Depal
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 48,444
- 194,235
Hapa saa 9 kule saa 8. Uje uniambie ni nini inakufanya usilale usiku wote huo. 😁Kuna kipindi nilikuwa napenda kunywa amarula occasionally na hasa nikipata ofa[emoji2957]
Nakumbuka best angu alikuwa na birthday hivyo nikajikoki nikanunua ile kubwa. Tumekula vizuri tukaanza kunywa...mara best akaniambia hii kitu haijachangamka tuchanganye na k vant...yeye ni mtu wa pombe tofauti na mimi...bwana bwana si nikakubali nikawa naweka kidogo kidogo.
Chupa ilivyokaribia kuisha nikashangaa ulimi unakuwa mzito mdomoni[emoji2]Story haziendi tena ikabidi tuite tax. Hatukufika mbali kichefuchefu hiki hapa, mikono mizito sikuweza hata kufungua kioo nikatapikia ndani kwenye miguu...yani nililegea hatari. Dereva akamind akataka tumlipe na ya kuosha gari[emoji2]
Kufika home naona nyota tu nikaingia chooni kwa kutambaa....nilifanikiwa kuvua suruali tu[emoji85]
Tangu siku hiyo mapenzi na amarula yakaisha...nimekuja kuionja mwaka jana baada ya kama miaka 4 hivi ila niliinywa kwa tabu sana so nimeachana nayo.