Ni Nini tofauti kati ya Guest house, Lodge, Hoteli na Motel?

Ni Nini tofauti kati ya Guest house, Lodge, Hoteli na Motel?

Kwa uelewa wangu zote zinatoa huduma ya chakula na malazi ila zinatofautiana maeneo. Hotel mara nyingi ziko katikati ya mji, lodges zipo nje rural areas (porini huko), motel ni kwaajili ya wanaosafiri na motor vehicles hence the name, guest houses ni kwaajili ya wageni wanaotoka mbali na sehemu hiyo. Haina hadhi ya hizo hapo juu
 
Na hizi huwa sielewi Bar, Pub, Grocery
Kwa maana halisi japo wabongo tumeharibu maana

1. Grocery:- unanunua pombe na kwenda kunywea kwenu.
Yaani hunywei hapo, unaenda kunywea kwenu.

2. Bar = unanunua pombe na kunywea hapo. Unanunua na kunywa hapohapo.

3. Pub = Public = sehemu ambayo wakubwa wanakutana kunywa pombe ila watoto nao wanakuwepo (public). Kwamba watu wazima wanakutana na kunywa mitungi pamoja na watoto (ila watoto hawanywi) = Public Meeting.

Ila kibongo bongo TUMEHARIBU MAANA.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Guest ni mahali unaweza kulala tu bila ya kuwepo chakula! Lodge niseme I umelala then kuna breakfast,chakula,nk hotel ni sehemu Unalala ipo na hadhi ya kuwa na chakula na baa ikiwa na hadhi kuanzia na nyote,Motel ni hotel unaingia na gari kwa maana ni juu mnapaki naingia hotelini ukitoka unaingia katika gari unashuka chini na gari yako
 
Gemini Ai

1. Guest (Guest House)

Ni malazi ya kawaida kwa wageni, mara nyingi ni sehemu ndogo yenye vyumba vichache.

Inaweza kuwa sehemu ya nyumba ya mtu binafsi au jengo dogo lenye vyumba vya wageni.

Huduma zinaweza kuwa za msingi, kama kitanda na bafu, lakini bila huduma nyingi za kifahari kama hoteli.

Mara nyingi hutumiwa kwa malazi ya muda mfupi.

2. Lodge

Ni aina ya malazi yanayopatikana zaidi katika maeneo ya utalii au sehemu za vijijini.

Huwa na mazingira ya asili, kama vile karibu na mbuga za wanyama au fukwe.

Huduma zinaweza kuwa za kiwango cha kati au cha juu, kulingana na lodge husika.

Baadhi ya lodges zina nyumba za kujitegemea, mabanda ya mbao, au hata mahema ya kifahari.

Tofauti Kuu:

Guest ni malazi ya kawaida kwa wageni wa muda mfupi, mara nyingi ndani ya miji au karibu na sehemu za biashara.

Lodge ni malazi yanayopatikana zaidi maeneo ya utalii au ya asili, yenye mazingira tulivu na wakati mwingine huduma za kifahari.
 
Kwa maana halisi japo wabongo tumeharibu maana
1. Grocery:- unanunua pombe na kwenda kunywea kwenu.
Yaani hunywei hapo

2. Bar = unanunua pombe na kunywe hapo. Unanunua na kunywa hapohapo.

3. Pub = Public = sehemu ambayo wakubwa wanakutana kunywa pombe ila watoto nao wanakuwepo (public). Kwamba watu wazima wanakutana na kunywa mitungi pamoja na watoto (ila watoto hawanywi).

Ila kibongo bongo TUMEHARIBU MAANA.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
anha unyama sana maelezo yamekaa poa ila YOU WILL WALK ALONE 😀
 
Na hizi huwa sielewi Bar, Pub, Grocery
Na restaurant
Guest ni mahali unaweza kulala tu bila ya kuwepo chakula! Lodge niseme I umelala then kuna breakfast,chakula,nk hotel ni sehemu Unalala ipo na hadhi ya kuwa na chakula na baa ikiwa na hadhi kuanzia na nyote,Motel ni hotel unaingia na gari kwa maana ni juu mnapaki naingia hotelini ukitoka unaingia katika gari unashuka chini na gari yako
Ahsantee sana
 
na canteen, cafe, cafeteria, catering
Kwa ninavyolewa restaurant ipo Public yaani kila mtu anaruhusiwa kwenda kununua chakula.
Cafe ni sehemu mahususi kwaajili ya chai au kahawa au maziwa au cappuccino yaani kiufupi kifungua kinywa.
Canteen ni kwaajili ya organizational fulani kama vile shule au kampuni.
Catering ni huduma ya kusambaza chakula kwenye masharehe au events mbalimbali.
 
Gemini Ai

1. Guest (Guest House)

Ni malazi ya kawaida kwa wageni, mara nyingi ni sehemu ndogo yenye vyumba vichache.

Inaweza kuwa sehemu ya nyumba ya mtu binafsi au jengo dogo lenye vyumba vya wageni.

Huduma zinaweza kuwa za msingi, kama kitanda na bafu, lakini bila huduma nyingi za kifahari kama hoteli.

Mara nyingi hutumiwa kwa malazi ya muda mfupi.

2. Lodge

Ni aina ya malazi yanayopatikana zaidi katika maeneo ya utalii au sehemu za vijijini.

Huwa na mazingira ya asili, kama vile karibu na mbuga za wanyama au fukwe.

Huduma zinaweza kuwa za kiwango cha kati au cha juu, kulingana na lodge husika.

Baadhi ya lodges zina nyumba za kujitegemea, mabanda ya mbao, au hata mahema ya kifahari.

Tofauti Kuu:

Guest ni malazi ya kawaida kwa wageni wa muda mfupi, mara nyingi ndani ya miji au karibu na sehemu za biashara.

Lodge ni malazi yanayopatikana zaidi maeneo ya utalii au ya asili, yenye mazingira tulivu na wakati mwingine huduma za kifahari.
Kumbe hizi lodge za wakina majaba hapa kitaa hazifai kuitwa lodge?

Ahsantee sana Kwa maelezo yako
 
Back
Top Bottom