Ni nini tafsiri hasa ya "Kufanya siasa za kistaarabu?"

Kama tafsiri ya kufanya siasa za kistaarabu haitatolewa tegemea yaleyale tuliyoyazoea kufanyika kwenye siasa. Chondechote wanasiasa, nchi hii ni yetu sote, tusitoe nafasi kwa Wagner kututembela huku.
 
“Siasa za kistaarabu” ni kauli isiyo na maana kama ile ya “kauli za uchochezi”.

Kisichotakiwa ni maneno na matendo ya kijinai ambayo tayari yanadhibitiwa na sheria km mashambulizi ya mwili (violence), matusi (insults) na uongo ambayo mtendewa hupaswa kushitaki.

Polisi hawatakiwi kuingilia maneno bali kuzuia mashambulizi ya mwilini pekee ili kulinda amani. Nje ya hapo, everything goes. Siasa ni mapambano. Tambo lazima ziwepo.
 
Ili watu wote tuwe kwenye ukurasa mmoja wa uelewa bila kujali itikadi zetu za kisiasa, elimu, jinsia na hata makabila na kanda zetu tunakotoka ni lazima neno "kufanya siasa za kistaarabu" lipewe tafsiri yake ili wadau wote wafahamu maana yake ili kama mtu mkifanya siasa zisizokuwa za kistaarabu kila mtu awe shahidi.

Siasa za kistaarabu ni nini na ni zipi?

Je, kufanya siasa zisizo za kistaarabu ni kufanya nini?

Je, ni nani anatakiwa kufanya hizo siasa za kistaarabu?
Je, ni nani atakaesema wewe umefanya siasa zisizo za kistaarabu?
Je, ni nani atawaadhibu wote wanaofanya siasa zisizo za kistaarabu bila kujali ni wa chama gani?

Na je, kusema uongo, kufichua ukweli ambao ulifichwa, kuiba kura, kuengua wagombea, kutumia mali ya umma kwenye siasa za vyama, kuzuia mikutanp ya vyama na maandamano na tumumia maneno ya kuudhi kwenye siasa ni sehemu ya siasa zisizo za kistaarabu pia?

Taifa lazima lisonge mbele na lionekane na wote likisonga mbele.
🤣 Siasa za kistaarabu ni kutompiga spana bibi titi! Ukimkandia tu vijana wake wanakuvaa
 
Watu washindane Kwa hoja,hakuna matusi,uzushi na uongo sio kusema tu ndege kubwa imetua Serengeti inabeba wanyama bila ushahidi. Na Serikali isiteke na kuua raia wake wanaoikosoa bali wawajibu wananchi kwa ushahidi kwamba hii ndege haibebi wanyama bali inakuja kufanya kitu fulani.
"Sote tunajenga nyumba Moja hatuna haja ya kugombania fito" by JK.
 
Jambo moja linaweza kuwa sio hoja, uzushi au matusi kwako na kwa mtu mwingine likawa kinyume chake.
Kama unahisi umetukanwa au kuna uzushi mahakama zipo za kudai haki yako kama walivyofanya Membe na Fatma Karume kwa Cyprian Musiba.
Watu washindane Kwa hoja,hakuna matusi,uzushi na uongo sio kusema tu ndege kubwa imetua Serengeti inabeba wanyama bila ushahidi. Na Serikali isiteke na kuua raia wake wanaoikosoa bali wawajibu wananchi kwa ushahidi kwamba hii ndege haibebi wanyama bali inakuja kufanya kitu fulani.
"Sote tunajenga nyumba Moja hatuna haja ya kugombania fito" by JK.
 
Watu washindane Kwa hoja,hakuna matusi,uzushi na uongo sio kusema tu ndege kubwa imetua Serengeti inabeba wanyama bila ushahidi. Na Serikali isiteke na kuua raia wake wanaoikosoa bali wawajibu wananchi kwa ushahidi kwamba hii ndege haibebi wanyama bali inakuja kufanya kitu fulani.
"Sote tunajenga nyumba Moja hatuna haja ya kugombania fito" by JK.
Uchaguzi ni kila baada ya miaka 5, lakini kuwa watu wanadhani na kuwaaminisha watu kuwa bila wao kuwa madarakani taifa litasambaratika, watu watapigana na muungano utasambaratika,
 
Siasa za kiustarabu lazima zizingatie mila na desturi za kitanzania na kiafrika,uungwana,lugha isiyo ya kuudhi kwa mtu binafsi na jamii, kukwaza, kumkwaza mwingine, dharau,matusi,uzushi na hii ni kwa pande zote. Ukweli,uwazi na lugha zenye kuleta uwajibikaji, kukemea,na kufichua maovu kwa lugha ya staha haiwezi kuwa sehemu ya lugha isiyo ya kiustaarabu kwenye majukwaa. Kufuata Kanuni na Taratibu za uchaguzi ni vichocheo vya siasa zenye ustaarabu, maridhiano na kuheshimiana, kushindana kwa sera na hoja,mantiki,kukosoa kwa ushahidi wa takwimu na vielelezo, na kwa kuzingatia katiba,sheria ili HAKI na WAJIBU vitamalaki katika siasa na uongozi nao ni ustaarabu pia,hivyo vigezo vya siasa za kiustaarabu ni pana ila kipimo ni pamoja na jamii kubwa inakuonaje na siasa zako unavyoziendesha iwe chama tawala au cha ushindani? Huna budi kujitafakari kwa maslahi mapana ya nchi
 
Kama wanasiasa wote tutatenda kama hivi Tanzania itabaki kuwa kubwa kuliko vyama vyetu. Tufike mahali tujione kama watu wote wanaojenga nyumba Yao ya kulala na familia zao. Kila mtu awe na uelewa sawa juu ya nini ni siasa za kistaarabu, nini maana ya muungano na nini maana ya uchumi wetu na tunachokitaka kitokee bila kujali ni Chama gani kinaongiza nchi. Mbona wenzetu kule Ulaya, Marekani na kwingine wanaweza?
 
Ili watu wote tuwe kwenye ukurasa mmoja wa uelewa bila kujali itikadi zetu za kisiasa, elimu, jinsia na hata makabila na kanda zetu tunakotoka ni lazima neno "kufanya siasa za kistaarabu" lipewe tafsiri yake ili wadau wote wafahamu maana yake ili kama mtu mkifanya siasa zisizokuwa za kistaarabu kila mtu awe shahidi.

Siasa za kistaarabu ni nini na ni zipi?

Je, kufanya siasa zisizo za kistaarabu ni kufanya nini?

Je, ni nani anatakiwa kufanya hizo siasa za kistaarabu?
Je, ni nani atakaesema wewe umefanya siasa zisizo za kistaarabu?
Je, ni nani atawaadhibu wote wanaofanya siasa zisizo za kistaarabu bila kujali ni wa chama gani?

Na je, kusema uongo, kufichua ukweli ambao ulifichwa, kuiba kura, kuengua wagombea, kutumia mali ya umma kwenye siasa za vyama, kuzuia mikutanp ya vyama na maandamano na tumumia maneno ya kuudhi kwenye siasa ni sehemu ya siasa zisizo za kistaarabu pia?

Taifa lazima lisonge mbele na lionekane na wote likisonga mbele.
Napenda kutoa shukurani zangu za dhati, kwa Mada hii.

Kwa mda mrefu nimekuwa nikikataa utumiaji wa lugha hiyo misamiati hiyo yaani Kistaha-arabu na Ki- Ungwana au Ngwana Kwa sababu Una ukimbari.

Again, nakushukuru sana sana, na uendelee kupata rehema za Mwenye enzi.

Ni maoni yangu, kuwa ni Wakati muafaka wa kukataa maneno haya kutumika Serikalini.

Nitaendelea kusimama kidete katika suala hili.

Aluta Continuq.
 
Ili watu wote tuwe kwenye ukurasa mmoja wa uelewa bila kujali itikadi zetu za kisiasa, elimu, jinsia na hata makabila na kanda zetu tunakotoka ni lazima neno "kufanya siasa za kistaarabu" lipewe tafsiri yake ili wadau wote wafahamu maana yake ili kama mtu mkifanya siasa zisizokuwa za kistaarabu kila mtu awe shahidi.

Siasa za kistaarabu ni nini na ni zipi?

Je, kufanya siasa zisizo za kistaarabu ni kufanya nini?

Je, ni nani anatakiwa kufanya hizo siasa za kistaarabu?
Je, ni nani atakaesema wewe umefanya siasa zisizo za kistaarabu?
Je, ni nani atawaadhibu wote wanaofanya siasa zisizo za kistaarabu bila kujali ni wa chama gani?

Na je, kusema uongo, kufichua ukweli ambao ulifichwa, kuiba kura, kuengua wagombea, kutumia mali ya umma kwenye siasa za vyama, kuzuia mikutanp ya vyama na maandamano na tumumia maneno ya kuudhi kwenye siasa ni sehemu ya siasa zisizo za kistaarabu pia?

Taifa lazima lisonge mbele na lionekane na wote likisonga mbele.
Tafsiri yake ni kufata taratibu na kanuni zilizopo katika katiba ya chama cha siasa ikizingatia sheria za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Ulianza kuelezea vizuri, Unauelewa. bahati mbaya sio mfano mzuri.

Kwa tafsiri nyingine ni sawa na Kusema , tuiname tu na kusokomezwa. Tusujudu tu, kwa vile "Watawala" Watwaa ndio wamesema.

Kuwa ndio 'Sharia' Kuwa ndio anataka Mungu au ndio maandiko makuu yanavyotutaka tuyafuate. PSALM 136?
Shabash
 
Tafsiri yake ni kufata taratibu na kanuni zilizopo katika katiba ya chama cha siasa ikizingatia sheria za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tatizo lililopo watu wameaminishwa kuwa ni wapinzani TU wasiofanya siasa za kistaarabu. Polisi, mwajili wa vyama, maDC, RC, wakurugenzi, mawaziri na wengi TU wanaamini hivyo. Hii inasababisha shida nyingi sana kwenye siasa zetu za kistaarabu. Anaewaita watu malofa, dogs, wahuni na majina mengine ya kuudhi, wanaoengua wagombea, na wanaoiba kura hawaonekani wanakosea.
 
Brow uwezi kuwa na usawa wa kisiasa angali anaeifanya iyo siasa ajui nn anachokifanya.
 
Uchaguzi ni kila baada ya miaka 5, lakini kuwa watu wanadhani na kuwaaminisha watu kuwa bila wao kuwa madarakani taifa litasambaratika, watu watapigana na muungano utasambaratika,
Stick on the Topic. Usiterereke.

Hajatukanwa mtu na Watu wasitukanwe. Hii ni mada Muhimu na ina Hoja zilizosimama.Wasikuyumbishe.

Usikubali kuyumbishwa na wanyanyasaji na wadumazi.na Wapuuzi
 
Kutoiba kura kama CCM ndio siasa za kistaarabu, kupiga wapinzani,kuzuia mikusanyiko/mikutano ya watu kwa kutumia wakuu wa wilaya na polisi, kubadilisha matokeo, kubambikiana kesi etc ndio siasa za chama cha ovyo sana kinachoitwa CCM kuwahi kutokea Tanzania, umaskini wa Tanzania sababu kubwa ni CCM, tujaribu Chadema, CCM wameshindwa, nao wakishindwa tunapiga chini
 
Naona Kuna Umuhimu wa Baraza la Kiswahili Tanzania kutoa chochonde kuhusu Hoja zilizowasilishwa.

Kuna umuhimu wa kutoa Tafasiri na asili ya Maneno hayo.

Hatuwezi kuendelea kuwa jamii Limbukeni wa Lugha.
 
Ili watu wote tuwe kwenye ukurasa mmoja wa uelewa bila kujali itikadi zetu za kisiasa, elimu, jinsia na hata makabila na kanda zetu tunakotoka ni lazima neno "kufanya siasa za kistaarabu" lipewe tafsiri yake ili wadau wote wafahamu maana yake ili kama mtu mkifanya siasa zisizokuwa za kistaarabu kila mtu awe shahidi.

Siasa za kistaarabu ni nini na ni zipi?

Je, kufanya siasa zisizo za kistaarabu ni kufanya nini?

Je, ni nani anatakiwa kufanya hizo siasa za kistaarabu?
Je, ni nani atakaesema wewe umefanya siasa zisizo za kistaarabu?
Je, ni nani atawaadhibu wote wanaofanya siasa zisizo za kistaarabu bila kujali ni wa chama gani?

Na je, kusema uongo, kufichua ukweli ambao ulifichwa, kuiba kura, kuengua wagombea, kutumia mali ya umma kwenye siasa za vyama, kuzuia mikutanp ya vyama na maandamano na tumumia maneno ya kuudhi kwenye siasa ni sehemu ya siasa zisizo za kistaarabu pia?

Taifa lazima lisonge mbele na lionekane na wote likisonga mbele.
Hongera mkuu 'kavulata' ni mada makini sana hii.

"Siasa za kistaarabu" haya maneno yamesikika yakisemwa na watu/viongozi wa ngazi za juu kabisa katika vyama.

Hawa ndio wenye majibu sahihi ya swali lako kuhusu ni kipi hasa walicholenga wao.

Je, Samia akishindwa kutimiza baadhi ya ahadi zilizotolewa kwenye maridhiano, bado atakuwa anaonekana kufanya "siasa za kistaarabu"?

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakiona hadaa alizofanya Samia kwa mwenyekiti wao na wao wakaziibua na kuzitumia majukwaani, hawa watasemwa kuwa "hawafanyi siasa za kistaarabu"?

Kama unavyoona, maswali ni mengi, lakini inaonekana msemo huo ni njia ya kuziba watu wasihoji viongozi vitendo na kauli za viongozi wao.
 
Kuwa tungi ndio mwanzo wa siasa za kistaarabu.
 
Ila kuiba kura, kuteka wapinzani, kuengua wapinzani kwa mizengwe kwenye chaguzi ni sehemu ya siasa za kistaarabu!
Kiongozi kuhadaa, kufanya ujanja ujanja na kutumia lugha tamutamu kuahidi anayojuwa hayawezi kutimizwa, huku akilenga chama chake kuendelea kunufaika na hadaa hizo, ambazo hazimtii mtu yeyote kilema, wala kumsweka ndani; hizi zinaweza kuonekana kuwa ni siasa za kistaarabu kwa watu wengi!
 
Back
Top Bottom