Tripple MM
JF-Expert Member
- May 31, 2023
- 417
- 567
lodge je mkuu yenyewe ipoje?Guest house unakutana na ndala zipo tofauti alafu zimekatwa kidogo..
Guest house hakuna huduma ya chakula, parking,mlinzi
Guest house Mali zako zikipotea utajua mwenyewe.
Excellent madam unajua mpaka unaboa, we ni mtu wa hospitality na recreations.-Hotel ni sehemu unayoweza kupata huduma ya chakula, vinywaji na maladhi kwa pamoja na huduma nyinginezo mfano huduma za utalii, kuvua kwa hotel zilizo kando ya bahari , SPA massage nk.
star(nyota)/hadhi ya hotel inapewa kulingana na huduma ya hotel kwa ujumla haiangaliwi majengo yake, hotel inaweza ikawa ghorofa lakini isiwe na hadhi yoyote.
Lodge hizi ni aina ya hotel zinazopatikana nje ya mji.
Motel hizi ni aina ya hotel zinatakiwa ziwe kwenye main road zinazo unganisha nchi, mikoa kwa ajili ya wasafiri na madereva. Mara nyingi zinatakiwa ziwe na kituo Cha mafuta karibu na huduma za service za magari
Guest house hizi zinatoa huduma ya maladhi tu.
Resort hizi ni aina ya hotel zinazopatikana pembezoni mwa bahari, ziwa au mto.
LoungeNgoja niuongezee misamiati:
Bistro
Tavern
Eatery
Cafe
Inn
Restaurant
Ngoja waje wasiojua tofauti ya TUNDU, SHIMO NA TOBONa hizi huwa sielewi Bar, Pub, Grocery
hapo kwenye yanga bingwa anatembea peke yake pia 😁anha unyama sana maelezo yamekaa poa ila YOU WILL WALK ALONE 😀
Vyote ni kitu kimoja location ndiyo inasema iitwe hotel hiyo iwe lodge ,motel, inns au resort.1. Guest House
• Ni nyumba ya wageni ambayo mara nyingi huwa na vyumba vichache kwa ajili ya malazi.
• Huduma zinazotolewa ni za kawaida kama chakula na usafi, lakini si za kiwango cha juu kama hoteli.
• Mara nyingi ni sehemu ya biashara ndogo au familia inayowakaribisha wageni kwa gharama nafuu.
2. Lodge
• Inahusiana zaidi na malazi ya kitalii, hasa maeneo ya asili kama hifadhi za wanyama na mbuga za taifa.
• Inaweza kuwa na huduma za kifahari kulingana na hadhi yake, ikiwa na nyumba za mbao au mahema ya kifahari (luxury tents).
• Inalenga zaidi watalii na wapenzi wa mazingira.
3. Hoteli
• Ni sehemu kubwa ya biashara ya malazi inayotoa huduma mbalimbali kama vyumba vya kulala, mgahawa, baa, spa, na hata kumbi za mikutano.
• Huwa na hadhi tofauti (kama nyota 3, 4, au 5) kulingana na ubora wa huduma na vifaa vilivyopo.
• Inahudumia wageni wa aina tofauti, kuanzia wasafiri wa biashara hadi watalii wa kawaida.
4. Moteli
• Neno linatokana na “Motor” na “Hotel,” na linamaanisha sehemu za malazi zilizo karibu na barabara kuu kwa ajili ya wasafiri wa safari ndefu.
• Vyumba vyake mara nyingi huwa na maegesho ya magari karibu na mlango wa chumba.
• Huduma zinazotolewa ni za msingi, zikilenga kutoa sehemu ya kupumzika kwa wasafiri wa muda mfupi.
Guest House ni ile ya kulala Masikini kama Mimi na Wewe, Lodge ni ile ya kulala ambao wanaanza sasa kuamka Kiuchumi, Hoteli ni ile ambayo wanalala Watu ambao tayari Uchumi wao wa Kimaisha umeshasimama (angalau wanajiweza) na Motel ni ile ambayo Wanalala Matajiri au Watu ambao Uchumi wao si wa Wasiwasi, wa Kubahatisha na wa Mawazo.Wakuu ebu nipeni majawabu kujifunza hakuishi. karibuni
Hivi ulishawai kukata leseni au unahadithiwa.Kama kila gari ni gari basi kusingekuwa na mabasi ,sedani,hatch,malori na n.kVyote ni kitu kimoja location ndiyo inasema iitwe hotel hiyo iwe lodge ,motel, inns au resort.
Msingi wa hotel lazima iwe na vinywaji(bar), iwe na chakula (restaurant) na rooms. Vikishakamilika hivyo hata ikiwa na vyumba 10 inajitosheleza kuitwa hotel...
Star ya hotel inaangalia service kwa ujumla ndio itaipa hotel iwe nyota ngapi au isiwe na nyota kabisa iwe hotel ya kawaida.
Hii Tanzania Ina Vizazi Vyake AiseeHotel maji moto utapata labda na breakfast
Lodge utapata majimoto na kunguni free
Guest house maji ya kopo kuoga ukikaa vbaya kunguni na utaamshwa watu wapige short time
Ok bossHivi ulishawai kukata leseni au unahadithiwa.Kama kila gari ni gari basi kusingekuwa na mabasi ,sedani,hatch,malori na n.k
👍Ok boss
Ila Kuna hotel zina 28 rooms
Zina four star
Halafu Kuna hotel zina zaidi ya vyumba 50 Zina one star
Naongea kitu ninachokiishi sio kusikia.
Gust hadhi yake ndogoWakuu ebu nipeni majawabu kujifunza hakuishi. karibuni
na cafe?Na restaurant?
Gesti ni ile bei maelewano....Wakuu ebu nipeni majawabu kujifunza hakuishi. karibuni
Ukishasema Guest house na Lorge tayari umemaliza tafsiri na tofauti zake.Wakuu ebu nipeni majawabu kujifunza hakuishi. karibuni