Ni nyimbo zipi za Sugu zenye Ujumbe na zilizohit sana kuliko za Professor J?

Ni nyimbo zipi za Sugu zenye Ujumbe na zilizohit sana kuliko za Professor J?

Mitoto ya siku hizi sijui mnakula nn mnasikiliza miziki mi3 mshajifanya wachambuzi hivi unamjua 2 proud aka mr 2 wa 1990-2000 au sugu wa wakati umewajua wanawake hebu tujifunze kuheahim wakubwa basi kama prof j aliwaelewesha wazazi wako kusikiliza bongo flava basi sugu ndo aliowarusha debe wazazi wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Haaah haaah mkuu nimejikuta nacheka tu
Kizazi cha Chanjo kinashida sana kwenye maswala ya utambuzi msamehe ni athari za vaccination zinawasumbua maana zinaharibu mfumo wa kujitambua
 
Sugu hawezi kusikilizwa au kuujuwa kutokea kuupenda mziki wake kwa kijana ambae kazaliwa mwaka 2000. unadai nyimbo za sugu hana verce kama nyimbo gani kwa mfano
 
Mkuu naomba ufahamu kuwa nina track zoote za tokea zamani za 2 proud na nimemfuatilia tokea kitambo kipindi hicho na za Prof J

Nyimbo za Sugu sio kali kama za J.
Unajua Sugu ana albums ngapi, mpaka sasa? Ishu sio nani mkali kati ya Prof J na Sugu, ila unatakiwa ku-appreciate mchango wa kila mmoja kwenye sanaa hii ya bongo.
 
Tafta. HOLD ON BY SUGU

HAYAKUA MAPENZI BY SUGU

ni ww tu na mama hamkuniita mr two bali Joseph/
nilijiona dume mm mara nying uliposema hakuna penz kama ninalokupa mimi/
......
Tafta. HOLD ON BY SUGU

HAYAKUA MAPENZI BY SUGU



naamini nilikupenda ndo maana sikupenda ulipoamua kwenda/
mpaka leo najiuliza sijui ningefanya nini ndo nisingekupoteza/
nilifanya kila kitu nilichoweza/
kumbuka ni mara ngapi mtu mzima uliniliza chozi/
sikutaka tuachane tulijuana kwa mapana na marefu/
na tulifurahia pamoja music uliponipa umaarufu/
nami sikuvimba kichwa kwa mapenz yangu kwako yaliongezeka maradufu/
nawe herufi ya jina langu uliliweka kwenye kidani cha mkufu/
na ni wewe tu na mama hamkuniita mr two bali Josefu/
nilijiona dume mimi/
mara nying uliposema hakuna penz kama ninalokupa mimi/
ukaapa kuishi nami na ikibid kufa nami/
lkini ukabadilika na siamini kama leo haupo nami/

sugu_hayakuwa_mapenzi
 
Hiyo namba 3 naikubali sana



niliamini kitakachofuata ni uchumba/
daima penz langu kwako halikuyumba/
ulipata matatizo madaktari waliposema ungeweza kuwa mgumba/
bado nilikua tyari kwani maisha yetu ya mbele nilimwachia muumba/
Mungu ndo anampangia kila mmoja/
wangapi walizaa watoto na wote wakawa mateja/
na sasa japo uko mbali/
nakukumbuka dinner kwenye hotel kali kali/
sometime peke etu sometime na washikaji mbalimbali/
mambo yalipokuwa mazuri/
nilikua mwanamuziki tu sikuwa mfanyabiashara/
na mara nying mishiko niliipata kwenye ziara/
kumbuka nilipga show toka arusha mpka mtwara/
yote ni kusaa hela/kilichonisikitisha kwako hayakuwa mapenzi/
 
Mimi team Sugu tangu nipo darasa la kwanza nasikiliza tape zake
 
Bongo dsm ya prof jay kakopi idea kwa Sugu, Dar Dsm. Af kufananisha wanamzikii ktk nyakati tofauti ni dhahiri kuwa hamfahamu mziki. Huwezi mshindanisha Belafonte na Lionel Richie au Maneti na Moshi, mtachekwa kila mmoja alifanya mziki kutokana na jamii iliyokuwepo wkt huo hata production hazikufanana
 
Mtoa mada atakuwa ndo hawa watoto waliozaliwa wakati Jakaya yupo madarakani...Sugu wa kumbeza kweli??

Sikiliza
Ndani ya bongo
Nje ya bongo
Deiwaka
Hali halisi
Muziki na maisha
Mikononi mwa polisi
Hali yangu
Maisha yangu
Chini ya 18
Mambo ya fedha
Haki
Hapo zamani
Kiburi
Namshukuru mungu
Alekhmslam
Itikadi
Nikianguka
Hayakuwa mapenzi

Na nyingine kibao yani ni madini tosha
tntumie basi nyimbo kama,hapo zamani, nje ya bongo, haki
 
Back
Top Bottom