Uchaguzi 2020 Ni nini mwelekeo na nafasi ya Tundu Lissu kisheria kugombea nafasi yoyote ya uongozi hususani Ubunge na Urais katika uchaguzi mkuu mwaka - 2020?

Uchaguzi 2020 Ni nini mwelekeo na nafasi ya Tundu Lissu kisheria kugombea nafasi yoyote ya uongozi hususani Ubunge na Urais katika uchaguzi mkuu mwaka - 2020?

Kwa kweli maswali ni mengi sana. Lakini all in all, Tundu A. M. Lissu akiwa mgombea wa CHADEMA/UKAWA kupambana na mtesi wake, kwa hakika, uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 kuanzia kampeni utakuwa wa kipekee sana na tutashuhudia msisimuko na amsha amsha ya kisiasa kali maradufu kuliko ilivyokuwa ktk uchaguzi uliopita wa 2015 nyakati za kina Edward Ngoyai Lowassa...

Tujadili....
Daaah . . . . naona watanzania tumemiss amsha amsha. Anyway, uchaguzi utakuwa wa kipekee kutokana na utani na vijembe na hoja zitakazokuwepo
 
"....he survived death in order to tell the tale....."

Kwa akili zako unadhani for the name of SYMPATHY pekee ni kigezo tosha chankumsimamisha mtu Kama mgombea wa nafasi nyeti kama Urais?

Mwanaharakati hawezi kuwa Rais wa nchi Mkuu, nchi inahitaki Kiongozi na dola inahitaji Mtawala.

Madhara ya wanaharakati ni pamoja na kutuletea Ndoa za Jinsia moja, kukubali zile Sheria zote ambazo ni universal mfano, watoto kutokuadhibiwa, wanafunzi kujifungua na kurudi mashuleni, utoaji mimba kuwa haki ya kisheria, nk

Kumbuka Sheria hizo inawezekana sio mbaya kwa jamii za waasisi wa Sheria hizo kwakua wamefanya tafiti zankutosha na kujiridhisha na madhara ambayo yatajitokeza.

Ila kwa kuabsisi tutalazimishwa kusaini kwa ajili ya kuonekana tuko pamoja na Jumuia za kimataifa na kupata misaada madhara yatakua na athari kubwa kihisia na kijamii.

Wewe kuna kila dalili kuwa hujui siasa...

Lengo kuu la chama cha siasa chochote ni kushika dola...

Ndilo lengo la CHADEMA, ndilo lengo la CCM na vivyo hivyo CUF ama ACT Wazalendo...

Kuchukua dola huhitaji mtu mwenye sifa fulani maalumu fixed....

Kushinda uchaguzi unahitaji hata kichaa tu ili mradi ana ushawishi kwa watu, anachagulika....

John Pombe Magufuli wa CCM ni miongoni mwa viongozi wasio na sifa ya kuwa viongozi ktk nafasi ya Urais, lakini huyo yupo ni Rais....

Ni Rais kwa sababu, CCM hawakuangalia yale unayoyatazama wewe. Walihitaji kushinda uchaguzi, basi....

Edward Lowassa, honestly mwaka 2015 wala hakuwa hata na sifa wala mvuto wa kuwa viongozi Rais kwa nchi....

Ni mtu ambaye hata kujieleza tu kwa ufasaha kwa dakika 10 ingalau alikuwa hawezi...

Lakini CHADEMA, waliona kitu kingine chenye manufaa kisiasa kwao kuliko mvuto wake....

Na kitu hicho kilisaidia na wakashinda uchaguzi japo hakutangazwa na badala yake akatangazwa, Magufuli wa CCM....

Hivi ndivyo ilivyo mwaka huu 2020. Hatuangalii uanaharakati wa Tundu Lissu. Tunaangalia anaweza kutupa kura za ushindi?

Jibu ni NDIYOOOO kwa sauti kubwa....

Haijalishi kura hizi ni za "huruma" au kwa sbb "anapendwa tu". Tunachotaka ni ushindi....

By the way, Tundu Lissu is far better than John Pombe Magufuli kwa vipimo vyote...!!
 
Sifa za mtu kugombea nafasi ya urais zipo na zinajulikana.

Haya mapya unayoyaeleza, na kwa kiaina kama kuwastua wasiopenda Lissu agombee yatazuliwa kama sababu na kulazimisha iwe hivyo watu watake au wasitake.
Hili linajulikana kwa wote.

Kwa hiyo, kwa kifupi kujibu uliyoyaandika; ni kazi ya CHADEMA na wengine wote wanaokataa maovu ya kila aina ya hawa watu, kujizatiti kukataa mbinu za kila namna watakazotumia CCM katika kuvuruga uchaguzi kwa sababu yoyote ile, ikiwa ni pamoja na hii ya kumwekea mizengwe mgombea wa CHADEMA, kama atakuwa ni Tundu Lissu.

Ofcoz ndivyo ilivyo...

Yatazushwa tu ili mradi Tundu Lissu asije akam - challenge mtesi wake aliyetaka kumuua...

Ni wazi CCM na Magufuli wasingependa huyu mtu akapata nafasi hii na yaliyompata (jaribio la kumuua) ikawa agenda ktk kampeni za uchaguzi...

Hili itakuwa shida kwao. Badala ya kueleza Sera na utekelezaji wa ilani yao, watalazimika muda mwingi kutumia kijibu tuhuma....

CHADEMA, wafanye kila njia wazuie hili. INAWEZEKANA...!
 
Kwa kanuni hizi za uchaguzi na tume hii; mpinzani yeyote haoni mbali. That is why Bia Yetu & Co. are celebrating.

Wana "celebrate" hewa...

Wana "celebrate" mimba ambayo ndo tu imetungwa...

Wanasahau kuwa kuna uwezekano mimba ikaharibika ama kukawa na "pre mature delivery" ya mtoto....

Kuiangusha CCM ni wajibu na lazima kwa 100% kwa sheria na kanuni hizohizo za kulazimisha...

Nguvu ya umma (people's power) ikiamua kubadilisha mambo, hakuna cha kuzuia, hakuna linaloshindikana.....!!
 
Ukiniuliza swali hili; Je, ungependa Tundu A. M. Lissu awe mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA katika uchaguzi mkuu wa 2020?

Hakika jibu langu haraka haraka na pasipo kupepesa macho huku nikitabasamu, ningekujibu tu....YES, HUYU NDIYE...!!

Huyu ndiye si kwa sababu kina Zitto Z.R. Kabwe ama wengine wowote wale hawafai ama hawatoshi...

Ni kwa vile tu ukiwaweka katika mizania, Tundu Lissu anawazidi kwa kiwango kikubwa sana wenzake na ni kwa sababu;

".......he survived death in order to tell the tale...."

Nina hakika hata wengi wa wapenda mabadiliko nje ya CCM wanaweza kukubaliana kuwa, Tundu A. M. Lissu ndiye mgombea sahihi na mwenye uwezo kisiasa (ingalau kwa sasa) wa kukabiliana na CCM ikiyokufa chini ya mgombea wao (hopefully, Magufuli)...

Lakini changamoto pekee anayokabiliwa nayo ndugu Tundu A. M. Lissu ni ya kisheria....

Na huu ndiyo msingi wa mjadala katika mada hii ya leo na tunaomba wataalamu wa katiba na sheria waliomo nasi ktk jukwaa hili watusaidie kutupa mwanga juu ya aidha INAWEZEKANA ama HAIWEZEKANI kwa ndugu huyu kutumia haki yake ya kiraia ya kupigiwa kura kwa mazingira ya sasa....

Hii ni kwa sababu kila mtu anafahamu kuwa, Tundu A. M. Lissu ana mlolongo wa kesi mahakamani...

Na moja ya kesi ni ile ya uchochezi na mwenzake mwandishi wa gazeti la (Mawio? MwanaHalisi?) ambayo siku chache zilizopita kidogo isababishe wadhamini wake kutaka kufungwa na mahakama na baadaye kuwaamuru wamlete mshitakiwa mahakamani...

Sasa tujaribu kujiuliza maswali kadhaa wa kadhaa ya kutuongoza ktk mjadala wetu;

1. Je, wapinzani wake kisiasa hususani CCM wana nafasi gani kutumia kesi hizi kama mapingamizi kumzuia Tundu A.M. Lissu asigombee Urais?

2. Katiba na Sheria ya uchaguzi inasemaje kuhusu mgombea mwenye kesi ya jinai mahakamani kugombea nafasi ya uongozi hasa ktk ngazi ya Urais?

3. Najua katiba na sheria inam - disqualify mtu ama mgombea yeyote kama alishahukumiwa kifungo cha miezi 6 au zaidi kwa makosa fulani fulani ya jinai au uaminifu kugombea nafasi ya uongozi...

Hebu sasa tujiulize, CCM ndio wanaongoza serikali kwa sasa. Mgombea wao (possibly) anaweza kuwa huyu huyu Bwana Magufuli ambaye ndiye Rais mpaka siku anaapishwa Rais mpya.....!!

Na katika jambo ambalo Magufuli na CCM wasingependa kuliona linatokea, ni ndugu Tundu A.M. Lissu kusimama kama mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA akipambana na Magufuli...!

Unadhani ni mipango gani (kwa kutumia dola: TISS na mahakama) inafanyika ktk viunga vya Lumumba kuhakikisha hili halitokei?

4. Unadhani wataweza kumzuia huyu ndugu huyu na kuzima ndoto ya Tundu Lissu mwenyewe, wananchi wanaomuunga mkono na CHADEMA/UKAWA yenyewe?

5. Je, unadhani CHADEMA wenyewe wanalijua hili? Je, Tundu Lissu mwenyewe anajua hili? Je, unadhani wana mkakati gani thabiti kukabili hujuma hizi na kufanya quick counter attack kuizima?

6. Je, una macho makali na mangavu ktk kutazama mambo kwa kina chake? Kama jibu lako ni ndiyo, sasa eleza kwa hoja thabiti kabisa, kwamba, unaweza kuunganishaje "dots" kwa hiki kinachotokea sasa kwa CHADEMA kushambuliwa kwa namna hii?

Je, unadhani anayetafutwa ni Freeman Mbowe? Au ni jambo kubwa zaidi linatafutwa na Mbowe ni kama "WAY IN" tu kuingia huko na kumaliza shughuli?

Kwa kweli maswali ni mengi sana. Lakini all in all, Tundu A. M. Lissu akiwa mgombea wa CHADEMA/UKAWA kupambana na mtesi wake, kwa hakika, uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 kuanzia kampeni utakuwa wa kipekee sana na tutashuhudia msisimuko na amsha amsha ya kisiasa kali maradufu kuliko ilivyokuwa ktk uchaguzi uliopita wa 2015 nyakati za kina Edward Ngoyai Lowassa...

Tujadili....
Tungu akifika hapa tu pingu amelisaliti taifa na kulichafua pia
 
Ila waachie acacia wabebe makinikia bure huyu yeye akiingiziwa 20%
 
Kuchukua dola huhitaji mtu mwenye sifa fulani maalumu fixed....

************
Kujibizana na watu kaliba yako ni kupoteza muda wangu. Ikiwa wewe tu huwezi kukamata mwanamke yeyote ukalala naye achilia mbali kumfanya kuwa mke.

Unaanzaje kupuuzia sifa za mgogembea nafasi nyeti kama ofisi ya Rais?

***********
John Pombe Magufuli wa CCM ni miongoni mwa viongozi wasio na sifa ya kuwa viongozi ktk nafasi ya Urais, lakini huyo yupo ni Rais....

Ni Rais kwa sababu, CCM hawakuangalia yale unayoyatazama wewe. Walihitaji kushinda uchaguzi, basi....

MANENO YA THOMAS SANKARA aliyekua Rais wa Burkinafaso na akaweka alama japo alikaa kwa muda wa miaka minne tu.

KULETA MAPINDUZI YA KWELI KATIKA TAIFA YAKUPASA KUWA NA AINA FULANI YA UWENDA WAZIMU

Dr. John Joseph Pombe Magufuli anachowachanganya walio wengi ni Jambo moja tu "HE IS BEYOND NORMAL STAFF" hafanyi kutimiza muda wake bali anatenda kuikomboa jamii yake iliyokua imetopea kwenye ULARUSHWA, UMIMI, UMANGIMEZA, UKABAILA NA UONGOZI WA MAZOEA.

************
Hivi ndivyo ilivyo mwaka huu 2020. Hatuangalii uanaharakati wa Tundu Lissu. Tunaangalia anaweza kutupa kura za ushindi?

ALIPOKUA KATIKA ZIARA YAKE NCHINI MAREKANI ALIULIZWA SWALI KUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA

Tafuta ule mdahalo wake alafu utafakari kama unataka Tanzania ambayo ipo siku mwanao wa kiume atakuja na mwanaume akuambie kua baba huyu ndio chaguo la moyo wangu

NB
Unapotaka kuzungumza nami kuhusu siasa inabidi ujitafakari kwanza Mkuu kabla ya kuingia aibu?
 
Kwa mustakabali na maslai mapana ya Taifa letu John Pombe Joseph Magufuli, haifai kupewa hata dakika moja, au nafasi nyingine ya kuongoza taifa letu, ametutia aibu Sana , ameturudisha nyuma Kama taifa kwa miaka zaida ya 10, hasara aliyotupa wajukuu zetu hawataweza kulipa
 
Wana "celebrate" hewa...

Wana "celebrate" mimba ambayo ndo tu imetungwa...

Wanasahau kuwa kuna uwezekano mimba ikaharibika ama kukawa na "pre mature delivery" ya mtoto....

Kuiangusha CCM ni wajibu na lazima kwa 100% kwa sheria na kanuni hizohizo za kulazimisha...

Nguvu ya umma (people's power) ikiamua kubadilisha mambo, hakuna cha kuzuia, hakuna linaloshindikana.....!!
Kuna kitu umezungumzia hapa ambacho wengi hawajui. Hizi harakati zooote na makombora yooote anayopigwa nayo Mbowe, siyo kwamba wanamwona Mbowe ni tishio kubwa. Hofu yao kuu iko kwenye mtu anayeweza kusimamishwa na Chadema kugombea urais. CCM na hasa viongozi wa juu na watu wa kitengo wanajua kabisa kuwa Magufuli sasa hivi hakubaliki na sehemu kubwa ya wananchi (labda ukindoa kanda ya Ziwa na hasa maeneo ya karibu na nyumbani kwake.) Na mbaya zaidi ndani ya CCM yenyewe kuna watu wengi wanaugulia na kulaani chinichini. Hii hali inafanya uchaguzi ujao uwe unpredictable, na hasa kama Chadema itasimamisha mtu kama Lissu. Naomba nisisitize CCM wasiwasi wao hasa uko kwenye ''kinachoweza kutokea'' wakati watakapoiba kura siku ya uchaguzi (wanajua kabisa kuiba ni lazima na wamejipanga, na ndivyo watakavyofanya). Shida iko kwenye ''je wakiiba wananchi hawawezi kukiamsha na ikatokea fujo kubwa kabisa?''. Hapo sasa ndiyo wanamekuja na mkakati wa kuhakikisha Chadema inayumbushwa ili wakati wa uchaguzi isiweze kujipanga. Na ili kuhalalisha mambo imebidi watafutwe vibaraka kama kina Mbatia na Lipumba.
 
"....he survived death in order to tell the tale....."

Kwa akili zako unadhani for the name of SYMPATHY pekee ni kigezo tosha chankumsimamisha mtu Kama mgombea wa nafasi nyeti kama Urais?

Mwanaharakati hawezi kuwa Rais wa nchi Mkuu, nchi inahitaki Kiongozi na dola inahitaji Mtawala.

Madhara ya wanaharakati ni pamoja na kutuletea Ndoa za Jinsia moja, kukubali zile Sheria zote ambazo ni universal mfano, watoto kutokuadhibiwa, wanafunzi kujifungua na kurudi mashuleni, utoaji mimba kuwa haki ya kisheria, nk

Kumbuka Sheria hizo inawezekana sio mbaya kwa jamii za waasisi wa Sheria hizo kwakua wamefanya tafiti zankutosha na kujiridhisha na madhara ambayo yatajitokeza.

Ila kwa kuabsisi tutalazimishwa kusaini kwa ajili ya kuonekana tuko pamoja na Jumuia za kimataifa na kupata misaada madhara yatakua na athari kubwa kihisia na kijamii.
Kwa akili zako unadhani mleta hoja anatumia only ""....he survived death in order to tell the tale....." kumtambulisha TL kwenye post yake? Mleta hoja anajua kuwa JF ni platform yenye watu wasiohitaji kuelezwa sifa za TL kwa kuwa wanamfahamu. Halafu unataka kutuambia nini kuhusu JPM kutuletea sheria za kuzuia wengine wasifanye siasa isipokuwa yeye tu unapolinganisha na hao unaowaita wanaharakati?
 
Back
Top Bottom