Ni nini tafsiri hasa ya "Kufanya siasa za kistaarabu?"

Siasa ambazo siyo za kistaarabu ni kama Ile ya June 2021 baada ya Mdude kuachiliwa na Mahakama ya Mbeya kwenye kesi ya mihadarati. Kwenye mkutano wa Baracuda Mdude Chadema alisikika akisema "Mwambieni na huyo mama yenu, niyamnyoa kwa wembe uleule niliomnyolea Magufuli"
 
Jambo moja linaweza kuwa sio hoja, uzushi au matusi kwako na kwa mtu mwingine likawa kinyume chake.
Kama unahisi umetukanwa au kuna uzushi mahakama zipo za kudai haki yako kama walivyofanya Membe na Fatma Karume kwa Cyprian Musiba.
Inakuwaje kama utatukanwa na mtu mwenye Kinga ya kutokushitakiwa?
 
Stick on the Topic. Usiterereke.

Hajatukanwa mtu na Watu wasitukanwe. Hii ni mada Muhimu na ina Hoja zilizosimama.Wasikuyumbishe.

Usikubali kuyumbishwa na wanyanyasaji na wadumazi.na Wapuuzi
Wadau waje kwenye meza ya duara wadadavue na kuja na kijitabu Cha orodha ndefu ya aina ya siasa zisizotakiwa kufanywa na mtu wa aina yoyote yule bila kujali kwao ni wapi pamoja na adhabu zake. Kijitabu hiki kisambazwe hata shule za msingi waliko watanzania wa kesho. Tuusiijenge nchini yetu kwa matukio TU, bali tuwe na mpango mkubwa juu ya mwelekeo wetu. Tuje na sifa za mtu anaetaka kuwa kiongozi wa umma hata wa kitongoji mpaka taifa, kuanzia kuzaliwa kwake, malezi, elimu mpaka tabia.
 
 
Ili neno la kufanya siasa za kistaarabu liwe na maana lazima vitendo kama vile vya jecha salim jecha aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar visiwepo kabisa. Mtu hawezi kufanyiwa vile halafu abaki kufanya siasa za kistaarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…