Wapendwa habari zenu,
I hope everybody enjoyed the weekend.
Nimekuwa nikijiuliza hili swali bila kupata majibu, naomba mnisaidie.
kwa mfano uko kwenye mahusiano na mtu wako halafu ikatokea unataka kuachana naye kwa sababu zozote zile. Je ni njia ipi sahihi ambayo wewe ungeitumia kufikisha ujumbe kwa mpenzio au wewe unaipenda njia ipi mpenzi wako aitumie kukufikishia ujumbe kuwa hayuko tayari kuendelea na wewe? Baadhi ya njia zifuatazo zimekuwa zikitumika na watu wengi:
1. Kunyamaza kimya na kukata mwasiliano bila kuongea chochote?
2. kumpigia simu mlengwa na kumwambia ukweli kuwa hauhitaji kuwa naye.
3. Kumtumia sms na kumweleza lililo moyoni mwako.
4. Kumfanyia vituko ili akate tamaa yeye mwenyewe.
Je njia hizo ni sahihi kutumiwa au huwa zinatumika kwa makosa? Tujadili kwa pamoja tuone ni njia ipi sahihi ya kutumia kufikisha ujumbe (ambao sio mzuri kwa anayeachwa). Au kama kuna njia nyingine basi be free kuiweka wazi kwa faida yetu wote.
FUNGUKA MWANADADA, FUNGUKA MWANAKAKA UWANJA NI WAKO!