Ni Njia Gani Sahihi ya Kumwambia Mpenzi Wako Kuwa Hauko Tayari Kuendelea Naye?

Ni Njia Gani Sahihi ya Kumwambia Mpenzi Wako Kuwa Hauko Tayari Kuendelea Naye?

Jamani ! haya mambo msiyachukulie juu juu sana kwan mini napenda kujiuliza wakati unamtokea ulitumwa au ? na kama ilikua ni hiyari yako sas nini kinakubadilisha nia na ghafra kuanza kutafuta sababu zinazofaa kuwaumiza watoto wa wenzenu ! . ushauri wa bure tujifunze kutofautisha love na like better ukakaa na mtu hata miaka mia usimtamkie km unampenda ili hata mkishindwana hatojutia but sisi tuliowengi the 1st day tu nime kupenda na mbwembwe nyingi unakuja kujua mapungufu yangu unasumbua watu eti ipi njia sahihi sio pouwa sahihi ni kutokua na mahusiano kabisa tusichoshane hapa
 
Mimi huwa napenda ukweli zaidi kwani hata mimi namwambia mtu ukweli. bora mtu aniambie X naona hatuwezi endelea kuliko danadana. Najua ntaumia tena sana ila maumivu ya muda, kuliko mtu kunipotezea Muda wangu. kusema kweli kutengana kwa wapenzi inakuwa ni kipindi kigumu sana ila ikishakuwa hivyo inabidi ujifariji mwenyewe.
 
Unapotaka kumwacha mtu lazima utakuwa na sababu hivyo ni bora ukamwita mkakaa kikao cha maana na ukamwambia kwa unyenyekevu unayotaka kuyafanya ukimjuza tatizo lipo wapi hata ili kama ana matatizo fulani akipata mtu mwengine ajirekebishe kuliko kumchunia au kuleta ugomvi havisaidii kujenga zaidi ya kubomoa......

Impact inaweza kuwa kubwa kama kunywa sumu kwa wanawake wengine ( ni mfano tu) hivyo uwe tayari kujua utalimaliz vp baada ya hapo
 
Back
Top Bottom