Ni nini tafsiri hasa ya "Kufanya siasa za kistaarabu?"

Ni nini tafsiri hasa ya "Kufanya siasa za kistaarabu?"

Ili watu wote tuwe kwenye ukurasa mmoja wa uelewa bila kujali itikadi zetu za kisiasa, elimu, jinsia na hata makabila na kanda zetu tunakotoka ni lazima neno "kufanya siasa za kistaarabu" lipewe tafsiri yake ili wadau wote wafahamu maana yake ili kama mtu mkifanya siasa zisizokuwa za kistaarabu kila mtu awe shahidi.

Siasa za kistaarabu ni nini na ni zipi?

Je, kufanya siasa zisizo za kistaarabu ni kufanya nini?

Je, ni nani anatakiwa kufanya hizo siasa za kistaarabu?
Je, ni nani atakaesema wewe umefanya siasa zisizo za kistaarabu?
Je, ni nani atawaadhibu wote wanaofanya siasa zisizo za kistaarabu bila kujali ni wa chama gani?

Na je, kusema uongo, kufichua ukweli ambao ulifichwa, kuiba kura, kuengua wagombea, kutumia mali ya umma kwenye siasa za vyama, kuzuia mikutanp ya vyama na maandamano na tumumia maneno ya kuudhi kwenye siasa ni sehemu ya siasa zisizo za kistaarabu pia?

Taifa lazima lisonge mbele na lionekane na wote likisonga mbele.
Siasa ambazo siyo za kistaarabu ni kama Ile ya June 2021 baada ya Mdude kuachiliwa na Mahakama ya Mbeya kwenye kesi ya mihadarati. Kwenye mkutano wa Baracuda Mdude Chadema alisikika akisema "Mwambieni na huyo mama yenu, niyamnyoa kwa wembe uleule niliomnyolea Magufuli"
 
Jambo moja linaweza kuwa sio hoja, uzushi au matusi kwako na kwa mtu mwingine likawa kinyume chake.
Kama unahisi umetukanwa au kuna uzushi mahakama zipo za kudai haki yako kama walivyofanya Membe na Fatma Karume kwa Cyprian Musiba.
Inakuwaje kama utatukanwa na mtu mwenye Kinga ya kutokushitakiwa?
 
Stick on the Topic. Usiterereke.

Hajatukanwa mtu na Watu wasitukanwe. Hii ni mada Muhimu na ina Hoja zilizosimama.Wasikuyumbishe.

Usikubali kuyumbishwa na wanyanyasaji na wadumazi.na Wapuuzi
Wadau waje kwenye meza ya duara wadadavue na kuja na kijitabu Cha orodha ndefu ya aina ya siasa zisizotakiwa kufanywa na mtu wa aina yoyote yule bila kujali kwao ni wapi pamoja na adhabu zake. Kijitabu hiki kisambazwe hata shule za msingi waliko watanzania wa kesho. Tuusiijenge nchini yetu kwa matukio TU, bali tuwe na mpango mkubwa juu ya mwelekeo wetu. Tuje na sifa za mtu anaetaka kuwa kiongozi wa umma hata wa kitongoji mpaka taifa, kuanzia kuzaliwa kwake, malezi, elimu mpaka tabia.
 
Wadau waje kwenye meza ya duara wadadavue na kuja na kijitabu Cha orodha ndefu ya aina ya siasa zisizotakiwa kufanywa na mtu wa aina yoyote yule bila kujali kwao ni wapi pamoja na adhabu zake. Kijitabu hiki kisambazwe hata shule za msingi waliko watanzania wa kesho. Tuusiijenge nchini yetu kwa matukio TU, bali tuwe na mpango mkubwa juu ya mwelekeo wetu. Tuje na sifa za mtu anaetaka kuwa kiongozi wa umma hata wa kitongoji mpaka taifa, kuanzia kuzaliwa kwake, malezi, elimu mpaka tabia. Huwezi kuwa na kiongozi mkuu anaempiga mkewe, aliyemkimbia mumewe, aliyetelekeza watoto wake, au ambae alichelewa kulia wakati anazaliwa.
 
Kutoiba kura kama CCM ndio siasa za kistaarabu, kupiga wapinzani,kuzuia mikusanyiko/mikutano ya watu kwa kutumia wakuu wa wilaya na polisi, kubadilisha matokeo, kubambikiana kesi etc ndio siasa za chama cha ovyo sana kinachoitwa CCM kuwahi kutokea Tanzania, umaskini wa Tanzania sababu kubwa ni CCM, tujaribu Chadema, CCM wameshindwa, nao wakishindwa tunapiga chini
Ili neno la kufanya siasa za kistaarabu liwe na maana lazima vitendo kama vile vya jecha salim jecha aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar visiwepo kabisa. Mtu hawezi kufanyiwa vile halafu abaki kufanya siasa za kistaarabu.
 
Back
Top Bottom