kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ili watu wote tuwe kwenye ukurasa mmoja wa uelewa bila kujali itikadi zetu za kisiasa, elimu, jinsia na hata makabila na kanda zetu tunakotoka ni lazima neno "kufanya siasa za kistaarabu" lipewe tafsiri yake ili wadau wote wafahamu maana yake ili kama mtu mkifanya siasa zisizokuwa za kistaarabu kila mtu awe shahidi.
Siasa za kistaarabu ni nini na ni zipi?
Je, kufanya siasa zisizo za kistaarabu ni kufanya nini?
Je, ni nani anatakiwa kufanya hizo siasa za kistaarabu?
Je, ni nani atakaesema wewe umefanya siasa zisizo za kistaarabu?
Je, ni nani atawaadhibu wote wanaofanya siasa zisizo za kistaarabu bila kujali ni wa chama gani?
Na je, kusema uongo, kufichua ukweli ambao ulifichwa, kuiba kura, kuengua wagombea, kutumia mali ya umma kwenye siasa za vyama, kuzuia mikutanp ya vyama na maandamano na tumumia maneno ya kuudhi kwenye siasa ni sehemu ya siasa zisizo za kistaarabu pia?
Taifa lazima lisonge mbele na lionekane na wote likisonga mbele.