....

Kushinda uchaguzi unahitaji hata kichaa tu ili mradi ana ushawishi kwa watu, anachagulika....

John Pombe Magufuli wa CCM ni miongoni mwa viongozi wasio na sifa ya kuwa viongozi ktk nafasi ya Urais, lakini huyo yupo ni Rais....

Ni Rais kwa sababu, CCM hawakuangalia yale unayoyatazama wewe. Walihitaji kushinda uchaguzi, basi....

Edward Lowassa, honestly mwaka 2015 wala hakuwa hata na sifa wala mvuto wa kuwa viongozi Rais kwa nchi....

Ni mtu ambaye hata kujieleza tu kwa ufasaha kwa dakika 10 ingalau alikuwa hawezi...

Lakini CHADEMA, waliona kitu kingine chenye manufaa kisiasa kwao kuliko mvuto wake....

Na kitu hicho kilisaidia na wakashinda uchaguzi japo hakutangazwa na badala yake akatangazwa, Magufuli wa CCM....

Hivi ndivyo ilivyo mwaka huu 2020. Hatuangalii uanaharakati wa Tundu Lissu. Tunaangalia anaweza kutupa kura za ushindi?

Jibu ni NDIYOOOO kwa sauti kubwa....

Haijalishi kura hizi ni za "huruma" au kwa sbb "anapendwa tu". Tunachotaka ni ushindi....

By the way, Tundu Lissu is far better than John Pombe Magufuli kwa vipimo vyote...!!
 

Ofcoz ndivyo ilivyo...

Yatazushwa tu ili mradi Tundu Lissu asije akam - challenge mtesi wake aliyetaka kumuua...

Ni wazi CCM na Magufuli wasingependa huyu mtu akapata nafasi hii na yaliyompata (jaribio la kumuua) ikawa agenda ktk kampeni za uchaguzi...

Hili itakuwa shida kwao. Badala ya kueleza Sera na utekelezaji wa ilani yao, watalazimika muda mwingi kutumia kijibu tuhuma....

CHADEMA, wafanye kila njia wazuie hili. INAWEZEKANA...!
 
Kwa kanuni hizi za uchaguzi na tume hii; mpinzani yeyote haoni mbali. That is why Bia Yetu & Co. are celebrating.

Wana "celebrate" hewa...

Wana "celebrate" mimba ambayo ndo tu imetungwa...

Wanasahau kuwa kuna uwezekano mimba ikaharibika ama kukawa na "pre mature delivery" ya mtoto....

Kuiangusha CCM ni wajibu na lazima kwa 100% kwa sheria na kanuni hizohizo za kulazimisha...

Nguvu ya umma (people's power) ikiamua kubadilisha mambo, hakuna cha kuzuia, hakuna linaloshindikana.....!!
 
Tungu akifika hapa tu pingu amelisaliti taifa na kulichafua pia
 
Ila waachie acacia wabebe makinikia bure huyu yeye akiingiziwa 20%
 
Kuchukua dola huhitaji mtu mwenye sifa fulani maalumu fixed....

************
Kujibizana na watu kaliba yako ni kupoteza muda wangu. Ikiwa wewe tu huwezi kukamata mwanamke yeyote ukalala naye achilia mbali kumfanya kuwa mke.

Unaanzaje kupuuzia sifa za mgogembea nafasi nyeti kama ofisi ya Rais?

***********
John Pombe Magufuli wa CCM ni miongoni mwa viongozi wasio na sifa ya kuwa viongozi ktk nafasi ya Urais, lakini huyo yupo ni Rais....

Ni Rais kwa sababu, CCM hawakuangalia yale unayoyatazama wewe. Walihitaji kushinda uchaguzi, basi....

MANENO YA THOMAS SANKARA aliyekua Rais wa Burkinafaso na akaweka alama japo alikaa kwa muda wa miaka minne tu.

KULETA MAPINDUZI YA KWELI KATIKA TAIFA YAKUPASA KUWA NA AINA FULANI YA UWENDA WAZIMU

Dr. John Joseph Pombe Magufuli anachowachanganya walio wengi ni Jambo moja tu "HE IS BEYOND NORMAL STAFF" hafanyi kutimiza muda wake bali anatenda kuikomboa jamii yake iliyokua imetopea kwenye ULARUSHWA, UMIMI, UMANGIMEZA, UKABAILA NA UONGOZI WA MAZOEA.

************
Hivi ndivyo ilivyo mwaka huu 2020. Hatuangalii uanaharakati wa Tundu Lissu. Tunaangalia anaweza kutupa kura za ushindi?

ALIPOKUA KATIKA ZIARA YAKE NCHINI MAREKANI ALIULIZWA SWALI KUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA

Tafuta ule mdahalo wake alafu utafakari kama unataka Tanzania ambayo ipo siku mwanao wa kiume atakuja na mwanaume akuambie kua baba huyu ndio chaguo la moyo wangu

NB
Unapotaka kuzungumza nami kuhusu siasa inabidi ujitafakari kwanza Mkuu kabla ya kuingia aibu?
 
Kwa mustakabali na maslai mapana ya Taifa letu John Pombe Joseph Magufuli, haifai kupewa hata dakika moja, au nafasi nyingine ya kuongoza taifa letu, ametutia aibu Sana , ameturudisha nyuma Kama taifa kwa miaka zaida ya 10, hasara aliyotupa wajukuu zetu hawataweza kulipa
 
Kuna kitu umezungumzia hapa ambacho wengi hawajui. Hizi harakati zooote na makombora yooote anayopigwa nayo Mbowe, siyo kwamba wanamwona Mbowe ni tishio kubwa. Hofu yao kuu iko kwenye mtu anayeweza kusimamishwa na Chadema kugombea urais. CCM na hasa viongozi wa juu na watu wa kitengo wanajua kabisa kuwa Magufuli sasa hivi hakubaliki na sehemu kubwa ya wananchi (labda ukindoa kanda ya Ziwa na hasa maeneo ya karibu na nyumbani kwake.) Na mbaya zaidi ndani ya CCM yenyewe kuna watu wengi wanaugulia na kulaani chinichini. Hii hali inafanya uchaguzi ujao uwe unpredictable, na hasa kama Chadema itasimamisha mtu kama Lissu. Naomba nisisitize CCM wasiwasi wao hasa uko kwenye ''kinachoweza kutokea'' wakati watakapoiba kura siku ya uchaguzi (wanajua kabisa kuiba ni lazima na wamejipanga, na ndivyo watakavyofanya). Shida iko kwenye ''je wakiiba wananchi hawawezi kukiamsha na ikatokea fujo kubwa kabisa?''. Hapo sasa ndiyo wanamekuja na mkakati wa kuhakikisha Chadema inayumbushwa ili wakati wa uchaguzi isiweze kujipanga. Na ili kuhalalisha mambo imebidi watafutwe vibaraka kama kina Mbatia na Lipumba.
 
Kwa akili zako unadhani mleta hoja anatumia only ""....he survived death in order to tell the tale....." kumtambulisha TL kwenye post yake? Mleta hoja anajua kuwa JF ni platform yenye watu wasiohitaji kuelezwa sifa za TL kwa kuwa wanamfahamu. Halafu unataka kutuambia nini kuhusu JPM kutuletea sheria za kuzuia wengine wasifanye siasa isipokuwa yeye tu unapolinganisha na hao unaowaita wanaharakati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…