Ni nyimbo zipi za Sugu zenye Ujumbe na zilizohit sana kuliko za Professor J?

Ni nyimbo zipi za Sugu zenye Ujumbe na zilizohit sana kuliko za Professor J?

ukitoa wimbo wa Haki,Chini ya 18 na Hold on labda kidogo Hayakuwa Mapenzi nyimbo zote zilizobaki za sugu ni kelele tu...na ukizungumzia nyimbo za harakati Sugu agusi hata robo ya Roma Mkatoliki tofauti yao itakuwa sugu alianza kuchana zamani basi
Sugu ndo ameifanya hip hop bongo ikuwe
 
Sistaduu anapokugeuza wewe ndio dingi
Mapenzi kidogo mizinga mingi
Leo atataka versace na mini skirt
Kesho atataka passport
Keshokutwa atataka tiketi aende London au America
Si bora nifanye part japo sio pasaka
Sugu alituonya kitambo sana kuhusu wadangaji
 
ukitoa wimbo wa Haki,Chini ya 18 na Hold on labda kidogo Hayakuwa Mapenzi nyimbo zote zilizobaki za sugu ni kelele tu...na ukizungumzia nyimbo za harakati Sugu agusi hata robo ya Roma Mkatoliki tofauti yao itakuwa sugu alianza kuchana zamani basi
Umesahau wimbo unaitwa "Hali halisi" wa Sugu ni noma
 
Naelewa sana ile wanakwita sugu ft stara pale p funky alipiga kinanda cha hatari na aliishibisha beat vya kutosha
 
Asilimia kubwa ya wanaomchukulia poa Mr Sugu ni hawa vijana waliozaliwa hivi karibuni ambao sa hivi ndo wanavaa modo na kupaka poda.!
Ila Kwa sisi wahenga ambao miaka ya 2000 - 2001 ndio tunaomjua Mr 2 "Sugu " ni nani.
Mie sinaga muda wa kusikiliza hizi nyimbo za kina
"Dawamondu "
Mie zangu ni zile za enzi hizo
J, moe, Prof Jay, Mr 2, Ay,J nature nk.
 
Sugu hana mziki wa maana wowote anaharishaharisha kwenye beat tu.
Wewe umezaliwa mwaka 2003 utamjulia wapi Sugu?
Uliza sisi baba zako wadogo ndo tunawajua hawa wasanii wa miaka hiyo vizuri,
Elewa unapozungumzia Sugu unazungumzia moja ya watu waliofanya muziki wa kizazi kipya ukubarike kwenye jamii kama hivi leo.
Ukiweza tafuta nyimbo za Mr 2 zifuatazo:-
-Mikononi mwa polisi
-Mambo ya fedha
-Chini ya 18
-wanakuita Sugu
-Hayakuwa mapenzi
-Hali halisi
Na nyingine nyingi ukizisikiliza ndo utajua kuwa Sugu ni nani!
 
Napenda nyimbo ambazo ni "sauti ya moyo".....kwa Sugu ni wimbo wa yale hayakuwa mapenzi, kwa prof Jay ni wimbo kama jina langu na mtu kama Solo Thang ni wimbo wa kilio changu
Umenikumbusha mbali Sana Duh..!
Solo thang..."hakuna S bila O"[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Nadhani mtoa post hamujui 2 proud Bali anamjua sugu Tu, uliza wimbo unaitwa chini ya 18, siku nikianguka, mikononi kwa polisi, far dsm, deiwaka, nje ya bongo, wapi tunakwenda, unaweza kubeza kazi za ii proud au umezaliwa Na kumjua akiwa anaitwa sugu tayari?
Yaani umegusa penyewe kabisa mkuu!
Nilichogundua asilimia kubwa ya members humu ni watoto waliozaliwa miaka ya 90 hivyo ukiongelea msanii kama Sugu wao wanajua ndo ameanza kuimba miaka hii!
Mfano kuna mtu nilishakuta anabishana kuhusu msanii Jmoe huyu aliyeimba "nisaidie kushare" eti ni msanii MPYA kwenye game nikawaambia ogopa Sana wasanii hawa Jmoe, Sugu, ProfJ, Nature, Ay, Mwana FA, Complex,Dudu baya.. Yaani hawa jamaa wameanza muziki kitambo, mfano Sugu ameanza kurap enzi kukiwa na Radio station moja tu nchi Nzima "RTD"
 
Mleta thread naamini humjui vizuri Sugu, pengine sababu ya umri wako, nikipata muda nitakuwekea albamu zake zote hapa.

Kuhusu Prof Jay, sikiliza nyimbo zake zote yeye anasimulia hadithi na matukio.
Uko sawa kabisa mkuu...tena ingekuwa mwisho wa mwezi ningekutumia vocha Kwa point nzuri sana. [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Sugu hana mziki wa maana wowote anaharishaharisha kwenye beat tu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] ndo shida ya mliozaliwa 2010. Kabka hajaitwa Sugu, huyu jamaa alikuwa anaitwa 2 Proud. Baadae akajiita Mr. II. Sikikiza wumbo wake unaitwa Barua kwa Rais, Mikononi Mwa Polisi ama Siku Nikianguka. Utajua ni mtu wa namna gani
 
Sugu hana mziki wa maana wowote anaharishaharisha kwenye beat tu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] ndo shida ya mliozaliwa 2010. Kabla hajaitwa Sugu, huyu jamaa alikuwa anaitwa 2 Proud. Baadae akajiita Mr. II. Sikikiza wumbo wake unaitwa Barua kwa Rais, Mikononi Mwa Polisi ama Siku Nikianguka. Utajua ni mtu wa namna gani
 
Yah bila kumsahau Afande Sele...aliimba sana kwenye albam za Sugu kabla hajatoka...
Sele ana wimbo wake "Afande anasema""

Kimya kimya afande anasema wote kimya...
Kimya kimya afande anasema...

Sijui hizi nyimbo nazipata wapi aisee!!
Tutazi upload hapa muda sio mrefu
 
Back
Top Bottom