Ni njia gani sahihi ya kujikinga na U.T.I wakati wa sex?

Ni njia gani sahihi ya kujikinga na U.T.I wakati wa sex?

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,875
Reaction score
12,665
Jf doctors nipeni muongozo wakuu, ukiachilia mbali UKIMWI ambao tunaweza jikinga kwa kuvaa condoms huu ugonjwa wa U.T.I hata ukivaa condom unaupata

Je ni njia gani sahihi ya kujikinga na huu ugonjwa yahivi hata ukikutana na mwenye U.T.I asiweze kukuambukiza

Natanguliza shukran
 
Jambo la kwanza naoma TUTAMBUE:

1: UTI: Urinary Tract Infection ( maambukizi ya njia ya mkojo).

2: STI: Sexual Transmited Infection(Maambukizi yatokanayo na tendo la ngono).

Hivyo, UTI si STI Kwani wadudu wanaoambukizwa kwa njia ya ngono wamejitanabaisha/kuwa na uwezo wa kuambukizwa kwa njia husika.

Na kila mdudu atakaeweza kuhamishwa toka mtu mmoja kwenda mwingine kwa njia ya ngono basi huwekwa kwenye kundi la STI.

Asilimia 80-90 (80-90%) ya maambukizi ya UTI yanatokana na mdudu aitwaye E.Coli ambaye huishi kwenye njia ya chakula. Hivyo, maambukizi yake hutokana na kuhamishwa/self contamination kutoka njia ya chakula/haja kubwa kwenda kwenye njia ya mkojo.

Utofauti uko:
1: Aina ya wadudu
2: Eneo linaloshambuliwa
3: Baadhi ya dalili
4: Aina ya tiba
5: Vipimo vya kutambua ugonjwa
 
Kojoa mkojo kabla na baada ya kukutana.
Muoge na kujisafisha sana sehemu zote kabla
Na Mwisho kunywa maji sana ili kusafisha uchafu huo
Kama umepata UTI basi Inabidi utibu kwa antibiotics

Kweli unaweza kupata UTI kwa njia hiyo ingawa sio ugonjwa wa zinaa kama inavyojulikana STD
 
Jambo la kwanza naoma TUTAMBUE:

1: UTI: Urinary Tract Infection ( maambukizi ya njia ya mkojo).

2: STI: Sexual Transmited Infection(Maambukizi yatokanayo na tendo la ngono).

Hivyo, UTI si STI Kwani wadudu wanaoambukizwa kwa njia ya ngono wamejitanabaisha/kuwa na uwezo wa kuambukizwa kwa njia husika.

Na kila mdudu atakaeweza kuhamishwa toka mtu mmoja kwenda mwingine kwa njia ya ngono basi huwekwa kwenye kundi la STI.

Utofauti uko:
1: Aina ya wadudu
2: Eneo linaloshambuliwa
3: Baadhi ya dalili
4: Aina ya tiba
5: Vipimo vya kutambua ugonjwa
Unaambukizwa kwa njia ya mkojo lakini mara nyingi ukisex na mtu mwenye U.T.I unaupata kwanini?
 
Unaambukizwa kwa njia ya mkojo lakini mara nyingi ukisex na mtu mwenye U.T.I unaupata kwanini?
Si kweli, tatizo liko kwenye kutanabaisha ulichokipata ni UTI au STI?

Ukikutana kingono na mtu mwenye STI utapata STI.

Ukikutana na mtu mwenye UTI hautaambukizwa UTI kwani hii si njia rasmi ya kuhamisha mdudu husika.

Hivyo, ndo maana ukisoma jinsi ya kujikinga na UTI utaambiwa:
1: Kunywa maji ya kutosha
2: jisafishe ukitokea mbele kwenda nyuma
3: jisaidie haja ndogo mara tu unapohisi hitaji husika
4: Hakikisha choo chako ni kisafi kwa matumizi ya dawa za kusafishia.

Jinai ya kujikinga na STI
1: Usijihusishe na ngono nzembe
2: Tumia kondom na kwa usahihi
3: Pata chanjo kwa magonjwa yenye chanjo(HPV &Hepatitis).
4: Fanya vipimo kutambua hali yako ya maambukizi ya STI
5: Kutojihusisha na ngono kabisa
6: Usijihusishe na ngono wakati ukiwa umelewa.
 
... 1) Usikae mbali na sabuni DETTOL!
2) Tumia Kondom na uivae kabla hata hamjaanza shuuli yaani hata mikono yake isiguse kifaa chako peku!
3) Usivue Kondom kizembe, ... ukimaliza tendo, mwanawane, nenda bafuni na sabuni yako ya Dettol na osha kifaa chako na mazingira yote ya jirani kwa sabuni Dettol bila kuvua kondom. ... vua kondom pale tu unapohakikisha mikono yako na mazingira yanayozunguka kifaa ni salama na yamedhibitiwa vyema na sabuni Dettol!
4) UKIOGOPA KUAMBIWA UNANYANYAPAA SHAURI YAKO!
 
Si kweli, tatizo liko kwenye kutanabaisha ulichokipata ni UTI au STI?

Ukikutana kingono na mtu mwenye STI utapata STI.

Ukikutana na mtu mwenye UTI hautaambukizwa UTI kwani hii si njia rasmi ya kuhamisha mdudu husika.
U.T.I mkuu hata vipimo vinasema hivyo, stdi ni kama gono na kisonono hivyo sina
 
Jf doctors nipeni muongozo wakuu, ukiachilia mbali UKIMWI ambao tunaweza jikinga kwa kuvaa condoms huu ugonjwa wa U.T.I hata ukivaa condom unaupata

Je ni njia gani sahihi ya kujikinga na huu ugonjwa yahivi hata ukikutana na mwenye U.T.I asiweze kukuambukiza

Natanguliza shukran
Mhh,kumbe hata ukivaa condom unaupata?
 
... 1) Usikae mbali na sabuni DETTOL!
2) Tumia Kondom na uivae kabla hata hamjaanza shuuli yaani hata mikono yake isiguse kifaa chako peku!
3) Usivue Kondom kizembe, ... ukimaliza tendo mwanawane nenda bafuni na sabuni yako ya Dettol na osha kifaa chako na mazingira yote ya jirani kwa sabuni Dettol bila kuvua kondom. ... vua kondom pale tu unapohakikisha mikono yako na mazingira yanayozunguka kifaa ni salama na yamedhibitiwa vyema na sabuni Dettol!
4) UKIOGOPA KUAMBIWA UNANYANYAPAA SHAURI YAKO!
Dettol au sabuni kali kuoshea sehemu nyeti ya Mwanamke hapana aisee...haiwi recommended kiafya, unaua bacteria wote wa kumprotect pale
 
Hivyo, maambukizi yake hutokana na kuhamishwa/self contamination kutoka njia ya chakula/haja kubwa kwenda kwenye njia ya mkojo.
Hapo ndo kuna jibu,
Kuna vijana wanafurahia kupakua matope badala ya kuchakata mbususu.

Au pengine mtalimbo uligusa huko bahati mbaya ukaondoka na wadudu wa kutosha
 
Back
Top Bottom